Mkataba wa bandari Wanirudisha Kanisa Katoliki

KOLOKOLONI

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
2,477
2,360
Mkataba wa Bandari Wanirudisha kanisa katoliki.
Wazee salama humu.

Kwanza nikiri tu miaka mingi sana sijatia Mguu wangu Pale Kanisani inakaribia miaka 13 ila kinachoendelea Nchini juu ya Mkataba wa bandari wacha nijisogeze nione ni kweli wanausoma huo Waraka ni Maaskofu wa kanisa Katoliki. Nilijuavyo kanisa katoliki na Wasomi wake.

Nakumbuka zamani wakati nasoma wale wenzetu wenye vipaji maalumu kitaaluma ambao ni Wakristo Wakatoliki Walifanya mitihani ya seminari nje ya Ule wa darasa la saba na Waliofaulu vizuri sana Walikwenda kusoma shule bora kabisa za kiseminari nisiwe mnafiki kweli kabisa wakali wa darasa wengi walikwenda huko na wachache sana walikwenda shule za Sekondari za vipaji maalum .

Jinsi ninavyozifahamu zile shule no janja janja Wasomi wao ni wasomi konk hasa . Sehemu pekee katika Afrika ukiniambia kalete Msomi safi wasio na makandokando bila shaka nitawapata kwenye Kanisa katoliki.

Mkatoliki aliyesoma shule za kikatoliki mpaka kafikia chuo kikuu juwa kabisa hapo unaongea na Mtu mwenye kipaji maalum kwenye ubongo wake. Sasa ukisikia ni PHD Weka mbali na Watoto kule hakuna michongo michongo kwenye Elimu Nyeupe ni Nyeupe na Nyeusi ni Nyeusi.

Sasa Watu hawa wenye akili nyingi namna hii wamenena jambo zito hivyo Aisee hapo taa nyekundu imewaka ukiforce ni chumba cha kuhifadhi maiti. Jumapili nitarudi Kanisani jimbo kuu la Dar es salaam St Joseph karibu na sehemu ya kupandia boat kwenda Zanzibar kuwasikiliza hivi ni kweli ule Waraka ni wao na wamechukizwa na Mkataba kuwa siyo salama kwa Nchi yetu?

Kama ni kweli Aisee Watz wenzangu nisiwe Mnafiki nitakuwa nao pamoja kimawazo sina mashaka nao hata kidogo katika upeo wao wa kufikiri.
 
Tena chukua bodaboda uwahi kufika.

Huku mwache Mama yetu Samia, The Mother of Modern Tanzania, aijenge nchi.
 
Back
Top Bottom