mjukuum
JF-Expert Member
- Dec 8, 2014
- 5,257
- 2,850
Mwambie kwa kumanisha inawezekana unasema kama utani ndio maana ila madhara yake ni makubwa sana mwite kwa utofauti mwambie kuwa hupendi kwa kumanisha
Salam ndugu zangu.
Nina rafiki yangu ambaye yeye anaishi na kufanya kazi Singida na mimi nakaa Mwanza. Hapa Mwanza yupo mke wake ambaye naye ni mfanyakazi wa benki. Kwahiyo, rafiki yangu huja Mwanza kumsalimia mke wake na kurudi zake Singida, anapokuwa Mwanza mimi ndiye kampani yake mwanzo mwisho. Tumeanza urafiki miaka 6 iliyopita kwahivyo familia zetu zimekuwa kama ndugu tu.
Sasa basi, huyu rafiki yangu anapokuwa hayupo (akiwa Singida), mke wake hupenda sana kunitumia threads, clips au picha zinazpashiria uvunjifu wa amri mojawapo ya vitabu vitakatifu. Anapenda sana kunitumia nyakati za usiku.
Nyakati zingine hujipiga picha akiwa kitandani na kunirushia zikiwa na ukumbe "karibu tulale". Video za kugegedana anapenda sana kunitumia.
Nimemkanya sana lakini haachi, mke wangu sijamwambia na siwezi mwambia kwani wataharibu uhusiano. Anaweza kunitumia video nyingiii, mimi simjibu hata moja lakini hakati tamaa.
Naombeni ushauri nifanye nini ndugu zangu,
Asanteni