Case nyingine jamani khaa....Ukataji wa msumeno ni kwa kupeleka mbele na nyuma, kwa hiyo mtu katega paja na kukatwa!
Anyways, sina uhakika kama kuna haki ya mtu mmoja kumuumiza mwingine, regardless ya kosa, awe mwanaume au mwanamke. Kwa sababu tu case iliyopo mbele yetu ni ya mke na mume, je angekatwa na mtu tofauti na mumewe angepeleka kesi polisi? kama ndio, basi bado haki yake itabaki pale pale. Tatizo tu ni kwamba mambo ya upendo yana vizungumkuti vyake, wape wiki mbili tatu mambo yapoe utakutana nao barabarani wameshikana mikono. Na bibie akimsimulia mumewe kuwa vizabinazabina ndio walimsukuma ampeleke polisi, lakini yeye akhuuu....wala hakutaka!