Mkasa wa kweli: Nilijua nimeua

Mkasa wa kweli: Nilijua nimeua

SEHEMU YA 09

ILIPOISHIA

Baada ya kupelekwa wodini Dk Kweka aliniita, nikaenda wodini na kumuona mke wangu. Hali aliyokuwa nayo wakati anapelekwa kufanyiwa usafishwaji, siyo aliyokuwa nayo wakati ametolewa. Alikuwa na afadhali sana.

Nikamshukuru Dk Kweka nay eye akanishukuru pia.

“Unaweza kurudi naye nyumbani” akaniambia.

“Tatizo lake limekwisha kabisa?” nikamuuliza.

“Limekwisha isipokuwa kila wiki umlete kuangalia maendeleo yake”

“Lilikuwa ni tatizo gani?”

“Mimba ilikuwa haikushika sawa sawa. Ana udhaifu kwenye kizazi chake. Katika hali kama hiyo anapopata mshituko, hofu au fadhaa, mara moja mimba inaweza kutoka”

Nikahisi ile ndoto aliyoota ndiyo iliyomshitua na kusababisha mimba hiyo kuporomoka.

“Asante dokta, sasa unatushauri nini?”

“Kama nilivyokwambia kila wiki mlete hapa hospitali, nione maendeleo yake”

“Sawa dokta, nitafanya hivyo”

SASA ENDELEA

Baada ya hapo niliondoka na mke wangu tukarudi nyumbani. Kila wiki nikawa nampeleka hospitali kufanyiwa uchunguzi na Dk Kweka. Wiki nyingine ambazo sikuwa na nafasi alikuwa akienda mwenyewe.

Zoezi hilo lilichukua wiki sita ndipo tukaacha kwenda hospitali. Dk Kweka akanihakikishia kuwa tatizo la mke wangu halikuwepo tena.

“Kama unataka mimba nyingine kazi kwako” Dk Kweka akaniambia kwa utani.

“Asante sana. Kwa kweli ninakushukuru kwa msaada wako” nikamwambia.

Siku moja ambayo sitaisahau maishani mwangu nilikuwa kwenye kiwanja cha ndege cha Tanga. Kulikuwa na ndege ya abiria iliyotua kutoka Zanzibar.

Nikapata abiria mmoja ambaye alivutia sana hisia zangu. Alikuwa ni kijana ambaye nilisoma naye katika shule ya sekondari ya Usagara. Mimi nilikomea kidato cha nne, yeye alifanikiwa kuendelea kidato cha tano na cha sita. Alikuwa anaitwa Zacharia.

Tangu tulipoondoka shule hatukukutana tena hadi siku ile. Miaka minane ilikuwa imeshapita. Mbali ya kufurahi kumuona pia alinishitua, kwanza kumuona akishuka kwenye ndege na kwa jinsi alivyokuwa amevaa na kupendeza.

Alikuwa amevaa suti nyeusi. Koti lake alikuwa amelivua na kulipachika begani. Ndani ya suti kulikuwa na shati jeupe na tai yangi nyekundu. Uso wake uliokuwa umenawiri ulionesha mwenzangu alitoka kwenye neema

Kukutana kwangu na Zacharia baada ya kufarakana kwa karibu miaka minane kulikuwa ndio mwanzo wa masahibu niliyokutana nayo amabayo sitayasahau kamwe.

“Oh Machawi! Habari za siku?’ Hivyo ndivyo Zacharia alivyonisalimia huku akinipa mkono mara tu aliponiona ndani ya jengo la kiwanja cha ndege.

Machawi lilikuwa jina langu la utani ambalo vijana wenzangu walikuwa wakiniita shuleni. Walianza kuniita mchawi kwa sababu nilikuwa na tabia ya kutoroka toroka shule. Naweza kuonekana msitarini lakini wanafunzi wakiingia darasani hawanioni! Nimeshatoroka. Nikaitwa mchawi. Baadaye jina hilo likabadilika likawa Machawi.

“Nzuri Zacharia. Kumbe unaishi Zanzibar?”

“Nilienda kwa muda, niko Dar”

“Kikazi uko wapi?”

“Baada ya kuchukua shahada yangu ya sheria niliajiriwa na Wizara ya mambo ya nje”

“Nimefurahi kukuona, karibu tena Tanga”

“Asante. Nahitaji teksi ya kunipeleka mjini”

“Mimi pia ni dereva wa teksi. Hapa nimefuata abiria”

“Kumbe unaendesha teksi! Vizuri sana. Basi twenzetu”

Nikatoka naye. Mara tu baada ya kujipakia kwenye teksi mazungumzo yakaanza.

“Ajira zimekuwa ngumu sana. Nimeangukia kwenye udereva” nilimwambia Zacharia wakati nikiiwasha teksi.

“Kwa sasa hivi sekta binafsi ndio kimbilio la watu wengi. Hata mimi kuna uwezekano mkubwa nikaacha kazi na kujiajiri mwenyewe”

“Wewe mwenzetu una shahada yako ya sheria, unaweza kujiajiri mwenyewe. Taabu ni kwetu sisi tulioishia sekondari”

“Hapana. Ajira ni ajira tu. Hata kuendesha teksi ni ajira, ilimradi tu unapata riziki yako na maisha yanakwenda. Kwani teksi ni ya kwako mwenyewe?”

“Hapana si yangu”

“Lakini masilahi yapo”

“Nashukuru, si sawa na kukosa kabisa”

“Mimi nataka kuwa wakili wa kujitegemea. Nitakuja kufanya kazi zangu hapa Tanga”

“Itakuwa vizuri sana. Huduma ya uwakili inahitajika sana na katika mkoa wetu tuna mawakili wachache sana”

“Pengine mwakani nitakuwa nimeshapata leseni”

“Nakuombea mafanikio. Unakwenda wapi?”

“Mtendele Hotel”

“Pale Chuda?”

“Ndiyo Chuda. Nitakuwa pale kwa wiki moja hivi”

“Zanzibar ulifuata nini?”

“Nilienda kikazi”

‘Tulifika Mtendele Hotel. Wakati anashuka alinikaribisha. Na mimi nikashuka na kumfuata.

“Hatuwezi kuachana haraka. Hatujakutana miaka mingi” aliniambia wakati tunapenya katika lango la hoteli hiyo mpya.

Wakati anaandikisha chumba aliniambia nikae kwenye kiti, akaniagizia bia.

Alipopatiwa chumba alirudi tukaakaa sote. Na yeye akaagiza bia. Tulikunywa huku tunazungumza hadi nikakata chupa nne. Baada ya kulipia bia tulizokunywa alinipa shilingi laki mbili.

“Chukua hizo rafiki yangu” akaniambia. Nikamshukuru sana.

“Nipatie namba yako ya simu ili kama nitahitaji teksi nikuite” akaniambia.

“Sawa”

Nikampa namba yangu na yeye akanipa yake. Tukaagana na nikamuacha hapo hoteli.

Usiptwe na uhondo huu
 
SEHEMU YA 10

ILIPOISHIA

Niliisikia waziwazi sauti yake ikihitimisha hukumu yangu kwa maneno yasemayo.

“Nimeridhika na ushahidi uliotolewa kwamba wewe mshitakiwa umemuua mke wako kikatili kwa kumkatakata na panga. Kwa sababu hiyo mahakama hii imekutia hatiani. Adhabu yako ni kunyongwa kwa kitanzi hadi ufe!”

Yale maneno “Utanyongwa kwa kitanzi hadi ufe” yalizindua akili yangu, nikazinduka kama mtu aliyetoka kwenye ndoto. Nikashusha pumzi ndefu na kuikazia macho maiti ya mke wangu.

Nisipobuni maarifa ya kufanya, nilijiambia, picha iliyonijia akilini nikihukumiwa kunyongwa itakuwa kweli!.

Nitatumia akili gani kuokoa maisha yangu? Nikajiuliza bila kupata jibu.

Nikaendelea kujiuliza, itakuwa sahihi kweli mke wangu afe na mimi ninyongwe?

Hapo hapo nikapata wazo. Nilitoka nje nikaiwasha teksi yangu kisha nikafungua mlango wa nyuma wa teksi na kuuacha wazi. Nilirudi ndani nikazima taa ya nje, nikaenda uani na kuibeba maiti ya Halima. Nikaenda nayo hadi mlango wa mbele ambao sikuwa nimeufunga kabisa.

SASA ENDELEA

Niliufungua kwa mguu nikachungulia nje. Barazani kwangu kulikuwa giza baada ya kuzima taa. Na hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akipita barabarani usiku huo.

Nikatoka haraka na maiti ya Halima na kuipakia kwenye teksi kwa kutumia mlango wa nyuma niliouacha wazi. Niliilaza ile maiti kwenye siti kisha nikafunga mlango wa teksi na kurudi ndani.

Nilikwenda chumbani nikachukua tochi yangu ya mawe sita, nikatoka chumbani na kwenda stoo kuchukua shepe.

Nikiwa nimeshika shepe na tochi nilitoka nje nikafungua boneti la nyuma la teksi yangu na kuliweka lile shepe pamoja na tochi kisha nikalifunga boneti.

Nilikwenda kwenye mlango wa dereva nikajipakia na kuiondoa teksi.

Eneo la makaburi halikuwa mbali sana na mtaa niliokuwa ninaishi pale Msambweni. Nikaiendesha teksi taratibu hadi katika eneo hilo la makaburi. Niliingiza teksi ndani kabisa ili isionekane mahali hapo. Nilikuwa nimezima taa za mbele na za nyuma.

Nilipofika mahali nilipopataka niliisimamisha teksi nikafungua mlango na kushuka. Nilikwenda nyuma ya teksi nikafungua boneti na kutoa shepe pamoja na tochi. Nikawwa natafuta mahali pa kuchimba kaburi ili niizike ile maiti ya Halima nipoteze ushahidi.

Baada ya kumulikamulika tochi nilipata sehemu nzuri ambayo haikuwa na kaburi. Nikatazama huku na huku, nilipoona kulikuwa kimya nikaanza kuchimba.

Mchanga ulikuwa mgumu lakini nilijitahidi hivyohivyo, jasho likawa linanitoka. Nilipochoka nilipumzika kwenye gari kisha nikarudi tena kuendelea kuchimba. Nilichimba hadi nikapata shimo la kutosha. Nikaliweka shepe chini nikaenda kwenye teksi na kuutoa mwili wa Halima.

Sikuwa na nguvu za kuubeba kwa vile nguvu nyingi nilizitumia kuchimba kaburi hilo. Niliuweka chini kisha nikauburuza kuelekea kwenye lile kaburi. Nilipolifikia nikausukumia ndani ya kaburi hilo.

Ulivyoangukia ndivyo hivyo hivyo nilivyoufukia. Sikuwa na muda wa kuingia ndani ya kaburi hilo na kuuweka sawa.

Nilipomaliza kufukia nilisawazisha mchanga na kuushindiliankwa miguu. Wakati nafanya hivyo niliona kama kulikuwa na mtu nyuma ya mti uliokuwa ubavuni kwangu akinichungulia. Nikashituka!.

Niliinama chini nikaichukua ile tochi na kumulika pale kwenye mti. Ule uso uliokuwa ukinichungulia ulipoona mwanga ulijificha nyuma ya mti.

Nikapata hofu na wasiwasi kwa sababu sikujua mtu yule alikuwa nani na kama alikuwa akinifuatilia mimi.

Nilijiambia kama mtu huyo alikuwa ananifuatilia mimi atakuwa ameshgundua siri yangu na ilikuwa si siri tena.

Dukuduku la kutaka kumjua likanipata. Nilitaka nijue kama ni mtu niliyekuwa namfahamu au yeye ananifahamu mimi.

Nikalishika lile shepe kama silaha yangu na kunyemelea kunako ule mti huku nikiendelea kumulika tochi.

Nilinyemelea kuuzunguka ule mti nikiuambaa kwa mbali kwa kuhofia kushambuliwa ghafla kwani sikuwa nikijua aliyekuwa nyuma ya mti huo alikuwa nani.

Nilipozunguka nusu tu ya mti huo nikamuona mtu amechutama chini ya mti huo. Nikammulika kwa tochi ili niweze kumuona vizuri. Nilimuona alikuwa msichana na alikuwa uchi wa mnyama! Nguo zake alikuwa amezishika mkononi akikinga uso wake usimulikwe.

Kitendo cha kumuona msichana yule mahali pale na usiku ule tena akiwa uchi, kwa kweli kilinitisha. Maswali mawili yakanijia.

Alikuwa nani?

Alikuwa akinichunguza mimi au alikuwa na lake?

Sikutosheka kujiuliza peke yangu kwa sababu nisingepata jibu, nikaikaza sauti yangu na kumuuliza.

“Wewe nani?”

“Zima tochi kwanza!” akaniambia. Sauti yake ilikuwa ya chini lakini ilikuwa ya ukali.

Nikazima ile tochi lakini mwanga wa mbalamwezi ulitosha kuyafanya macho yangu yamuone.

Alipoona nimezima tochi alisimama akavaa nguo zake haraka haraka huku akiniambia “Subiri hapo hapo”

Alipomaliza kuvaa akaniambia.

“Samahani kaka yangu, mimi nilikuwa na ishu yangu hapa ndiyo nikakuona wewe unafukia hilo kaburi. Nadhani wewe pia ulikuwa na ishu yako. Sote ni wachawi, tusidhuriane”

Sote ni wachawi? Ina maana yeye ni mchawi? Nikajiuliza.

“Ulikuwa na ishu yako ipi?”

“Kaka usiwe na wasiwasi na mimi. Mimi nilikuja kuzika vitu vyangu kwenye kaburi”

“Vitu?”

“Ndiyo vitu”

“Vitu gani?”

“Ni vitu vya uganga. Nilipewa na mganga wangu. Aliniambia nije nivizike usiku kwenye kaburi”

“Wewe ni mchawi?”

“Hapana, si mchawi”

“Mbona umeniambia sote ni wachawi tusidhuriane”

“Nimekwambia hivyo kwa maana tunavyovifanya hapa ni vitendo vya kichawi vya kufukua makaburi usiku”

“Hivyo vitu ulivyozika vinahusu nini?”

“Ni mambo yangu binafsi”

“Kwa hiyo huna tatizo jingine?’

Msichana akabetua mabega.

“Mimi sina tatizo, ni wasiwasi wako tu”

Nikamsogelea karibu na kumuuliza.

“Hivyo vitu umevizika kwenye kaburi gani?”

Akanionesha kaburi lililokuwa upande wa pili pembeni mwa ule mti.

Wakati nalitazama hilo kaburi aliniuliza.

Je alimuuliza nini n nini kitatokea?
 
Majombi ni baba yako? Taksi ya Majombi ninayoikumbuka ni ya miaka ya 80-90 nikiwa mdogo, alibeba harusi ya dada yangu pia. Nafikiri ilikuwa Ford ile. Kumbe uliendeleza biashara, kila kwa kheri!
 
Majombi ni baba yako? Taksi ya Majombi ninayoikumbuka ni ya miaka ya 80-90 nikiwa mdogo, alibeba harusi ya dada yangu pia. Nafikiri ilikuwa Ford ile. Kumbe uliendeleza biashara, kila kwa kheri!
Majombi mzee ameshafariki alikuwa anakaa kwaminchi sabasaba
 
panga story vizuri na wikiendi iendee vizuri
 
SEHEMU YA 07

ILIPOISHIA JANA

“Ni elfu sita”

“Punguza, fanya tano. Mimi ni mteja wako wa kila siku”

“Haya nipe”

Mariam akafungua pochi na kutoa noti ya shilingi elfu tano akanipa. Akafungua mlango wa teksi na kushuka.

Aliagana na mwenzake na kwenda kubisha mlango wa nyumbani kwao. Nami nikaanza safari ya kuelekea Kange.

Nilipofika Kange Nilimuuliza msichana anakwenda mtaa gani, akaniambia nikate kushoto. Nilipokata kushoto akanielekeza mtaa ambao anaoishi.

Nilipofika katika mtaa huo alinionyesha nyumba aliyotaka nimpeleke. Ilikuwa nyumba nzuri kuliko aliyokuwa anaishi Mariam.

“Unanidai kiasi gani?” Msichana akaniuliza niliposimamisha teksi.

“Nipe elfu kumi”

SASA ENDELEA

Msichana hakubishana. Alifungua pochi yake akatoa noti ya shilingi elfu kumi na kunipa. Akafungua mlango na kushuka.

Alikwenda kwenye baraza ya ile nyumba na kupiga simu.

Nilimsikia akisema.

“Asiya nifungulie mlango”

Nikaiondoa teksi na kumuacha hapo hapo.

Wakati narudi jijini nilikuta gari limeegeshwa kando ya barabara. Taa zake za nyuma zilikuwa zinawaka. Wakati nalikaribia gari hilo niliona mtu aliyekuwa kando yake akinipungia mkono kunisimamisha.

Wazo nililolipata kwanza ni kuwa gari hilo lilikuwa limeharibika na kwamba mtu aliyekuwa akinipungia mkono ama alikuwa anataka msaada au alikuwa anahitaji huduma ya teksi yangu.

Kwa vile nilikuwa kwenye mwendo wa kasi nililipita gari hilo na kwenda kusimama mbele. Hapo hapo mawazo yangu yakabadilika. Niliwaza kwamba huenda gari hilo liliegeshwa kwa hila lionekane limeharibika kumbe ni majambazi wanaosubiri magari yasimame waanze kupora watu.

Nilikuwa nimechelewa kufikiria hilo. Nilikuwa nimeshasimamisha teksi na jamaa aliyenisimamisha alikuwa ameshafika kwenye dirisha la teksi yangu!

Chini ya siti yangu ya dereva, siku zote huweka parange (sime ya kimasai) kwa ajili ya kujihami endapo kutatokea tatizo la kuvamiwa na mtu au watu wenye nia mbaya.

Kwa vile sikuwa na uhakika kuwa mtu huyo aliyenisimamisha alikuwa na nia mbaya au nzuri, tayari nilishapeleke mkono wangu wa kulia kuushika mpini wa parange iliyokuawa chini ya siti niliyokalia.

Nilikuwa nimejiweka tayari, kama atakuwa na nia mbaya niweze kukabiliana naye.

“Samahani bwana” Mtu huyo akaniambia. Ingawa sauti yake ilikuwa tulivu nay a kibinaadamu, ilikuwa imeficha taharuki.

“Unasemaje?” nikamuuliza nikiwa nimemkazia macho kusoma mawazo yake.

“Mimi ni daktari wa hospitali ya Bombo. Nimepigiwa simu kuitwa hospitali, kuna mama mjamzito anahitaji kufanyiwa operesheni ya dharura sasa hivi. Kwa bahati mbaya gari langu limeharibika njiani. Naomba unipeke Bombo haraka” akaniambia.

“Kusema kweli nilimuelewa. Nikamuuliza.

“Na hilo gari lako je?”

“Ningeomba kama itawezekana unisaidie kulivuta niliondoe mahali hapa”

“Hiyo itakuwa ni kazi nyingine” nikamwambia.

“Naomba msaad wako kaka, sina jinsi na siwezi kuliacha hapa”

“Unataka nilivute hadi wapi?”

“Hadi Bombo. Nitaliegesha sehemu. Kutakapokucha nitajua la kufanya”

“Utanilipa kiasi gain?”

“Sema wewe”

“Kulivuta hilo gari lako pamoja na kukufikisha wewe Bombo utanilipa elfu ishirini”

“Sawa. Nitakulipa”

Alipokubali kima changu nilifungua mwa gari nikashuka.

“Una kamba?” nikamuuliza.

“Kamba sina’

Nilikuwa na kamba ya akiba kwenye boneti la teksi yangu. Nilikwenda nyuma ya gari, nikafungua boneti na kutoa kamba. Nikaiweka chini.

Kisha niliisogeza teksi mbele ya gari la mtu huyo lililokuwa pembeni. Nikashuka tena na kufunga ncha moja ya kamba nyuma ya gari langu na ncha nyingine nikaifunga mbele ya lile gari. Nilipomaliza nilimwambia mtu huyo ajipakie kwenye gari lake.

Wakati anajipakia na mimi nilikwenda kwenye mlango wa teksi nikaufungua na kujipakia. Nilitia gea na kuiondo teksi taratibu. Kamba ilinyooka na kukaza kabla ya kuanza kulivuta gari la nyuma.

Niliingia barabarani nikawa naendesha taratibu. Kwa vile niliendesha kwa mwendo mdogo tulifika Bombo saa kumi na mbili asubuhi.

Nilishuka kwenye teksi nikaifungua ile kamba na kuiweka kwenye boneti.

ITAENDELEA
Mbona unarudiarudia story babu
 
SEHEMU YA 10

ILIPOISHIA

Niliisikia waziwazi sauti yake ikihitimisha hukumu yangu kwa maneno yasemayo.

“Nimeridhika na ushahidi uliotolewa kwamba wewe mshitakiwa umemuua mke wako kikatili kwa kumkatakata na panga. Kwa sababu hiyo mahakama hii imekutia hatiani. Adhabu yako ni kunyongwa kwa kitanzi hadi ufe!”

Yale maneno “Utanyongwa kwa kitanzi hadi ufe” yalizindua akili yangu, nikazinduka kama mtu aliyetoka kwenye ndoto. Nikashusha pumzi ndefu na kuikazia macho maiti ya mke wangu.

Nisipobuni maarifa ya kufanya, nilijiambia, picha iliyonijia akilini nikihukumiwa kunyongwa itakuwa kweli!.

Nitatumia akili gani kuokoa maisha yangu? Nikajiuliza bila kupata jibu.

Nikaendelea kujiuliza, itakuwa sahihi kweli mke wangu afe na mimi ninyongwe?

Hapo hapo nikapata wazo. Nilitoka nje nikaiwasha teksi yangu kisha nikafungua mlango wa nyuma wa teksi na kuuacha wazi. Nilirudi ndani nikazima taa ya nje, nikaenda uani na kuibeba maiti ya Halima. Nikaenda nayo hadi mlango wa mbele ambao sikuwa nimeufunga kabisa.

SASA ENDELEA

Niliufungua kwa mguu nikachungulia nje. Barazani kwangu kulikuwa giza baada ya kuzima taa. Na hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akipita barabarani usiku huo.

Nikatoka haraka na maiti ya Halima na kuipakia kwenye teksi kwa kutumia mlango wa nyuma niliouacha wazi. Niliilaza ile maiti kwenye siti kisha nikafunga mlango wa teksi na kurudi ndani.

Nilikwenda chumbani nikachukua tochi yangu ya mawe sita, nikatoka chumbani na kwenda stoo kuchukua shepe.

Nikiwa nimeshika shepe na tochi nilitoka nje nikafungua boneti la nyuma la teksi yangu na kuliweka lile shepe pamoja na tochi kisha nikalifunga boneti.

Nilikwenda kwenye mlango wa dereva nikajipakia na kuiondoa teksi.

Eneo la makaburi halikuwa mbali sana na mtaa niliokuwa ninaishi pale Msambweni. Nikaiendesha teksi taratibu hadi katika eneo hilo la makaburi. Niliingiza teksi ndani kabisa ili isionekane mahali hapo. Nilikuwa nimezima taa za mbele na za nyuma.

Nilipofika mahali nilipopataka niliisimamisha teksi nikafungua mlango na kushuka. Nilikwenda nyuma ya teksi nikafungua boneti na kutoa shepe pamoja na tochi. Nikawwa natafuta mahali pa kuchimba kaburi ili niizike ile maiti ya Halima nipoteze ushahidi.

Baada ya kumulikamulika tochi nilipata sehemu nzuri ambayo haikuwa na kaburi. Nikatazama huku na huku, nilipoona kulikuwa kimya nikaanza kuchimba.

Mchanga ulikuwa mgumu lakini nilijitahidi hivyohivyo, jasho likawa linanitoka. Nilipochoka nilipumzika kwenye gari kisha nikarudi tena kuendelea kuchimba. Nilichimba hadi nikapata shimo la kutosha. Nikaliweka shepe chini nikaenda kwenye teksi na kuutoa mwili wa Halima.

Sikuwa na nguvu za kuubeba kwa vile nguvu nyingi nilizitumia kuchimba kaburi hilo. Niliuweka chini kisha nikauburuza kuelekea kwenye lile kaburi. Nilipolifikia nikausukumia ndani ya kaburi hilo.

Ulivyoangukia ndivyo hivyo hivyo nilivyoufukia. Sikuwa na muda wa kuingia ndani ya kaburi hilo na kuuweka sawa.

Nilipomaliza kufukia nilisawazisha mchanga na kuushindiliankwa miguu. Wakati nafanya hivyo niliona kama kulikuwa na mtu nyuma ya mti uliokuwa ubavuni kwangu akinichungulia. Nikashituka!.

Niliinama chini nikaichukua ile tochi na kumulika pale kwenye mti. Ule uso uliokuwa ukinichungulia ulipoona mwanga ulijificha nyuma ya mti.

Nikapata hofu na wasiwasi kwa sababu sikujua mtu yule alikuwa nani na kama alikuwa akinifuatilia mimi.

Nilijiambia kama mtu huyo alikuwa ananifuatilia mimi atakuwa ameshgundua siri yangu na ilikuwa si siri tena.

Dukuduku la kutaka kumjua likanipata. Nilitaka nijue kama ni mtu niliyekuwa namfahamu au yeye ananifahamu mimi.

Nikalishika lile shepe kama silaha yangu na kunyemelea kunako ule mti huku nikiendelea kumulika tochi.

Nilinyemelea kuuzunguka ule mti nikiuambaa kwa mbali kwa kuhofia kushambuliwa ghafla kwani sikuwa nikijua aliyekuwa nyuma ya mti huo alikuwa nani.

Nilipozunguka nusu tu ya mti huo nikamuona mtu amechutama chini ya mti huo. Nikammulika kwa tochi ili niweze kumuona vizuri. Nilimuona alikuwa msichana na alikuwa uchi wa mnyama! Nguo zake alikuwa amezishika mkononi akikinga uso wake usimulikwe.

Kitendo cha kumuona msichana yule mahali pale na usiku ule tena akiwa uchi, kwa kweli kilinitisha. Maswali mawili yakanijia.

Alikuwa nani?

Alikuwa akinichunguza mimi au alikuwa na lake?

Sikutosheka kujiuliza peke yangu kwa sababu nisingepata jibu, nikaikaza sauti yangu na kumuuliza.

“Wewe nani?”

“Zima tochi kwanza!” akaniambia. Sauti yake ilikuwa ya chini lakini ilikuwa ya ukali.

Nikazima ile tochi lakini mwanga wa mbalamwezi ulitosha kuyafanya macho yangu yamuone.

Alipoona nimezima tochi alisimama akavaa nguo zake haraka haraka huku akiniambia “Subiri hapo hapo”

Alipomaliza kuvaa akaniambia.

“Samahani kaka yangu, mimi nilikuwa na ishu yangu hapa ndiyo nikakuona wewe unafukia hilo kaburi. Nadhani wewe pia ulikuwa na ishu yako. Sote ni wachawi, tusidhuriane”

Sote ni wachawi? Ina maana yeye ni mchawi? Nikajiuliza.

“Ulikuwa na ishu yako ipi?”

“Kaka usiwe na wasiwasi na mimi. Mimi nilikuja kuzika vitu vyangu kwenye kaburi”

“Vitu?”

“Ndiyo vitu”

“Vitu gani?”

“Ni vitu vya uganga. Nilipewa na mganga wangu. Aliniambia nije nivizike usiku kwenye kaburi”

“Wewe ni mchawi?”

“Hapana, si mchawi”

“Mbona umeniambia sote ni wachawi tusidhuriane”

“Nimekwambia hivyo kwa maana tunavyovifanya hapa ni vitendo vya kichawi vya kufukua makaburi usiku”

“Hivyo vitu ulivyozika vinahusu nini?”

“Ni mambo yangu binafsi”

“Kwa hiyo huna tatizo jingine?’

Msichana akabetua mabega.

“Mimi sina tatizo, ni wasiwasi wako tu”

Nikamsogelea karibu na kumuuliza.

“Hivyo vitu umevizika kwenye kaburi gani?”

Akanionesha kaburi lililokuwa upande wa pili pembeni mwa ule mti.

Wakati nalitazama hilo kaburi aliniuliza.

Je alimuuliza nini n nini kitatokea?
Inaonekana ni bonge la story ila unavyoruka ruka epsode, yaani unashindwa kujua ulipoishia episode iliyopita ili upate muendelezo wa epsode nyingine
 
Back
Top Bottom