Mke anaomba talaka baada ya kujua mmewe kamjengea shemej yake kisirisiri

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,555
99,409
Nna rafiki yangu wa miaka mingi Ni ustadhi yule swala 5 pure. Yeye hujishughulisha na uwakala wa miamala ya Simu na kibenki. Mara nyingi miamala yangu ya Simu na kibenki huwa nafanyia kwake. Ana matawi kadhaa Hapa dar na mengine morogoro mjini

Huyu ustadhi Tunaaminiana Sana Kias kwamba hata password yangu ya baadhi ya card zangu za kibenki huwa anazijua nami zake nazijua kitu ambacho hata MKE wangu wa ndoa au mzazi wangu huwa hajui. Mana Kuna MDA huwa anatumia account zangu kupitishia fedha zake. Nami sometimes hufanya hivo hivo kwa account zake kutokana na mazingira kadha wa kadha ya kiuchumi na tusaidiana sana kifedha Hapa na pale.

Hivi karibun karibun kanishirikisha Jambo lake khs familia yake nami kwa heshima ya hii jf nikaona Bora nililete huku tunaweza saidia kupata mwafaka.

Nna iman kubwa sana na jf ktk USHAUR bora wa kuinusuru ndoa na familia yake iliyoko mbioni kuparanganyika baada ya mkewe kujua ustadh kamjengea shemej yake nyumba kisirisiri.
 
Ni hivi
Ustadh amezaliwa ktk familia ya watoto wawili, baba na mama Yao wote walishafariki. Yeye Yuko dar,mdg wake Yuko mkoani anaishi na ndugu zao kwa kuunga unga Hana kazi ya kueleweka.

Sasa Miaka 7 iyopita baada ya ustadhi kuoa alimchukua huyo mdg wake wa kiume kutoka mkoan aje dar wasaidizane Kupiga KAZI za miamala ili maisha yaweze kusonga. Akampa chumba Cha uani awe anaishi humo.

Kama ujuavyo mambo ya vijana
Mdg wake huyo akaanza maswala ya wanawake, Kuna binti akawa na mahusiano nae akawa akipata nafas anamleta kwenye hicho chumba Chake cha uani Wanafanya ya kufanya kisha binti anaondoka kwenda kwao.

Siku ya siku
Binti kamletea taarifa kijana kua ni mjamzito, kijana akajaribu kumbadilikia binti ili akaitoe mimba hajajipanga bado kimaisha na pale anaishi kwa Kaka ake,hili litakua balaa.Binti kagoma kuitoa.
Zaid Zaid binti akaenda kwao akabeba mabegi yake na kuamia jumla kwenye kichumba Cha kijana. Kijana akamfukuza, binti kang'ang'ania hatoki chumban anataka kuolewa.

Binti alipoulizwa kwann anang'ang'ania kuolewa akasema kafukuzwa na Bibi yake Hana pa kwenda Maana Ni yatima wote baba na mama walishafariki akiwa mchanga hata sura zao hazijui.
Kwaiyo Hata kwa upanga shingoni aondoki pale anachotaka Ni kuolewa TU.

Sasa hizo Taarifa zilipomfikia ustadh,
Akasema hata msimbugudhi uyo binti,
Kupata mtoto ni jambo la heri na pia kijana kuoa Ni Jambo la heri sana.
Kijana na binti waozeshwe haraka Sana. Baada ya ndoa kijana na mkewe wakaendelea kukaa pale mpk binti alipojifungua na akahudumiwa mke was ustadh mpk kupona kabisa.
 
Mambo kiuchumi yalivoenda vizur,
ustadh akapata pesa akafungua tawi jingine morogoro mjini. Ikabd huyo mdg wake ndo akasimamie Lile tawi na akampangia nyumba nzima na kuwahamishia uko mdg wake na huyo mkewe.

Mdogo wake na mkewe wakaishi vizur Sana, ilipofika 2017 wakaongeza mtoto mwingine. Hawakukawia Sana 2019 tena wakaongeza mapacha wawili. Jumla wakawa na watoto wanne. Yaani wa miaka 6, wa miaka 5 na mapacha wa miaka 3.

Sasa kwa bahat mbaya
Miez miwili baada ya uyo mkewe kujifungua mapacha bwana mdg alipata alipata ajali ya Basi akafariki akitokea kwao dodoma kusalimia.

Baada ya bwana mdg kufariki,
Ustadh akachukua jukumu la kuitunza ile familia yake uko Moro anawatumia pesa ya kuishi Kila Mara maana MKE wa Dogo alikua Ni mama wa nyumbani.
Na pale kwenye ofisi akatafta mtu mwngn akamuweka. Hawakukaa Sana ile ofisi ikalega lega ikawa inapigwa matukio mfulurizo ya utapeli na ujambazi ikabd ustadhi kuifunga maana Ni Kama mtaji unapotea bure.

Baada ya uchumi kuyumba Sana kipind Cha korona, ustadh akaona Ni changamoto Sana kulipa Kodi,kulipa Ada na huduma mbali mbali za familia sehemu mbili tofauti tofauti na amepanga nyumba kubwa Sana vvyumba vingine hata havitumiki.

Wakashauriana na mkewe kua MKE na watoto wa bwana mdg warudi dar wakae nae watakula hicho hicho kdg kinachopatikana ukzingtia Kuhudumia daily familia ya MKE na watoto 4, wawili mapacha wa Miezi 2 wakiwa kulekule Ni gharama na changamoto Sana.

Sasa baada ya MKE wa Dogo kuhamia dar, mke wa ustadh akiwa mjamzito ikaanza misuguano ndani ya nyumba dhidi ya Hawa wanawake wawili. Ikabd awakalishe chini kutatua migogoro yao Kisha taratibu za kufua,kupika na mapishi watakua wakiwekeana zamu wao kwa wao na yeye kama baba wa familia ataacha kila siku pesa ya pamoja kutekeleza Hilo. Ila msimamizi mkuu wa pesa zote za familia Ni MKE wa ustadh.
Ikawa imeisha hivyo.

Hawakukaa Sana,
Misuguano ikarudi upya chanzo Ni wakitofautiana tu MKE wa ustadh mjamzito ananuna anamnyima hadi pesa za mahitaji binafsi MKE wa dogo na kumpangia ratiba ngumu za majukumu pale nyumbani maana yeye ndo kakabidhiwa rungu la ukuu wa Kaya pale nyumbani ustadhi akienda kwenye utafutaji.
 
Ustadh akaona Hii haifai,
hawa Watu hawaivi chungu kimoja.
Akaamua kuwaachia kila mmoja na pesa ya familia yake. Yaan akiondoka asubuh anaacha pesa kwa mke wake na pesa nyingine kwa MKE wa Dogo.
Hali ikawa Kama vile imetengamaa kwan miez kadhaa kila mmoja anaishi na familia yake kwa utulivu Sana mpk MKE wa ustadh kajifungua salama.

Sasa timbwili jingine likahamia kwa ustadhi, kila wakiwa na migogoro kdg na mkewe hampikiwi,hapakuliwi chakula Wala hamfuliwi nguo.
Anawez akitoka kazin usiku akifika nyumbn mkewe kanuna hajapika chochote, atamwita MKE wa Dogo na kumwomba Kama Kuna chochote apakuliwe ale.

Na MKE wa Dogo bila hiyana atampakulia, atamnawisha na kusubiri amalize kula Kisha kuondoa vyombo kupeleka jikoni Kisha ustadh ataingia chumban kwake kulala. Mkewe bado kanuna anapika Cha watoto wake TU.

Sasa Hali ile ilivoendelea ustadh nae akaacha kumsemesha mkewe, akifika jion utaratibu Ni ule ule. MKE wa Dogo anapakua chakula,anamnawisha, anakula, story mbili tatu, vyombo vinaondolewa. Kisha Ustadh anaingia chumban kwake analala.

Nguo sometimes akisusa anampa shemej yake anafua na kunyoosha Kisha kumkabidhi zikiwa Safi kabisa.

Ghafla mkewe akaanza kumtuhumu kua ustadh anatembea na shemej yake. Ustadh alivyokuja kuomba USHAUR tukamshaur amuondoe MKE wa mdg wake pale. Hawa Watu wakishaanza kutuhumiana mambo kama haya hawachelewi kuwekeana sumu kwny vyakula wakauana.
 
Ustadh akatwambia kule moro Kuna pagale la marehemu mdg wake liliishia kwny lenta, labda afanye kulimalizia haraka Kisha MKE wa Dogo arudishwe morogoro na atafutiwe na mtaji. Tukasema "utakua umefanya vizur"

Basi ustadh hakukawia Sana,
Akakopa hapa na pale Akaanza kumalizia kozi za juu, funika paa,madirisha na milango
Kisha ndani ya mwezi mmoja tu bila hata sakafu chini akamtoa pale MKE wa Dogo na watoto wake na kumrudisha morogoro na kufufua Tena ile ofisi ya miamala akampa MKE wa Dogo ndo aiendeshe aweze kujikimu.


Sasa kwasababu
Ile ofisi bado Ni changa akawa kila Mara anaenda Moro kufuatilia uendeshaji wake uku akimalizia ujenzi ule kidg kdg. Muda ukimtupa sana mkono basi atatafuta lodge uko uko Moro atalala kisha atarudi kesho yake dar.

Na kwasababu yeye na mkewe hawakua na mawasiliano mazur (kisirani MDA wote kanuna).
hivyo michakato yote ya kujenga, kufufua ofisi ya miamala na kumhamishia MKE wa dogo moro hakumshirikisha kabisa mkewe maana mpk MKE wa Dogo anaondolewa pale ulkua Ni ugomvi mkubwa hawasemeshani na hakuuliza kabisa Ni wapi anapelekwa.
 
Sasa timbwili limeibuka upya,
Ustadh Yuko Moro saiti anasimamia ufungaji wa umeme kwenye ile nyumba, mkewe kainuka ghafla na kufanya vurugu kubwa akidai ustadh kamjengea MKE wa mdg wake kwa sababu Ni hawara yake.

MKE wa ustadh anadai talaka aondoke zake kwao anadai kwann ustadh amjengee shemej yake spidi spidi wkt wao wanaishi nyumba ya kupanga miaka Zaid ya 8 Sasa na Hawana hata kiwanja.

Anadai Kuna nn kinaendelea Hapa Kama yule sio hawara yake na siku zote kumbe ustadh asizolala kwake kumbe huwa anakuja kulala Moro kwa shemej yake.

Wakuu,
Ustadh anasema Hii kesi imeenda Hadi mskitini wameshindwa kuitatua.
Ustadh anadai mkewe bado ana mpenda na Hana mahusiano yoyote na shemej yake huyo.

Haya majukumu yote aliyoyabeba Ni kwasababu ya kupambana kuisitiri familia ya marehemu mdg wake Mana MKE na watoto wale Hawana ndugu mwngn watamkimbilia Zaid yake yeye.

Ila matokeo yake mkewe anawazia mambo mengine tofauti kabisa.

Nmejaribu kumfata shemej yangu nimuweke sawa, Ni mkali Kama pilipili haskilizi la mtu anasema Mimi na mumewe wote Ni wale wale TU.

Nmejaribu kumhoji ustadhi kiume zaidi labda kuna siku Aliwahi kumla shemej yake kimasihara hata kwa bahat mbaya ustadh kakataa kata kata na kuapia jina la mungu wake.

Nikiangalia kiukweli ustadh naweza kubaliana nae mana Sijawai mskia na mambo ya Michepuko hata kwa bahat mbaya. Yeye Ratiba yake Ni kazini, mskitini na nyumbani kwake TU.Hana kabisa mambo ya wanawake.

Ustadh anadai Mkewe kaenda mbali zaidi hadi kwny mahakama za kiraia anadai wagawane Mali ,gari mbili na bajaji za ustazi viuzwe wagawane na ile nyumba alojenga anadai iuzwe nayo wagawane.

Hebu tunaliwekaje wakuu tumshaur vema ustadh maana Inaonekana baada ya mkewe Kuidai talaka kawa Kama vile kachanganyikiwa.
Nmemwambia subir tukitoka kazn mapema au kesho asbh nikatulia kichwa ntakuchek nikushaur vema zaid ndugu yangu. Kasema "sawa"

Binafs,
Ushaur wangu Ulikua wa kumwambia ustadh asihangaike Tena kumbembeleza na kumpigia magoti mkewemaana ndo anazid kumpa bichwa.
Ampuuze TU, ndoa huwa haibembelezwi
Maana Anachomtuhumu mmewe hakina hata mantiki maana Hana ushahidi wowote kwamba anatembea na shemeji yake.

Nmemwambia shemej yangu (mama ustadh) kua Kama kamchoka ustadh wa Watu anyooshe maelezo na sio anamtaftia TU vijisababu vsivyo na msingi anamfrustrate tu kichwa chake.
Madai yake hayana msingi wowote ule

NAWASILISHA
 
Nilivyosoma heading nikajua mdogo wa mke wake ndio kajengewa nyumba hapo ningekuwa upande wa wife.
Back to story ushauri wako nauumga mkono 100% asiendelee kumbembeleza, mwanamke anakuwa na roho gani kwa mwenzie aliye mjane wa watoto 4???

Hiyo nyumba mumewe kaimalizia hakujenga yote kama anavyocompare wao hawana hata kiwanja, mume wa mdogo wake ndio kajenga. Kiufupi ustadhi AMPUUZIE kabisa mkewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mke wa ustaadh hakuwa na shida huko mwanzo, basi amini kuna kitu bwana ustaadhi anakuficha.

Aidha ashakula mke wa dogo au amekuwa anaflirt naye somehow na mkewe ana haki ya kuonesha kuchukizwa na yaliyojiri.

Anyways tuassume kwamba Ostaadh hana hayo makandokando adhaniayo mkewe, partner wako akimjengea mtu unayemuhisi vibaya ni kama kaunderline hizo tuhuma whether ni sahihi au la. Inasemekana wanawake wengi hawafikiri rationally kama wanaume. Ni hisia tu zinafanya kazi hapo.
 
Mjane itakuwa ni pisi kali kumzidi mama ustadh, hapo kuna wivu wa kike,
Mama ustadh ana roho mbaya, akinuna mjane anamuhudumia shem wake hivyo inamchoresha zaidi kuwa hafai na anapwaya kuwa mke

Ostadh ampe hiyo talaka, mwanamke mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake,, na ikiwezekama amuoe mjane, tiba ya mwanamke jeuri ni mwanamke mwenzie
 
Back
Top Bottom