mende 2014
JF-Expert Member
- Apr 13, 2014
- 763
- 131
Ama kweli mke wa mtu ni sumu kali sana. Jamaa mmoja alikuwa anatembea na mke wa mtu kwa mda mrefu kabla mme wa mke hajagundua. Sasa baada ya mda kupita, alipata taarifa kuwa kuna jamaa anamla mke wake lakini hakuamini ila alichokifanya ni uchunguzi. Siku zikaenda, wiki zikapita lakini hatimaye siku za mwizi ziliwadia. Jamaa siku hiyo alimuona mke wake akielekea sehemu na mke hakujua kama mmewe anamuona. Mme akafuatilia taratbu na hatimaye kumuona mkewe anakutana na jamaa na kuelekea eneo la shamba la migomba. Mme aliendea kunyatia taratibu hadi wahusika walipofika ndani ya shamba hilo na kuanza manjonjo yao. Mme alinyatia na kukuta mkewe kalaliwa na huyo jamaa. Kilichotokea ni kuwa mme akateka panga alilokuwa nalo jamaa na mme kuanza kumdunda jamaa vibao. Mme alikuwa na RUNGU na akawa tena na panga la adui wake. Kilichoendelea ni kwamba jamaa alipigwa kipigo cha kufa mtu kama vile jambazi sugu. Huyo jamaa alipigwa vibaya sana hadi akawa kiwete hadi leo hii. Haya ni ya kweli maana nilishuhudia live bila kusimuliwa na mtu. Jamani, mke wa mtu ni sumu.