Nimemuonesha mke wangu wanawake wanaojiuza ili ajue thamani yake

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,648
Habari,
kumekuwa na mijadala mingi sana ya kuhusu ndoa humu ndani na wengi wakiwa wanalalamika kuhusu wake zao kuchapiwa/usaliti/mateso na changamoto mbali mbali za ndoa.

Kwa upande wangu, nimeoa mwanamke mzuri i mean kwenye kila sekta tabia sura na hata matendo na tupo kwenye ndoa mwaka wa 5 sasa lakini hatukuwahi kugombana wala kufanyiana mambo ya ajabu.

Kutokana na thread nyingi zilizokuwa zinakuja humu JF jana nikaamua kufanya yafuatayo.

Kwenye saa 7 mchana nikampigia simu mke wangu kuwa leo asipike futari badala yake tutaenda kula futari hotelini alifurahi sababu huwa namfanyia mara nyingi out za kula.

Kwenye saa 11 nikampitia na kumpeleka sehemu tukapata futari then kuna sehemu tukapitia mpaka mida ya saa 6 usiku tukiwa njiani kurudi akiwa na furaha kama kawaida yake.

Nikapita na gari mpaka Sinza X ni mitaa ambayo huwa mida hiyo kuna malaya wa kila aina tena mpaka wa elf 10, nikapaki gari kati kati yao then nikafungua vioo vyote, walivyoona gari wakaizunguka na kuanza kutaja offer yao tena mbele ya wife.

Mke wangu akabakia tu kustaajabu, mie nikaondoa gari mpaka Shekilango nikapaki gari then nikamwambia kuwa wale unaowaona pale kuna wengine ni wazuri tena kushinda wewe lakini biashara wanayoifanya mwanaume anaweza kuwa na elf 20 akamlala na hata mimi kwa kipato changu naweza kubadilisha kila siku ndani ya mwaka mzima lakini nimewaaacha wote na kuja kukuoa wewe na kukuweka ndani kama mke wangu.

Aliniangalia tu huku akitabasamu na kunikumbatia na kunambia nakupenda mme wangu na mengine yakaendelea.

Lengo la kuleta uzi huu ni kuwakumbusha wanaume au wanawake ambao wapo ndani ya ndoa kujitahidi kuonyesha kwa waume au wake zao thamani waliyonayo kwao mpaka wakachukua jukumu zito la kuacha wote na kuja kukubali kuishi nawe milele ukimuwin kwa hilo mwenzio hakika ndoa utaiona tamu

Ramadhani Kareem
 
Hapo na wewe unajiona umemuweza na unamfahamu mwanamke na ndoa?. Bado hujamfahamu mwanamke anaeitwa mwanamke. Unamfahamu mwanamke kwa upande wa mbele tu. Nasisitiza bado na huji kumfahamu mwanamke. Siku ukimfahamu utakuwa umechelewa ndio siku ya kufa
 
Back
Top Bottom