Mkataba wa google na Mozilla umeisha

Mkataba wa google na Mozilla umeisha

Joined
Jun 3, 2014
Posts
28
Reaction score
16
Sababu ya tangazo hili.


firefox1.png


Kwa watumiaji wa browser ya firefox mnaweza kuwa mmeliona tangazo hilo hapo juu mlipotembelea mtandao wa Google hivi karibuni. Tangazo hili ambalo halitokei iwapo unatumia browser zingine, linakushauri uifanye search engine ya google kuwa search engine ya msingi kwenye browser yako.

Sababu ya tangazo hili ni kumalizika kwa mkataba wa kibiashara kati ya Google na kampuni ya Mozilla inayomiliki browser ya firefox. Hapo mwanzo Google ilikuwa na mkataba na firefox, mkataba ambao ulilazimisha firefox kutumia search engine ya Google kama search engine ya msingi katika browser hiyo.

Kumbuka kuwa browser ya firefox inatolewa bure, mtumiaji halipii chochote. Biashara ambayo firefox inategemea ni mikataba kama hii ya Google ambapo kwa kutumia boksi la ku-search (pale juu kulia) kwenye browser ya firefox, moja kwa moja unakuwa ni mteja wa Google.

Kwa kuwa firefox inaongoza kwa kutumiwa na watu wengi duniani, hii ilikuwa ni chanzo kikubwa cha traffic kwa Google kwani inakadiriwa kuwa watumiaji wa firefox wanafanya searches zaidi ya milioni 100 kwa mwaka. Na hivyo makampuni ya search kama Google huwa tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha kwa browsers kama firefox ili search engine zao ziwe ndizo za msingi.

Hata hivyo hivi karibuni kampuni ya firefox imeamua kuachana na Google na kuingia mkataba na yahoo. Hivyo kwa sasa search engine ya msingi katika browser ya firefox ni ile ya yahoo. Hii ndio sababu iliyopelekea Google kuweka tangazo hilo ambalo linawafundisha watumiaji wa firefox jinsi ya kuirudisha Google kuwa search engine ya msingi badala ya yahoo.


firefox2.png

source: bofyatz.com
 
Kati ya browser ninayoikubali ni mozilla.
 
uliisha zaman tu na ndoa ya mozilla na yahoo ni us tu, maeneo mengine kama tanzania still google ni default
 
Back
Top Bottom