Mume amepewa jina la Mopao ( sio jina halisi)
Mke amepewa jina la Mopa (sio jina halisi)
Mkasa wa Kweli Uliomkuta Kigogo wa Serikali Aliyetumbuliwa Baadaye Kutimuliwa na Mkewe.
Mkasa wa kusikitisha unaomuhusisha Kigogo mmoja aliyeishi maisha mazuri kwa kuitumikia Serikali moja barani Afrika.
Kigogo huyu almaarufu Mopao aliishi na mkewe almaarufu Mopa waliishi maisha ya furaha wakijaaliwa kupata Watoto wawili.
Mungu aliwabariki wote hao kwa nyadhifa nzuri, Mopao akiwa Mkurugenzi Serikalini huku Mopa akihudumu kwenye Taasisi nyeti ya Kifedha akiwa Mwanasheria.
Wanandoa hao waliishi kwenye nyumba ambayo Mke alipewa na Taasisi ya Kifedha aliyofanyia kazi.
Maisha yalibadilika ghafla kufuatia Mopoa kutumbuliwa kazini. Serikali ya nchi hiyo ilishaamua kurejesha nidhamu kwa Watumishi wa Umma!
Wanandoa hao waliendelea kuishi pamoja wakipambana na changamoto mbalimbali zilizotokana na Mume kukosa ajira!
Mume akihangaika kutafuta maisha huku akimtegemea Mkewe kwa makazi, malazi, matibabu, usafiri n.k
Kwa wastani Mopa alikuwa mkarimu na alimruhusu Mopao kutumia hata gari lake la kisasa kabisa.
Hata hivyo mambo yalibadilika tena baada ya siku moja Mopao kurejea nyumbani na kukuta mlango umepigwa kufuli huku nguo zake zikiwa zimetupwa nje.
Mopao aliamua kuvunja mlango na alipoingia ndani alikuta nyumba ikiwa tupu!
Mopa alishaamua kuhama na kukabidhi nyumba huku akiacha ujumbe wenye tuhuma lukuk
Kwamba alikiuka maadili ya ndoa kwa kuchepuka
Kwamba amekuwa akitumia kwa anasa mali za mkewe
Kwamba amekuwa mlevi mkubwa huku akitumia hela za Mkewe
Tuhuma zote hizo Mopao alizikanusha vikali sana huku akidai kukosa kipato ndiyo chanzo cha yote hayo!
Kama vile haitoshi Mopa alimshtaki Mopao Polisi kwa madai ya kuvunja mlango na kufanya uharibifu wa nyumba aliyopewa na Taasisi
Mopa alienda mbali zaidi kwa kufungua kesi mahakamani akidai taraka kutoka kwa Mopao
Ndugu yetu Mopao amechanganyikiwa, haelewi afanye nini, hajui aanzie wapi wala aende wapi
Mkewe alimfanyia hisani kwa kwa kumpatia Mumewe kiasi kidogo cha fedha akaanze maisha
Hatujui nani ni msemakweli ila Ndugu yetu Mopao amechanganyikiwa, haelewi afanye nini, hajui aanzie wapi wala aende wapi
Nitumie fursa hii kuwaomba tumshauri mwenzetu aliye kwenye uhitaji mkubwa wa faraja.
Aksanteni