Mkata umeme underground za Kariakoo amekosa heshma kwa wakubwa wa Chama na Serikali

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Ukistaajabu ya ukosefu wa dola za marekani kwenye bank na bureau Tanzania utayaona ya ukataji wa umeme maduka ya underground kariakoo.

Kuna maeneo ya kukata umeme na kuna maeneo ya kuyaacha huru kutokana na aina ya watu na mazingira

Hivi mtu na akili timamu unakata umeme kwenye underground za Kariakoo,Maduka na biashara zipo chini ya ardhi halafu mtu anakata umeme.

Kuna wakati ni heri kuajiri vijana wa mjini kuliko kuajiri vijana waliozaliwa na kukulia ukingani kama mimi GUSSIE kusimamia maslahi ya Taifa hasa umeme eneo la kariakoo underground.

Wakinga sisi miaka nenda rudi kule makete tulizoea umeme wa mafuta ya diseli,Ukiona umeme hakuna week nzima ilikuwa ni kawaida kutambua gari za mafuta hazijafika.

Vichekesho na sis wakinga siku hizi tumeungwa Grade ya Taifa ya umeme kama watu wa Dar es Salaam wanaolia lia.

Mkata umeme amegusa maslahi ya watu hakika nakutakia safari njema huko kwenye simu.

Eti mkata umeme anatoa haki sawa makete kule ukingani kwetu na kwenye biashara za wakubwa Dar es Salaam.
 
Ukistaajabu ya ukosefu wa dola za marekani kwenye bank na bureau Tanzania utayaona ya ukataji wa umeme maduka ya underground kariako...
Endelea kumchefua uone,hata hiyo simu yako anao uwezo wa kuizima na kukunyima mawasiliano wewe tuuu🤸🤸🤸
 
Back
Top Bottom