Nivea,
kama umeichki kwa makini nimeeleza tulioanzia hadi tunakokwenda tokea
mwanadamu wa kale. na kwanini kazi imekuja kuchukua muda wa malezi.
Nikuhakikishie, ukiishi maisha ya kuajiriwa pekee bila kufanya kitu
kingine pembeni utaishia tu kuwa na hela ya kubadilisha mboga hadi mtu
unazeeka na ka pensheni. idara nilyoko naona watu na vitambi vyao
wanavyokuja kulilia mikopo ya ada na kodi ya nyumba pamoja na kulipwa
mishahara mikubwa. so mshahara sio mkombozi bado bali naona kujiajiri
mwenyewe inalipa na mtu unakuwa huru sana na muda na vitu vingine.
point yangu ni hii, kama shida ya kuajiriwa ni kutafuta pesa, ni bora
mkapanga projects za nyumbani ambazo mke atasimamia na nyingine mme au
wote kwa pamoja. unaweza kufikiri iko ki-theory zaidi, lakini those who
believe on them selves wamefika and i have some few role models.
Bro wetu mmoja (alikuwa ameajiriwa) akalima eka 30 ya mpunga hapo
morogoro, Mungu saidia akapata milioni zake kadhaa almost 200% faida kwa
kila hekta. amefungua miradi yake, kaweka wafanyakazi na mke wake ndiye
anaendesha mradi mmoja wapo tena kwa mafanikio sana. Mkewe alikuwa mtu
wa masoko kabenk kamoja hapa mjini lakini aliacha kazi mwenyewe kuja
kumpa nguvu mumewe, na sasa wameajiri watu zadi ya 10 (kwenye pesa
points nazozijua bado wana miradi mingine) mke sasa hayupo confined na
mastress ya kuajiriwa na anaweza panga mambo yake ya familia kwa uhuru
zaidi so these things vipo kwa wachache wanaotaka kuwa hivyo.
Najua ni changamoto kubwa kwa kizazi cha leo, kwa binafsi yangu nachukia
kuajiriwa lakini kwa sasa niko kwa ajira strategically (napenda kuwa
huru) na naamini nikiweka juhudi naweza kufanya kile ninachokitamani na
kukipanga.