Mkataba mwengine wa (madudu) reli

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Tuesday, 22 February 2011 21:07 (MWANANCHI)

Ramdhan Semtawa
Akiwasilisha Taarifa ya Utendaji wa Kampuni ya Reli nchini kwenye kamati hiyo, jijini Dar es Salaam jana, Nundu alisema mkataba huo, umeathiri uendeshaji reli kwa kiasi kikubwa."Hisa za TRL ni hasi na serikali haitakuwa na gharama ya kununua hisa za Rites," alisisitiza Nundu.

Nundu alisema Rites walipewa mamlaka makubwa, ikiwamo kuingiza watu watatu kati ya watano kwenye bodi, kuendesha menejimenti pia ikiwa na hisa asilimia 51."Sisi watu wawili na usiombe itokee mmoja akiwa hayupo tumekwenda na maji," alisema.

Kwa mujibu wa waziri Nundu ambaye anaonekana kuweka mikakati madhubuti kufufua reli hiyo. Kitendo hicho cha kukabidhi mamlaka makubwa kwa Rites, kimeliweka shirika hilo, kwenye hali ya hatari na limedhoofika kwa kiasi kikubwa.

Alisema kitendo hicho, kimelifanya shirika la reli kujiendesha kwa hasara kipindi chote cha miaka mitatu tangu kuwa chini ya menejimenti ya kukodi.
"Hili la mkataba tusiseme ni CCM hao...hapa tunazungumza kama Watanzania, kwani kwenye taasisi (zinazohusika na mikataba) kuna watu kutoka Chadema, CUF na CCM.

Akitoa takwimu, Waziri Nundu alisema mwaka 2007, zilisafirishwa tani 570,000 za mizigo, mwaka 2008 tani 475,485, mwaka 2009 tani 450,000 na mwaka 2010 tani 253,000 na kufafanua kwamba pia idadi ya abiria waliosafirishwa ilishuka mwaka hadi mwaka.

"Kwa mfano, mwaka 2007 walisafirishwa abiria 585,310, mwaka 2008 abiria 458,819 na mwaka 2009 abiria 543,001. Hali ya sasa ya TRL sio ya kuridhisha na kutokana na hali hiyo, kuna safari mbili za treni ya abiria kwenda Kigoma pekee na hakuna treni ya kwenda Mwanza ikilinganishwa na mahitaji ya treni tano kwa wiki zinazokwenda Mwanza na Kigoma,"alisema.

Kuhusu Menejimenti ya Kampuni

Nundu alifafanua kwamba, tathmini iliyofanywa na mtaalamu mshauri, imebainisha kuwa, thamani za hisa za TRL ni hasi, hivyo hazina thamani na kuweka bayana kuwa, gharama itakazoingia serikali baada ya kuchukua kampuni hiyo kwa asilimia 100, itakuwa ni kulipa dola 23.1 milioni za Marekani (karibu Sh24 bilioni) kwa ajili ya kulipia madeni.

Alisema uamuzi huo, ni makubaliano ya pamoja kati ya Rites na serikali, ambayo tayari pia imetangaza muundo wa menejimenti mpya ya wazalendo itakayokuwa na wajumbe wa bodi watano kama ilivyo sasa.

Katika muundo huo, wa menejimenti ya mpito, Waziri Nundu alisema tangu Julai 8, mwaka jana, tayari ameteuliwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye atafanya kazi na Rites kwa lengo la kurahisisha makabidhiano ya uendeshaji TRL wakati menejimenti hiyo ya India itakapoondoka.
Alisema katika muundo huo, kuna Mkurugenzi mtendaji anayesaidiwa na manaibu wawili; mmoja atashughulikia uendeshaji na mwingine huduma na watasimamia idara tisa.

Kuvunja mkataba
Waziri Nundu alisema tayari wizara imekamilisha taratibu mbalimbali, ikiwamo kuwasilisha maombi Wizara ya Fedha na Uchumi kwa ajili ya malipo ya awali ya Rites kwa lengo la kuvunja mkataba wa wanahisa wa Kampuni ya Reli na kuwasilisha nyaraka za kuvunja mkataba huo (Deed of Settlement) na Rites ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya upekuzi (Vetting).

"Baada ya hapo taarifa itawasilishwa Rites na hatimaye kusainiwa na pande zote mbili za wanahisa, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumevunja rasmi mkataba na menejimenti ya Rites ndani ya TRL kuondoka," alisema.

Kuboresha Reli
Kipindi cha miezi mitatu, Waziri Nundu alisema mpango ni kufanyia matengenezo na kuimarisha reli, kununua mashine ya kuokolea (Crane) wakati wa ajali, kukarabati injini na mabehewa ya mizigo na abiria na kuweka fedha za uendeshaji wa kampuni na kwamba, kazi hizo zinahitaji Sh27.45 bilioni.

Kuhusu kipindi cha mkakati wa miezi sita, alisema malengo ni kutengeneza kiwanda cha kuzalisha kokoto kilichopo eneo la Tura, kutengeneza mfumo wa mawasiliano kati ya Dar es Salaam na Ngerengere na kununua injini za mabehewa.

Nyingine ni kutengeneza vituo vya magenge, kununua mashine za kushindilia kokoto kwenye tuta la reli na kuendelea kuweka fedha za uendeshaji, kazi ambazo zote zitahitaji Sh63 bilioni.

Awali, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, alitaka wajumbe kujadili mambo hayo kwa uwazi ili kupata mwafaka.
 
Kama aliyokwisha fanya yalikuwa hayatoshi, kumbe Chenge alisaini na Mkataba na Rites. Kinachoshangaza ni Nundu kusema kuwa mkataba ule ni wa Watanzania, wakati Nundu kakubali katika taarifa hii kuwa mkataba ni kati ya Rites na serikali, na ikiwa serikali ni ya CCM, tena hapa CHADEMA na CUF wanahusika vipi? Au Watanzania tunahusika vipi? Tutaendelea kufanywa wajinga mpaka lini?
 
Tuesday, 22 February 2011 21:07 (MWANANCHI)

Alisema kitendo hicho, kimelifanya shirika la reli kujiendesha kwa hasara kipindi chote cha miaka mitatu tangu kuwa chini ya menejimenti ya kukodi.
"Hili la mkataba tusiseme ni CCM hao...hapa tunazungumza kama Watanzania, kwani kwenye taasisi (zinazohusika na mikataba) kuna watu kutoka Chadema, CUF na CCM.

Nundu kama approch yako itakuwa si kutafuta chanzo cha tatizo nawe hautafika mbali. Kumbuka kabla ya huo mkataba wa Rites, serikali ya JK ilipoingia madarakani ilipiga stop mchakato uliokuwa unaendelea juu ya kubinafsisha shirika la reli kwa madai ya kuakikisha wanapata mwekezaji mzuri. Motokeo yote tunayajua na ndiyo matunda ya akina CHENGE!

Lakini nafikiri wote ni mashaidi kwa huu uhuni uliokuwa unaendelea pale Rites! Nundu akumbuke kuwa ili kuondokana na tatizo hilo ni lazima awawajibishe waliotufikisha hapo. Kinyume chake wengine watatuingiza katika mikataba ya namna hiyo......!

For the Record:
Nundu asitake tuamini eti walioingia mikataba ya kihuni ni ccm, chadema na cuf; Hapana. Hapa kama kuna makosa kwenye mikataba ni ccm peke yake anayestahili lawama. Akumbuke tukisema barabara za lami zimejengwa hatusemi pongezi ziende kwa cuf walachadema, hapo tunasikia ccm imefanya hivi na vile.
 
Back
Top Bottom