Samahani wadau,
Thread inautata kidogo ila mnisaidie nakwepaje hili suala.
Mie mwenyeji wa Newala, Mtwara, Tanzania.
Now niko mwaka wa pili kule utumishi Magogoni DSM.
Wakati nasoma Newala day secondary kule Mtwara mwaka wa mwisho I mean form 4, nyumbani jirani yetu alikua na matatizo.
Mume wa huyo mdada alikua anataka kuoa mke wapili ila walikua hawajakubaliana suala ambalo lilimtesa yule dada, baadae mume akaoa kinguvu so mke mkubwa akawa anakesha analia kila siku, majirani tulijaribu kukaa nae na kumsihi ahimili lile suala, ikawa ngum and kila siku ikawa anakuja home na kunisimulia mambo mengi nyuma ya panzia mie nikawa nammbembeleza tu na kumfariji kwa kupga nae story kwa charting text sms.
Nilikua namheshimu kama dada maana kanipita hata miaka 7 nadhan, na amenishuhudia hatua mbali mbali za ukuaji wangu tokea utotoni,
Shida imekuja baada ya mimi kutoka na kuanza chuo, amekuwa akinitumia sms za mapenzi hata mwishowe akasema what's wrong with her to me, akawa analia kila siku akibembeleza nimkubalie nilivyokua nikienda likizo ndo anazidi mpaka watu wakaanza kunihis vibaya.
Sasa now days ndo kanipa mtihani anasema nikirudi atanifanyia kitu mbaya kama simkubalii ku do nae atanitengenezea kesi, na huyo mumewe ni kauzu sana.
Nisaidieni nisolve vipi na nyumbani naitwa na mother naishia kumzungusha guys help me!
Please make it serious, naumia kichwa hili suala