Mkataba na Kampuni ya TATA Mkoa wa Arusha Je?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkataba na Kampuni ya TATA Mkoa wa Arusha Je??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Rumanyika, Dec 29, 2010.

 1. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wa-Tanzania tusizike tu kichwa kwenye mikataba ambamo tayari kumeshaingizwa mjini, je na mikataba mingine ambayo HAIJALIPUKA BADO NA TAYARI YAMESAINIWA nchini tuyapekue haraka kabla ya kufikia haya ya M-Dowans na Richmond.

  Kwa tabia ya Edward Lowassa wananchi tulivyokwisha kumfahamu ukimuona tu kajipitishapitisha mahala mara kibao ujue kuna dalili za WIZI ZINAZOANDALIWA KITAALAM mahala.

  Gwiji huyu wa ufisadi ameonekana kukazania project moja ya Multi-Billions of dolars na Kampuni ya TATA duniani kujenga kitu kule mbugani Arusha. Mkataba huo kauvalia njuga mpaka mtu kwa akili ya kawaida unajiuliza kuna nini.

  Na mpaka hapo kawachuuza ndugu zetu wamasai wanafukuzwa huku na TATA ila Mfalme wa Kiarabu yeye anawaua kabisa na kucheka na watoto wake.

  Hoja yangu ni kwamba Wa-Tanzania tusipende kusubiri mpaka MPANGA WA UFISADI UJE UKATULIPUKIE bora tukaanza nayo mapema sana. Je, kwa mkataba kati ya nchi yetu na kampuni ya TATA na mikataba mingineo WALIPAKODI tuko salama kiasi gani????
   
Loading...