Mke wangu amejiunga na kanisa la 'kiroho' na inapelekea kutugombanisha; naomba ujanja wa kukabiliana na tatizo hili

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
13,160
10,007
Wakuu JF, Amani iwe nanyi

Kwanza kabisa nipende kutambua kuwa humu JF kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali kama utajipa nafasi na muda wa kufanya hivyo.

Nina kisa ambacho kimenitokea, mnaweza kunicheka but i wont mind, what i need ni njia sahihi ya namna ya ku deal na Wife.

Najua huku kuna watu wameshapitia Changamoto mbalimbali kwenye mahusiano na ndoa zao, pia wapo walio come-out na njia/suluhu sahihi ya ku deal na hizo changamoto pasi kuathiri mahusiano/ndoa zao.

Iko hivi, I married this lady about 2 years back. Ndoa ni ya Kanisa(Lutheran), kila kitu kilikuwa sawa bin sawia. Baada ya muda mwenzangu akaniambia ameanza kusali kwenye Makanisa(Madhehebu) ya Kiroho hivyo basi yeye na u-Lutheran bye bye. Nikambishia kidogo, nikaona hii italeta shida kidogo kwa mtoto wetu mmoja tuliye naye, akakomaa sana nikaona sio issue kwanza ni yeye na Mungu wake hivyo nikampa go ahead.

With time kukazuka ratiba nyingine Church kwao kuwa Jumanne na Jumatano jioni wanaenda kusali mpaka kwenye saa mbili. Nikaona this must be a step to another surprise, nikapiga marufuku. Akakomaa nikamwambia aende anakoenda kusali ila ikifika saa moja jioni awe ndani nyumba. Tukafunga topic kwa kupeana game la maana that night.

Sasa nimekuja kujua kuwa kumbe ratiba (Jumanne na Jumatano) ya mpaka saa mbili iko pale pale, kinyume na makubaliano, hususan ni pindi ninapokuwa out of home. Mimi ni Mfanyabiashara mkubwa (sio wa nganda) na most of the time nakuwaga safarini. Pia nikaja kujua kuwa activities nyingi sana za kanisani kwao zinakuwa coordinated kutoka nyumbani kwangu.

Hili Binafsi limenistua, nimefikiri namna ya ku-deal na hili suala ila naona kila njia inayokuja kichwani kwangu imebeba kama ushetani fulani. Sitaki kumkosea Mungu wangu, nikaona sio issue ngoja nijaribu kupata uzoefu kutoka JF.

So far hajanionesha utovu wowote wa nidhamu, ila kuna kagiza na hisia mbaya inakuja kichwani kwangu.

IMPORTANT

Sitaki kusikia ushauri wa kujiunga na dini yao, nimeona inawa Brainwash kwa namna fulani.

Natanguliza shukrani

Copy to Mshanajr
 
Ulikosea mwanzoni kumruhusu kujoini huko, mke anapokuwa kwako hana Uhuru tena anaoutaka yeye ndio iwe hapana, kwahiyo hukutakiwa kumruhusu otherwise kama labda na wewe ungekuwa umeshift, hata kusikiliza tena itafika point ukimkataza kitu atakuambia shetani shindwa au rudi nyuma, mtoto automatically atafuata dhehebu la mama hii kiiman haiko sawa, Ushauri wangu kuwa mkali usizubaishwe na gemu hiyo ni haki yako kwa namna yoyote ile ataanza kukuambia kuna mkesha wa maombi kumrudisha itakuwa ngumu, bado mapema unaweza kumdhibiti ni hayo tu
 
mkuu simna wazazi na wakubwa huko kwenu ...!!?
jaribu " kumfikisha" kwa wakubwa wenu '" kisha uwaeleze hizo kero zako " but uwe na sababu za msingi"" zaidi ya hzi .." naimani mtapatiwa "ufumbuzi"
hawa wanawake huwa wanapigwa "brain washed mnoo""
 
1. Makanisa huweka kambi kwa muumini mwenye hela.
2. Utaanza kuona hela zinaenda kanisani kujenga nyumba za wachungaji na kununulia magari.
3. Mke wako soon ataolewa na kanisa.
4. Wachungaji watahamia kwako kukutoa mapepo.

Nini cha kufanya...
1. Piga marufuku harakati za kanisa nyumbani kwako.
2. Ongea na mkeo vizuri sana na ukishindwa shirikisha hata washauri wenu wa kindoa au wazazi.
3. Mdhibiti kwenye matumizi ya hela.
4. Kanisani ni jumapili tu kuanzia asubuhi mwisho saa 8.
5. Ongeza mtoto mkuu.
6. Kuwa mkali kweli kweli.....

Anyway yangu ni hayo
 
Pole sana kaka hapo una Mitihani mizito mno hujasimama kiume suala la program zake zinatakiwa ziishe SAA 12.Tayari awe nyumbani kulea watoto vinginevyo wote tukirudi SAA mbili nani atakua amepata kamuda kakionhea na mtoto ukiacha beki 3.

Jitahidi kusimama tu maana mwisho wa siku utakuja kulaumu wacbungaji kuwa wanapiga wife kama Yule mbasha na Gwaji .Piga marufuku utaratibu ambao haujanyooka la sivyo italeta shida hapo baadae.
 
Naamini mpaka dakika hii umeshachapiwa sana mke wako,kaka sio mara ya kwanza duniani kutokea hilo tatizo.Mimi ni muislam but nimeishi sana karibu na jamii za wakristo tena nina ndugu ambaye nimezaliwa nae tumbo moja mjomba wake upande wa baba ni NABII maeneo fulani lakini sio TITO.Nimekutana na case kama hizo sita mpaka sasa na yako wewe ni ya saba,lakini matokeo ya uchunguzi wa hizo Case ni kwamba wanawake za watu hua wagongwa huko huko kanisani.
 
Mkuu usipokuwa makini na kusimama kama mwanaume unaweza achana na mke wako sijui kwa nini sisi baadhi ya wanawake tukishaenda kwenye hayo makanisa ya manabii sijui walokole akili inabadirika kabisa hii sio ya kwanza kuisikia tena mwanamke yupo radhi kabisa kuachana na mumewe
 
Mimi wangu alianza hivyo baadaye akaanza kurudishwa na gari saa sita usiku binti wa kazi anamfungulia mlango, akija chumbani simfungulii mlango, anaenda kulala kwa watoto baadaye watoto wakaanza kulalamika kuwa mama kila akirudi anakuwa amelewa na kwenye gari huwa anakuwa na mwanaume anambusu, hapo nilimtimua haraka sana
 
Mimi wangu alianza hivyo baadaye akaanza kurudishwa na gari saa sita usiku binti wa kazi anamfungulia mlango, akija chumbani simfungulii mlango, anaenda kulala kwa watoto baadaye watoto wakaanza kulalamika kuwa mama kila akirudi anakuwa amelewa na kwenye gari huwa anakuwa na mwanaume anambusu, hapo nilimtimua haraka sana
Pole sana, inaonekana alikengeuka huyo
 
Back
Top Bottom