Mke wangu atasababisha nife kwa kweli...

Mke wangu atasababisha nife kwa kweli...

Sodoku

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,277
Reaction score
2,933
Toka nimemuoa huu ni mwaka wa 2 nampenda sana kiasi hata yeye anajua kuwa kwake sipumui, sihemi yaani nakuwa kama fala tu. Kiukweli nilihangaika sana kumpata nimemfukuzia kama miaka 2 hivi siku moja kama ndoto akakubali basi tukaanza uhusiano ila aliniambia nisifikirie kabisa habari za kukamuana mpaka ndoa basi nikawa mimi nauza naye sura tu. Ananipigia simu nimpeleke au nikamchukue sehem fulani siku nyingine akiwa ana kunywa na rafikize wa kike na kiume then ananiambia nikamchukue naenda bila hiyana nampeleka kwake.

Kipindi chote hicho alikuwa akinitambulisha kwa rafikize kuwa mi ni rafikiye nilimuuliza why akanambia hatujawa wachumba so hawezi niita mpenzi wakati bado, ila nilikuwa naenjoy sana kuuza naye sura maana ameumbika sana huyu dada alikuwa anaweza nipigia simu hata saa nane usiku nikamchukue klabu naenda namrudisha kwao alikuwa anapenda sana kwenda klabu na rafiki yake anaitwa Benny. Huyu jamaa alikuwa rafiki yake sana na alinambia hamna wa kuwatenganisha urafiki wao mpaka leo huwa ananiaga anaenda kumsalimia Benny.

Sasa nimemuoa yaani napata unyumba wakati mwingine kwa week mara moja tu nami sipendi kumsumbua sana maana sipendi niichoshe sehemu yake ya siri tena nikipiga moja tu anasema basi anataka kulala mi mashine inakuwa bado inataka tena but siwezi mlazimisha, hivyo nakunywa mafuta ya taa hamu inaisha nalala siku nyingine anarudi amechoka sana ananambia nimletee chakula room ale akila anajitupa kitandani basi natoa vyombo na kusafisha meza tunalala hapo hataki hata nimkumbatie na kiukweli kukumbatiana nako kuna joto sana basi namwacha mke wangu mpenzi alale.

Mimi ntakufa tu kwa mapenzi maana nampenda huyu mwanamke acha kabisa salary yangu yeye ndo huenda kutoa nlimpa kadi ya bank na password alibadilisha akaweka anayoijua yeye tu ili nisiwe natoa hela halafu naonga michepuko so huwa anatoa kkisha ananipa kiasi ya nauli kwa mwezi. ananonekana ananipenda ana wivu sana. akirudu toka kwenye mizunguko yake huwa anaoga tu na kuangalia tv mimi inabid ndo nimwandalie kila kitu kwa jinsi tunavyopendana.

kuna siku alirudi amelewa tukalala naye akawa maskini anaota anamtaja benny nikamwonea huruma jinsi ambavyo analalamika kuwa benny anamuumiza afanye polepole ikabidi nimuamshe ili asiumie zaidi nikamwambia ndo akasema huyo benny alikuwa anamkuna mgongoni hivyo alikuwa anamwambia amkune polepole. basi ndo hivyo mapenzi yangu jaman na huyu mwanamke yamfika mlima kilimanjaro...yaani tunapendana kufa.
 
aha sasa sikiza mpeleke akakae kwa beny ili kila siku asiwe anamuota af wewe uwe unaenda kumsalimia hapo itakusaidia kwa maana utakua wala hupik kila siku maana beny atakua kashampikia rafik ake sawa enhee
 
ooh wajinga ndio waliwaooo ..... wajinga ndio waliwao.
 
Back
Top Bottom