MKE MWENYE AJIRA v/s MAMA WA NYUMBANI

alexmahone

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
482
405
Najaribu kuzitazama nyumba hizi mbili ya Enginia Jerome ambaye mke wake ameajiriwa halmashauri kama mgavi na Enginia Shaban ambaye mke wake ni mama wa nyumbani..
Mrs Jerome akiondoka sa moja nyumban muda wa kurudi ni sa moja au mbili usiku.Hii ratiba inabadika jumapili ambapo huenda kazini sa nne na kurudi sa tisa.Kazi za nyumbani zote ikiwa ni pamoja na maandalizi ya mtoto kwa ajili ya kwenda shule hufanywa na Yaya.
Mrs Shabani ana mapacha wawili,huamka asubuhi na kuwaandaa watoto wake pamoja na baba yao.Kisha huwapeleka shule na kurudi nyumbani kwa maandalizi ya mlo wa mchana.Mara nyingi bwn shaban hurudi nyumban kupata mlo wa mchana na kurudi tena kazini lakini bwan Jerome kamwe harudi mchana yeye hula hotelini.
Haya ni baadhi ya niliyoyasema,je we una lipi..?
 
Kikubwa ni kila mtu kuwa na upendo na mwenzake na kutimiza wajibu wake!
 
Ninavyoona mimi hiyo familia ya Engr Shaban itakuwa yenye maadili na maisha bora, mama yuko fultime nyumbani anaangalia watoto wake na bwana pia anatoa good time yake nyumbani.

Ukija kwa Engr Jarome, japokuwa maisha magumu lazima tuwe saa nyingine tunaridhika na kidogo tunachopata kwa ajili ya kujenga familia bora. Kazi ambayo inachukua muda mrefu na mwingi wa mama si nzuri, nikimaanisha mama ndio mlezi wa jamii na muda wa kukaa na watoto utakuwa mchache sana.

Kwahiyo hasa wanaume waweke balance katika maisha, mambo ya sharing 50/50 lazima yatoweke, mmoja wapo awe ni bread winner mwengine ni mlezi. Kama anaulazimu wa kufanya kazi, zipo kazi ambazo hazichukui siku nzima na atakuwa na muda wa kurudi nyumbani mapema kujua mambo ya kifamilia.

Lakini simlaumu huyu dada, wengine hutafuta kazi ili kiwe kisingizio cha kutokaa nyumbani muda mrefu labda mume mwenyewe time yako yote anamalizia na barmaid au kunyanyaswa, yes kuna wanaume wanyanyasaji ukiwa goalkeeper.
 
kiuwajibkaji w kazi za nyumbani mama shabaan yuko juu ila sasa tusisahau kwamba maisha yana kesho takuwaje kesho yake???

Nahisi mama shabani atachoka mapema lasivyo watafute mfanyakazi kupunguza mzigo kwake! Kinyume na hapo ana weza kukomaa mapema na kuchakaa!

Napengine mzee shabani ana rudi kula nyumbani sababu chakula kina pikwa vizuri lakini siku itafika atachoka kwa kazi na mapishi pengine yaka badilika na ndio hapo baba shaban ataanza kusema leo sitakuja kula, hapo ndio mtanange utaanza.
 
Kwa kweli hiyo ni challenge kwa wanawake ambao tuna kazi.. Na inawezekana nikawa natoka kazini mapema mfano saa kumi na moja lakini mpaka nifike home inakuwa tayari saa moja au mbili maana folen hasa kwa tunaoishi Dar! Kinachotakiwa hapo tuu ni maelewano baina ya wawili hao! Muda mchache utakaopatikana inabidi mwanamke autumie kwa ajili ya kuwa na familia yake ipasavyo...

Ndio maisha hayo, mimi nimehangaika na shule leo hii ukiniambia niache kazi niwe mama wa nyumbani siwezi kukuelewa hata kidogo.. Pia kwa kufanya kwangu kazi kuna faida za kimaendeleo ninazochangia kwenye maendeleo ya familia yangu.
 
Kwa kweli hiyo ni challenge kwa wanawake ambao tuna kazi.. Na inawezekana nikawa natoka kazini mapema mfano saa kumi na moja lakini mpaka nifike home inakuwa tayari saa moja au mbili maana folen hasa kwa tunaoishi Dar! Kinachotakiwa hapo tuu ni maelewano baina ya wawili hao! Muda mchache utakaopatikana inabidi mwanamke autumie kwa ajili ya kuwa na familia yake ipasavyo...

Ndio maisha hayo, mimi nimehangaika na shule leo hii ukiniambia niache kazi niwe mama wa nyumbani siwezi kukuelewa hata kidogo.. Pia kwa kufanya kwangu kazi kuna faida za kimaendeleo ninazochangia kwenye maendeleo ya familia yangu.

Tafuta housegirl akusaidie!
 
kuna wamama wengine chapombe kutwa kucha kiguu na njia, hivo kuwa mama wa nyumbani sio tija sana..unaeza kuwa na mama mfanyakazi bado akawa na familia bora kuliko mama wa nyumbani mvivu na mzembe. maisha hayanaga formula kwamba ukiingiza coefficients basi unapata jibu 100/100..#hamnagakitukamahicho.
 
Na kingine mama wa nyumbani wengi wanapoteza mvuto mapema ukilinganisha na wafanya kazi...wengi kushinda na kanga 24/7 hawaoni shida. Kuoga mara moja kwa siku etc...Si wote lakini wapo wanaojiweka soap soap.
 
Kila kitu kina faida na hasara zake..muhimu ni jinsi ya kuminize hizo risks!.
 
I will go for eng. Shabani's family kwa kweli. Kuwin bread ni vizuri ila tusisahau kwamba na nyanja zingine za ulezi ni muhimu pia. Habari za mtoto kukua without close relationship ya hata upande mmoja wa wazazi ni mbaya sana- It better usizae kama huna uwezo wa kakuaa na mwanao...
 
I will go for eng. Shabani's family kwa kweli. Kuwin bread ni vizuri ila tusisahau kwamba na nyanja zingine za ulezi ni muhimu pia. Habari za mtoto kukua without close relationship ya hata upande mmoja wa wazazi ni mbaya sana- Its better usizae kama huna uwezo wa kakuaa na mwanao...
 
Na kingine mama wa nyumbani wengi wanapoteza mvuto mapema ukilinganisha na wafanya kazi...wengi kushinda na kanga 24/7 hawaoni shida. Kuoga mara moja kwa siku etc...Si wote lakini wapo wanaojiweka soap soap.

Hilo ni kweli kabisa NK wanaoshinda nyumbani hujisahau kabisa na kuwa nyeng'e nyeng'e, hawajijali kabisa muonekano wao huwa wapo wapo tu. Unaweza kudhani ni msaidizi wa ndani kumbe ndio mama mwenye nyumba!!! Halafu kujitetea kwao ni kwamba wanakuwa busy na kazi za nyumbani!!! hivyo kukosa muda wa kujipiga soap soap, kitu ambacho hakina ukweli wowote.
 
mama wa nyumbani tukiangalia kwa mtazamo wa saivi utaona ni bora kwa kuwa analea familia ila ikitokea mume amefariki na familia inamuangalia yeye ndo ugum unapoanza. kufanya kazi ni vizur pia ni ni vigumu kupata muda mzuri kwa ajir ya familia yako.
 
Back
Top Bottom