Wasalamu salimini, natumaini mu kheri,
Swali hili si la dini, ninauliza shauri,
Limezonga akilini, nshachoka kufikiri,
Mume akipata jiko, mke amepata nini?
Tangu enzi na enzi, hii kauli si ngeni,
Inawahusu wapenzi, waliojifunga moyoni,
Na jamii yawaenzi, kwa harusi asilani,
Mume akipata jiko, mke amepata nini?
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Safarini