Mke wangu jini

Ok9

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
4,556
Reaction score
4,162
Ilikuwa ndani ya dakika tano tu , Munil aliingia
kwenye baa hiyo akiwa amebadili nguo. Alivaa
gauni nyeupe , refu hadi kufunika miguu wakati
awali alivaa gauni jekundu pia refu !
SASA ENDELEA MWENYEWE :
Alikuja moja kwa moja nilipokaa mimi kwenye
meza ya peke yangu, akanibusu kwanza kisha
akavuta kiti na kukaa huku akiniangalia kwa
uso uliojaa tabasamu laini. Kwa mara ya kwanza
mimi na Munil tulikaa pamoja hapo kwenye baa .
Nilianza kuhisi ni mwanamke wa tofauti sana
kwani walio wengi hawapendi kukaa baa , hasa
kwa mwonekano wake wa kiimani . Hakuwahi
kuniambia wa imani gani lakini jina lake , Munil
lilitosheleza kunijulisha yeye ni nani. Kwa hiyo
kuja kwake baa niliamini kulitokana na upendo
wake kwangu ambao ulitimilika . Nilifurahi sana
maana hata wakati anakaa hakutoa kauli ya
kuashiria kwamba hapendi kukaa baa .
SWALI LA KWANZA KWA MUNIL
“Munil sikumbuki kama nimewahi kuisevu namba
yako , lakini ghafla kwenye simu yangu
imeonekana kuseviwa kwa jina la Munil One
halafu sasa Munil Only , ni nini kimetokea
mama ?”
Wakati namuuliza hivyo Munil nilimkazia macho
nikiamini ataogopa kama anajua mchezo lakini
wala ! Aliniangalia kawaida na nilipomaliza
akaachia tabasamu lakini huku akisema :
“Jamani, mimi ndiyo nikuulize wewe mwenye
simu lakini wewe ndiyo unaniuliza mimi. Mimi
mwenyewe mfano simu yangu, namba unaweza
kuisevu kabisa lakini ukinipigia badala ya
kutokea jina zinaonekana namba tu . Kuhusu
kusevu inawezekana ulinisevu ila umepitiwa na
kumbukumbu, mbona hilo ni suala la kawaida
sana baba. ”
Munil alivyoniita baba, nilifurahi sana . Nilijiona
mimi ndiyo mimi hakuna mwingine duniani .
Munil alikuwa msichana mzuri sijapata kuona
tangu nimezaliwa . Hata alipoingia pale baa
alitazamwa na kila mtu .
Kuhusu alilolisema la simu, nilikumbuka tatizo
lake hata kaka analo kwenye simu yake,
anasevu jina lakini zinatokea namba kwa hiyo
kaka kila akipigiwa simu huwa na kazi ya
kumuuliza mpigaji , nani mwenzangu? Nikaamini
kuwa huenda ni matatizo ya simu yangu.
Niliyafanya mambo hayo yawe yameisha,
akaagiza soda kama nilivyofanya mimi. Lakini
pia akataka na sambusa mbili kwa kumwambia
mhudumu. Wakati tunakunywa huku yeye
akisubiri sambusa zake , mimi nilihisi muda
umekwenda na anaweza kumaliza soda yake bila
kinywaji kuletwa kwa hiyo nikamuhimiza
mhudumu aharakishe.
“Usijali baba, nitakwenda mimi mwenyewe , ”
alisema Munil , mimi nikainama kuangalia meseji
kwenye simu yangu, kuinua kichwa nikaona
sambusa kwenye kisahani cha chai ,
nikashtuka. “Nani kaleta ?” niliuliza . Kisa cha
kuuliza ni kwa sababu kuinamisha kwangu
kichwa chini kusoma meseji na kuinua ilikuwa
ndani ya sekunde kama kumi tu, halafu
nilipoona hiyo sahani sikumwona mhudumu
akiondoka kwenye meza yetu na wala
sikumwona Munil akirudi kuja kukaa .
Kwa wakati ule haikuwa rahisi kusema yote,
lakini baada ya kuyapitia yaliyotokea ndiyo
maana nayasema haya kwani niligundua
baadaye sana kwamba nilikuwa nimepatikana
kwa mke wangu ambaye alikuwa nusu ni mtu ,
nusu ni jini kamili .
Nilipata wakati mgumu sana kuwaza kuhusu
sambusa , Munil aliniambia amezifuata yeye
lakini kusema ule ukweli hakuzileta yeye na
wala hazikuletwa na mhudumu wa baa ile .
Nilinyamaza tu lakini akili ikiendelea
kuchangamka kuwaza .
“Baba, ” aliniita Munil baada ya kuwa kimya kwa
muda mrefu .
“Niambie mama . ”
“Utakwenda kuzika ?”
“Kwani mwili unakwenda kuzikwa wapi ?”
“Lushoto . ”
“Itabidi niende sijui ? We unasemaje ?”
“Twende wote. ”
“We utaenda?”
“Mimi tena , yaani ndugu halafu nikose ?!”
“Basi na mimi nitaongozana na wewe. ”
“Sawasawa. ”
Siku hiyo baada ya kuachana na Munil
nilikwenda nyumbani. Niliwaambia majirani
kwamba nitasafiri kwenda Lushoto , Tanga kwa
mazishi . Lakini kwa sababu ya uchovu niliamua
kutokwenda msibani kulala mpaka kesho yake
ambapo ningesafiri , hata kaka nilimwambia
hivyo.
Ilikuwa usiku wa saa nne nikiwa kitandani,
nilimkumbuka Munil kwamba hatujawasiliana kwa
muda mrefu , tangu tulipoachana kule baa ,
nikachukuwa simu ili nimtwangie lakini kabla
simu haijaita , mlango mkubwa uligongwa,
nikakata simu na kuuliza .
“Nani ?”
“Munil . ”
Nilishtuka , nikaguna kwanza na kujiuliza
mwenyewe:
“Amepajuaje hapa au hanitafuti mimi. ”
“Nakuja, ” nilisema kwa sauti nikitoka kitandani.
Nilifungua mlango, nikakutana na macho ya
Munil. Safari hii alikuwa mzuri zaidi ya wakati
wowote ule . Alizidi kuwa mweupe pee! Aliwaka
mtoto kama Mwarabu vile . Akaachia tabasamu .
“Karibu Munil. ”
“Asante, ” alisema akiingia ndani.
“Umepajuaje hapa Munil ?”
“Nimeulizia . ”
“Umeniuliziaje ? Maana sijawahi kukwambia
naitwa nani. ”
“Si unaitwa Abigael jamani au ?”
“Ndiyo lakini lini nilikwambia hilo jina langu
Munil?”
“Na wewe bwana , hebu tuyaache hayo . ”
Niliamua kuyaacha kweli kama alivyotaka Munil ,
nikamkaribisha chumbani huku nikimuuliza :
“Msibani umeaga unakwenda wapi ?”
Je, nini kiliendelea hapo ?
 
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
“Si unaitwa Abigael jamani au ?”
“Ndiyo lakini lini nilikwambia hilo jina langu
Munil?”
“Na wewe bwana , hebu tuyaache hayo . ”
Niliamua kuyaacha kweli kama alivyotaka Munil ,
nikamkaribisha chumbani huku nikimuuliza :
“Msibani umeaga unakwenda wapi ?”
SASA ENDELEA …
“Nimesema nakwenda kwangu . ”
“Kwani we hukai pale?”
“Hapana . ”
“Unakaa wapi ?”
“Si hapo nyuma tu . ”
“Hapo nyuma tu? Kwenye nyumba ya nani?”
“Nyumba ya mzee Ngurumo . ”
“Mzee Ngurumo ! Kwani pale pana wapangaji?”
“Si ndiyo mimi sasa . ”
“Mh!” Nilijikuta nikiguna tena maana nyumba
aliyoitaja kweli ipo. Mzee Ngurumo namjua
vizuri sana lakini pale nyumbani kwake hapana
mpangaji , ni familia tu na tena ana watoto wa
kiume pekee !
“Mbona kama umeshangaa sana , vipi ?”
“Sijashangaa sana ila nimeshangaa . ”
“Umeshangaa nini?”
“Si huyo mzee Ngurumo . ”
“Kwamba ?”
“Kwamba ana wapangaji pale kwake. Nilikuwa
sijui . ”
Munil aliniambia atalala kwangu usiku huo hadi
alfajiri ya saa kumi na moja atarudi msibani .
Hata asingesema hivyo yeye, mimi mwenyewe
nilitaka kumwambia asiondoke ili tuandike
historia ya kwanza katika uhusiano wetu .
Tuliongea mengi sana na Munil hadi kufikia
kuwekana wazi kwamba nini anataka , nini
hataki. Kitu kimoja kilinishangaza sana , Munil
alisema katika mambo anayoyapenda maishani
mwake ni mafuta mazuri , yaani pafyumu au
manukato.
“Ni kwa nini ?” nilimuuliza kwa kusisitiza
mshangao.
“Basi tu , yaani nimejikuta nikipenda sana.
Unajua baba, mama , wadogo zangu na hata
ndugu wengine wote wanapenda sana mafuta
mazuri. ”
Wakati Munil ananiambia hayo , alikuwa akinukia
mafuta mazuri sana.
Sasa ulifika muda wa mimi na Munil kulala .
Nilimwambia apande kitandani, akasema
anapenda kulala mwanzo wa kitanda lakini kwa
sababu amenipenda sana anakubaliana na mimi.
Alitangulia kupanda kisha nikafuata mimi.
Ilikuwa mara yangu ya kwanza kulala na Munil
na kukutana naye kimapenzi. Alinioamba tuzime
taa , nilikataa lakini akasisitiza kwamba huwa
anajisikia vizuri zaidi akiwa na mwanaume
kwenye chumba chenye giza nene.
Ili kuzima taa ilibidi mimi nitoke kitandani
kuifuata swichi , nikaweka mguu mmoja chini ,
kabla sijaweka wa pili, Munil akasema :
“Ngoja niende mimi. ”
Niliona ugumu yeye kwenda kwenye swichi
maana kama ni kutoka ingebidi aniruke kwanza .
Kilichotokea , nilimwona Munil akiamka kitandani
lakini sikumbuki nini atap ! Giza !
“He !” Nilishtuka , nikapapasa ubavuni kwangu ili
kuona kama Munil yupo au , nikamwona amejaa
tele !
“Umezimaje taa Munil?”
“Si nilikwenda. ”
“Siyo kweli Munil . Hujatoka kitandani. ”
“Ha ! Sasa kama nisingetoka kitandani
ningezimaje?” Munil aliniuliza akinishangaa .
Niliamua kukubaliana naye lakini kutoka moyoni
nilikataa kwamba, Munil aliizima taa bila kutoka
kitandani! Sasa nikawa najiuliza
alifanyajefanyaje? Ina maana alipeleka mkono
mpaka kwenye swichi? Haiwezekani . Nilikataa
kimoyomoyo .
Basi, mimi na Munil tuliingia kwenye tukio la
kihistoria ambapo kwa mara ya kwanza
tulifanya mapenzi tena bila kondom na cha
kushangaza sana ni kwamba, Munil
nilipomwambia habari ya kondom alisema haina
haja kwa sababu kama mimi nina Ukimwi siwezi
kumwambukiza yeye na kwamba yeye ni mzima
wa afya!
Nilishangaa sana kwa tamko lake hilo , nilianza
kuhisi sipo na mwanamke wa kawaida lakini hilo
pia nikalivumilia kwa namna nyingine
tena . Tulipomaliza, bado kukiwa na giza , Munil
alitaka kwenda chooni, akaniambia anaomba
kwenda chooni , nikamwambia unapajua ? Maana
choo chenyewe kilikuwa ndani kabla hujatoka
uani.
Aliniambia anapajua , nikashangaa. Nikamuuliza
uliwahi kuingia kwenye nyumba hii , akasema
ndiyo . Nikamwambia basi nenda nione . Niliamini
amesema tu lakini hakijui choo kilipo . Alipotoka
kitandani alivaa taulo langu lakini nilishikwa na
mshtuko kusikia akitembea kwa kunyata tena
kama mwanaume aliyevaa viatu vya
mchuchumio, maana vilikuwa vikilia ‘ koo , koo ,
koo. ’
Alipofungua mlango nikatoka haraka sana
kwenda kuwasha taa ili nione alikuja na viatu
gani. Nilijua kama sitaona viatu basi nitajua
alivaa viatu vya mchuchumio na ndivyo vilivyotia
mlio wa koo .
Ile nawasha taa tu, nikasikia sauti ikiniuliza:
“Hivi mbona kama una wasiwasi na mimi, kuna
nini kwani ?”
Alikuwa Munil amelala kitandani akiniangalia
kwa macho makali na yenye hasira .
“Ha ! Kwani si ulisema unakwenda nje
kujisaidia?” nilimuuliza nikitetemeka.
“Mimi sijatoka kitandani baby. Sasa kama ni
kwenda chooni si ningekwambia unisindikize, mi
napajua chooni kwenu ?” alisema Munil .
Nilizima taa ili nirudi kulala lakini wakati
nazima kabla ya tendo hilo niliangalia chini na
kubaini kwamba hakukuwa na viatu vyovyote.
Nilitupia macho kiaina miguuni kwa Munil pale
kitandani lakini sikuona kitu kwani miguu yote
ilikuwa ndani ya shuka.
Nilirudi kulala , ile namalizia tu kujifunika
shuka, mlango ukasukumwa, akaingia mtu .
Nilijua ni mwizi sasa, nikauliza :
“Wewe ni nani unayeingia?”
“Jamani baby, kwani si nilikwambia nakwenda
chooni, mbona unachanganyikiwa lakini ?”
Je, nini kiliendelea hapo ?
 
Oya story zako si uzimalizie kwenye thread moja,yaani kila mwendelezo unakuja na thread mpya ndani ya dk 7 mpaka asubuhi si itakuwa threads 600
 
Namba moja ni wapi.niwekee link plzz.
 
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Nilirudi kulala , ile namalizia tu kujifunika
shuka, mlango ukasukumwa, akaingia mtu .
Nilijua ni mwizi sasa, nikauliza :“ Wewe ni nani
unayeingia?”
“Jamani baby, kwani si nilikwambia nakwenda
chooni, mbona unachanganyikiwa lakini ?”
SASA ENDELEA MWENYEWE . . .
Kabla sijamjibu nilipeleka mkono pembeni yangu
kuona kama Munil alikuwepo, lakini hapakuwa
na mtu !
“Munil , ” niliita huku nikitoka kitandani na
kusimama katikati ya chumba nikiwa nahema
kwa kasi , woga ulinishika, miguu ilitetemeka
kama mtu aliyekutana na kiumbe wa ajabu
kwenye njia iliyosonga akiwa peke yake.
“Abee , ” aliitika Munil aliyeingia.
“Kwa nini unanifanyia mambo haya?”
“Yapi dear?” Munil aliniuliza huku akifunga
mlango na kuzima taa .
“Inakuwaje nikuone kitandani halafu pia wakati
huohuo nikuone unaingia , halafu kitandani
haupo?” nilisema kwa sauti ya juu . Nadhani
hata nje walisikia kama kulikuwa na watu.
“Baby hilo ndilo tatizo lako . Yaani wewe
umenifanya mimi ni jini siyo? Niwe kitandani
halafu niwe nimetoka nje , inawezekanaje?”
alihoji Munil akiwa amewasha taa sasa .
Alisimama mlangoni akiniangalia kwa macho
yaliyojaa mshangao.
“Baby, kwani una nini ?” aliniuliza.
Nilimsimulia hali ilivyokuwa , akasema itakuwa
nina mawazo mengi juu yake ndiyo maana
namuwewesekea mpaka namwona mara
mbilimbili.
Basi, nilijipa moyo, nikamshika mkono Munil na
kumpandisha kitandani kisha na mimi
nikapanda. Niliamua mara hii tulale na mwanga
hivyo sikuzima taa . Sikuchukuwa muda mrefu
sana nilipitiwa na usingizi na kuota ndoto.
Niliota niko kwenye jumba moja kubwa sana la
kifahari . Ukuta wote ulipambwa kwa dhahabu ,
juu badala ya kuezekwa mabati, kulipigwa
madini ya shaba. Ilikuwa sehemu ya peke yake.
Eti humo nilikwenda kuulizwa ukweni kama
nitamuoa binti yao au la ! Binti mwenyewe
alikuwa amenipeleka kwa wazazi wake nikaulizwe
vile alisimama katikati ya sebule kubwa
akiniangalia kwa macho mazuri huku akiachia
tabasamu laini. Alikuwa binti mzuri kwa namna
yoyote ile, sura hadi umbo lakini alionekana si
mtu mweusi , kama Mwarabu au Mzungu
aliyechanganya damu .
Wazazi wake waliniangalia kwa macho ya
kunikubali huku baba mtu akiniambia kama
nitakubali kumuoa binti yao atanipa sehemu ya
mali yake ili kuendeshea maisha na binti yao
lakini kama sitakuwa tayari kwa ndoa, yule
baba aliniambia angenichinja kwa sime akitumia
mkono wake .
Wakati anasema kama siko tayari kumuoa binti
yake atanichinja kwa sime , alitoa mfano,
akaenda kwenye kona ya sebule , alitumbukiza
mkono mahali na kutoa sime , akanifuata na
kuniwekea shingoni , wakati anaanza kuchinja
nikashtuka kutoka usingizini huku nahema sana
na jasho jembamba likinishuka mwilini.
“Vipi baby?” aliniuliza Munil baada ya kuamka
kwangu huku nikihema kwa kasi .
“Da ! Nimeota ndoto mbaya sana, ” nilisema.
“Ipi ?” Nilimsimulia ndoto hiyo Munil lakini kila
nilipokuwa namuweka wazi yeye alikuwa
akicheka tu mwishowe akasema:
“Baby. ”
“Naam. ”
“Kwani hujui kwamba ndoto huja baada ya
shughuli nyingi mpenzi wangu ?”
“Ndoto huja baada ya shughuli nyingi wakati
umeona mtu anataka kunichinja na sime ?”
nilimuuliza kwa kumshangaa sana. “Ni kweli ,
lakini ni ndoto tu. Kwani umewahi kuota ikawa
kweli ?” aliniuliza.
“Sijawahi . ”
“Sasa kwa nini hii unaogopa sana ?”
“Nahisi kama kweli , si unaona jasho! Tena ngoja
niamke niswali , ” nilisema lakini kabla sijaamka
Munil alinizuia akisema haina haja ya kuswali
kwa vile ile ni ndoto tu.
* * *
Alfajiri, Munil aliniamsha akiwa ametoka kuoga ,
akasema anakwenda msibani . Nilitoka
kitandani, akaniuliza kwa nini naamka ,
nikamwambia nataka kumpa pesa, akacheka
sana.
“Sasa sisi wanawake tunataka usawa kila siku,
si inatakiwa mimi nikupe pesa wewe badala ya
wewe kunipa mimi?” Wakati Munil akisema hivyo
alitumbukiza mkono kwenye mkoba wake na
kutoa noti mpya za shilingi elfu kumi,
akanitupita kitandani kisha akasema baadaye .
Sikumbuki kama nilimwona Munil akiondoka
japokuwa alifungua mlango . Ninachokumbuka ni
kwamba, akili yangu ilihamia kwenye zile pesa,
kwamba ni shilingi ngapi . Niliinua shingo
kuangalia nje kupitia dirisha ili nimwangalie
Munil anavyotoka lakini sikumwona nikashangaa
kwani asingeweza kutoka eneo hilo la nyumbani
bila kuonekana kwa kupitia dirisha . Halafu ,
ghafla nilisikia kama sauti ikiniambia …’ hivi kwa
kumbukumbu zako , Munil alivaa viatu gani ?’
Nikajiuliza hivi kweli , Munil alivaa viatu gani?
Sikupata jibu , nikachungulia chini sikuona.
Ghafla kwa nje nikasikia ko ko ko ! Munil
anaondoka sasa. Nilichungulia tena dirishani,
mlio wa viatu chini ulisikika lakini nikawa
simwoni mtu na uelekeo ukitokea nyumbani ni
mmoja tu, njia inakwenda imenyooka.
Nywele zilinisisimka, nikaa kitandani na kusema :
“Ee Mungu , kama huyu mwanamke ni jini
nijulishe , kama si jini pia nijulishe . ”
Nilipomaliza kusema , nikaulizwa na sauti
akilini . “ Hivi, hata Munil alipokuja pale baa
kukusaliamia ulimwona amevaa viatu
gani?” Moyoni nilijijibu kwamba , sijamwona Munil
akiwa amevaa viatu tangu nimemfahamu.
Je, nini kiliendelea hapo ? Usikose kusoma mwendelezo next week
 
ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Nywele zilinisisimka, nilikaa kitandani na
kusema :
“Ee Mungu , kama huyu mwanamke ni jini
nijulishe , kama si jini pia nijulishe . ”
Nilipomaliza kusema , nikaulizwa na sauti akilini .
“Hivi, hata Munil alipokuja pale baa kukusalimia
ulimuona amevaa viatu gani ?”
Moyoni nilijijibu kwamba, sijamuona Munil akiwa
amevaa viatu tangu nimemfahamu.
SASA ENDELEA …
Nilifika msibani asubuhi ya saa kumi na mbili na
nusu baada ya kaka kunipigia sana simu
kunitaka tukaungane . Macho yangu yalicheza
kumtafuta Munil . Sikuwa na mtu wa kumuuliza
zaidi ya kumtumia meseji .
“Uko wapi baby, mbona sikuoni ?” niliandika
kwenye meseji .
Meseji hiyo ilijibiwa kwa maneno haya:
“Mxwakabamshhaka . ”
Niliguna kwanza baada ya kukutana na meseji
hiyo ya ajabu . Nilijiuliza amekosea au ? Na
kama amekosea alitaka kuandika nini maana
hata pale nilipojaribu kuunganisha maneno
sikupata maana hata moja.
Nikatuma meseji nyingine ya kumwambia
kwamba amekosea kuandika , akanijibu hivi :
“Pkamahsdioaha ***- - - . ”
Niliamua kwenda pembeni ili nimpigie , simu
iliita mpaka ikakatika . Nikapiga tena ,
akapokea .
“Baby vipi ?” aliniuliza Munil . “ Mbona unakosea
kuandika meseji wewe?” nilimpelekea swali moja
kwa moja.
“Nalikosea kuandika meseji kivipi jamani?”
“Si unaandika mambo yasiyojulikana, sijui ni
maandishi gani yale!”
“Mbona nimeandika sawa. Halafu hii simu
ninayo mwaka wa kumi sasa sijawahi kuambiwa
na mtu hata siku moja kwamba nimeandika
meseji vibaya . ”
Kwanza nilishtuka kumsikia akisema simu ile
anayo kwa mwaka wa kumi kwani ni mpya
halafu si rahisi kwa msichana kama yeye akae
na simu miaka kumi, pia Munil aliniambia ana
miaka ishirini na nne , ina maana alianza
kumiliki simu akiwa na miaka kumi na nne ?
Nilitamani kumuuliza kuhusu hilo lakini kila
nilipotaka kuuliza nilijikuta nashindwa na
midomo kuwa mizito huku akili ikiniambia
wasichana wa siku hizi wanaweza , wala si ajabu .
“Ina maana mimi nimeona vibaya ? Maana
sijafuta meseji zako ujue . ”
“Umeona vibaya mume wangu , we soma vizuri
au simu yako ndiyo inachanganya herufi . ”
“Oke ngoja niangalie , nitakwambia . Uko wapi ?”
nilimuuliza mwisho, akasema yumo ndani kwenye
msiba huo .
Nilirudi na kukaa , nikafungua meseji, ya
kwanza iliandikwa:
“Nipo msibani baby, wewe je umeshafika
kwenye msiba?”
Nilishtuka sana kukutana na maneno hayo
badala ya yale ya mwanzo. Nikasoma meseji ya
pili, ilisema hivi :
“Nimekoseaje baby, mbona nimeandika sawa tu,
labda simu yako . ”
“Noo , si kweli , ” nilisema na kumshangaza kaka,
akaniuliza.
“Si kweli nini wewe ?”
“Ah ! Kuna meseji hapa imenishangaza sana . ”
“Sasa meseji ikushangaze wewe halafu kusema
useme na sisi , wewe vipi bwana?!”
“Kaka we acha tu. ”
***
Gari la kusafirishia mwili wa marehemu lilifika ,
watu tukatangaziwa kwamba, kwa vile gari hilo
ni dogo, watakwenda watu wa karibu zaidi na
marehemu. Mtangazaji akaanza kutaja majina
ya watakaosafiri .
Nilitega sikio kusikiliza jina la Munil lakini
matokeo yake nikasikia jina la kaka.
Nikamtumia meseji .
“We huendi baby?”
Akajibu : “ Nakwenda. ”
“Mbona sijasikia jina lako . ”
“Limeitwa mbona baby. ”
“Limeitwaje ?”
“Si Munil. Tena wamesema Munil Rashid Sultan
el Said . ”
Moyo ulinikatalia kwamba jina hilo halijatajwa
lakini pia nikasema moyoni kwamba, kama
lilitajwa kweli nitamuona kwenye kuingia
kwenye basi hilo la Coaster.
Watu walikunywa chai , maiti ikafuatwa
hospitalini, watu wakajipanga kwa safari.
Nilikuwa mbele sana ili nimuone Munil akiingia
kwenye basi lakini mpaka mtu wa mwisho
anapanda sikumuona .
Palepale nikamtumia meseji kumuuliza :
“Mbona sijakuona ukipanda kwenye basi baby?”
Nilisimama jirani na dirisha , nikashtuka
kuguswa kichwani . Nilipoangalia , alikuwa Munil :
“Vipi?” aliniuliza .
“Poa , sikukuona . ”
Tukaagana akaondoka zake . Dakika tano mbele
baada ya basi kuondoka , kaka akanitumia
meseji:
“Huyu dada uliyesemezana naye ni nani?”
Nikamwambia ndiyo yule aliyenipa taarifa za
msiba. Kaka akaguna tu ! Mh!
Saa sita mchana, kaka akanitumia meseji
akaniuliza hivi :
“Unakumbuka yule dada alivaa nguo gani ?”
Nikamjibu gauni jeusi . Akasema hata mimi
nilimuona hivyo lakini nashangaa hapa namuona
amevaa jekundu sijui amebadilishia wapi wakati
basi halijasimama popote ! Na mimi nikaguna tu !
***
Usiku wa siku hiyo , nilikuwa kwenye baa moja
napata bia mbili tatu kabla ya kwenda kulala .
Meseji ikaingia kwenye simu yangu, ilitoka kwa
Munil na aliiandika hivi :
“Mimi sipendi tabia yako ya kukaa baa usiku
kama huu . ”
Nilipomaliza kuisoma niliangalia kulia na kushoto
nikiamini nitamuona. Nilishtuka kwamba
amesafiri nikamuuliza :
“Umejuaje niko baa ?”
“Nimeambiwa na mtu . ”
Hapo pia nikawa na utata napo , nani amwambie
mimi niko baa wakati hakuna mtu hata mmoja
anayejua kama mimi na yeye tuna ukaribu au ni
wapenzi?“ Munil, kuna mtu anajua mimi na wewe
ni wapenzi mapema hii ?” nilimuuliza kwenye
meseji, naye akajibu hivi :





Je, nini kiliendelea hapo ? nxt week
 
hii stori yako mbona inakinzana na haieleweki mwanzo wake na mwisho wake mkuu


 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…