Mke wangu amejiunga na kanisa la 'kiroho' na inapelekea kutugombanisha; naomba ujanja wa kukabiliana na tatizo hili

Hilo ni balaa Ndugu yangu, hakikisha unamtoa kwenye hiyo imani mpya na arudi Lutheran. Mimi jambo hili lilimikuta mpaka nililazimika kuachana mke wangu niliyezaa naye watoto wawili.
Ilianza hivyohivyo Kama utani, aliacha kusali katoliki na kujiunga na hayo makanisa ya kilolole, akawa na ratiba za kila siku kwenda kanisani, usiku anaamka na kuanza kuomba kwa sauti, nikampiga marufuku kuomba usiku kwa sababu ulikuwa ni usumbufu mkubwa na nilikuwa nashindwa kulala, akaamia sebuleni kuendelea kuomba kila siku usiku wa saa nane na kuendelea.
Kero ilizidi na ikawa siku nyingine anasema wana mfungo na wanalala hukohuko kanisani kwao, ukimkataza kwenda kulala huko kunakuwa na ugomvi mkubwa na ndani maelewano hakuna.
Kiujumla alibadilika sana tabia yake na akawa jeuri Sana, mbaya zaidi Kama wewe mwamaume utakuwa mbali na hilo kanisa analosali utapigwa vita kutoka huko kanisani kwao.
Mimi niliambiwa kuwa amembiwa na mchungaji wake kuwa sio chaguo sahihi na MUNGU atamletea mume sahihi, nilishangaa Sana, kwa ujumla matatizo yalikuwa mengi na yote siwezi kuyaelezea hapa, ila mimi nakushauri mapema Kama unataka ndoa yenu idumu, ama na wewe uingie hilo kanisa au yeye atoke hilo kanisa na arudi Lutheran.
 
Real life example,
Pole sana Mkuu na ninashukuru kwa ushuhuda wako
 
huu ujinga hata wa kwangu kauanza siku za karibuni juzi nimetoka kumbe kawaleta home na sasa mipango mingi wanapanga wenyewe nimemwambia asinilaumu nikija kuwafukuz mlangoni
Mkuu nikadhan niko alone.
So Mpaka sasa yupo huko ?
 
Mkeo kwa hela zako unazosema unazo kaanza kuonekana wa muhimu kanisani,.. na inawezekana kapewa kacheo na watu wengi wanapenda tuvyeo hata kama twa hovyo,ndio maana na misa zimeanza kufanyika kwako na kwa cheo chake lazima ziambatane na menu la uhakika na michango mikubwa ili hadhi isishuke,...uko njiani kufilisika,..walokole hawanaga mchezo kwenye kupukutisha kiuchumi au kiakili Stay tuned......
Mkuu i am alerted already.
Nimefurahi kuona kumbe hili sio tatizo langu tu kumbe.
Natumai wapo wengi kama mimi,tunaendelea kupata la kujifunza hapa
 
Kosa ulifany mwenyewe kumruhusu mke anatakiwa awe chini ya imaya yako na akusilize kama umemkanya na hajakusikiliza tayar ashapoteza sifa ya mke bora anyway ongea nae kwa ustaraabu yeye ni binadamu atakususiliza

Nimewahi fanya kosa kama hlo nilimruhusu mchumba wangu ambae tulikuwa mbion kuoana kwenda kufanya kazi mbali na kwao.. aiseeh ndo uchumba ulivunjika hata mwezi haukuisha
 
Usipishane na mkeo kwasababu ya imani yake umesema vyema kuwa kaenda kanisa la kiroho ni vizuri kwakuwa rutherani si kanisa la kiroho binafsi sioni sababu ya kupingana naye wewe nenda pamoja naye huko utajua ukweli baada ya hapo fanya maamuzi sahihi kama hakufai ludini wote kama unabarikiwa salini wote huko. Nayo madhehebu yetu haya yapo kwaajili ya kuzikana tu hayamwandai mtu kuingia mbinguni ndio maana ukienda bar gest kanisani sura watu ni hao hao tofauti na makanisa ya kiroho wao vingine hawashiriki tulizana mkuu kweli utaifahamu
Nyie wa madhehebu ya "kiroho" NI WANAFIKI na WAPUUZI TU kama wengine. Mnanikera sana mnapojiona bora kuliko wengine.

Note: Nimesali Pentocostal Churches for 10 years
 
Pole sana mkuu,Kosa la kwanza ni kukubali yeye ajiunge na hilo kanisa.Kwa ushauri tu haya makanisa ya mitaani mengi yapo kibiashara na mmiliki ni mtu mmoja .Nakushauri mwambie afanye maamuzi either arudi kanisani kwako kama mwanzo na mlipofunga ndoa au aondoke nyumbani kwako mwenyewe na asirudi tena.

Siku zote katika ndoa ni lazima msali kanisa moja ,labda kama mlifunga ndoa ya mseto ( ie Romani na lutherani).Ila kwa manufaa ya ndoa yenu na amani nyumbani msihi sana arudi lutherani mkuu.
 
Uko sawa kabisa, hawa jamaa ni wapuuzi sana, kuna binti namjua alikuwa mshahara wake wote anapeleka kanisani na ni msomi mkubwa, mpaka kufikia kusahau kulipa kodi eti hela kapeleka kwa mchungaji... sijui wanawapa nini... mkuu piga marufuku huo ujinga...
Kuna kanisa la Kilokole niliendaga miaka ya nyuma. Mchungaji wao anataka kila mwajiriwa apeleke Pay Slip kwake ili ajue kiasi cha mshahara ili eti akuombee vizuri na ili usikwepe kutoa Fungu la Kumi.

Na kuna watu wanamfuata. Ujinga hautaisha dunia hii
 
ongea na bibie wekeaneni mikakati kila mtu asimame kwenye nafasi yake kama kuna wivu kati yenu jaribuni kujirekebisha ndani ya ndoa mtu akiishi kwa kutambua umuhimu wake mbona mambo yataenda mwambie asali sana ikibidi abadili hata na dini kabisa ila asisahau wajibu wake km mke ujue kuna watu hupenda kufanya yale mambo wanayokatazwa ili tu kuleta kero mpotezee km hujali mambo yake hadi ajistukie
 
Wakuu JF, Amani iwe nanyi

Kwanza kabisa nipende kutambua kuwa humu JF kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali kama utajipa nafasi na muda wa kufanya hivyo.

Nina kisa ambacho kimenitokea, mnaweza kunicheka but i wont mind, what i need ni njia sahihi ya namna ya ku deal na Wife.

Najua huku kuna watu wameshapitia Changamoto mbalimbali kwenye mahusiano na ndoa zao, pia wapo walio come-out na njia/suluhu sahihi ya ku deal na hizo changamoto pasi kuathiri mahusiano/ndoa zao.

Iko hivi, I married this lady about 2 years back. Ndoa ni ya Kanisa(Lutheran), kila kitu kilikuwa sawa bin sawia. Baada ya muda mwenzangu akaniambia ameanza kusali kwenye Makanisa(Madhehebu) ya Kiroho hivyo basi yeye na u-Lutheran bye bye. Nikambishia kidogo, nikaona hii italeta shida kidogo kwa mtoto wetu mmoja tuliye naye, akakomaa sana nikaona sio issue kwanza ni yeye na Mungu wake hivyo nikampa go ahead.

With time kukazuka ratiba nyingine Church kwao kuwa Jumanne na Jumatano jioni wanaenda kusali mpaka kwenye saa mbili. Nikaona this must be a step to another surprise, nikapiga marufuku. Akakomaa nikamwambia aende anakoenda kusali ila ikifika saa moja jioni awe ndani nyumba. Tukafunga topic kwa kupeana game la maana that night.

Sasa nimekuja kujua kuwa kumbe ratiba (Jumanne na Jumatano) ya mpaka saa mbili iko pale pale, kinyume na makubaliano, hususan ni pindi ninapokuwa out of home. Mimi ni Mfanyabiashara mkubwa (sio wa nganda) na most of the time nakuwaga safarini. Pia nikaja kujua kuwa activities nyingi sana za kanisani kwao zinakuwa coordinated kutoka nyumbani kwangu.

Hili Binafsi limenistua, nimefikiri namna ya ku-deal na hili suala ila naona kila njia inayokuja kichwani kwangu imebeba kama ushetani fulani. Sitaki kumkosea Mungu wangu, nikaona sio issue ngoja nijaribu kupata uzoefu kutoka JF.

So far hajanionesha utovu wowote wa nidhamu, ila kuna kagiza na hisia mbaya inakuja kichwani kwangu.

IMPORTANT

Sitaki kusikia ushauri wa kujiunga na dini yao, nimeona inawa Brainwash kwa namna fulani.

Natanguliza shukrani

Copy to Mshanajr

Mpeleke kwa mganga wa kienyeji au mwambie aende akashinde bar na casino atasahau mambo ya kanisani na Lutheran ataenda vizuri tuu,ikishindikana mpige chini sisi tunao nena kwa lugha tuchukue,maana kama haupendi mkeo awe karibu na Mungu,mwache ,ndoa ni agano juu ya mwili wake siyo roho yake,sisi tunaojua kutunza vipawa vya wanawake na kuwafanya wampende Mungu zaidi tufaidi.
 
Nyie wa madhehebu ya "kiroho" NI WANAFIKI na WAPUUZI TU kama wengine. Mnanikera sana mnapojiona bora kuliko wengine.

Note: Nimesali Pentocostal Churches for 10 years
Mimi ni mruteli mkuu niliyo zungumza ni kutokana na matendo yetu uharisia wake na mtazamo wangu kwa kuwa unafahamu madhehebu ya kiroho vizuri naamini una uwezo mkubwa wa kuamua jambo hili kwa hekima kubwa bila kuathiri ndoa yako amua kwa busara mkuu samahani pale nilipo kukwaza nisamehehe tu
 
Mkuu kwanza pooleh. Mbili simamia familia yako vizuri Biblia yenyewe imesema mwanaume ndio kichwa cha familia kama mtu ana jenga misingi ambayo haiendani na makubaliano yenu sio safi sana. Ni viuzri ukamweka chini tena uka mweleza kuwa kuna mambo ana fanya kinyume na makubaliano na mlikwisha ongelea hamna haja ya kuendelea kuwa kimya zaidi. ili atakapo shindwa kukuelewa utakapo chukuwa uamuzi mgumu awe ashajuwa tatizo lake.
 
ISSUE NINAYOIONA HAPA NI MTOTO AKIWA MDOGO KUMYUMBISHA KIIMANI SIO SAHIHI....kuhama dhehebu ni kosa kubwa la kutokuwa na imani dhabiti....ONGEA NAE TARATIBU TUMIA CHAPLAIN WENU KWA KUANZIA SIMAMIA ISSUE YA MALEZI YA MTOTO WENU KIROHO....
2.ISSUES ZA KUTOA SADAKA KWENYE CONGRATIONS MBILI ZITAWALETEA SHIDA HUTAWEZA MUAMINI HATA KUMUACHIA HELA ZA SITE NA VITU VINGINE VYA MAENDELEO.....
ONGEA NAE POLE POLE KWA BUSARA...
 
Piga marufuku tena kuwa mkali mkuu
52a36f5c7d081bda8cf10bc568d39f83.jpg
 
Mpige stop! Ila mzizi mkuu huwa wachungaji wao wanawateka sana waumin wa kike kisaikolojia hasa akijua kwako kuna kakipato fulani.
Ushaur wangu piga stop, kisha nyanyua sim pigia mchungaji wake mwambie mke wangu marufu kusali kwako na staki umshirikishe shugul za kanisa lako. Atasali lutheran ninakosali.
Itakusumbua kwa muda with time lazima uishi your life
 
Mpeleke kwa mganga wa kienyeji au mwambie aende akashinde bar na casino atasahau mambo ya kanisani na Lutheran ataenda vizuri tuu,ikishindikana mpige chini sisi tunao nena kwa lugha tuchukue,maana kama haupendi mkeo awe karibu na Mungu,mwache ,ndoa ni agano juu ya mwili wake siyo roho yake,sisi tunaojua kutunza vipawa vya wanawake na kuwafanya wampende Mungu zaidi tufaidi.
Jamaa siyo kwamba hataki mkewe aende church tatizo mke ame lowea kanisani kasahau kama ana ndoa ana mume wa kuheshimiwa hivi tuache unafiki unajidai kumpenda mungu usiye muona mtu anaacha kumpenda mmewe kisa dini?
 
Back
Top Bottom