Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Saratani ya Ocean jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa Watanzania kusaidia watu wenye mahitaji. Akiwa hospitalini hapo, Mama Magufuli, amesema ameamua kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa hospitalini hapo kwa kutoa msaada huo kwa kuwa yeye alizaliwa katika hospitali hiyo tarehe na mwezi kama wa leo ambapo pia alipata fursa ya kuwaombea afya njema wagonjwa wote na kuwatia moyo ndugu wanaouguza kuendelea na jukumu hilo zito