Mke wangu kakutana na EX wake tukiwa pamoja, kafurahi hakuna mfano!

"Binti huyu alinibembeleza sana kuwa nisimtaje kabisa kama yy ndie source ya hiyo habari"

Huu ni umbea sasa.. yeye shemeji yako yanamuhusu nini?Ukifanya mchezo mtaachana kisa umbea wa shemejio yake yamemshinda anaanza kukufukunyua na nyie yakushinde shoga wake naye awe ameachika...

Think big mwanaume acha kufuatilia umbea babue.. kama mkeo hajawahi kukucheat ya nyuma yanakuhusu nini? we umefanya mafinyo finyo mangapi kabla ujakutana na mkeo... ACHA KUFUATILIA HABARI ZA UMBEA NDOA ITAKUSHINDA LOH....

Hug,kisses na shangwe la furaha mpaka kwenda kutambulishwa..umbea wa ukweli,unahitajika na wala sio shida,na amekili...!mpe ampe tu second chance,ila huyo demu kimeo,hawezi shangilia tu kwa kurupuka kurupaka..kwanza anaonesha hakuheshim na hajari hisia za mwana; vuta pumzi,ikotokea once..more,akasalimie kwao kwanza
 
Aisee achana na yaliyopita..utakufa bure kwa pressure jamaa achukuwe mzigo...tulia asee tunza mkeo..mengine tupa kule
 
Mashosti wengine wanahitaji vijiti vya makalio pambaff, japo mkeo nae hajafanya vizuri....UNAPOKUA NA MWENZIO JITAHIDI KUBEHAVE KUNA MAMBO YA KITHENGE HUTAKIWI KUFANYA, pole ni ex past has gone, mkanye mwambie ukikuta hata mawasiliano tu na huyo ex atabeba zubeda ahamie huko

Huyo shosti anamtaka huyo mume sio bure, kenge baridi kweli.
 
"Binti huyu alinibembeleza sana kuwa nisimtaje kabisa kama yy ndie source ya hiyo habari"

Huu ni umbea sasa.. yeye shemeji yako yanamuhusu nini?Ukifanya mchezo mtaachana kisa umbea wa shemejio yake yamemshinda anaanza kukufukunyua na nyie yakushinde shoga wake naye awe ameachika...

Think big mwanaume acha kufuatilia umbea babue.. kama mkeo hajawahi kukucheat ya nyuma yanakuhusu nini? we umefanya mafinyo finyo mangapi kabla ujakutana na mkeo... ACHA KUFUATILIA HABARI ZA UMBEA NDOA ITAKUSHINDA LOH....

Ila kumbuka mbea anatoa taarifa sahihi ila kwenye sehemu isiyo sahihi,Kwahiyo akili kumkichwa
 
Kwa mwanaume yoyote lazima uhumie lkn ukweli ni kwamba kama mke ukumkuta na bikira huna aja ya kuumiza kichwa,tujiulize ni wanaume wangapi wamebahatika kukuta bikira kwa wake zao.anza kumlinda mkeo toka siku mlipofunga ndoa na usitake kizijua habari zake kabla ya ndoa yenu!
 
Wewe Navindippe si ndo huyo mkeo aliebakwa na wale madalali kule bagamoyo.

Ulisema huwa hakushiriki mambo yake kisa Ana Mali za urithi alioachi na baba yake .

Hivi mlishasuluhushwa maana ulisema unamlia bati yeye na familia yake kisa wanakudharau.

Si ndo wewe au mwingine?

Cc Tyta kwa kuweka mambo sawa.

Mkuu kumbe huyu jamaa ndo yule wa ule Uzi wa "mke wangu amebakwa na sijaskia maumivu yeyote"..wale madalali bagamoyo..

Sasa itakua ameoa mwingine huyu anaefurahia kuliona JITU lake la maktaba..

Hizii story za kutunga na kuwaada umma wote wa jf..!!??!
safii lakinii ww mjanja.
 
Last edited by a moderator:
mkuu, huyo dada kakwambia ukweli mtupu. Wanawake wanao cheat hata kama mwanaume huna kosa, mashosti wake hata kumi huwa wanajua. I tell you, na wote huwa wanamwita huyo kidume shemeji...ndio maana madada wote humu wamechukia mwanamke mwenzao kukwambia ukweli, nawakimjua huyo dada mbona watamla nyama. Na ukimchapa huyo shem habarii zitamfikia wife. Women always talk of their conquests pia kwa mashosti wao....na huyo shosti ataropoka tu vitatembea we mwishowe wife atajua tu, hilo timbwili lake sasa.....nahapo mkuu kakupa kipande kidogo ukimchapa atakwambia mpaka may be hata recently washatiana, na ikiwezekana nyumbani kwahuyo huyo shosti. Ila hawa madada wanaotoa hizi habari huwa anakua anakutaka ndio maana anatoa news, wanaoneana wivu, au wife anabimjuliwa sana pembeni kiasi shem anataka ajue mkuu unakasoro gani akaongezee ubuyu, au kama una fweza anataka kukugeuza mradi, ila huwa wanabumbulukiwa na inakua ugly hata kwako. Mambo ya mujini ...kazi kweli.
 
Mkuu kumbe huyu jamaa ndo yule wa ule Uzi wa "mke wangu amebakwa na sijaskia maumivu yeyote"..wale madalali bagamoyo..

Sasa itakua ameoa mwingine huyu anaefurahia kuliona JITU lake la maktaba..

Hizii story za kutunga na kuwaada umma wote wa jf..!!??!
safii lakinii ww mjanja.

Aisee kumbe inaweza kuwa ya kutunga?
 
Wewe Navindippe si ndo huyo mkeo aliebakwa na wale madalali kule bagamoyo.

Ulisema huwa hakushiriki mambo yake kisa Ana Mali za urithi alioachi na baba yake .

Hivi mlishasuluhushwa maana ulisema unamlia bati yeye na familia yake kisa wanakudharau.

Si ndo wewe au mwingine?

Cc Tyta kwa kuweka mambo sawa.

blalfuu!...naishia hapa kusoma comments hadi aje atoe maelezo,asije kuwa anatuokota hapa!
cc: navin dippe
 
Last edited by a moderator:
Wakuu nawasalimu.

Nimetatizwa sana na jambo moja. Last Sunday tulienda Mlimani City na wife kwa matembezi ya jioni na kununua mahitaji machache ya ndani. Wakati tumefika mataa ya Mwenge, akampigia girlfriend simu wakutane hapo maana anaishi Survey jirani na hapo. Hivyo tukawa watatu kwenye mizunguko ya humo mall; mimi, wife na girlfriend who is a family friend to us ingawa mimi sina mazoea nae kiiivile.

Mwisho tukakaa nje tukawa tunakunywa pombe zetu taratibu. Kwenye saa mbili kasoro usiku akajitokeza jamaa mmoja, baada ya kutuona akaja kutusalimia, ambapo wife aliinuka kwa shangwe kubwa kumlaki kwa hugs na zile kiss za mashavuni wanaopiganaga wale wanaojifanya wazungu.

Wife akanitambulisha kuwa "he is a longtime friend". Lile jitu likazungusha round ya vinywaji, na pia likaniomba liende limtambulishe wife kwenye meza yao nikakubali ingawa moyoni nilikua nimefura kwa hasira, sema sikutaka kuonesha, bahati mbaya zaidi meza ya hilo jitu ilijaa wanaume pekee.

Tukabaki wawili wakati wife anaongea na meza ile, yule girlfriend akasema "shemeji naomba namba yako hapa mjini huwezi kujua ya kesho na keshokutwa", nami nikajibu ni kweli kabisa, tukabadilishana namba.

Monday yule binti akanipigia simu nikiwa kazini akaniambia shemeji kuna jambo nataka kukuambia ila usinitaje, nikajibu poa, akasema, "Yule jamaa wa jana ni ex wa mkeo. Walikua wapenzi kwa miaka yote mitatu chuoni wakiishi chumba kimoja nje ya chuo kama mke na Mume".

Na kwamba kwa kipindi chote cha hiyo 3 yrs alitoa kama mimba 2 hivi za huyo mshikaji, pia uhusiano wao ulienda hadi mtaani after university life. Walikuja kuachana kila mtu alipopata kazi yule ndugu akapelekwa Bukoba. Since then hawajawahi kuonana hadi hiyo jumapili pale Mlimani City, na kwamba lile jitu limerudishwa hapa Dar na halijaoa bado ila lina mapene sana.

Binti huyu alinibembeleza sana kuwa nisimtaje kabisa kama yy ndie source ya hiyo habari. Huyu binti ni rafiki wa wife tangu chuo ila bahati mbaya ndoa yake ilipata shida kidogo na kushindikana kutokana na uzinzi wa mwanaume

Ndugu wana JF, niliporudi home jioni ya monday nikaamua kulianzisha, ambapo wife alidai hakuona busara kunitambulisha kwamba yule bwana alikua ex wake.

Nikamuuliza ilikuaje ukafurahi na kushangilia kiasi kile na kushindwa kuficha kabisa hisia zako? Akabaki anajiuma uma tu na kushindwa kujibu.

Kiukweli sijaridhika na majibu yale na bado nina hasira. Nimekaa kimya bila kumuongelesha chochote wala kumsemesha kwa salaam wakati nikitafakari hatua ya kuchukua.

Nimekuja kwenu kwa msaada zaidi..

Yaan hapo ndugu yangu umeshagongewa bila shaka, msisitize tu mkeo atumie condom.
 
Back
Top Bottom