My dear yaani huwezi kuamini hizi tuu nilitoka Ku discuss hii issue kibiblia na Pastor Fulani. Katika kuongea na yeye na kuchambua vizuri neno la Mungu .Watu wengi sana huwa tunatafakari neno la Mungu vibaya. Sisemi hivi eti mlioolewa muanze kuabuse ndoa zenu hapana . Kitu ninachotaka kusema ni kuwa Mungu hakuaahidi kuwa hatutapitia majaribuni, la hasha. Ila alitiuahidi ni kuwa na furaha ya milele kwa wale wamtegemeao. Honestly biblia au Quaraan haikusema kuwa ukae na mateso kwenye ndoa yako. Nimetaja Biblia na,Quraan kwa sababu ya nilikuwa Muislam so naelewa na now Niko mkristo naelewa pia ingawaje Bado najifunza , okay.
Neno la Mungu siku zote linazungumzia kuishi maisha ya furaha ya ndoa. Na hii ni kwa sababu Mungu aliiweka ndoa kuwa kitu takatifu na faraja kubwa kwetu sisi . Katika ups and downs za ndoa Hakuna neno au mstari unasema kuwa kwenda kusaliti ndoa yako ni sawa, au kumpiga mkeo au mumeo ni sawa . Kuvumilana katika ndoa mpaka kifo kitutenganishe ni kwenye shida na Raha. Hii ina maanisha kwenye maradhi mmoja wapo anaumwa umuuguze na kumvumilia. Na kwenye ki financial imetokea mmoja wapo ameanguka , mvumiliane kwa hilo.Na mambo mengine , plus ya kiundani zaidi.
Utakuta MTU anapigwa kila siku kan ngoma, na kuteswa kihisia , kuletewa mpaka wanawake au wanaume na ameshaongea na mwenzie kuhusu Haya majanga lakini Bado mwenzie anaendelea. Badala ya kusingizia ooh ni Ndoa mpaka kifo kikutenganishe, no no no. Wewe ni Mtoto Wa Mungu hebu piga goti chini mueleze Baba yako aliye juu, akuonyeshe mlango Wa kutokea ili utoke . Hebu jiulize kwa wale waliokaa na hayo na maumivu wako wapi Leo hii, kama si waathirika Wa Ukimwi , au kama hawajauliwa , na kadhalika. Mungu na yeye anataka sisi maamuzi kwa Imani haswa pale baada ya kumuomba . Tumekuwa tunajibweteka kwa kila kitu na kusingizia Mungu amependa iwe hivi No hiyo si sahihi kama alipenda kwa nini alikupa uwezo ubongo au uwezo Wa kufikiri. Mungu hapendi tuteseke especially kama tuwaaminifu kwake. Kuna matatizo mengine tinajitakia wenyewe halafu tunamsingizia Mungu . Kumbuka hata Yesu alifundisha , na baada ya hapo alisema mwenye masikio na asikie. Alifundisha si kwa hukumu bali kwa authority . Sisemi usifuate maandiko tafadhali usinichukulie, hivyo . Jua maandiko na kuyatafakari kwa undani zaidi . Hakuna kwenye Biblia inasema uwe na MTU mzinzi au anayekufanya ngoma kila siku. Na tunafikiri IPO jiulize kwa nini Yesu alikuwa anazungumzia kuhusu hukumu za wale wanaoweka Uzinzi mbele, na wale wayafanyao kinyume cha maandiko. Kwa Kweli tuwaombee tuu Wanaopitia Haya kwa kuwa wengi wao wana woga na kuona aibu kutoka katika hali kama hizi. Mungu atusaidie. Mtoa maada Mimi nimekulewa na Asante kwa maada hii ya kutukumbusha . Thanks.