Mkataba wa kununiana

Mkataba wa kununiana

badshah

Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
51
Reaction score
33
Wanandoa wawili walikuwa na ugomvi baina yao. sasa wakaandika mkataba wa kununiana na wakwanza kuuvunja ndiye atakuwa mkosa.

Siku moja Jamaa alihitajika katika safari yake ya kibiashara awahi ndege ya asubuhi sana muda wa saa kumi na mbili alfajiri, na anayeamka muda huo siku zote ni mkewe hivyo jamaa akahitaji kumwambia mkewe kuwa akiamka tu nayeye aamshwe ili awahi safari yake.

Kwa kuogopa asije kuvunja mkataba ikabidi aandike katika karatasi kuwa "NIAMSHE SAA KUMI NA MBILI, USISAHAU TAFADHALI" akaiweka mahala ambapo anajua mkewe lazima aione.

Asubuhi ijayo jamaa alipoamka akshtuka ameshachelewa safari yake kwani ilikuwa saa tatu asubuhi na ameshachelewa ndege yake. hivyo akapatwa na hasira sana kuona kwanini mkewe hajamuamsha.


wakati anajiandaa kutoka kitandani ili akamlaumu mkewe akaona kikaratasi kimewekwa pembeni yake na kukisoma kimeandikwa hivi: "MUME WANGU AMKA UWAHI NI ALFAJIRI SASA"

Daaaah!! kwakweli mkataba ilibidi uvunjwe tu.

Staryte - Education, Entertainment & Development - Elimu, Burudani na Maendeleo
 
Hehehhe ndoa zina ishu sana hahaha mpaka kununiana

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom