Mke na mme mwema

Mke na mme mwema

rubii

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
14,113
Reaction score
18,744
Bwana Yesu asifiwe!

Nimeona vyema kuwapa faraja wachumba ambao leo hii wametengana! Yawezekana ndugu yangu umeachwa na mchumba wako, tuliza akili yako ni sawa tu, unaonaje?

Je ni bora akuache kwenye uchumba au kwenye ndoa? Nadhani jibu ni kwamba bora akuache kwenye uchumba.

Napenda niseme kwamba kuna kitu ambacho watu wengi wanakosea halafu inakuja kuwacost sana katika ndoa zao, kitu hicho ni KUVUMILIA WAKATI WA UCHUMBA!

Kwa kawaida ndugu yangu kama wewe hujaoa au kuolewa na unataka Bwana akupe mke/mume mwema, usijaribu kuvumilia tabia mbaya za mchumba wako!

Kama mchumba wako anapenda michepuko huku wewe hupendi michepuko, achana naye na usijaribu kumfundisha! Huwezi kumbadilisha wewe kwa sababu amekaa na wazazi kwa muda wa miaka mingi wewe uje umbadilishe mtu mzima?

Vijana wengi wanahangaika sana katika mahusiano kwa sababu ya kuvumilia tabia mbaya za wachumba wao.

Kama unaona mchumba wako ana tabia ambayo huipendi kabisa achana naye!

Napenda nikufariji wewe ambaye umekataliwa, siyo kosa lako wewe! Hiyo ndiyo hali halisi. ukubali usikubali uchumba wa kuvumiliana una athari kubwa katika maisha ya vijana wengi.

Napenda nikwambie kwamba maisha ya kuvumiliana ni katika ndoa, ukianza kumvumilia mtu wakati wa uchumba, je ikifikia wakati wa ndoa utafanyaje sasa?

Wakati huu unaweza kufikiri kwamba mchumba wako ana matatizo madogo madogo, lakini nataka niseme kwamba hayo siyo madogo, ukianza kuishi naye atayaongeza maradufu. kwa hiyo chagua mchumba ambaye anakufaa!

Mchumba mwema utamchagua mwenyewe siyo suala la Mungu. Mungu hutoa mke mwema! maana yake nini?

Namaanisha kwamba ni jukumu lako kuchagua mchumba anayekufaa na ambaye mnaelewana naye na baadaye Mungu hubadilisha mke/mume awe na sifa za kuwa mume/mke.

Kumbuka kwamba huwezi kupata mchumba mwenye sifa za kuwa mke/mme kwa sababu wakati huo anakuwa hana sifa hizo, na ndiyo maana nakwambai kwamba NI JUKUMU LAKO KUPATA MCHUMBA ALIYE MZURI na baadaye MUNGU ATAMPATIA SIFA ZA KUWA MKE/MUME MWEMA. Hauhitaji kuhangaika sana, ni masuala ya kawaida tu.
 
Huyu Mungu ana kazi sana. Imagine mtu keshajionea/keshajitafutia 'mchumba', wameshatiana nje ndani, then ndio anapiga magoti kumuomba 'mungu' amfunulie.

Nami nawapa pole waliomwagwa, ndio maisha!
 
Ujumbe mzuri sana huu. hakuna kitu kibaya kama kuvumilia tabia mbaya ya mtu kisa ni mchumba. Ila wengi wanafanya kuvumilia kwa kuogopa watu watawaonaje kuachana wakati tayari wachumba
 
Ngoja nikaufanyie kazi!
 
Nimekuelewa sana aisee na nimejifunza kitu
 
Acha porojo,Mume mwema ni yule mwenye kipato cha kutosha kutunza familia siku hizi...Mke mwema ni mwenye uwezo wa kumuheshimu mwanaume huyo kipindi ana fedha za kutosha za kumtunza yeye na watoto...Vice versa is true!
Acha maneno mingi tunaelewa dunia ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom