Nyleptha
Member
- Jun 19, 2012
- 69
- 47
Habari wadau? Natumaini mna enjoy weekend yenu vizuri.
Kwa muda mrefu sana ninatafakari nafasi yangu kama mama katika familia, naona umuhimu wa mama kuwepo nyumbani muda mwingi ili kuangalia mambo yanavyokwenda hapo nyumbani yahusuyo afya ya watoto, mume, chakula, usafi wa nyumba n.k na nimeshuhudia familia nyingi ambazo mama anakuwepo muda mrefu zina maendeleo mazuri tu, ni mara chache kukuta watoto watukutu au wenye tabia za hovyo hovyo kwani mama anasimamia vema nidhamu ya familia. Japo zipo pia familia CHACHE hata mama ashinde masaa 24 mambo bado yatakuwa hovyo!
Sasa basi huu utandawazi umetushika pabaya wanawake, na sisi tunataka kutumia elimu zetu kwa kuajiriwa maofisini, binafsi naona hakuna ubaya hapo kwani ni kuongeza kipato kwa familia. Kinachonitatiza ni pale ambapo majukumu haya mawili yanapoingiliana na kuharibu mfumo mzima wa maisha. Mfano hai: Mimi ni mama na pia nimeajiriwa, najikuta niko njia panda wakati huu ambapo nina watoto wananihitaji nyumbani kuangalia maendeleo yao na mume pia angependa kuhudumiwa na mkewe na kufanyiwa mengine mengi badala ya kuajiri housegirl, na kazini ndio hivyo tena kuanzia asubuhi hadi jioni kama sio usiku, unaondoka watoto wamelala unarudi wamelala! Familia unaipenda na kazi unaitaka, hapo unajigawaje? Kuna mambo mengi sana yanatokea nyumbani tunapowaacha watoto wetu na housegirl kwani hawana uwezo wa ku-handle mambo hayo kama ambavyo mama angefanya.
Wenye situation kama hii plz tupeane mawazo, mnakabiliana vipi na majukumu haya yote mawili? hata wanaume pia mko katika msimamo upi, unataka mkeo aende kazini na kuacha nyumba mikononi mwa housegirl au abaki akusubiri ulete kila kitu (bila kumnyanyasa!).
NB: Najua wapo watakaozungumzia kujiajiri lakini huko nako pia nina mengine mengi ya kueleza.