Mke anaomba talaka baada ya kujua mmewe kamjengea shemej yake kisirisiri

Kwani kuoa mjane si ni sunna kwa dini yetu ya kiislamu?

..namshauri Ostaadh amchukue huyo shemeji yake awe bi mdogo rami.
 
Sasa timbwili limeibuka upya,
Ustadh Yuko Moro saiti anasimamia ufungaji wa umeme kwenye ile nyumba, mkewe kainuka ghafla na kufanya vurugu kubwa akidai ustadh kamjengea MKE wa mdg wake kwa sababu Ni hawara yake.

MKE wa ustadh anadai talaka aondoke zake kwao anadai kwann ustadh amjengee shemej yake spidi spidi wkt wao wanaishi nyumba ya kupanga miaka Zaid ya 8 Sasa na Hawana hata kiwanja.

Anadai Kuna nn kinaendelea Hapa Kama yule sio hawara yake na siku zote kumbe ustadh asizolala kwake kumbe huwa anakuja kulala Moro kwa shemej yake.

Wakuu,
Ustadh anasema Hii kesi imeenda Hadi mskitini wameshindwa kuitatua.
Ustadh anadai mkewe bado ana mpenda na Hana mahusiano yoyote na shemej yake huyo.

Haya majukumu yote aliyoyabeba Ni kwasababu ya kupambana kuisitiri familia ya marehemu mdg wake Mana MKE na watoto wale Hawana ndugu mwngn watamkimbilia Zaid yake yeye.

Ila matokeo yake mkewe anawazia mambo mengine tofauti kabisa.

Nmejaribu kumfata shemej yangu nimuweke sawa, Ni mkali Kama pilipili haskilizi la mtu anasema Mimi na mumewe wote Ni wale wale TU.

Nmejaribu kumhoji ustadhi kiume zaidi labda kuna siku Aliwahi kumla shemej yake kimasihara hata kwa bahat mbaya ustadh kakataa kata kata na kuapia jina la mungu wake.

Nikiangalia kiukweli ustadh naweza kubaliana nae mana Sijawai mskia na mambo ya Michepuko hata kwa bahat mbaya. Yeye Ratiba yake Ni kazini, mskitini na nyumbani kwake TU.Hana kabisa mambo ya wanawake.

Ustadh anadai Mkewe kaenda mbali zaidi hadi kwny mahakama za kiraia anadai wagawane Mali ,gari mbili na bajaji za ustazi viuzwe wagawane na ile nyumba alojenga anadai iuzwe nayo wagawane.

Hebu tunaliwekaje wakuu tumshaur vema ustadh maana Inaonekana baada ya mkewe Kuidai talaka kawa Kama vile kachanganyikiwa.
Nmemwambia subir tukitoka kazn mapema au kesho asbh nikatulia kichwa ntakuchek nikushaur vema zaid ndugu yangu. Kasema "sawa"

Binafs,
Ushaur wangu Ulikua wa kumwambia ustadh asihangaike Tena kumbembeleza na kumpigia magoti mkewemaana ndo anazid kumpa bichwa.
Ampuuze TU, ndoa huwa haibembelezwi
Maana Anachomtuhumu mmewe hakina hata mantiki maana Hana ushahidi wowote kwamba anatembea na shemeji yake.

Nmemwambia shemej yangu (mama ustadh) kua Kama kamchoka ustadh wa Watu anyooshe maelezo na sio anamtaftia TU vijisababu vsivyo na msingi anamfrustrate tu kichwa chake.
Madai yake hayana msingi wowote ule

NAWASILISHA
Kwanza kabisa nampa pole ustadhi inaelekea mwanamke wake hana dini kama angekua na dini angejua maana ya yatima kwakua hao watoto ni yatima na uatadhi ameliona hilo kwakutaka kwastil na ndio mana tunaona watoto wa mitaani kama wote kwakua familia nyingi zinaacha watoto baada ya baba yao kufariki Allah amlipe ustadhi


Na lingene ambalo ndio suruhisho na muafaka kwa kinachoendelea ustadhi amuoe tu huyo mke wa mdogo wake dini yetu inaruhusu kumuoa mjane wa ndg yako katika kumstir yeye na watoto na pia hata zile mali zinakua zimebaki kwenye familia kwakuhofia huwenda anaweza kupata mwanaume na akakaa kwenye nyumba alioicha mume au mali azlizoziacha mume zikatumiwa na mwanaume mwimgine kwaio kuepusha maneno maneno ustadhi afate sheria ya mola wake kwakuendelea kumstir huyo mwanamke na aachane na huyo mwanamke mpuuuzi

Na kama anataka mali wagawane na wagawane mali inatafuta lkn amani ya nafsi ndio kila kitu abaki mana huyo mwanamke ni kama kaingiwa na matamanio ya maslahi kuliko utu na kifupi hapo huyo mwanamke mapenzi yameisha kabisaaa ...zaidi ya hapo atamuua kwa presha kwa visa vyake afanya suruhisho lakumuacha.
 
Back
Top Bottom