Mkataa pema pabaya panahitaji

Mkataa pema pabaya panahitaji

Nipo kwenye wakati mgumu wa kuchagua mtu sahii wa kufanya naye maisha

Nina wanawake wawili ambao nina pendana nao na wote na wapenda ila kwa mujibu wa imani yangu ni lazima ni mchague mmoja tu

Mmoja ni msomi na ni mfanya biashara mdogo
Na pia ni muajiriwa kwenye campuny ndogo ya kuchapisha picha kwenye nguo na mengine
Tabia zake huyu
Ni mkali saana sio mtu wakukaa kimia pale ninapo mkosea
Na akiamua kitu harudi nyuma kwa ufupi ni mwepesi wa asira saana
Na sio mtu wa show off

Huyu wa pili ni msomi pia kwao kuna kidogo yaani nina maana wazee wake wana pesa sio muajiriwa wala hana biashara yeyote zaidi ya kumiliki biashara ya wazazi wake

Tabia zake huyu

Ni mpole saana
Hana kiburi
Ni mcheshi
Pia ni mwepesi wa asira ukimchanganya utasoma namba
Na ni mtu ambaye ana penda kutumia pesa nyingi kutengeneza mwili wake kwa ufupi ana penda urembo

Sasa ina nipa shida kuchagua mtu sahii wote na wapenda saana
Je kufuata na tabia zangu hizi
Una fikiri ni nani anaweza kuwa sahii kwangu kwa hawa wanawake wa wili?

Kwa ufupi mimi mchafu yaani sijui kujitengeneza kama vijana wa kisasa
Pia mimi sio msomi
Tatu mimi ni mcheshi saana sio mwepesi wa asira
Mwisho najua kutafuta pesa lakini sijui kuzitumia nina weza kupata pesa nisipo kuwa na mtu sahii wa kuniongoza zote nina weza kuzimaliza kwa vitu vya kijinga

Je una fikiri yupi ndo anaweza kunifaa?
Kwa uzoefu wangu wa miaka 23 kwenye mahusiano huyu wa pili ni mke mzuri zaidi tabia zake zinaweza kuwa shaped na ukamcontrol vizuri zaidi huyo wa kwanza ni Feminist atakusumbua sana, atakuburuza sana yaani utajuta kuingia kwenye jambo linaoitwa NDOA, Kila la kheri.
 
Muacheni apambane na laana zake huyu... Kuwa nao wote kwa pomoja huku ukijua huna malengo nao unatafuta nini!?!? Gafla uje umuache mmoja hatujui umekaa nao muda gani,nae aje kuanza upya tena!?!? Acheni kucheza na hisia za watu.

Utaenda kula kiapo cha kifo kiwatenganishe huku umekuja kufanya ana anado hapa!!! Mtu hata moyo wako haujui unataka nini mpaka usaidiwe!?!? Natamani wangekusoma hapa waone lihewa linalo wachanganya.
 
Yule aliekiss na mmexican umemuacha au na yeye yupo umeamua kukaa kimia
 
Back
Top Bottom