Mke wa mtu Sumu.

TaiJike

JF-Expert Member
Dec 14, 2011
1,483
667

Hii ni kweli imetokea ktk kijiji kimoja, Jamaa mmoja alikuwa anazini na mke wa mtu kwa muda mrefu huku wakimaliza kuku wake aliodhani wanatafunwa nap aka shume. Za mwizi ni 39 ya 40 ananaswa. Jamaa baada ya kupata habari za uhakika kuwa mkewe si mwaminifu alipanga safari ya uongo, alitoka alfajiri na kuaga kuwa anasafiri safari ambayo iliishia nje ya nyumba yake juu ya mwembe mkubwa na kujificha humo kutwa nzima huku akiangalia pilika zote za nyumbani kwake kwa kutwa nzima.

Muda ulifika mama alishatuma salamu za uhuru kwa siku hiyo kwenda kwa buzi lake kupitia shogaye, nay eye kuendelea na maandalizi kama kawaida yake akakamta kuku aliye kuwa akitaga na kumuandaa vizuri kwa wali, baada ya hapo alienda kutoa taarifa kwa shost mambo tayari hivyo mgeni akae mkao wa kula. Jamaa baada ya kuona wife ametoka naye alishuka juu ya mwembe na kuingia ndani, akakuta sinia la ubwabwa na bakuli la nyama ya kuku vimefukwa kwa kawa, alichimbua wali na kushusha kimba kubwa kisha akufunika kwa wali vizuri juu yake na kurudisha kila kitu kama alivyokikuta na kutoka kwa kuonya watoto wasiseme kwa mama yao kama jamaa alikuwepo nyumbani kisha akatokomea zake.

Mama alirudi na kubebelea mizigo mpaka kunako kituo cha madhambi yake na kukuta buzi lilikuja na rafikie, akawakaribisha msosi na kutoka nje kuendelea na stori na shosti yake. Jamaa wakajipinda kupata mpunga, mara baada ya matonge kadhaa rafiki wa mzinzi alitafuna ladha tofauti na kumeza kisha akamuuliza mzinzi mbona ladha imebadilika? Akamwabia we acha utani msosi safi kabisa huu mara naye akatafuna na kunusa harufu ya kinyesi, walivyopasua wali kuangalia kulikoni ndipo walipokuna na mzigo umetulia. Mama akaitwa ndani kwa ghadhabu na kukutana na makonde yaliyong’oa meno ya sebuleni, kisha akurudi kwake akiwa amevimba uso, na kumkuta baba mwenye nyumba akiwa kajaa tele alipoulizwa kulikoni alijibu amepata ajali ya baiskeli jamaa alimpa pole kisha, alitoka nje na kucheka peke yake akijua ametibu.
 
Hii ni kweli imetokea ktk kijiji kimoja, Jamaa mmoja alikuwa anazini na mke wa mtu kwa muda mrefu huku wakimaliza kuku wake aliodhani wanatafunwa nap aka shume. Za mwizi ni 39 ya 40 ananaswa. Jamaa baada ya kupata habari za uhakika kuwa mkewe si mwaminifu alipanga safari ya uongo, alitoka alfajiri na kuaga kuwa anasafiri safari ambayo iliishia nje ya nyumba yake juu ya mwembe mkubwa na kujificha humo kutwa nzima huku akiangalia pilika zote za nyumbani kwake kwa kutwa nzima.

Muda ulifika mama alishatuma salamu za uhuru kwa siku hiyo kwenda kwa buzi lake kupitia shogaye, nay eye kuendelea na maandalizi kama kawaida yake akakamta kuku aliye kuwa akitaga na kumuandaa vizuri kwa wali, baada ya hapo alienda kutoa taarifa kwa shost mambo tayari hivyo mgeni akae mkao wa kula. Jamaa baada ya kuona wife ametoka naye alishuka juu ya mwembe na kuingia ndani, akakuta sinia la ubwabwa na bakuli la nyama ya kuku vimefukwa kwa kawa, alichimbua wali na kushusha kimba kubwa kisha akufunika kwa wali vizuri juu yake na kurudisha kila kitu kama alivyokikuta na kutoka kwa kuonya watoto wasiseme kwa mama yao kama jamaa alikuwepo nyumbani kisha akatokomea zake.

Mama alirudi na kubebelea mizigo mpaka kunako kituo cha madhambi yake na kukuta buzi lilikuja na rafikie, akawakaribisha msosi na kutoka nje kuendelea na stori na shosti yake. Jamaa wakajipinda kupata mpunga, mara baada ya matonge kadhaa rafiki wa mzinzi alitafuna ladha tofauti na kumeza kisha akamuuliza mzinzi mbona ladha imebadilika? Akamwabia we acha utani msosi safi kabisa huu mara naye akatafuna na kunusa harufu ya kinyesi, walivyopasua wali kuangalia kulikoni ndipo walipokuna na mzigo umetulia. Mama akaitwa ndani kwa ghadhabu na kukutana na makonde yaliyong'oa meno ya sebuleni, kisha akurudi kwake akiwa amevimba uso, na kumkuta baba mwenye nyumba akiwa kajaa tele alipoulizwa kulikoni alijibu amepata ajali ya baiskeli jamaa alimpa pole kisha, alitoka nje na kucheka peke yake akijua ametibu.

jamaa mjanja,ila mi nisingemwacha hivi na talaka juu nilivyo na wivu
 
jamaa mjanja,ila mi nisingemwacha hivi na talaka juu nilivyo na wivu

Wivu wa nini we mwadhibu kimya kimya, hapo stori nimeikata ni ndefu kwani baadaye wazinzi walijua nani aliwalisha kinyesi. Mbona mi siku nivyokukuta na yule mdada nilikusubiri umalize haja zako kisha nikakushika mkono na kukuambia "Baby twenzetu home"
 
Daaaaah................Hiyo komesha jamaa kamezeshwa kimbaaaaaaaaaaaaaaaaaa kiboyaaaaaaaaaaaa....komaaaa kula kikojoleo cha mtu.
 
Japo umesema ni story ya kweli kushinda juu ya mwembe ? Ina maana pia mkewe hakumsindikiza mumewe ?

Searching...
 
Japo umesema ni story ya kweli kushinda juu ya mwembe ? Ina maana pia mkewe hakumsindikiza mumewe ?

Searching...

DJAYZZ, huyu bw. alitoka alfajiri hivyo si rahisi kwa mama kusindiza kwa mwendo mrefu sana aliishia mlangoni na kurudi ndani.
 
Back
Top Bottom