Mke wangu amepata ujauzito tena

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,497
605
Wana JF naombeni msaada hasa madaktari au wenye uelewa kuhusiana na hili.mke wangu amepata ujauzito ambao umri wake ni mwezi mmoja sasa,wakati mwaka jana mwezi wa nane alijifungua tena kwa upasuaji.mtoto wetu kwa sasa ana umri wa miezi 7.je hii mimba alioupata kwa sasa hivi haiwezi kumwathiri huyu mwanetu ambae bado ananyonya? na je kuhusu hali yake ukizingatia alijifungua kwa upasuaji haitoweza kumwathiri kiafya mama watoto.nawasilisha.
 
Mungu saidia waja wako ili wajitambue kuwa ili mwanamke apate mimba ni lazima wajamiiane, na uwafungue akili ili watambue kuwa kabla ya kuomba ushauri kama huu wangekuja kabla ili washauriwe kabla ya kuanza kujamiiana.

Ushauri mpeleke mkeo kwa madaktari bingwa wa maswala ya uzazi ili wakushauri jinsi ya kulea hiyo mimba, kwangu mimi tatizo si mimba tatizo ni huo upasuaji make sidhani kuwa hicho kidonda kitakua kimepona labda kama alifanyiwa upasuaji mdogo, wahi hospital ndugu kumnusuru mkeo na hadha nyingine.
 
Hakuna madhara yoyote yatakayojitokeza hata kama alijifungua kwa upasuaji. Hata akiendelea kunyonya pia hakuna madhara. Usumbufu tu Wa kulea ndo utapata ndugu. Wazungu kila baadae ya miezi sita huwa anabeba mimba akimaliza kuzaa ndo anaingia kwenye shuguli zake.
 
mkolosai una maana gani mkuu funguka ninamua kivip?
 
Mungu saidia waja wako ili wajitambue kuwa ili mwanamke apate mimba ni lazima wajamiiane, na uwafungue akili ili watambue kuwa kabla ya kuomba ushauri kama huu wangekuja kabla ili washauriwe kabla ya kuanza kujamiiana.

Ushauri mpeleke mkeo kwa madaktari bingwa wa maswala ya uzazi ili wakushauri jinsi ya kulea hiyo mimba, kwangu mimi tatizo si mimba tatizo ni huo upasuaji make sidhani kuwa hicho kidonda kitakua kimepona labda kama alifanyiwa upasuaji mdogo, wahi hospital ndugu kumnusuru mkeo na hadha nyingine.
Nimesoma uzi wa huyu mkuu mpaka nimesisimka kwa kweli, tena mkewe alijifungua kwa kisu walihitaji umakini mkubwa sana. Solution ni hii uliyomwambia, Mungu awasaidie sana naimagine walivyo na kipindi kigumu.
 
Kwani toka kupata balekhe yako Huyo mkeo ndio mwanamke wa kwanza kutenda tendo hilo na ndoa
Uoni hata aibu mtoto miezi 7 mimba mwezi 1 wewe mwanga nje kama huwezi lamba kondom
 
Pole sana.Nenda tu kwa dr.ukapate ushauri utakao kusaidia namna ya kulea huyo wa tumboni na wa duniani.
Mwanao analingana na wangu najaribu kuimagine nami ningeakua nna mimba sasa.
 
Kwann usimwage nje mkuu, mpaka mtoto akue hata na miaka miwili, tatizo huo mshono tumbo likiwa kubwa unaweza ukampa shida sna
 
Mtoto kunyonya muachisheni asap.

Pata daktari mzuri sababu, ni muhimu ajifungue tena kwa section, kuepuka kupatwa matatizo haswa kupasuka ndani kwa ndani na kuvuja damu. Na ifanyike wiki 2 au moja kabla ya tarehe anayotegemea mtoto kuwahi asijetoka mwenyeww. (nimeongeza tu haya)

Mtoto atakua kawaida anzeni kumpa lishe nzuri atazoea.
 
Nyege zengine mbaya mkuu.Hata mshono hajapona vizuri unakula papuchi?
Hapo umesham-bemenda mtoto na mama.
 
Suluhsho apo n kuitoa hiyo mimba kwa ajili ya kuokoa afya ya mama na huyo mtoto anaenyonya
 
Sidhan kama kuna shida ya umri wa anaekuja na aliopo. Cha muhimu hapo ni kumuona mtatibu akupea mawili matatu hasa kama alifanyiea op kubwa.
 
Aendelee tu kumnyonyesha mtoto, mimba haina madhara katika kunyonyesha lakini hakikisha anakula milo yenye afya (balanced diet). Kuna uwezekano mkubwa atajifungua kwa caesarean section tena, baada ya hapo ombeni maelekezo ya njia za uzazi wa mpango kabla hajatoka hospitali.
 
Unapiga pump bila mipango then unakuja humu kuuliza axe,hapo jifanye huna akili mzee wa kwanza anyonye zqke moaka mwingine azaliwe ulee wote halafu unakua umemaliza mchezo watakua wametosha ila kwa akili zako na mkeo mnaweza mkapata wengi kama kamat kuu ya nec
 
Back
Top Bottom