Mkataba wa Ulinzi wa Africa Mashariki vs Malawi

Mkataba wa Ulinzi wa Africa Mashariki vs Malawi

Sabayi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
2,310
Reaction score
1,003
Wadau naomba kuuliza kuhusu mkataba wa ushirikiano wa Kiulinzi wa A.Mashariki ambao Tanzania iligoma kuusaini.Mkataba huo ulikuwa unazitaka nchi zote za Afrika Mashariki kuingia vitani ikiwa nchi moja wapo itavamiwa au kuingia Vitani hadi mara ya mwisho kwa kumbukumbu zangu TZ tuligoma ku usaini kwa kuogopa kuingizwa vitani na maraisi wapenda vita kama M7 na Kagame kwa interest zao binafsi,na Kama tulisaini na mazungumzo ya Malawi yakaenda kombo (Kumbuka kuwa jana walijibu kauli ya membe kusimamisha tafiti za mafuta kwa kusema hawapo tayari kusimamisha kwa kuwa hilo ziwa lote ni lao hivyo hawawezi kupangiwa na nchi yeyote) na tukalazimika kuingia nao vitani je Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi zitakuwa tayari kuingia vitani na sisi kadri ya mkataba huo? Naomba kuwasalisha
 
hawawezi na sidhani kama ni kitu cha maana kusaini mikataba ya mitego namna hiyo
 
Nadhani ilikuwa myopic kwa Tanzania kukataa mkataba huo. Nadhani viongozi wetu waliangalia hali ya sasa tu na wala si miaka 25-50 ijayo wakati akina Museveni, Kagame etc. hawatakuwa mamlakani tena. Ushirikiano wa aina yeyote ile baina ya nchi jirani ni jambo la muhimu.
 
..Malawi ni mwanachama wa SADC ambayo ina mkataba wake wa ulinzi.

..vita baina ya Tz na Mlw ni jambo la mwisho kabisa ukizingatia uanachama wetu wa SADC.

..ikibidi kwenda vitani, kutokana na sababu za kijiografia, msaada mkubwa itabidi utoke kwa Msumbiji,Zambia,na Zimbabwe.

..mataifa hayo ndiyo ndugu wa damu wa wa-Tanzania. majeshi ya Msumbiji na Zimbabwe asili yake ni makambi ya wakimbizi kama Nachingwea, Kongwa, na Mgagao.

..hatuhitaji nchi za Afrika mashariki kutusaidia katika kutusaidia ktk vita na Malawi.
 
Back
Top Bottom