Mke wa mtu ni sumu

busy bees

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Posts
2,249
Reaction score
1,348
Kumekuwa na kauli itumikayo ktk jamii kwamba "mke wa mtu ni sumu" ikimaanisha kuwa kujihusisha "KIMAPENZI" na mke wa mtu ni HATARI sawa kama mtu "alobwia" sumu ....

SWALI: Kwani "mume wa mtu" si sumu?
 
Tumezoea kwamba mwanaume ndio anakua wa kwanza kuanzisha mjadala kwenye mambo ya mahusiano, ina maana wajue kabisa athari zinazoweza kutokea pale wanapoamua kujihusisha na wake za watu.

Mapenzi yeyote nje ya wanandoa stahiki ni sumu. Si mke wa MTU wala Mme wa MTU, wote sumu tu.
 
Mazoea ya mwanaume kuwa wa kwanza kuanzisha mahusiano iko saaaana vijijini .... but mjini huko wanawake wa "kileo" wamecharuka balaa
 
Mazoea ya mwanaume kuwa wa kwanza kuanzisha mahusiano iko saaaana vijijini .... but mjini huko wanawake wa "kileo" wamecharuka balaa

Siku hizi utandawazi umeharibu, watu wanajikuta wameshatumbukia kwenye mahaba hata bila kuja wameingiaje huko, herufi yenyewe ya jina la mwanzo haumfaham ila mmeshamaliza mambo kitambo.... simu zimechangia sana kurahisisha hili zoezi. Tuwe waangalifu kila kitu kinaanza kama masihara, inabadilika taratibu unajikuta imeshabadilika na kuwa kitu kingine.
 
Iko hivi Mwanamke hata akimfumania mumewe na mwanamke mwingine obvious reaction huwa ni ni ndogo kuliko mwanaume amfumanie Mkewe na Mwanaume mwingine Mara nyingi huwa hakuna adhabu nzuri kwa Mtu aliyefumaniwa watu wanaliwa mpaka ndogo kama kisasi wengine wanauawa hicho ndo kinasababisha mke wa mtu kuwa Sumu.
 
Kuna wanawake hatari na wenye WIVU ulopindukia kwa waume zao na hasa kama aligharamia vilivyo ama "anakunwa" ipasavyo .... hao ndg ni nooooma .... kutoa roho ya mtu ama kumuendea kwa "mzee wa busara" si ajabu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…