kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
Mkataba wa EPA unasema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki itafaidika kutokana soko kubwa na la uhakika la Umoja wa Ulaya, na bidhaa zake ambamo Jumuiya ya Afrika Mashariki itaruhusiwa kuingiza bidhaa zake pasipo kutozwa kodi wala kuwekewa ukomo wa idadi (duty free and quota free).
Ifahamike kuwa vikwazo dhidi ya biashara vipo vya aina mbalimbali. Vipo vinavyohusisha masuala ya kodi na idadi, na vingine vinahusu masuala ya kiufundi. Kwa hiyo, hata pale nchi za EU zinapoondoa kodi, bado huendelea kulinda soko lao dhidi ya bidhaa wasizozitaka kwa kutumia vikwazo vya kiufundi.
Aghalabu nchi za Ulaya huja na visingizio kuwa bidhaa kutoka nchi masikini huwa na madhara kwa afya za binadamu, wanyama na mimea (Sanitary and Phytosanitary Measures – SPS); au husema kuwa ubora wa bidhaa hizo, hasa namna zilivyofungashwa na hata kunakshiwa, ni wa hali ya chini na haufikii viwango vya soko la Ulaya (Technical Barriers to Trade – TBTs).
Kwa hiyo hata kama tungekuwa na uchumi wa viwanda, bado ingekuwa ngumu kuuza bidhaa zetu za viwandani katika soko la EU kwa sababu ya vikwazo vya kiufundi na viwango vya kiafya.
Tofauti nasi, nchi za Ulaya zitaendelea kutumia nguvu yao ya kiteknolojia na kiuchumi ili kutawala soko letu. Yaani, hii ni kusema kuwa nchi za Ulaya zitaweza kuuza bidhaa zao kwetu, ilhali soko lao litakuwa limefungwa. Mageti ya soko la Ulaya hufunguliwa kuingiza malighafi wanazozihitaji tu!
Jambo jingine linalohitaji kusisitizwa ni kwamba huo unaoitwa “upendeleo” hautolewi kwetu tu. Nchi za Ulaya zimeingia makubaliano ya aina hiyo na takribani nchi zote za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, pamoja na nchi za Karibiani na Pasifiki.
Nchi za Kusini mwa Amerika, na hata zile za Asia, nazo pia zina mikataba yenye “upendeleo” wa aina hiyo. Kwa kuwa sehemu kubwa ya nchi hizi huzalisha malighafi zinazofanana, maana yake ni kuwa huko katika soko la Ulaya kutakuwa na ushindani mkubwa wa uwingi wa malighafi zinazofanana, na huu ni ushahidi kwamba hakuna soko la uhakika huko Ulaya. Soko la uhakika halipo Ulaya bali lipo katika nchi hizo zenyewe na kinachohitajika ni ushirikiano baina ya nchi maskini zenyewe.
Kwa hiyo, hakuna cha ziada katika soko la EU tutakachofaidika nacho. Ni EU ndiyo inayofaidika na “upendeleo” itakaopata tutakapofungua masoko yetu, na sio kinyume chake.
EPA na Uchumi wa Viwanda
Uchumi tulionao sio uchumi imara. Ni uchumi uchwara. Uchumi imara hujitegemea na kujiendesha, uchumi uchwara ni tegemezi na hauwezi kujiendesha. Katika uchumi imara kuna utangamano kati ya sekta zalishaji na sekta tumiaji, katika uchumi uchwara hakuna utangamano huo; hivyo kunakosekana mwingiliano kati ya kilimo na viwanda.
Malighafi tunazozalisha ni kwa ajili ya viwanda vya nje, na sehemu kubwa ya vitu tunavyotumia tunaviagiza kutoka nje. Uchumi imara unapaswa kutengeneza ajira zenye staha ilhali uchumi uchwara hupora ajira.
Ndio maana, wakulima wadogo, wafugaji na wachimbaji wadogo ambao ndio wazalishaji wa msingi huporwa ardhi na hivyo hupoteza ajira zao.
Kama tuvyofahamu, sehemu kubwa ya bidhaa tusafirishazo kwenda nje ni bidhaa ghafi, ilhali Ulaya wanasafirisha bidhaa zilizozalishwa viwandani. Ulaya wameondoa kodi na ukomo wa idadi kwa sababu wanahitaji malighafi kwa ajili ya viwanda vyao! Na wanao mpango maalum kabisa ujulikanao kama Raw Materials Initiative, unaotamka kwamba kipaumbele cha diplomasia na mikataba ya ubia kiwe ni kuhakikisha kuwa Ulaya inapata malighafi inazohitaji kwa ajili ya viwanda vyake bila vikwazo vya aina yoyote.
Kwa nchi yoyote inayohitaji kujenga uchumi imara, basi sharti iwe na maendeleo ya viwanda. Na kwa nchi yoyote yenye kudai maendeleo ya viwanda, ni lazima ikatae mikataba ya kikoloni kama EPA inayolenga
Hili hata mabeberu wenyewe wanalifahamu. Inafahamika kuwa hadi kufikia karne ya 13, Uingereza haikuwa chochote katika uchumi wa Dunia. Mfalme Edward wa III aliyetawala katika karne ya 14 aliamua kuchukua hatua madhubuti za kulinda soko la ndani ili kujenga uchumi wa viwanda.
Alipiga marufuku uagizaji wa nguo za sufi kutoka nje, huku yeye mwenyewe akiwa ni mfano kwa kuvaa nguo za sufi zilizotengenezwa Uingereza.
Sera za aina hii ziliendelea hata ilipofika karne ya 18, pale Uingereza ilipokuwa imefanikiwa kuleta mapinduzi ya viwanda. Waziri Mkuu wa wakati huo, Robert Walpole, alinukuliwa akisema “ni wazi kuwa mchango pekee katika ustawi wa umma hutokana na kusafirisha bidhaa za viwandani kwenda nchi zingine na kuingiza malighafi kutoka nje”.
Serikali ya Walpole ilichukua hatua madhubuti zizolenga kulinda viwanda vyao, na wakati huohuo kutawala masoko na mifumo ya kiutawala ya nchi zingine kupitia sera ya kikoloni.
Uingereza iliendelea na sera hizo za kulinda soko lake la ndani mpaka karne ya 19 ambapo Uingereza baada ya kuwa nchi yenye viwanda na inayoongoza katika uchumi wa dunia kwa kumiliki makoloni ikaanzisha sera ya biashara huria.
Marekani ambayo ilikuwa imejinyakulia uhuru wake kutoka kwa Uingereza haikuhadaika na ujuha wa kihalaiki uliokuwa ukienezwa na Uingereza, eti hizo zilikuwa zama biashara huria na hivyo kila nchi ilipaswa kufungua milango yake.
Hivyo haishangazi kwamba aliyekuwa Rais wa Marekani kati ya 1868 na 1876 alitoa tamko kali kukataa biashara huria iliyokuwa ikishadadiwa na Uingereza.
“Kwa karne kadhaa sasa,” alisema Ulysses Grant, “Uingereza imekuwa ikitegemea sera za kulinda viwanda vyake na imezitekeleza sera hizo kupita kiasi na imepata matokeo ya kuridhisha. Hakuna shaka kwamba nguvu za kiuchumi za Uingereza zimetokana sera hizo. Baada ya karne mbili (za kulinda viwanda vyake), Uingereza imeona ni mwafaka kutekeleza biashara huria kwa sababu inafikiri sera za ulindaji viwanda haziwezi tena kuiletea manufaa ya ziada.
"Vema kabisa, mabwana, uelewa wangu juu ya nchi yetu (ya Marekani) unanifanya niamini kuwa Marekani itakuwa tayari kutekeleza biashara huria baada ya miaka 200 ijayo wakati ambapo tutakuwa tumeshavilinda viwanda vyetu na kupata manufaa yote yatokanayo na sera hizo (kama ilivyofanya Uingereza)”.
Kati ya mwaka 1816 na1945, Marekani ilitunga sheria mbalimbali kwa ajili ya kulinda viwanda vyake kwa kuzitoza bidhaa kutoka nje kodi kubwa zaidi kupita kiasi. Ni baada tu ya Vita ya Pili ya Dunia ndipo Marekani ilipoanza kuhubiri juu ya soko huria, na wakati huo Marekani ilikuwa imeshaipoka Uingereza mamlaka ya kiuchumi, na hivyo kuwa kiranja wa dunia (super power) katika nyanja zote.
Naweza kuendelea kutoa mifano ya nchi za Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi, Uswisi, na zinginezo ambazo zote zilikuwa na sera za kulinda viwanda vyao pamoja kutoza kodi kubwa kwa bidhaa kutoka nje na dola kuingilia katika uchumi.
Ili kuleta maendeleo ya viwanda, nchi za Ulaya zilizikataa sera za aina ya “EPA”. Lakini zinataka nchi maskini zikumbatie sera hizo. Tunapaswa kuwaambia Ulaya kuwa sisi sio madodoki. Hatuzitaki sera hizo!
Itaendelea