Mke arudi nyumbani kwake ,watengana vyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke arudi nyumbani kwake ,watengana vyumba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 7, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MWANAMKE aliyekutwa na aibu ya kumfumania mume wake na msichana wa kazi, amejikuta akirudi nyumbani kwake baada ya kupata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali lakini amejitenga na mume wake huyo kwa sasa
  Mwanamke huyo alirudi nyumbani kwake juzi, majira ya jioni baada ya wazazi na washauri mbalimbali kumtaka arudi nyumbani kwake kwa kuwa huenda mume wake huyo alikuwa amepitiwa na shetani.

  Hata hivyo imedaiwa kuwa, kwa kuwa alikuwa akiwaheshimu sana wazazi wake na alionekana kuonekana mkaidi mbele ya wazazi wake hao alikubali kwa shingo upande na aliwaeleza kuwa endapo hali hiyo itajitokeza tena atavunja maandiko matakatifu yanayosema ndoa ikifungwa haivunjiki na kudai yaye ataivunja endapo hali hiyo itajitokeza na hatakwenda kushitaki kanisani walipofungia ndoa hiyo.

  Hivyo imedaiwa mwanamke huyo, alirudi nyumbani hapo kwa sharti moja alilompa mume wake huyo kuwa watengane vyumba.

  Hivyo hali inaonekana kuwa ngumu kwa mume huyo na kumtaka mke wake huyo amsamehe moja kwa moja kwani asingeweza kurudia tena uchafu huo.

  Chanzo cha habari hii, kilidai kuwa mwanaume huyo aliendelea kuomba suluhu na kutinga ukweni kuomba msamaha na kuelezea anachokihitaji mkew ake huyo na wazazi hao kuahidi watakutana kumaliza mgogoro huo wa wanandoa hao.

  Hata hivyo mwanamke huyo alidai kuwa kwa sasa hatakubali kuishi chumba kimoja na mume huyo labda hadi wapime afya na atarudi katika hali ya awali kwa kumpa masharti magumu mumewe huyo.
   
 2. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hivi huu mfumo dume utaisha lini????!!!!! Ingekuwa mwanamke ndio amefumaniwa huyo mwanamme angemsamehe mkewe??? Ebu sikiliza wimbo huu.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. p

  pierre JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Masharti magumu hayasaidii,kinachotakiwa ni huyo mume awe tayari kubadli mawazo maana atayatimiza masharti yote wakati anaendelea na kamchezo kake.Kwanza huyu mama atafute chanzo cha kwa nini atembee na housegirl,nini cha mni anachopata kwake anakosa ndio mambo mengine yaendelee
   
Loading...