Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,700
- 1,721
Wakuu, nasikia klabu ya Simba inafukuzia asilimia ishirini toka kwa klabu ya T. P. Mazembe kwa mchezaji wake (Mazembe) Mbwana Samata kuuzwa (?) Ubelgiji. Hivi historia ya mchezaji huyo tumeambiwa kuwa Simba walimtolea nje katika kuwekeana mkataba. Mchezaji huyo aliwapa masharti ambayo wao waliona si maslah hivo akaamua kwenda Mazembe. Juhudi zake binafsi na uongozi bora wa klabu hiyo ndo kumepelekea ajulikane hata nje ya Afrika. Sasa viongozi wa Simba mbona wanashinda mlangoni mwa mchezaji huyo? Kama mkataba wa vilabu hivo uliishia pale tu mchezaji huyo aliposajiriwa na Mazembe basi ni heri TFF iingilie kati kulinda wachezaji dhidi ya viongozi wa vilabu vyetu kusubiri jasho la wachezaji wetu.