Mke ana gari, amekasirika mume nimenunua gari

Mke ana gari, amekasirika mume nimenunua gari

DAVE2014

Member
Joined
Aug 27, 2014
Posts
31
Reaction score
11
WanaJF hii mnaionaje,

Mke wangu ana gari, alikuwa nalo tangu tulivyoingia kwenye mahusiano. Tumekuwa tunalitumia pamoja lakini unajua tena gari likiwa siyo lako huwezi kuwa free, ukilikwangua ni balaa, na hata huwezi sema ngoja nichomoke niende mkoa kutoa salamu maana gari si lako au kulitumia kwa minajili binafsi.

Kwa muda amekuwa akitaka niendeshe mimi kumpeleka kazini na sababu akitoka hupita ninapofanyia kazi kwa kudaka lift ' kuepuka foleni za katikati ya mji' na kufika kituo cha karibu, ama ofisini, hii imekuwa inanilazimu nisubiri hadi afike au yeye anisubiri ikiwa amewahi kabla ya mida ya kutoka. Mara nyingi nimemtaka awe anakwenda na gari ofisini lakini amekuwa akitoa sababu sababu.

Hii imekuwa inani limit sana, siwezi ongeza muda pale ofisini, na pia lazima niende moja kwa moja nyumbani mara tu baada ya masaa ya kazi, isipokuwa zile siku inapomlazimu atangulie ofisini/apite direct nyumbani akiwa na gari mimi hutumia daladala ama treni. Hizi siku zilianza kupungua kidogo kidogo akiwa na visababu.

Upande wa kisaikologia imeniumiza kwanza kwa kutumia gari la mke, na pia kwa kuona wanafamilia wananichukuliaje. Lakini kwa kuwa sikuwa na jinsi nikawa natulia nikijipanga. Mbaya zaidi pale inapobidi wikiendi naenda kwa mama mdogo ama kwa dada, so inabidi kidume niendeshe hadi kwa wanafamilia wa upande wa mke ama wa upende wangu

Hivi majuzi kuna mpango nikafanya na nikapata kahela fulani nikajipa likizo ya wiki mbili since niko between jobs na, nikatenga kwaajili ya mradi wa kuku, ujenzi wa banda kubwa la angalau kuku 200, huku kiasi kingine na nikaona ni muhimu ninunue kausafiri kwa bei nafuu kinachobaki mahitaji madogo madogo ya nyumbani.

Baada ya ujenzi wa banda la kuku kuanza nikamshirikisha mke kuhusu uamuzi wa kuongeza usafiri wangu. Alipinga sana with reasons kuwa usafiri tulionao unatosha.

Lakini nilisisitiza na akakubali, nilikuwa nimeshapata gari, so kesho yake nikaenda kulipia.

Gari ikatoka yard ikafanyiwa service ya kutosha na nikalipeleka home mida ya saa mbili.

Hakutaka kutoka hata kuja kuliona badala yake aliingia chumbani na mtoto ( tuna mtoto wa mwaka na nusu) na kwenda kulala ( hiyo ilikuwa saa mbili na nusu). Hata kahongera sikuambulia. Next day akatoka akajiandaa na kwenda kazini bila hata salamu.

Kuhusu gari ya wife mimi huwa nalisimamia maservice, vifaa vya kubadili ila wese tumekuwa tukishare costs kutokana na siku. Na pale inapobidi mambo yamekaa vibaya basi yeye huchangia service.

Hebu mniambie
 
Kaa nae chini mwongee mkuu. Hiyo itakua rahis yeye kukueleza kwa nn amekasirika and from there it will be easy to solve your problems. Be patient
 
Wewe mjinga( samahami lakini) umeruhusu ajue kuwa hupendi kutumia vyake...ni kosa....ungetumia akili kumpanga ajue kuwa una sababu positive za kununua Gari na sio kushindana nae,sasa kazi unayo kumuondolea hiyo hofu alanayo.....
 
Watu wengine bana kama watoto. Tatizo vijana wa siku hizi wanaoana bado wakiwa wadogo.
 
uko sawa mkuu songa mbele umethubutu umeweza na sasa unasonga mbele.
 
Mpwa umechomoka kwenye mtego lazima anune tu, no way! Ulikuwa huwezi hata kuchomoka kwenye "kusafisha bunduki" maana unakua uko na Waziri Mkuu kila mahali. Hongera lakini usibadilike. Thanks

Kusafish binduki...ha ha ha! Mpwa unatisha.

Hivi mpwa nasikia na wewe una simu ya ziada isiyojulikana na wife..kulikoni!!!
 
cha msingi ongea nae taratibu atakuelewa tu na Fanya kama hakuna kilichobadilika mpeleke kazini kama kawaida na ratiba yako isibadilike coz hapo ashaanza kujenga hofu na wewe labda utakuwa free sana na kusahau majukumu yako
 
Kaa nae chini mwongee mkuu. Hiyo itakua rahis yeye kukueleza kwa nn amekasirika and from there it will be easy to solve your problems. Be patient

Si kila ishu unakaa na mtu unaongea nae, mengine unaacha tu ataabsorb mwenyewe with time goes on.

Ya nini kutia maelezo kana kwamba umefanya kosa wakati tayari ana taarifa
 
Hana sababu ya kufanya hivyo, ila muelewe its not that bad.
Alipenda sana mumewe aendeshe gari lake....Giving is Loving. Na alijua utaona anakupenda sana kwa kukubali kupanda daladala ilhali gari kanunua. Now she may be feeling like she has little to give. Mtoe out na umhakikishie bado unafaidi mengi sana kutoka kwake.

Pia uamuzi wa kununua gari mi naona ni mzuri, ila sababu ulizotumia si bora. Najua ni usumbufu kutumia gari moja lakini hali haikua mbaya kihivyo. Pia shinikizo la kijamii kusukuma maamuzi ndani ya familia yenu si vizuri.

Ikiwezekana we endelea kutumia gari lake mpe hilo jipya la kwenu.

BUT: Honestly speaking mkuu, mkeo ni mke mzuri sana. Just find a way to not make her feel bad?
 
DAVE2014

Gari ni mambo madogo asilete wivu wa kijinga hata hivyo wewe ni head wa nyumba hatakiwi kuhoji mamuzi yako yeye ni kutekeleza tuu,kuna mambo ya kujadiliana ila sio kununua gari
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom