Mkasa Wa Kweli: Tamaa Mbele Mauti Nyuma

Mkasa Wa Kweli: Tamaa Mbele Mauti Nyuma

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
Mbinguni kuna nyota tatu zilizofuatana katika mstari mmoja. Ukitazama angani wakati wa usiku unaweza kuziona. Wahenga wanasema nyota hizo zinaashiria kuwa tamaa kwa binaadamu iko mbele, mauti yako nyuma na binaadamu yuko katikati.

Wakati binaadamu anaikimbiza tamaa na yeye anakimbizwa na mauti!

Nyota hizo zinawakilisha ukweli kwamba siku zote binaadamu anaongozwa na tamaa. Lakini amesahau kuwa mauti nayo yako nyuma yake!



SASA ENDELEA.



Shangwe Mpya ilikuwa moja ya hoteli maarufu jiji Tanga. Haikuwa maarufu kwa sababu ya mandhari yake ya kupendeza au kuwa katika mtaa ambao ni maarufu, ilikuwa maarufu kwa sababu ilikuwa hoteli ya miaka mingi.



Ilikuwa hoteli ya ghorofa moja tu iliyokuwa katika barabara ya Eckenford. Pengine ilikuwa hoteli ambayo haikuvutia wageni kwani idadi ya wageni waliofika katika hoteli hiyo haikuwa kubwa.



Hoteli ya Shangwe Mpya ilivutia zaidi wenyeweji wa Tanga. Sababu kubwa ni kuwa kulikuwa na vyakula vya kiasili na bei yake ilikuwa nafuu sana. Pengine hilo ndilo lililofanya hoteli ya Shangwe Mpya kuwa maarufu sana.



Saa moja usiku Dastan Seseko aliisimamisha pikipiki yake mbele ya hoteli ya Shangwe. Akaiegesha kwenye eneo la kuegesha pikiki na kuelekea kwenye mlango wa kuingia hotelini humo.



Ilikuwa kawaida yake kwenda kula chakula cha jioni kila ifikapo saa mbili usiku lakini usiku huo aliwahi kufika. Alikuwa na sababu moja kubwa iliyomfikisha mapema mahali hapo.



Kwa siku tatu mfululizo kila alipofika hotelini hapo alikuwa akikutana na msichana mmoja aliyekuwa akienda kula chakula cha jioni. Lakini mara zote hizo Dastan anapofika, msichana huyo huwa ameshamaliza kula na kutoka.



Hivyo usiku huo Dastan alifika mapema zaidi kuliko muda wake ili aweze kumuona vyema msichana huyo.



Dastan aliingia katika eneo la wazi la hoteli ambalo lilitapakaa viti na meza kwa ajili ya wateja.



Kwanza alizungurusha macho katika eneo hilo ambalo halikuwa na watu wengi muda huo. Baada ya kutomuona msichana aliyekuwa akimtaka alitafuta meza ya pembeni na kwenda kuketi.



Aliagiza nyama choma na juisi kisha akayaelekeza macho yake kwenye mlango wa kuingia katika eneo hilo.



Aliamini kuwa msichana aliyesababisha afike mahali hapo mapema angewasili wakati wowote.



Dastan alikumbuka siku ya kwanza alipomuona msichana huyo alistushwa na umbile lake pamoja na sura yake jamali. Akajiambia hakuwahi kukutana na msichana aliyeugusa moyo wake kiasi kile kama ilivyokuwa kwa msichana huyo.







Siku ya pili alimuona tena akitoka. Alipomtazama alijiridhisha kuwa mawazo yake yalikuwa sahihi. Msichana huyo alikuwa mrembo na mwenye mvuto.



Siku ya tatu alikutana naye tena. Bahati mbaya siku zote hizo hakupata muda wa kutosha angalau wa kumsalimia.



Ulikuwa ni upumbavu ambao ungeweza kumnasa mwanaume yeyote anayekutana na msichana mrembo. Dastan alitaka kuzungumza naye na amueleze kuwa alikuwa amempenda.



Wakati Dastan analetewa nyama choma aliyoagiza pamoja na bilauli ya juisi akamuona msichana huyo akiingia. Moyo wake ulishituka kidogo akaacha kuitazama sahani ya nyama choma na kumuangalia msichana huyo huku vyakela vyote alivyoagiza akivipiga pindu na kumwagika chini.



Alitamani aende akaketi katika meza aliyoketi yeye lakini ilikuwa sivyo. Msichana alikwenda kukaa katika meza nyingine.



Wakati Dastan akiendelea kumtazama huku akisifia uzuri wake alijiambia baada ya muda kidogo ataamisha makazi kwenye meza ya msichana huyo ili aweze kuzungumza naye.



Msichana aliletewa nyama choma na ndizi za kuchoma. Wakati anaanza kula, kuna jamaa aliingia na kwenda kukaa katika meza aliyokaa msichana huyo. Kitendo hicho kilimkera Dastan na kumfanya ajilaumu kwa kuchelewa kwenda kuketi yeye.



Baada ya muda kidogo aliwaona wawili hao wameingia katika mazungumzo. Dastan alikuwa akiumia kimoyomoyo huku akienndelea kujilaumu.



Lakini baadaye kidogo alipata shaka kwamba watu hao huenda walikuwa wanajuana kwani baada ya kumaliza kula waliondoka pamoja.



Dastan alikuwa amemaliza kula kitambo baada ya kuagiza mlo mwengine baada ya ule wa awali kuupiga pindu. Baada ya kulipa bili yake aliinuka na kuwafuata nje.



Aliwaona wakijipakia kwenye gari la msichana na kuondoka.



Kihoro kilikuwa kimemshika Dastan. Na yeye akawasha pikipiki yake na kuwafuata.



Gari hilo lilikamata barabara ya Eckenford, baadaye lilikata kushoto likaingia eneo la Bombo. Dastan alikuwa bado akiwafuata nyuma.



Walilivuka daraja la Mkwakwani kisha wakakata kulia. Dastan naye alikata kulia. Gari hilo baada ya kuumaliza mtaa huo, lilikata kushoto na kusimama mbele ya nyumba moja iliyokuwa upande wa kulia wa barabara.



Dastan alilipita gari hilo na kwenda kusimama mbele, mahali ambapo palikuwa na kiza kilichotokana na mti wa muarubaini uliokuwa umeota pembeni mwa barabara.



Ili aweze kuwaona vizuri, aliigeuza pikipiki yake ielekee upande ule aliotokea na kuendelea kuwatupia macho watu hao.



Aliwaona wawili hao wakishuka kwenye gari na msichana akafungua mlango wa ile nyumba na kuingia ndani pamoja na mtu huyo.



Dastan aliendelea kusubiri kuona kama wangetoka tena. Ukapita muda mrefu. Wakati inakaribia kuwa saa tano usiku, Dastan aliona taa ya mbele ya nyumba hiyo ikizimwa, kukawa kiza. Lakini kulikuwa na mwanga hafifu uliotoka katika nyumba za jirani.



Baadaye Dastan alimuona yule msichana ametoka peke yake. Akaangalia kila upande. Mtaa huo ulikuwa kimya na hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akipita.



ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 02


ILIPOISHIA



Dastan alilipita gari hilo na kwenda kusimama mbele, mahali ambapo palikuwa na kiza kilichotokana na mti wa muarubaini uliokuwa umeota pembeni mwa barabara.



Ili aweze kuwaona vizuri, aliigeuza pikipiki yake ielekee upande ule aliotokea na kuendelea kuwatupia macho watu hao.



Aliwaona wawili hao wakishuka kwenye gari na msichana akafungua mlango wa ile nyumba na kuingia ndani na mtu huyo.



Dastan aliendelea kusubiri kuona kama wangetoka tena. Ukapita muda mrefu. Wakati inakaribia kuwa saa tano usiku Dastan aliona taa ya mbele ya nyumba hiyo ikizimwa, kukawa kiza. Lakini kulikuwa na mwanga hafifu uliotoka katika nyumba za jirani.



Baadaye Dastan alimuona yule msichana ametoka peke yake. Akaangalia kila upande. Mtaa huo ulikuwa kimya na hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akipita.



SASA ENDELEA



Msichana akarudi ndani. Baada ya muda kidogo alitoka tena sasa akiwa anamburuza chini yule jamaa aliyeingia naye ambaye upande wake wa kichwani ulikuwa umetapakaa damu.



Alikuwa amemshika mabega yake akimburuza na kutoka naye nje. Aliendelea kumburuza hadi kwenye gari lake. Akafungua boneti la nyuma la gari lake. Akajaribu kuubeba mwili wa mtu huyo ambao haukuonesha dalili yoyote ya kuwa hai, akautia kwenye boneti la gari kisha akalifunga.



Baada ya hapo msichana huyo alikwenda kufunga mlango wa nyumba kisha akajipakia kwenye gari na kuondoka.



Gari hilo lilikuwa linakwenda upande ule aliokuwa Dastan. Dastan aliwasha pikipiki akaigeuza na kuiondoa haraka kuelekea kule kule lilikoelekea gari hilo.



Alikuwa amelitangulia gari hilo ambalo halikuwashwa taa za mbele. Dastan naye hakuwasha taa za mbele wala nyuma. Alihofia kuwa kama msichana huyo angemuona angegundua kuwa alikuwa anamchunguza.



Dastan aliuvuka mtaa uliokuwa mbele akaendelea kwenda huku mara moja moja akitazama nyuma.



Akaliona gari hilo likikata upande wa kulia nyuma yake. Ulikuwa ni ule mtaa aliouvuka. Dastan akaigeuza pikipiki na kulifuata. Alikata upande ulioelekea gari hilo akaliona limesimama chini ya vivuli vya miti. Upande wa kulia wa mahali liliposimama kulikuwa na makaburi yaliyokuwa yamezungushiwa ukuta.



Dastan naye akasimamisha pikipiki yake pembeni mwa barabara kwenye kivuli cha mti.



Alimuona yule msichana akifungua boneti la nyuma la gari lake akautoa mwili wa yule mtu na kuutupa chini. Baada ya kulifunga boneti aliuburuza ule mwili hadi kwenye ule ukuta uliozunguka makaburi akauacha mwili huo na kurudi kwenye gari. Akaliwaha na kuondoka.



Gari hilo lilipoondoka Dastan aliiendesha pikipiki hadi mahali hapo akaumwilika ule mwili kwa taa za pikipiki yake na kugundua kuwa alikuwa ni yule jamaa aliyeondoka na yule msichana kule hoteli na kutokana na damu iliyokuwa imeenea kichwani mwake alihisi alikuwa ameshakufa.



Dastan alishuha pumzi akatazama barabarani kuona kama angeliona tena lile gari la msichana lakini hakuliona tena. Akaondoka mahali hapo.



**********



Dastan Seseko alikuwa fundi maarufu wa kompyuta. Ofisi yake ilikuwa mtaa wa barabara nane mkabala na barabara ya Taifa. Alikuwa akishirikiana na fundi mwenzake Ali Msela.



Wote wakiwa vijana waliohitimu kutoka chuo cha Veta na kuamua kujiajiri wenyewe, walikuwa wanatoka katika familia tofauti. Ali alikuwa anatoka katika familia ya kawaida yenye baba na mama akiwa na asili ya Tanga.



Dastan alitoka katika kituo kimoja cha yatima mjini humo ambacho mbali ya kumlea tangu alipokuwa mdogo pia kilimpatia elimu kuanzia ya msingi, ya sekondari hadi Chuo cha Veta. Hakuwa akimjua baba yake wala mama yake.



Dastan alipomaliza msomo ya Veta ndipo alipoanza kujitegemea mwenyewe na kupangisha chumba eneo la Chumbageni.



Tangu alipoanza kujiajiri mwenyewe akishirikiana na Ali Msela aliyekutana naye Veta, Dastan aliona maisha yake yalikuwa yakielekea kuwa mazuri. Kipato alichokuwa anapata kilitosha kumuwezesha kimaisha.



Baada ya kuona alikuwa amefikia umri wa kuwa na mke, Dastan alianza kutafuta mchumba. Akiwa katika harakati hizo ndipo alipokutana na msichana aliyeona kuwa angefaa kuwa mke wake.



Lakini katika kumfuatilia akakutana na tukio ambalo hakukitegemea.





Tangu siku ile Dastan alijiambia suala la kuchagua mchumba si la kuchukulia kimzaha. Kwa mtindo aliokuwa ameutumia angeweza kujikuta anapoteza maisha yake kama alivyomuona mwenzake ambaye aliingia nyumbani kwa yule msichana akiwa mzima na kutoka akiwa maiti.



Wiki moja baada ya tukio hilo Dastan alikuwa amekaa katika chumba chake cha kazi akishughulikia kompyuta iliyokuwa na tatizo la kuwekewa program.



Mwenzake Ali alikuwa akiunganisha nyaya za kompyuta nyingine.



Ghafla waliona gari likisimama mbele ya duka lao. Akashuka msichana ambaye Dastan alipomuona tu, moyo wake ulishituka. Alikuwa ni yule msichana aliyemuua mtu wiki moja iliyopita. Alikuwa ameshika laptop mkononi.



Mara tu baada ya kushuka kwenye gari alitembea kuelekea kwenye mlango wa duka hilo. Dastan alikuwa akimkodolea macho.



Alipoingia ndani ya duka hilo aliwasalimia kisha akaiweka laptop yake juu ya meza kubwa aliyokuwa kando ya mlango.



“Lapto yangu ina tatizo” akasema huku akimtazama Dastan aliyekuwa upande wa pili wa meza hiyo.



“Ina tatizo gani?” Dastan alimuuliza huku akimtazama kwa macho ya tashiwishi.



“Haiwaki, sijui ni kwanini?”



Dastan aliikamata laptop hiyo akaifungua na kujaribu kuiwasha. Laptop haikuwaka.



“Itabidi tufungue tujue tatizo lake. Tuachie tutaishughulikia”



“Nije muda gani?”



“Njoo kesho, kwa muda huu tuna kazi tulizokwisha zianza”



“Kesho, nije saa ngapi?”



“Njoo saa sita mchana”



“Sawa. Nitakuja muda huo”



Msichana akageuka na kuondoka. Dastan alimsindikiza kwa macho hadi alipokuwa anaondoka na gari lake. Alitaka kumueleza mwenzake kuhusu aliyoyashuhidia kwa msichana huyo wiki moja iliyopita lakini akanyamaza.



Kilichomfanya abaki kimya ni kuwa kulikuwa na taarifa ya polisi katika vyombo vya habari iliyoeleza juu ya kupatikana kwa mtu aliyekutwa ameuawa kando ya eneo la makaburi katika mtaa mmoja wa eneo la Bombo.



Taarifa hiyo ambayo ilitolewa kwenye vyombo vya habari siku tatu baada ya tukio lile, ilieleza kwamba mtu huyo asiyefahamika ambaye alikutwa asubuhi akiwa ameuawa alikuwa na jaraha kichwani lilionesha kuwa alipigwa na kitu chenye ncha kali.



Dastan aliogopa kueleza kuwa aliliona tukio hilo kwa vile mtuhumiwa mwenyewe alikuwa hajakamatwa, akaamua kunyamaza kimya.



Mara tu michana huyo alipoondoka, Dastan aliifungua ile laptop na kugundua kuwa ilikuwa na tatizo dogo. Kulikuwa na kiwaya kilichokuwa kinasambaza umeme kwenye mashine yake, kilikatika. Alikiunganisha na laptop ikawaka hapo hapo.



Latop ilipowaka Dastan aliingia katika chumba cha ndani na kuanza kuipekua. Alikuta taarifa mbali mbali za kidaktari pamoja na picha zilizoonesha maeneo mbali mbali ya ndani ya mwili wa mwanaadamu ambayo yalikuwa yakielezewa kitaalamu.



Dastan alijiuliza yule msichana anafanya kazi gani? Kwanini laptop yake ina maelezo ya kidaktari na ina picha za viungo vya binaadamu?



Akafikiria kwamba huenda msichana huyo alikuwa akiua watu na kuchomoa viungo vya ndani ambavyo huviuza.



Baada ya kuoma taarifa hizo ambazo hata hivyo hakuweza kuzielewa, Dastan aliizima laptop akaiweka na kwenda kuendelea na kazi yake.



Siku ya pili yake saa sita mchana msichana akawasili tena. Laptop yake ilikuwa juu ya meza.



Baada ya kuwasalimia mafundi hao, alimuuliza Dastan.



“Laptop yangu ipo tayari?”



“Ipo tayari” Dastan alimjibu kwa kumchangamkia.



Aliifungua ile laptop akaiwasha. Msichana alipoona laptop yake inawaka alitabasamu.



Dastan alidhani msichana angemuuliza ilikuwa na tatizo gani, swali ambalo mafundi wengi hawalipendi. Lakini msichana hakuuliza swali hilo.



Aliishika laptop yake na kuingia kwenye program ambazo alitaka kuzijaribu. Aliporidhika akaizima.



“Ni kiasi gani?” akauliza.



Dastan akamtazama. Alimuhisi alikuwa msichana mrembo na mwenye ubinaadamu wa hali ya juu.



Wakati akimtazama, Dastan alikumbuka kwamba siku chache zilizopita msichana huyo aliua mtu na kwenda kuutupa mwili wake kwenye eneo la makaburi.



Akajiambia pengine urembo wake na ubinaadamu wake ulionekana kwa nje tu, kwa ndani yake alikuwa msichana katili na dhalimu.



Dastan alitaka amwambie ampe shilingi elfu ishirini lakini akabadili mawazo.



“Nipe elfu kumi” akamwambia.



Msichana alifungua mkoba wake akachomoa noti ya shilingi elfu kumi akampa Dastan.



“Asante”



Msichana allichukua laptop yake akawaaga mafundi hao na kuondoka. Dastan aliendelea kumtazama msichana huyo hadi alipojipakia kwenye gari yake na kuondoka.



Hata baada ya msichana kuondoka, Dastan aliendelea kujiuliza ni kitu gani kilitokea siku ile kati ya yule jamaa aliyeuawa na msichana huyo.



Akajiuliza tena kama watu hao walikuwa wakijuana au walikutana siku ile kwa mara ya kwanza.



“Inawezekana kwamba walikuwa wanajuana, isingekuwa rahisi kwa msichana kumpeleka nyumbani kwake mwanaume aliyekutana naye siku hiyo hiyo” Dastan akajiambia.



Hata kama walikuwa wakijuana, Dastan aliendelea kujiambia, Ni mtafaruku gani uliwatokea hadi msichana huyo alimuua mwenzake?



Zikapita tena wiki mbili. Siku hiyo Dastan aliamka asubuhi na kuona mwili wake ukimuuma na pia alikuwa akisikia kizunguzungu. Akahisi kwamba alikuwa na malaria.



Alipomudu kuinuka kitandani ilikuwa saa tatu. Wakati anavaa baada ya kuoga, mwenzake alimpigia simu.



“Habari ya asubuhi Dastan?” Ali alimsalimia baada ya Dastan kupokea simu.



“Nzuri. Sikuamka vizuri leo, najisikia kuumwa”



“Oh nini zaidi?”



“Nahisi nina malaria, huenda nisifike kazini leo”



“Sasa nenda kapime, kama ni malaria upate matibabu”



“Nikitoka hapa nakwenda hospitali”



“Sawa. Utanijulisha itakavyokuwa”



Baada ya kuzungumza na Ali, Dastan alitoka akapanda pikipiki yake na kuelekea katika zahanati moja iliyokuwa barabara ya kwanza.



Aliegesha pikipiki nje akaingia ndani. Alisubiri watu wawili waliokuwa katika msitari wa kuingia katika chumba cha daktari. Watu hao waliposhughulikiwa akaingia.



Mshangao alioupata Dastan ulionekana wazi usoni kwake. Yule msichana aliyekuwa akimuwazia akilini mwake ndiye aliyekuwa daktari!



“Hujambo bibie?” akamsalimia.



“Sijambo, karibu ukae” Msichana akamkaribisha kisha akaongeza.



“Nakukumbuka fundi wangu wa laptop”



Dastan akatabasamu.



“Nafurahi kuwa umenikumbuka, sikujua kama wewe ni daktari”



“Mimi ni daktari na niko hapa. Una tatizo gain?”



Dastan akamueleza alivyojisikia.



“Inawezekana una malaria lakini nenda ukapime kwanza. Tunapimia chumba cha tatu. Baada ya kupima utarudi tena hapa”



“Sawa” Dastan alimjibu na kutoka.



Aliingia chumba cha tatu na kushughulikiwa tatizo lake. Kipimo chake kilionesha kuwa alikuwa na vidudu vine vya malaria. Baada ya kuandikiwa cheti alirudi tena katika chumba cha daktari.



“Hebu nione cheti chako” msichana alimwambia alipomuona akiingia.



Dastan alimpa cheti hicho kisha akaketi..



“Una vidudu vinne” Msichana alimwambia na kuongeza.



“Nitakuandikia dawa ambazo utatumia kwa siku tatu”



Msichana aliandika cheti kingine akamwambia Dastan.



“Jina lako tafadhali”



“Naitwa Dastan Seseko”



Itaendelea
 
SEHEMU YA 03


ILIPOISHIA



Dastan akamueleza alivyojisikia.



“Inawezekana una malaria lakini nenda ukapime kwanza. Tunapimia chumba cha tatu. Baada ya kupima utarudi tena hapa”



“Sawa” Dastan alimjibu na kutoka.



Aliingia chumba cha tatu na kushughulikiwa tatizo lake. Kipimo chake kilionesha kuwa alikuwa na vidudu vine vya malaria. Baada ya kuandikiwa cheti alirudi tena katika chumba cha daktari.



“Hebu nione cheti chako” msichana alimwambia alipomuona akiingia.



Dastan alimpa cheti hicho kisha akaketi..



“Una vidudu vinne” Msichana alimwambia na kuongeza.



“Nitakuandikia dawa ambazo utatumia kwa siku tatu”



Msichana aliandika cheti kingine akamwambia Dastan.



“Jina lako tafadhali”



“Naitwa Dastan Seseko”



SASA ENDELEA



Msichana alishaanza kuandika jina hilo akasita na kumtazama Dastan. Uso wake ulionesha kuwa kulikuwa na jambo lililomshitua.



“Unaitwa Dastan Seseko?” akamuuliza tena Dastan.



“Ndiyo, Dastan Seseko”



“Kuna jina jingine hapo katikati?”



“Ndiyo lipo. Ni Dastan Lwanzo Seseko”



“Wewe ni Mkongo?”



Dastan akatabasamu akiwa hajui ni kwanini mwenzie amemuuliza hivyo.



“Hapana. Mimi ni Mtanzania”



“Ulitokea katika kituo cha yatima cha Kange”



Dastan alipoulizwa swali hilo na yeye alishituka.



“Umejuaje?”



Msichana hakujibu. Macho yake yaliyokuwa yakimtazama Dastan kwa tashiwishi yalianza kutiririkwa na machozi.



Ilikuwa kama vile hakuelewa kuwa macho yake yalikuwa yakitiririka machozi. Alipohisi matone yakigusa mashavu yake aliyapangusa haraka kisha akaendelea kuandika.



Dastan alikuwa ameduwaa akimtazama. Baada ya msichana kumaliza kuandika aliinuka akatayarisha sindano.



“Njoo ulale hapa” alimwambia Dastan akimuelekeza kwenye kitanda cha wagonjwa kilichokuwa nyuma ya meza yake.



Dastan aliinuka akalegeza suruali na kuisega kwenye tako moja kisha akajilaza kifudifudi kwenye kitanda hicho.



Msichana alimpiga sindano. Alipomaliza alimwambia.



“Inuka”



Dastan alinyanyuka akaipandisha suruali yake kisha akarudi kwenye kiti.



Msichana alimtolea vipakiti vya dawa na kumpa maagizo ya jinsi ya kuzitumia kwa siku tatu.



“Itakuwa kiasi gani?” Dastan akamuuliza.



Msichana alimtajia gharama yake. Dastan akalipa.



“Dastan nitapenda kuwa na mazungumzo na wewe baada ya muda wangu wa kutoka kazini” Msichana akamwambia Dastan.



“Kuna maswali najiuliza, kwanini ulishituka nilipokutajia jina langu na kwanini ulitambua kuwa nilitoka katika kituo cha yatima?”



“Nina sababu. Niambie tutakutana wapi ili tuweze kuongea zaidi?”



“Sema wewe.



“Mimi nitatoka kazini saa kumi jioni, nikitoka hapa ninarudi nyumbani”



“Unaishi wapi?” Dastan alimuuliza ili kupata uhakika zaidi wa mahali anapoishi.



“Ninaishi eneo la Bombo?”



Dastan akamkubalia kwa kichwa kabla ya kumuuliza.



“Kama sikosei katika siku za hivi karibuni nimekuwa nikikuona pale Shangwe Hoteli nyakati za usiku, au sio wewe?”



“Ni mimi, huwa ninapenda kwenda kula chakula pale. Basi unaonaje kama tutakutana hapo saa moja usiku?”



“Itakuwa vizuri kwa sababu hata mimi ninakula chakula cha jioni pale Shangwe”



“Basi tukutane hapo. Tafadhali usikose kaka yangu



“Sitakosa”



Dastan akanyanyuka kwenye kiti. Akamuaga msichana huyo na kutoka.



Alirudi nyumbani kwake akameza tembe za dawa kama alivyoagizwa. Alipojiona alikuwa na nafuu kidogo alipanda pikipiki yake akaelekea kazini kwake.



Karibu njia nzima Dastan alikuwa akijiuliza yule msichana aliwezaje kumtambua na alikuwa na kitu gani alichotaka kumueleza.



Pia alijiuliza ni kitu gani kilichofanya atiririkwe na machozi alipomkubalia kuwa alitoka kituo cha yatima?



Upande mmoja wa akili yake ulikosa imani. Alijiambia huenda msichana huyo hutumia mazingaombwe kuwalaghai wanaume na kwenda kuwaua nyumbani kwake.



Hata hivyo alijiammbia ni vizuri akutane naye na ajue atamueleza nini. Kama kutakuwa na suala la kwenda nyumbani kwake, Ddatan alijiambia, hatakwenda.



Sasa aligundua ni kwanini laptop ya msichana huyo ilikuwa ina maelezo ya kidaktari pamoja na picha za viungo vya binaadamu.



Alipofika kazini kwake Dastan alikutana na fundi mwenzake.



“Hali yako inaendeleaje?” Ali akamuuliza Dastan.



“Kidogo najisikia vizuri, ndio maana nimeweza kuja huku”



“Ulikwenda hospitali”



“Nimekwenda, imegundulika ni malaria”



“kwa hiyo umepata tiba?”



“Ndiyo iliyonisaidia kuweza kuja hapa”



“Siku hizi malaria ni nyingi sana. Inatakiwa tutumie vyandarua vyenye dawa”



“Unaweza kutumia na kuna siku utaumwa tu”



“Unajua si lazima mbu akung’ate kitandani, anaweza kukung’ta ukiwa mahali pengine”



Dastan akaanza kazi zake huku mawazo yake bado yakiwa kwa yule msichana. Alitaka kumueleza mwenzake lakini aliona ilikuwa mapema mno. Habari ya msichana akabaki nayo mwenyewe.



Saa kumi na moja jioni baada ya kufunga ofisi yao alirudi nyumbani. Alipumzika hadi saa kumi na mbili jioni. Akaenda kuoga. Baada ya kuoga alivaa nguo nyingine.



Ilkuwa saa moja kasoro dakika arobaini alipoondoka nyumbani kwake kuelekea Shangwe Hotel.



Wakati anaigesha pikipiki yake mbele ya hoteli hiyo, aliliona gari la yule msichana ambalo alikuwa amelikariri.



Gari hilo lilikuwa katika eneo la kuegesha magari. Akahisi msichana mwenyewe alikuwemo ndani.



Alipoingia ndani ya hoteli alimkuta msichana huyo ameketi katika meza iliyokuwa karibu na eneo la mlango.



Akamfuata.



“Nimekaa hapa karibu na mlango ili uweze kuniona kirahisi utakapofika” msichana akamwambia Dastan kisha akamalizia.



“Karibu ukae”



Dasta alivuta kiti na kukaa.



“Unajisikiaje?” Msichana akamuuliza Dastan.



“Ninajisikia vizuri kidogo, nimeweza hata kwenda kazini”



“Natumaini mpaka kesho utajisikia vizuri sana”



“Nitashukuru sana”



“Utakula nini?”



“Kwani wewe mwenzangu umeagiza nini?”



“Sijaagiza kitu, nimefika sasa hivi tu”



“Huwa mara nyingi nakula nyama choma na ugali au ndizi”



“Basi tuagize nyama choma na ndizi”



“Sawa”



Msichana alimuita mhudumu akamuagiza chakula walichohitaji. Mhudumu alipoondoka msichana alimuuliza Dastan.



“Uliondoka lini katika kituo cha yatima cha Kange?”



“Karibu miaka tisa iliyopita”



“Ulisomea wapi ufundi wa kompyuta?”



“Nilisoma Veta”



“Hivi sasa unaishi wapi?”



“Ninaishi Chumbageni”



“Maisha yanakwendaje?”



“Kwa kweli yanakwenda vizuri”



“Uliwahi kuelezwa historia ni kwanini wewe umekuwa katika kituo kile cha kulelea yatima?”



“Nilielezwa. Kwa kweli ni historia ya kuhuzunisha”



Dastan akamueleza historia yake. Alimwambia yeye na mdogo wake wa kike walifikishwa katika kituo hicho wakiwa wadogo sana.



Dastan aliambiwa alifikishwa katika kituo hicho akiwa na umri uliokadiriwa kuwa miaka mitano na mdogo wake akiwa na umri wa miaka mitatu.



Aliyewapeleka katika kituo hicho ni afisa ustawi wa jamii ambaye aliwaeleza viongozi wa kituo hicho kuwa mwanamke aliyekuwa na watoto hao alifariki dunia kwa ajali ya gari.



ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 04


ILIPOISHIA



“Ulisomea wapi ufundi wa kompyuta?”



“Nilisoma Veta”



“Hivi sasa unaishi wapi?”



“Ninaishi Chumbageni”



“Maisha yanakwendaje?”



“Kwa kweli yanakwenda vizuri”



“Uliwahi kuelezwa historia ni kwanini wewe umekuwa katika kituo kile cha kulelea yatima?”



“Nilielezwa. Kwa kweli ni historia ya kuhuzunisha”



Dastan akamueleza historia yake. Alimwambia yeye na mdogo wake wa kike walifikishwa katika kituo hicho wakiwa wadogo sana.



Dastan aliambiwa alifikishwa katika kituo hicho akiwa na umri uliokadiriwa kuwa miaka mitano na mdogo wake akiwa na umri wa miaka mitatu.



Aliyewapeleka katika kituo hicho ni afisa ustawi wa jamii ambaye aliwaeleza viongozi wa kituo hicho kuwa mwanamke aliyekuwa na watoto hao alifariki dunia kwa ajali ya gari.



SASA ENDELEA



Aliwaeleza kwamba mwanamke huyo akiwa na watoto hao walishuka kutoka katika basi lililotoka Nairobi nchini Kenya na walipanda teksi ambayo ilipata ajali ya kugongwa na lori.



Mwanamke huyo na watoto hao walikimbizwa hospitalini lakini saa chache baadaye mwanamke huyo alifariki dunia.



Kabla ya kufa aliwahi kutoa maelezo kuhusu mahali alikokuwa akitoka na watoto hao. Alisema yeye alikuwa Mtanzania na watoto hao alikuwa akiwalea huko Nairobi akiwa mfanyakazi wa ndani kwa mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la James Omondi



Alisema watoto hao alipewa na mtu huyo awalee na kuwafanya kama watoto wake.



Aliwatajia majina ya watoto hao. Mtoto wa kiume alikuwa Dastan lwanzo Seseko na wa kike Hilda Lwanzo Seseko.



Juhudi za maafisa wa ustawi wa jamii kumpata James Omondi kutoka Nairobi ili atoe maelezo kuhusu watoto hao zilishindikana na hivyo watoto hao wakapelekwa kituo cha kulelea yatima kilichoko Kange nje kidogo ya jiji la Tanga.



“Kwa hiyo baada ya wewe kuondoka katika kituo hicho, mdogo wako yuko wapi?” Msichana huyo akamuuliza Dastan.



“Mdogo wangu tulitengana tangu tukiwa wadogo na sijamuona tena” Dastan alimwambia.



“Mlitengana vipi?”



“Niliambiwa kuwa miezi michache tu baada ya kufikishwa katika kituo kile, mdogo wangu alichukuliwa na tajiri mmoja kwa nia ya kwenda kumlea na kumpatia elimu. Na atakuwa amekulia huko huko na kwa sasa si rahisi kumjua tena”



“Lakini bila shaka utakuwa una hamu ya kumuona mdogo wako?”



“Lazima. Si najua mtu ni ndugu yake”



“Nafurahi kukufahamisha kuwa mimi ndiye mdogo wako Hilda Lwanzo Seseko”



Mwili wa Dastan ulisisimka, akamkazia macho msichana huyo kama vile ndio kwanza alikuwa anamuona.



“Wewe ni Hilda?” akamuuliza kwa mshangao.



Msichana alifungua pochi yake akatoa kitambulisho chake na kumpa Dastan.



Dastan alikitazama na kuiona picha ya msichana pamoja na jina lake Hilda Seseko.



Akajikuta akiinuka kwenye kiti na kumfuata msichana huyo akiwa ameichanua mikono yake. Msichana akasimama, wakakumbatiana.



Baada ya hapo Dastan alirudi kwenye kiti.



“Kilichonitambulisha ni pale hospitali uliponitajia jina lako” Msichana alimwambia.



“Sasa ulinijuaje wakati ulichukuliwa ukiwa mdogo?”



“Ni hivi karibuni tu nilipogundua. Wale watu walionilea ndio niliokuwa nikijua ni wazazi wangu. Walinichukua mimi kwa sababu hawakujaliwa kupata mtoto. Baba alitangulia kufariki akabaki mama. Mama naye akapata ugonjwa wa moyo



“Siku chache kabla ya mama kufa akaniammbia kuwa wao hawakuwa wazazi wangu halisi bali ni wazazi wa kunilea tu, akanipa historia yote. Kule walikonichukua waliambiwa kuwa nilikuwa na ndugu yangu wa kiume anaitwa Dastan Lwanzo Seseko. Hapo ndipo nilipokujua”



“Sawa. Kwa hiyo wazazi waliokulea wote wameshafariki?”



“Mama alikufa mwaka jana wakati tayari nimeshaanza kazi ya udakatari. Baba alikufa wakati nikiwa chuo nikisomea udaktari”



“Sasa kwanini hukurudi tena kwenye kituo kuniulizia kaka yako?”



“Kilichotokea ni kwammba wale wazazi wangu walinificha wakati wote kuniambia ukweli huo. Mimi nilijua wao ndio wazazi wangu. Kwa hiyo sikujua kama nilikuwa na ndugu huko hadi mama aliponifichulia”



“Na alipokufichulia kwanini hukuja kuniulizia?”



“Kwanza mama aliponieleza nililia sana. Halafu nilikuja katika kile kituo kukuulizia. Kumbukumbu zikaonesha kwamba kweli nilitoka katika kituo kile, lakini wewe ulikuwa umeshaondoka na haawakujua uko wapi”



Dastan na msichana huyo waliletewa chakula walichokuwa wameagiza wakaosha mikono na kuanza kula.



“Mimi baada ya kumaliza masomo ya Veta nilifungua duka langu la ufundi wa kompyuta pale barabara ya nane nikishirikiana na mwenzangu ambaye ulinikuta naye siku ile” Dastan akamwambia msichana huyo.



“Nilikuwa nikikuwaza sana. Nilikuwa sijui kaka yangu unaishi maisha gain. Leo hii najisikia kuwa na furaha isiyo kifani”



“Uliniambia unaishi eneo la Bombo, ile nyumba unayoishi ni ya nani?”



“Ni yangu. Niliirithi kwa wale wazee walionilea, hawakuwa na mtoto mwingine wa kuwarithi. Tukitoka hapa tutakwenda nyumbani kwangu ukapaone”



Lile tukio la siku ile la yule mtu aliyeuawa na Hilda bado lilikuwa likizunguka akilini kwa Dastan.



“Kuna kitu kimoja nataka kukuuliza Hilda”



“Kitu gani?”



“Kuna siku moja ulikuja hapa hoteli mida kama hii halafu nilikuona wewe ukiondoka na jamaa mmoja. Mimi niliwafuatilia kwa pikipiki yangu. Niliwaona mkiingia katika nyumba moja katika eneo la Bombo, baadaye nikaona unamburuza yule mtu na kumpakia kwenye buti ya gari na kwenda kumuacha katika eneo la makaburi nyuma ya ule mtaa”



Msichana akagutuka.



“Kumbe uliona?”



“Nilikuona na nilipata hofu sana”



Msichana alinyamaza kimya kwa sekunde kadhaa kisha alisema.



“Yule mtu nilikutana naye kwa mara ya kwanza katika eneo la stendi. Alionesha kama alitaka tuwe marafiki. Lakini kadiri nilivyomzoea nilianza kugundua hakuwa mtu mwema na pia niligundua alikuwa anatoka Kenya.



“Kuna siku aliniambia dhamira yake. Aliniambia wazi kuwa alikuwa anamtafuta Dastan Lwanzo Seseko wakati tayari nilishaambiwa kuwa kuna kaka yangu anaitwa Dastan Lwanzo Seseko ambaye sijui aliko.



“Siku ile alikuwa amelewa na alinieleza kinaganaga kwamba anamtafuta Dastan amuue na kwamba alitumwa kutoka Nairobi na tajiri mmoja anayeitwa James Omondi.



“Aliniambia yeye ni Mkenya lakini ameshafika mara kadhaa hapa Tanzania na si mgeni wa jiji la Tanga. Nikamuuliza ni kwanini huyo Omondi amekutuma umuue huyo mtu, akanieleza kisa kirefu. Nisikilize kwa makini kaka yangu.



“Aliniambia alivyosikia kutoka kwa baadhi ya watu wanaomjua Omondi, mali aliyokuwa nayo Omondi si yake. Ni mali aliyotakiwa awarithishe Dastan na mdogo wake wa kike watakapofikia umri wa miaka kumi na minane.



“Lakini yeye aliwaondoa kwa hila Dastan na mdogo wake kutoka Nairobi na kuwapeleka Tanzania walelewe huko ili wakiwa wakubwa wasijue kuwa kuna mali wanayotakiwa kurithishwa.



“Hivi karibuni Omondi alipata habari kuwa Dastan ambaye ni wewe uko Tanga na wakati wowote unaweza kwenda Nairobi kudai hizo mali. Hapo ndipo Omondi alipotuma mtu kutoka Nairobi aje akuue.



“Ingawa wakati ule nilikuwa sijui uko wapi lakini baada ya kunieleza zile habari ndipo nilipomchukua nyumbani kwangu. Nilimpiga na chupa kichwani ili nimuue yeye kabla ya kuja kukuua wewe, kwa vile nilishajua kwamba wewe ni ndugu yangu na nilikuwa na tamaa kwamba iko siku tungeweza kukutana”



Hapo nikashusha pumzi ndefu.



Kumbe mimi ndiye niliyetakiwa kuuawa!



Kumbe Hilda alimuua mtu yule ili kuniokoa mimi!



Nilikuwa namtuhumu kwamba ni msichana muuaji kumbe sivyo!

Dastan alikuwa akiwaza akilini mwake.



“Sasa nimekuelewa vizuri. Lakini nikwambie licha ya kutojua kwamba wewe ni damu yangu sikumueleza mtu yeyote kuhusu tukio lile, nilinyamaza kimya” Nikamwambia Hilda.



“Ni kwa sababu ya damu. Damu nzito kuliko maji”



“Ni kweli. Sasa kuna swali nimekuwa nikijiuliza. Huyo Omondi ni nani. Mimi pia nilielezwa kwamba huyo mama aliyetuleta hapa Tanzania alikuwa mfanyakazi wa nyumbani kwa Omondi na yeye ndiye aliyetutoa sisi tuje huku tulelewe na huyo mama. Halafu kumbe ametuma mtu aje aniue”



“Bahati nzuri yule mtu aliingia mikononi mwangu”



“Nashukuru sana kwa kuokoa maisha yangu. Pengine angenigundua na angeniua. Huyo mtu atakuwa ni jambazi”



“Zake zimeshakwisha. Nimekuwa nikijiuliza hizo mali alizonazo Omondi zinatuhusu vipi sisi”



“Mimi nashukuru kuwa tumekutana na tumejuana. Tunayo sababu sasa ya kutafuta asili yetu, kuwajua wazazi wetu na kumjua huyu Omondi pamoja na hizo mali”



“Ukiangalia hili jina la Lwanzo Seseko ambalo bila shaka ni la baba yetu, asili yake ni Congo. Bila shaka wazazi wetu ni watu wa Congo”



“Lakini tunaelezwa kuwa tulitokea Nairobi tukiwa wadogo. Omondi naye yuko Nairobi. Katika historia yetu fupi, lwanzo Seseko hatajwi, anatajwa Omondi. Kuna haja ya kuanza kufanya utafiti”



Walikuwa wameshamaliza kula. Waliosha mikono. Hilda akalipa bili yote kisha wakatoka.



“Twende nyumbani” Hilda alimwambia Dastan akiwa amehamasika.



“Ile nyumba yako ninaifahamu. Panda gari yako, mimi nakuja na pikipiki”



“Sawa”



Hilda alikwenda kujipakia kwenye gari lake na Dastan alipanda pikipiki, wakaondoka.





ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 05


ILIPOISHIA



Gari la Hilda ndilo lililotangulia. Walikwenda hadi eneo la bombo. Msichana akasimamamisha gari katika nyumba ile ile ambayo Dastan alikuwa akiifahamu.



Dastan naye alisimamisha pikipiki nyuma ya gari hilo. Alitreremka kwenye pikipiki. Wakati huo Hilda alikuwa ameshashuka akifungua mlango.



“karibu kaka. Hapa ndio nyumbani kwangu” alimwambia Dastan na kufungua mlango.



Dastan alitangulia kuingia kisha akaingia Hilda na kufunga mlango.



Walitokea katika sebule pana ya kupendeza.



“Karibu ukae” Hilda alimwambia Dastan ambaye alichagua kochi mojawapo akaketi.



“Nikupatie kinywaji gani?”



SASA ENDELEA



“Dakika chache tu zilizopita tumekula na tumekunywa. Kwa kweli sihitaji kinywaji kwa sasa” Dastan alimwambia Hilda.



“Basi nisubiri kidogo”



Hilda alitoka katika mlango wa sebule akaingia katika chumba kimoja wapo. Baada ya muda kidogo alitoka na kwenda kuketi sebuleni.



“Unaishi na nani humu ndani?” Dastan akamuuliza.



“Ninaishi na mlinzi wangu. Mlinzi wangu pia anaishi hapa hapa, nimempa nyumba ya uani anakaa na mke wake”



“Hii ndio nyumba ambayo uliishi ulipochukuliwa na walezi wako?”



“Ndiyo, niliishi hapa. Nikasoma nikiwa hapa mpaka walezi wangu wakafariki, wakaniachia nyumba. Sasa imekuwa ni yangu”



“Umepata bahati sana Hilda. Inakupasa uwashukuru sana hao watu. Wana moyo wa ubinaadamu kweli”



“Kwa kweli nawashukuru sana. Hivi kaka yangu sijakuuliza, umeshaoa?”



“Bado”



“Unangoja nini?”



“Ndio niko kwenye mipango ya kutafuta mchumba”



“Mbona wasichana wako wengi sana, sema hujapata uliyempenda”



“Ni sawa. Sijapata yule ambaye analingana na mimi”



“Sasa kaka, nashukuru kuwa tumekutana na kujuana. Mimi nilikuwa na wazo moja”



“Wazo gani?”



“Wazo la kwenda Nairobi kuitafuta asili yetu. Inavyoonekana yule mama aliyekuja na sisi, alikuja kutulea. Alivyofariki ndio ikabidi tupelekwe katika kituo cha yatima. Kutokana na maelezo ya yule mtu niliyemuua inaonekana kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia”



“Ni wazo zuri. Kitu ambacho ninakiwaza sana ni huyo mtu aliyetumwa aniue ili nisiende Nairobi kurithi mali kwa Omondi”



“Sasa hayo yote tutayajua huko huko”



“Ninakubaliana na wazo lako. Tujiandae kwa safari ya Nairobi”



*************





Yapata miaka ishirini na minane iliyopita Lwanzo Seseko aliwasili katika jiji la Nairobi akitokea Congo DRC. Aliondoka kwao baada ya kijiji chao kuvamiwa na waasi wa serikali ya Congo. Nyumba zao zilichomwa moto na watu wengi waliuawa kwa kupigwa risasi.



Lwanzo aliyekuwa amelala chumbani mwake alisikia vurugu na milio ya risasi, alipotoka nje alimshuhudia baba yake na mama yake wakipigwa risasi na kufa hapo hapo.



Kijiji kizima kilikuwa kimeenea vurugu huku nyumba zikiungua moto. Lwanzo alirudi ndani akavunja ua na kupata nafasi ya kukimbia.



Katika safari yake ya kwenda Nairobi alikuwa na wenzake watatu ambao wote walikufa njiani, akabaki peke yake.



Mtu wa kwanza aliyekutana naye katika jiji la Nairobi alikuwa mkamba mmoja aliyeitwa Omondi.



Omondi alikuwa akifanya kazi katika duka la mfanya biashara mmoja mwenye asili ya Asia. Kazi yake ilikuwa ni kutoa vitu vilivyonunuliwa kutoka stoo.



Omondi alimwammbia Lwanzo kwamba tajiri yake alikuwa anataka kuongeza mfanyakazi mmoja wa duka.



Lwanzo akakubali kupelekwa kwa mfanyabiashara huyo kuanza kazi hiyo ya duka.



Alipokubaliwa akaanza kazi hiyo akiwa na wafanyakazi wenzake wasiopungua watatu.



Lilikuwa duka kubwa la vifaa vya ujenzi na umeme lililokuwa katikati ya jiji la Nairobi.



Lwanzo alikuwa akilala kwenye vibanda vya masikini nje kidogo ya jiji la Nairobi eneo wa Kibera ambako kunasadika kuwa na vurugu mara kwa mara. Alikuwa akitembea kwa miguu mwendo wa karibu kilometa saba kila siku kwenda na kurudi kazini kwake.



Ili kuwahi kazini, Lwanzo alikuwa akiamka saa kumi na moja alfajiri na kuanza safari ya miguu kuelekea Nairobi. Riziki aliyokuwa anaitia tumboni mwake asubuhi ni kikombe cha kahawa na kashata.



Mchana hula kipande cha muhogo wa kuchoma na masala na jioni huenda kupika mwenyewe ugali na kauzu wa kuchemsha.



Alifanya kazi katika duka hilo kwa miaka miwili. Lwanzo hakuwa akijua kuwa Muhindi waliyekuwa wakimuuzia duka alikuwa ni mfanya magendo mkubwa. Alikuwa akisafirisha meno ya tembo nje ya nchi na biashara hiyo ndiyo iliyompa utajiri mkubwa.



Fedha alizokuwa akipata kutokana na biashara hizo ni dola za Kimarekani ambazo kwa sababu ya kuhofia kugundulika kutakatisha pesa hakuwa akiziweka benki.



Alikuwa akizitunza kwenye boksi lililokuwa ofisini kwake.



Kulikuwa na siku moja shehena yake ya meno ya tembo ilikamatwa nchini China. Polisi wa INTERPOL wakafahamishwa kuwa mwenye mzigo huo ni wa mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia aliyeko Nairobi.



Wapambe wa Muhindi huyo walioko China walimpigia simu kumjulisha juu ya kukamatwa kwa mzigo wake na wakamwambia kuwa huenda saa chache zijazo akakamatwa huko huko.



Baada ya polisi wa INTERPOL kupata jina na anuani yake waliwasiliana na wenzao walioko Nairobi. Saa chache tu baada ya taarifa hiyo kuwasili Nairobi, makacherro sita wa Kenya walivamia duka lake.



Wakati makachero hao wanawasili, mfanyabiashara huyo ndio alikuwa anamaliza kuongea na mpambe wake aliyekuwa China. Alipowaona makachero hao akajua kuwa amefuatwa kukamatwa.



Katika vitu vilivyokuwa vikimpa mashaka ni boksi lenye dola lililokuwa ofisini kwake. Alijua kama dola hizo zitaonekana atashindwa kuzitolea maelezo na hivyo kumuweka mahali pabaya.



Kitu cha kwanza alichofanya ni kumtuma Lwanzo ofisini kwake atoe lile boksi na kwenda kulitia kwenye pipa la takataka.



Wakati lwanzo analitoa boksi hilo hakujua lilikuwa na nini. Alipishana na makachero hao kwenye mlango wa duka akatoka nje na kwenda kulitia kwenye pipa la takataka.



Lakini wakati analitia kwenye pipa la takataka, boksi hilo lilifunguka. Aliona kulikuwa na mfuko wa nailoni kwa ndani. Akataka kujua kilichokuwamo.



Alipoushikashika mfuko huo aligundua kulikuwa na kitu kama vibunda vya noti.



Mara moja aliutoboa na akaona vitita vya dola za Kimarekani. Alitazama kila upande wa barabara. Hakukuwa na watu waliokuwa wakimtazama. lakini hakuweza kuzichukua pesa hizo hapo hapo.



Alishuku kwamba tajiri yake alimwambia alitie hilo boksi ndani ya pipa la takataka kwa kuwahofia wale makachero walioingia dukani hapo.



Lwanzo alichungulia dukani akaona tajiri yake alikuwa anahojiwa, wakati huo huo gari la taka lilikuwa linapita Alikwenda kulifungafunga vizuri lile boksi kabla ya wafanyakazi wa gari la taka kulichukua pipa hilo na kumiminia taka ndani ya gari.



Gari likaoondoka. Lwanzo alifikiria zile pesa, akaona bora afe nazo. Akaanza kulifuata lile gari. Aliendelea kulifuata katika mtaa mmoja hadi mwingine. Gari liliposimama na yeye alisimama kulisubiri, lilipoondoka aliendelea kulifuata.



Gari hilo lilipojaza mzigo wa taka likaanza safari ya kuelekea mahali ambako taka hizo zilikuwa zinatupwa. Alikuwa akipafahamu kwani ndiko huko huko alikokuwa naishi.



Akapanda matatu (daladala za Kenya) kulifuatilia gari hilo. Wakati anafika katika eneo hilo alikuta gari hilo likimimina taka hizo. Kulikuwa na watu ambao walikuwa wakisubiri taka zimwagwe ili waanze kuchakua kutafuta vitu vya kwenda kuuza.



Maboksi yalikuwa mengi. lwanzo akawa makini na lile boksi lililokuwa na pesa. Alindelea kuchakua kulitafuta hadi alipoliona. Akalichukua na kuondoka nalo.



Kibanda alichokuwa anaishi hakikuwa mbali na mahali hapo. Alikwenda katika kibandani kwake akajifungia chumbani na kuutoa mfuko wenye dola za Kimarekani uliokuwa ndani ya boksi hilo.



Ule msemo wa kulala masikini na kuamka tajiri ukatimia kwa Lwanzo.





Siku ile alikutana na Omondi usiku. Omondi akamuuliza.



“Kwanini uliondoka kazini mchana?”



“Nilikimbia nilipoona polisi wameingia”



“Kumbe wewe muoga sana?”



“Niambie mlisalimika?”





Itaendelea
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi @Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad @Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya Lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO @multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij @addenbwii ONTARIO Kobe The Vein mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya SITAKI ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo @shedede kamtu33 SteveMollel Ngushi DONALD stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 Ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny @Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90 Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero agprogrammer JoJiPoJi @Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga ABB SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe salaniatz Natasha Ismail jiwe jeusi chibalangunamchezo
John Mloy conjuget Van Pauser great G Mtoto wa nzi Zeus1 hindustan Sci-Fi MAN OF PEACE kashata emnly danny baraka bb MTOTELA kbosho TEMLO DA VINCA Madame B
 
Hahaha unataka tusome au nasi tuandike? au tukubishie kwamba sio kisa cha kweli?
 
SEHEMU YA 07



ILIPOISHIA



“Patel amekamatwa. Anatumiwa kusafirisha meno ya tembo nchi za nje”



“Kumbe yule bwana anafanya magendo ya meno ya tembo?”



“Nilikuwa nikisikia hivyo lakini leo ndio nimethibitisha”



“Sasa kesho mtakwenda kazini?”



“Tutakwenda. Kama duka halitafunguliwa tutarudi”



“Mimi sitaki kazi tena, nitatafuta mahali pengine. Kama tajiri mwenyewe ameshakamatwa sidhani kama tutakuwa na ajira tena”



Lwanzo akawa amejiachisha kazi. Miezi michache baadaye akasikia kwamba tajiri yao huyo aliyekamatwa alihukumiwa na mahakama kifungo cha miaka kumi na mitano jela.



Wakati huo alikuwa bado ameficha zile dola. Baada ya hapo ndipo alipoanza kuzitumia.



Kwanza alinunua mashamba ya mirungi huko Meru kisha akanunua magari mawili ya kusafirishia mihadharati hiyo kutoka Meru hadi jijini Nairobi na Mombasa.



SASA ENDELEA



Biashara hii ilimuinua mara moja. akanunua hoteli mbili. Alifungua maduka karibu kumi ya vifaa vya ujenzi na alinunua mabasi madogo ishirini aliyoyafanya daladala.



Mwenyewe alinunua nyumba ya kifahari ya ghorofa moja aliyokuwa akiishi. Pia alinunua gari la heshima la kutembelea.



Hakumsahau mwenyeji wake Omondi. Alimuachia zile daladala ishirini azisimamie yeye. Lwanzo alikuwa akichukua hesabu tu kutoka kwa Omondi.



Maisha ya Lwanzo yakawa yamebadilika sana. Alipokuja Nairobi kutoka Congo alikuwa mtu asiyefahamika. Lakini baada ya kupata utajiri akawa maarufu na kufahamika na wengi.



Omondi alipokuwa ameajiriwa kwa tajiri wa kihindi maisha yake yalikuwa duni thamani. Alipopatiwa kazi ya kusimamia magari ya Lwanzo na yeye aliinuka na kuonekana mtu miongoni mwa watu.



Aliweza kujenga nyumba yake mwenyewe na kuwapeleka watoto wake katika shule za maana. Alimshukuru sana Lwanzo kwa kuweza kuyabadili maisha yake.



Siku moja Lwanzo alikuwa akipita na gari lake katika barabara moja jijini Nairobi. Alimkosakosa msichana mmoja aliyekuwa anavuka barabara bila kutazama magari. Alifanikiwa kumkwepa lakini pikipiki ikamkumba msichana huyo na kumtupa chini.



Mguu wake ukawa unavuja damu. Mwenye pikipiki hakutaka taabu na trafiki wa Nairobi. Alijua fika kwamba kosa halikuwa lake lakini trafiki wangembana yeye ili atoe pesa, akaamua kukimbia.



Kutokana na ubinaadamu wake Lwanzo alifunga breki akasimamisha gari. Alimfuata yule msichana ambaye bado alikuwa amelala chini akigwayagwaya , akamuuliza.



“Umeumia sana?”



“Mguu wangu unatoka damu” msichana alisema akiwa ameushikilia mguu wake.



“Inuka nikupeleke hospitali”



Msichana alijaribu kuinuka. Aliposhindwa Lwanzo alimsaidia kumuinua.



Akamkokota kuelekea lilipokuwa gari lake, akampakia na kwenda naye hospitali ya pesa.



Mguu wa msichana huyo ulipigwa picha na kugundulika kuwa ulikuwa umetenguka ukawekwa sawa na kuvalishwa plasta ngumu.



Pale palipokuwa na jeraha lililokuwa linavuja damu palisafishwa na kuwekwa plasta. Gharama zote alizilipia Lwanzo.



“Unaishi wapi nikupeleke?” Lwanzo akamuuliza wakati akimpakia tena kwenye gari.



“Pale nilipogongwa nilikuwa ninakwenda mahakamani lakini sasa nimeshachelewa”



“Ulikuwa na kesi?”



“Ndiyo nilikuwa na kesi na tarehe yake ilikuwa ni leo”



“Sasa acha nikufikishe mahakamani ili utoe taarifa kuwa ulipata ajali, vinginevyo unaweza kukabiliwa na kesi nyingine ya kudharau mahakama”



“Sawa. Nipeleke”



Wakati Lwanzo akimpeleka msichana huyo mahakamani alimuuliza.



“Umeshitakiwa kwa kosa gani?”



“Kosa la kuonewa tu na mwanaume. Amekwenda kunishitaki kuwa nilimuibia pesa zake shilinhgi laki tano (sawa na milioni kumi za Tanzania) wakati haikuwa kweli. Nilikamatwa kwa kudhalilishwa nikawekwa ndani siku mbili, siku ya tatu nikapelekwa mahakamani. Ndipo nikapatiwa dhamana”



“Huyo mtu aliyekushitaki ni nani?”



“Mjinga mmoja. Alikuwa mchumba wangu halafu nikajakumfumania na rafiki yangu wa chanda na pete nikavunja uchumba. Sasa hicho ndicho kilichomuudhi. Yule msichana anaendelea naye mpaka leo na mimi simtaki tena



“Alisema ulimuibia wapi pesa hizo?’



“Kwanza alishaniambia kuwa atanikomoa. Kuna siku nilikwenda nyumbani kwake kuchukua nguo zangu zilizokuwa kwake, yeye hakuwepo lakini mwanamke wake alikuwepo, tukagombana sana. Kwa vile mwenyewe hakuwepo sikuchukua kitu lakini siku ya pili yake akaniletea polisi nyumbani kwangu akidai kuwa nilimuibia shilingi laki tano. Yaani lengo lake anifunge”



“Huyo jamaa ni mpumbavu, akishakufunga atapata faida gani?”



“Si bado ananitaka na mimi simtaki tena. Sasa anataka kunikomoa”



“Huyo rafiki yako bado anaendelea naye?”



“Bado yuko naye”



“Abaki na huyo, kwanini anataka kukukomoa wewe?”



“Ni mwanaume mjinga na mpumbavu, yaani najuta kumfahamu. Yeye ndio amesababisha nigongwe na pikipiki kwa sababu nina uchungu mpaka sijielewi”



“Tulia. Nitakusaidia”



Msichana huyo aliposikia kauli hiyo ya Lwambo aliugeuza uso wake akamtazama usoni.



“Utanisaidiaje kakaangu?” akamuuliza.



“Nitakuwekea wakili”



“Wakili atakuwa na gharama kubwa”



“Ninajua”



Msichana akanyamaza kimya.



Lwanzo alimfikisha mahakamani. Alishuka naye kwenye gari na kuingia naye kwenye jengo la mahakama. Msichana akajitambulisha kwa makarani wa mahakama. Akaambiwa kwamba kesi yake imeahirishwa tena hadi kesho yake.



“Mdhamini wako ametakiwa hadi kesho akufikishe mahakamani vinginevyo atakabiliwa na adhabu” Msichana huyo aliambiwa.



“Nilipata ajali wakati nakuja mahakamani. Mnaona mguu wangu huu, ndio kwanza natoka hospitalini”



“Umefanya vizuri kuwahi kuja kutupa taarifa. Hakimu ameandika kuwa umedharau mahakama. Hilo ni kosa jingine. Sasa njoo kesho, kesi yako itaendelea”



“Sawa. Nnitakuja kesho”



Lwanzo akatoka na msichana huyo na kumpakia kwenye gari lake.



“Sasa twende tukamuone mwanasheria” Lwanzo akamwambia msichana huyo mara tu alipoliwasha gari.



“Asante kaka yangu”



Wakati gari likiwa kwenye mwendo Lwanzo alimuuliza msichana huyo.



“Hatujajuana vizuri, mimi naitwa Lwanzo Sseseko, wewe unaitwa nani?”



“Mimi naitwa Herieth, natokea Kiambu”



“Ndugu zako wako wapi?”



“Sitaki nikufiche, mimi sina ndugu yeyote hapa Nairobi. Nilikuwa na rafiki tu na ndiye huyo aliyenisaliti”



“Una maana kwamba ndugu zako wako Kiambu?”



“Huko pia karibu ndugu wote walishakufa. Wazazi wangu ndio sikuwajua kabisa. Walikufa nikiwa mdogo sana”



Pole sana. Ulikuja lini hapa Nairobi?”



“Kama miaka mitatu iliyopita. Na kilichonileta hapa ni kutafuta kazi. Ndiyo nikakutana na huyo rafiki yangu aliyenitafutia kazi ya baa”



Lwanzo aligeuza uso wake haraka akamtazama msichana huyo.



“Unafanya kazi baa?” akamuuliza.



“Ndiyo, nilikuwa nafanya baa hata huyo rafiki yangu anafanya hapo hapo”



“Mbona unasema ulikuwa, una maana hivi sasa hifanyi tena”



“Nimeacha baada ya huyo rafiki yangu kumchukua mchumba wangu. Hatuwezi kufanya kazi pamoja kwa sababu tumeshakuwa maadui”



“Kwa hiyo hivi sasa umeacha?”



“Nimeacha lakini natafuta mahali pengine. Siwezi kuacha kabisa. Kodi ya chumba nitalipa na nini. Mwanaume niliyekuwa nikimtegemea amechukuliwa na rafiki yangu”



itaendelea
 
SEHEMU YA 08


ILIPOISHIA



Lwanzo akanyamaza kimya. Dakika chache tu baadaye akalisimamisha gari mbele ya jengo lililokuwa na ofisi ya wakili wake.



“Tushuke, tumeshafika” Alimwambia Herieth huku akifungua mlango.



Herieth naye alishuka. Ilibidi Lwanzo amshike mkono ili aweze kutembea vizuri.



“Itabidi nikununulie magwato ya kutembelea”



“Nitashukuru”



Waliingia katika ofisi ya mwanasheria huyo ambaye aliwakaribisha kwenye viti.



“Oh bwana Lwanzo. Karibuni mkae”



Lwanzo na msichana huyo waliketi kwenye viti.



“Habari za mtokako?” Mwanasheria huyo akawauliza.



“Si nzuri sana. Nina tatizo. Ninahitaji msaaada wako” Lwanzo alimwambia.



“Una tatizo gani?”



SASA ENDELEA



Lwanzo alimueleza kuhusu tatizo la Herieth la kesi iliyokuwa inamkabili.



“Lakini mwenyewe atakueleza kwa undani zaidi. Herieth hebu eleza hilo tatizo likoje” Lwanzo akamwambia Herieth.



Herieth akaeleza kuhusu uhusiano wake na mwanaume aliyemtaja kwa jina la Njoroge. Akaeleza jinsi rafiki yake wa karibu alivyomsaliti na kumchukua mwanaume wake jambo lililosababisha avunje uchumba wake na mwanaume huyo.



“Yule mwanaume alitaka niendelee kuwa naye huku akiendelea kutembea na rafiki yangu. Hilo sikulikubali. Nikaamua tuvunje uchumba, lakini yule bwana aliendelea kuning’ang’ania”



Herieth aliendelea kueleza jinsi mwanaume huyo alivyombambikia kesi ya wizi wa shilingi laki tano ili amkomoe.



“Ninaamini polisi waliipokea ile kesi kwa misingi ya rushwa tu” akasema kwa hasira.



“Ana ushahidi gani kwamba ulimuibia hizo pesa?” wakili akamuuliza.



“Mmoja wa mashahidi wake ni yule mwanamke wake ambaye anasema aliniona nikichukua hizo pesa”



“Lakini wewe hukuchukua?”



“Sikuchukua. Ningepata pesa hizo ningekuwa katika hali hii jamani?”



“Umeshafikishwa mahakamani?”



“Nilifikishwa kwa mara ya kwanza wiki mbili zilizopita. Kesi ilitajwa kisha ikaahirishwa hadi leo lakini leo nako likatokea tatizo.

Wakati naenda mahakamani niligongwa na pikipiki, mguu wangu ukatenguka. Huyu kaka alisimamisha gari lake akanipeleka hospitali nikafungwa hili P.O.P. Kwa hiyo sikuweza kuhudhuria kesi”



“lakini ulifikisha taarifa kuwa ulipata ajali?”



“Sikuweza. Lakini baada ya kufungwa P.O.P, huyu kaka alinipeleka mahakamani nikajieleza kwa makarani wa mahakama wakaniambia kesi yangu imehirishwa hadi kesho”



“Hebu nieleza nini kilitokea siku hiyo ambayo unadaiwa kuiba hizo pesa?”



“Mimi nilikwenda kwa huyo mwanaume kuchukua nguo zangu zilizokuwa kwake kwa sababu uchumba wetu ulishavunjika. Nilipofika, mwenyewe sikumkuta lakini nilimkuta huyo hawara yake ambaye ni rafiki yangu. Kwa kweli tulijibishana maneno mabaya mpaka ikafikia kutaka kugombana”



“Nani alianzisha ugomvi huo?’



“Ni yeye. Aliniambia kuwa nilikuwa nimemfuata mwanaume ambaye hanitaki. Nikamwambia sikufuata mwanaume, nimefuata nguo zangu. Hapo ndipo ugomvi ulipoanza”



“Ulichukua hizo nguo zako?”



“Nilivyokuta mwenyewe hayuko sikuzichukua”



“Hizo pesa zinazodaiwa kuibiwa ziliibiwa mahali gani?”



“Chumbani kwa Njoroge”



“Njoroge ndio nani?”



“Ndiye huyo mwanaume”



“Wewe ulifika humo chumbani?”



“Ndio nilifika na ndiko nilikogombana na huyo msichana”



“Amedai hizo pesa uliziiba mahali gani?”



“Eti kwenye kabati la nguo?”



“Wewe ulilifungua hilo kabati?”



“Ndio nililifungua”



“Ulilifungua kwa madhumuni gani wakati ulisema hukuweza kuchukua nguo zako kwa sababu mwenyewe hakuwepo”



“Ni baada ya yule msichana kuniletea ujeuri lakini watu walinisihi kuwa nimsubiri mwenyewe. Nikaondoka”



“Hao watu walitokea wapi?”



“Ni wapangaji wengine wanaoishi katika ile nyumba”



“Kwa hiyo hao waliona kama hukulifungua hilo kabati?”



“Ndio waliona”



“Na waliushuhudia ugomvi wenu mwanzo hadi mwisho?”



“Waliingia mle chumbani waliposikia kelele lakini mpaka ninaondoka walikuwepo”



“Kumbe unao mashahidi waliiona kuwa hukuchukua kitu”



“Mimi ninajua hao hawawezi kwenda kunitolea ushahidi mimi. Wao na Njoroge lao moja”



“Kwanini?”



“Kwa sababu wanaishi pamoja. Atawafundisha uongo kama alivyomfundisha mwanamke wake”



“Kama watakwenda kutoa ushahidi wa uongo tutawahoji maswali watajikangaja tu”



Wakili akamtazama Lwanzo.



“Nitaishughulikia hii kesi. Kesho nitakuwepo mahakamani asubuhi”



“Umemuelewa vizuri huyu msichana?” Lwanzo akamuuliza.



“Nimemuelewa lakini kwa upande wa kesi yake itabidi nisome shitaka lake nione linasema nini”



“Ni shitaka la wizi” Herieth akadakia.



“Wizi uko wa aina nyingi. Itabidi nione shitaka lilivyoandikwa”



“Sawa. Kwa hiyo umesema utaishughulikia hii kesi” Lwanzo akamuuliza tena.



“Nitaishughulikia”



“Kutokana na maelezo machache uliyoyasikia hapa unaonaje, unaweza kumsaidia asipatikane na hatia?”



“Nitajitahidi”



“Utahitaji kiasi gani?’



“Nitakujibu kesho nitakapotoka mahakamani. Si utakuja?”



“Itabidi nije”



“Basi tutakutana hapo”



“Sawa. Kwa hiyo tunaweza kwenda?”



“Ndiyo. Mnaweza”



Lwanzo na herieth wakatoka ofisini. Walipojipakia kwenye gari Lwanzo alimuuliza msichana.



Unaishi wapi?”



“Naishi Langata”



Lwanzo akaliwasha gari.



“Umepangisha chumba au unakaa kwa mtu?”



“Nina chumba changu”



“Ngoja twende nikupeleke”



Lwanzo akatia gea na kuliondoa gari.



“Sisi wanaume tuna tabia tofauti. Kuna wanaume wana tabia za kike kabisa” Lwanzo alimwambia Herieth wakati gari ikiwa kwenye mwendo.



“Ni kweli. Wa kwanza ni Njoroge”



“Kama alimuona rafiki yako ni wa maana zaidi hapakuwa na haja ya kukubambikia kesi wewe”



“Tena yule msichana ndiye mshenga aliyetumwa na Njoroge alipokuwa ananitaka mimi”



“Halafu baadaye wakatakana wenyewe?’



“Kwanini wasitakane hapo mwanzo!”



“Huo ndio upuuzi wa baadhi ya wanaume. Mtu unapoongozwa na tamaa ya ngono unaweza kutembea hata na shemeji yako”



“Na yule rafiki yangu pia siye. Yeye ndiye chanzo cha yote. Aliona nikiolewa na Njoroge nitafaidi, nitapumzika nyumbani. Akaona aniharibie. Lakini mimi sijali na aolewe yeye afaidi yeye. Mungu ni mwema nitapata mwanaume mwingine wa maana zaidi”



ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 09


ILIPOISHIA



Eneo la Lang’ata lilikuwa kando kidogo ya jiji hilo. Lilikuwa eneo linaloishi watu wa vipato vya chini kama Herieth. Lwanzo alimpeleka msichana huyo hadi mlangoni mwa nyumba aliyokuwa anaishi.



Lakini walikuta kitu kilichowashitua.



Kwanza waliona gari la polisi lililokuwa limesimama pembeni mwa mlango. Halafu waliona polisi watatu wakitoka ndani ya nyumba hiyo pamoja na mtu mmoja aliyevaa kiraia ambaye alikuwa akifoka.



“Tutamkamata tu hata ande wapi. Kwao ninakujua ni Kiambu na hana pengine pa kukimbilia!”



“ Haa! Njoroge yule!” Herieth akamaka na kugwaya



“Amefuata nini nyumbani kwako?” Lwanzo akamuuliza.



Msichana akabetua mabega yake.



“Sijui. Tena amekuja na polisi!”



SASA ENDELEA



Lwanzo alilisimamisha gari nyuma ya gari la polisi.



“Hebu tushuke, tuwasikilize” lwanzo akamwambia Herieth huku akifungua mlango wa gari.



“Sijui huyu mwanaume ananitafuta nini mimi” Herieth alilalamika.



“Shuka tu, kama ni kesi yenu, tayari iko mahakamani. Hakuna sababu yoyote ya kuwa na wasiwasi”



Herieth akafungua mlango. Wakati anashuka kwenye gari, mtu aliyekuwa anafoka alimuona.



“Huyo hapo amefika “ akasema huku akimnyooshe kidole Herieth.



“Wewe Njoroge unanitafuta nini lakini…?” Herieth alimuuliza kwa hasira baada ya kushuka kwenye gari.



“Unajua wewe uko huru kwa dhamana, leo ulitakiwa kufika mahakamani lakini hukufika, umekiuka dhamana yako!”



“Wewe inakuhusu nini?”



Lwanzo akaingilia kati.



“Msibishane. Huyu msichana wakati anakuja mahakamani asubuhi alipata ajali ya gari, ametenguka mguu. Mimi ndiye niliyemsaidia kumpeleka hospitali”



“Sasa sisi hatujui. Tunajua kuwa amekiuka dhamana. Polisi wamekuja kumkamata”



“Lakini Njoroge hii ni kazi ya polisi na mahakama, wewe inakuhusu nini?” Herieth akafoka.



“Herieth nyamaza msogombane” Lwanzo alimtuliza.



“Anajifanya hodari sana wa kusema lakini safari hii jeuri yake itakwisha” Njoroge alimwambia Herieth kwa jeuri.



“Wewe unatakiwa kukamatwa kwa sababu mahakama haina taarifa kuwa umepata ajali. Sisi tumekuja kukukamata” Mmoja wa wale polisi akamwambia Herieth.



“Ndio mumkamate mkamuweke ndani hadi kesho atakapofikishwa tena mahakamani chini ya ulinzi wa polisi” Njoroge akasema.



“Hapa tunatoka mahakamani. Ameshatoa taarifa na ametakiwa kufika tena kesho” Lwanzo akawambia.



Polisi mmoja aliposikia hivyo alimgeukia Njoroge.



“Kama mahakama ina taarifa kuwa alipata ajali hatuwezi kumkamata tena” akamwambia.



“Wewe angalia sana!” Njoroge akamwambia herieh huku akimnyooshea kidole cha onyo.



Herieth hakumjibu kitu, alimtazama tu kisha akapanda kwenye baraza ya nyumba. Njoroge na wale polisi walishuka kwenye baraza wakajipakia kwenye gari na kuondoka.



“Karibu ndani kaka” Herieth akamwambia Lwanzo.



“Asante. Sitaingia ndani. Nitaishia hapa ila kesho asubuhi nitakufuata hapa nikupeleke mahakamani”



“Sawa. Asante kaka”



“Haya kwaheri”



“Karibu sana”



Lwanzo akarudi kwenye gari akaliwasha na kuondoka.



Wakati akiendesha kurudi nyumbani kwake aliwaza kwamba sheria zimeshindwa kuzuia unyanyasaji dhaidi ya wanawake kwa sababu pesa imewekwa juu ya sheria.



Aliendelea kujiambia, kwa sababu ya pesa mtu anaweza kutumia hata vyombo vya dola kumdhalilisha binaadamu mwenzake bila huku akijua fika kuwa hana kosa.



“Udhalilishaji dhidi ya wanawake bado ni tatizo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi na jamii nzima” Lwanzo akajiambia.



Hata hivyo alikuwa amepanga kumsaidia yule msichana hadi dakika ya mwisho ili ahakikishe kuwa haki imetendeka.



Herieth baada ya kuingia chumbani kwake alikaa kwenye kochi na kuanza kuufikiria mguu wake. Alijiambia alipoondoka asubuhi mguu wake ulikuwa mzima kabisa na hakufikiria kuwa angerudi nyumbani akiwa na P.O.P.



“Kweli binaadamu haishi kuumbwa” alijiambia huku akimshukuru Lwanzo, mtu ambaye hakuwa akimfahamu kabla, kwa msaada aliompa kumpeleka hospitali na kisha kumuwekea wakili.



“Kama si yule kaka, sijui ningekuwa katika hali gani leo?” alijiuliza bila kupata jibu.



Taratibu alianza kukumbuka jinsi wazazi wake walivyofariki huko kwao Kiambu na yeye kuamua kwenda jijini Nairobi kutafuta kazi. Alifika Nairobi akiwa na nguo moja tu ya akiba aliyokuwa ameitia kwenye mfuko wa plastiki.



Ilikuwa ni mara ya kwanza kufika katika jiji hilo na lengo lake lilikuwa kutafuta kazi, kazi yoyote tu ambayo angejaliwa kuipata, iwe kazi ya ndani au ya uchuuzi wa vitu vidogo vidogo.



Ilimchukua karibu saa nzima kuzunguka katika eneo la stendi la Nairobi akiwa hajui aende wapi. Alikuwa akizungumza na kila msichana aliyemuona anafanya biashara ndogondogo.



Hatimaye alikutana na msichana mmoja aliyekuwa akitembeza vitu vidogo vidogo.



“Naweza kupata kazi kama yako?’ akamuuliza.



“Kwani wewe unatoka wapi?”



“Natoka Kiambu, ndio nimefika sasa hivi”



Msichana huyo aliyeonekana kukomaa lakini mwenye umbo dogo alimtazama Herieth kuanzia kichwani hadi miguuni.



“Unataka kazi?” akamuuliza.



“Unaweza kunipatia?”



“Mimi pia nimeajiriwa kuuza hivi vitu, si kazi yangu”



“Na mimi pia nahitaji”



“Usifikiri ni rahisi, hapa haturuhusiwi kufanya biashara ndogo ndogo tunaibia tu, askari wa jiji wakija tunakimbia. Utaweza?’



“Nitaweza”



“Basi subiri nikiondoka nitakupeleka kwa mama mmoja anayetaka msichana wa kumuuzia biashra yake”



Ndipo Herieth alipopelekwa kwa mama mmoja wa Kijaluo ambaye alimwambia Herieth kuwa alikuwa anataka msichana wa kumsaidia katika kazi yake ya kuuza majungu katika soko moja lililokuwa kando kidogo ya jiji la Nairobi eneo la Kibera.



“Mimi sichagui kazi. Kazi yoyote utakayonipa nitafanya” Herieth alimwambia mwanamke huyo ambaye alimpokea Herieth na kumuajiri kazi ya kuuza majungu.



Herieth hakumaliza hata mwezi mmoja, akajakukutana na msichana mmoja aliyeitwa Sara ambaye alikuwa akiishi jirani na mwanamke huyo wa Kijaluo.



Herieth na Sara wakawa marafiki.



“Kwani mwenzangu unafanya kazi wapi?” Siku hiyo Herieth akamuuliza Sara.



“Nauza baa”



“Huyu mwanamke ninayemfanyia kazi yake ananinyanyasa sana. Nikipata mahali pengine nitamkimbia”



“Utaweza kuuza baa”



“Kwanini nisiweze?”



“Tena una umbo zuri la kuvutia wateja, nikikupeleka kwa tajiri yetu atakupokea mara moja”



“Sasa unajua tatizo ni nini?”



“Ni nini?”



“Ni mahali pa kulala. Hivi sasa nalala kwa yule mwanamke, nikiacha kazi kwake itabidi niondoke kwake”



“Kama ni kulala tu si tatizo, utala na mimi chumbani kwangu”



Siku ya pili yake Herieth akamtoroka yule mwanamke wa Kijaluo. Sara alimpeleka mjini katika baa aliyokuwa anafanya kazi ya ubaamed.



Mmiliki wa baa hiyo ambaye alikuwa ni mtumishi wa serikalini alipomuona Herieth alimpokea mara moja. Harieth akaanza kazi ya ubaamed.



Ni wakati huo ushamba ulipomtoka Herieth na kuonekana kama msichana wa mjini. Kutokana na pesa ndogo ndogo za chenji alizokuwa akiachiwa na bia za ofa ambazo alikuwa akiziuza kwa wateja wengine kwa kisingizio kuwa hawaruhuiwi kulewa wakiwa kazini, mara moja Herieth alibadilika. Aliweza kununua nguo za thamani na kuweza kujiwekea akiba. Urafiki wake na sara ukazidi kuwa mkubwa.



Siku moja Sara akataka kumchuuza mwenzake kwa mwanaume aliyekuwa akimtaka.



“Kuna jamaa atakuja usiku ana visenti vyake mbuzi, nataka ukamchune” Sara alianza kumwambia herieth mara tu walipoingia kazini saa kumi na mbili jioni.



“Ni jamaa gani?”



“Atakuja saa tatu usiku utamuona, ameniambia anakupenda sana”







ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 10

ILIPOISHIA



“Halafu nitoke naye?” Herieth akamuuliza Sara.



“Toka naye, kwani kuna tatizo gani! Atakuchuukua nyumbani kwake”



“Lakini pesa yake haina tabu?”



“Haina tabu kabisa. Dhamana yako ni mimi”



Saa tatu usiku jamaa huyo akawasili. Alikuwa Njoroge. Sara akamkutanisha na Herieth, wakayazungumza na kukubaliana kuwa usiku ule Herieth akalale kwa Njoroge.



Kutoka saa tatu usiku Njoroge aliendelea kunywa bia hadi saa sita baa ilipofungwa. Akaondoka na Herieth kwa teksi kuelekea nyumbani kwake.



Kutoka siku hiyo Herieth na Njoroge wakawa wapenzi. Mapenzi yaliponoga Herieth akahamia kwa Njoroge. Baada ya kuishi kwa mwaka mmoja wakakubaliana kuwa wachumba.



SASA ENDELEA



Wakati huo Herieth hakuwa Herieth yule aliyetoka Kiambu. Alikuwa Herieth mwingine aliyenawiri na kujisikia. Alikuwa mrembo ambaye shida ndogo ndogo zilimpitia mbali.



Sara alihisi kwamba Njoroge alikuwa mwanaume makini aliyeweza kutunza mwanamke kuliko alivyokuwa akimdhania. Aliamini kuwa yeye ndiye aliyebadili maisha ya Herieth.



Akajiambia laiti angempata yeye angeweza kuyabadili maisha yake na kuwa bora zaidi. Akaona kwamba alifanya kosa kumpeleka mwanaume huyo kwa rafiki yake badala ya kubaki naye yeye.



Ndipo alipoanza kufikiria kumnyang’anya Herieth mwanaume huyo. Alianza kwa kumrembulia macho Njoroge na kumfanyia dhihaka za makusudi ili Njoroge amuone kuwa alikuwa na kitu ndani ya moyo wake.



Wakati huo Herieth hakuwa ametambua kilichokuwa ndani ya mawazo ya mwenzake. Aliuchukulia mzaha wa Sara kwa mwanaume wake ni wa ushemeji tu.



Kulikuwa na siku moja ambayo Herieth na Sara walikuwa kwenye mapumziko. Njoroge alifika hapo baa na kukuta ujumbe kuwa amfuate Sara nyumbani kwake kwa vile alikuwa na shida naye muhimu.



Kutokana na wito huo Njoroge baada ya kupata chupa tatu za bia alindoka akapanda matatu na kwenda nyumbani kwa Sara.



Si unajua matatu ya Kenya hususani ya Mombasa yako na misemo kila aina na utachoka wewe mwenyewe kusoma na kila moja ni zuri zaidi ya mwenzake, mie matatu niliyopanda ilikuwa na jina lililoandikwa "Mpende akupendae"



Alipoingia chumbani kwake alikuta mambo ambayo hayakuwa ya kawaida. Juu ya meza alikuta chupa kadhaa za bia, nyingine zikiwa tupu na nyingine zikiwa hazijanywewa.



Sara mwenyewe alikuwa amejilaza kitandani akiwa amelewa chakari.



Siku hiyo Sara alikuwa amemtega Njoroge. Alikuwa amevua nguo na kubaki na nguo ya ndani halafu alilala kifudi fudi.



Njoroge alianza kuutupia macho mwili wa Sara akiulinganisha na wa Herieth. Alianzia kwenye miguu, akaona ilikuwa miguu ya bia. Macho yake yakapanda taratibu na kufika kwenye magoti. Yalikuwa magoti ya mfuto.



Macho yaliendelea kwenda. Sasa rangi ya ngozi libadilika, ilikuwa ngozi laini nyeupe kama ya mtoto mchanga. Macho yalizidi kwenda…



Mpaka anafika kwenye kiuno Njoroge alikuwa hoi. Alimeza funda la mate akahisi mwili ukimsisimka.



Zile bia tatu alizokunywa zikawa zimewasha moto ndani ya mwili wake.



Akasogea karibu na kitanda akamuwekea mkono kwenye bega na kumuita.



“Sara! Sara!”



Sauti ya Sara ikasikika kwa mbali ikimuitikia lakini hakuinuka wala kugeuka.



“Mbona uko hivyo?”



“Unasema nini…?” Sara ikamuuliza kilevi. Alikuwa bado ameuficha uso wake kwenye mto.



“Hebu geuka basi…umelewa kiasi hiki!”



“Nani wewe…?”



“Mimi Njoroge, niliambiwa unaniita”



Sara akaugeza uso wake na kumtazama Njoroge. Macho yake yalikuwa mekundu na hayakuwa yamefumbuka sawa sawa.



“Kaa hapa” Sara akamwambia Njoroge katika hali ya ulevi.



“Nikae wapi?”



“Kaa hapa”



Sara alimuonesha kwenye kitanda alichokuwa amelala. Njoroge akaketi pembeni mwa kitanda. Sara akaliweka paja lake juu ya paja la Njoroge.



“Unasema unatoka wapi?” akamuuliza.



“Natoka kazini kwako. Nimekuta ujumbe kuwa unaniita”



“Ndio nilikuachia ujumbe huo. Nilitaka tuje tunwe nyumbani”



“Una maana bia zote hizi ulikuwa unakunywa peke yako”



“Ni chache tu. Nyingine nimekuachia wewe”



“Mbona uko hivyo, kwanini umevua nguo?”



“Joto. Nilikuwa nasikia joto sana. Halafu nasikia…”



“Unasikia nini?”



Badala ya kumjibu Sara aliupeleka mkono wake akalipapasa tumbo la Njoroge kisha akaushusha mkono huo taratibu huku akiendelea kupapasa....



Usaliti wa Sara kwa Herieth ulianzia hapo. Baada ya kumtega Njoroge kama alivyoweza kumtega alifanikiwa kumpata siku ile.



Kinyume cha matarajio yake, Njoroge aliondoka nyumbani kwa Sara jua likiwa limeshakuchwa.



Tangu siku ile yeye na Herieth wakawa wanagawana penzi kwa Njoroge bila Herieth kujua.



Siku moja wakati Njoroge na Sara wamekaa nyumbani kwa Sara, Sara alimwambia Njoroge.



“Kwanini huachani na yule mshamba?”



“Kwanini?”



“Sasa wa kazi gani yule, hata halingani na hadhi yako. Huoni aibu kuwa na mwanamke kama yule?”



“Wewe si ndiye uliyenitafutia?”



“Nilikutafutia mbanjuke kwa siku moja tu. Naona mwenzangu sasa unataka uoe kabisa!”



“Nina mpango huo. Nimegundua Herieth ni msichana mtulivu sana”



“Na aende zake, ana utulivu gani, malaya mkubwa! Au ni kwa vile sijakwambia siri zake”



“Siri zake zipi?”



“Hebu achana naye bwana!”



“Siwezi kumuacha Herieth”



“Utamuacha tu, nitahakikisha unamuacha”



Wambeya wa pale baa walikuja wakamwambia Herieth kuwa rafiki yake alikuwa akimsaliti kwa Njoroge. Kwanza Herieth hakuamini lakini kulikuwa na siku moja Herieth alipigiwa simu na mmoja wa marafiki zake aliyemwambia kuwa aende nyumbani kwa Sara akajionee mwenyewe.



Siku hiyo Herieth alikwenda nyumbani kwa Sara kwa teksi. Aliona akipanda matatu angechelewa.



Alipofika alikuta mlango wa chumba cha Sara ulikuwa umefungwa kwa ndani. Akabisha.



Alibisha mara kadhaa hadi aliposikia sauti ya Sara ikitokea chumbani.



“Wewe nani?”



Herieth hakujibu, aliendelea kugonga tu. Hatimaye mlango ukafunguliwa. Sara akatoa kichwa.



Herieth akajitumbukiza ndani ghafla na kumkuta Njoroge akiwa kitandani. Alikuwa na suruali yake lakini hakuwa na shati.



Sara naye alikuwa amevaa khanga moja tu.



Ulikuwa ni mshituko uliotokea mle chumbani.



Mshituko ulianzia kwa Herieth baada ya kumkuta Njoroge akiwa kitandani chumbani kwa rafiki yake huku rafiki mwenyewe akiwa amevaa khanga moja.



Mshituko huo ulimkumba Njoroge baada ya kumuona Herieth akiingia mle chumbani hali iliyodhihirisha kuwa amefumaniwa.



Sara hakutarajia kuwa Herieth angetokea na angeingia mle chumbani kinguvu. Akawa ameshituka kwa kukutwa na mchumba wa rafiki yake.



Akapigwa na butwaa kwenye mlango.



“Za mwizi ni arobaini. Leo arobaini yenu imefika, nimewafuma. Nilikuja hapa kwa ajili ya kuwafumania nyinyi” Herieth aliwambia kwa hasira kabla ya kumtazama Sara.



“Sikutegemea rafiki yangu kuwa ungeweza kunisaliti kiasi hiki. Asante sana”



Njoroge na Sara walikuwa wamenyamaza kimya. Fumanizi hilo hawakuwa wamelitegemea.



“Nawaacha muendelee na starehe zenu lakini wewe bwana uchumba wetu unaishia hapa”



ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom