Mkasa wa kweli: Nilijua nimeua

Mkasa wa kweli: Nilijua nimeua

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,672
Kijuana kwangu na Halima kulikuwa kwa bahati sana. Awali sikuwa na mawazo kabisa ya kwamba nitakuja kukutana na kusuhubiana na msichana mrembo kama yeye.

Siku moja ambayo ninaikumbuka hadi leo nikiwa kwenye teksi yangu maarufu kama Majombi Teksi, nilikuwa ninatoka hospitali ya Bombo ambayo ni hospitali ya mkoa iliyoko Tanga.

Nilikuwa nimempeleka mama mmoja mjamzito kutoka hospitali ya Ngamiani. Mama huyo alipelekwa hospitalini hapo kujifungua lakini kutokana na umri wake kuwa mkubwa madaktari wakaamua wamhamishie Bombo.

Ndugu zake waliiona teksi yangu ambayo huiegesha karibu na hospitali hiyo kusubiri abiria, wakanikodi niwapeleke Bombo.
Wakati narudi kutoka Bombo mvua ilikuwa imeanza kunyesha.

Nikaona msichana aliyekuwa amesimama pembeni mwa barabara akinipungia mkono kwa bidii huku akitota na mvua. Ilikuwa wazi kuwa mvua ilimkuta ghafla njiani na mahali alipokuwa hapakuwa na sehemu ya kujisitiri. Mimi kama dereva wa teksi nilishukuru kwa hilo.

Nilipunguza mwendo na kuisimamisha gari pembeni mwa barabara. Nilikuwa nimempita kidogo. Alipoona teksi imesimama aliifuata haraka akafungua mlango wa nyuma na kujipakia.
“Unakwenda wapi?” nikamuuliza.
“Nipeleke barabara 20 nyuma ya CCM” akaniambia. Sauti yake ilikuwa nyembamba na nyororo.

Alijisogeza katikati ya siti ili kukwepa upepea wa mvua uliokuwa ukipenya kwenye dirisha. Nikawa namuona vizuri kwenye kioo cha gari cha kutazamia nyuma.

Wakati naiondoa teksi nilikuwa namkodolea macho kupitia kwenye kioo hicho bila mwenyewe kujua.
Uso wake ulikuwa umenywea kutokana na fadhaa ya kutoswa na mvua lakini alikuwa na sura jamali ya macho makubwa aliyoyapaka wanja mzito. Juu ya macho yake pembeni mwa kopi alikuwa amepaka rangi iliyoendana na nguo aliyokuwa amevaa.

Pua yake ilikuwa ndefu na midomo ya wastani aliyokuwa ameipaka rangi hafifu ya waridi.
Nilimuona tangu alipokuwa amesimama alikuwa mrefu , mweupe na mwenye mwili wa wastani. Vazi alilokuwa amevaa, dera la maua ya rangi ya bluu ya kung’aza na ushungi wake aliokuwa ameutanda kichwani vilimfanya aonekane alikuwa msichana aliyejistahi sana.

“Mvua za ghafla namna hii zinatuharibia bajeti” akasema kwa sauti ya kuchukia.
“Kwanini?” nikamuuliza huku nikitia gea ya pili.
“”Mahesabu yangu yalikuwa kupanda bodaboda, sasa nalazimika nipande teksi ili nisitote, huoni kuwa nimeshaharibu bajeti yangu?’

Nikatoa tabasamu jepesi.
“Na sisi ndio tunapata riziki zetu, usiilani”
“Kwa hiyo unaiombea ili upate abiria kwa wingi eti?”
“Ndiyo maisha yalivyo. Huwezi kumwambia daktari unaombea watu waumwe ili waje kwako upate pesa, au huwezi kumwambia muosha maiti kuwa anafurahia watu wafe apate kazi. Yeye pia anasikitika mtu akifa lakini ndiyo maisha. Kwa mmoja kukienda kilio kwa mwingine kunakwenda furaha”

“Sawa bwana, umeshinda wewe”
Nikacheka. “Sasa unataka nikalie wapi dadangu kama sio kwenu?”
“Basi nipunguzie kidogo”
“Ni shilingi elfu tano tu”
“Ndiyo nakwambia nipunguzie, nitakupa elfu tatu”

Nikatikisa kichwa. Tabasamu lililokuwa usoni kwangu likatoweka. Sikutaka masihara yaingie kwenye kazi yangu. Teksi ile haikuwa mali yangu. Nilikuwa nimeajiriwa na mwenyewe alitaka nimpelekee shilingi elfu ishirini kila baada ya masaa ishirini na nne, bila kujali nimeingiza kiasi gani.

“Elfu tano ndio kima chetu, haipungui. Petroli imepanda sana” nikamwambia.
Wakati nampa jibu hilo simu yake iliyokuwa kwenye mkoba wake ilianza kuita. Akaitoa na kuipokea.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 02

Alisikiliza kidogo kisha akaendelea.
“Nimekodi teksi…poa…”
Akairudisha simu kwenye mkoba.
Nilikuwa nimetokea kwenye eneo la Tangamano. Mvua ilikuwa imezidi. Eneo hilo lilikuwa halipitiki kwa maji. Niliipitisha teksi yangu kwa taabu kwa kutumia gea kubwa. Mpaka nakaribia kufika stendi ndio nilipata afadhali kidogo.

Nikaendelea na safari hadi barabara 20. Nilikata kulia, nikalipita jengo la ofisi ya CCM na kuingia mtaa wa nyuma yake. Mtaa huo ulikuwa umejaa matope
“Twende kwenye nyumba ile pale” abiria wangu akaniambia
Alinionesha nyumba iliyokuwa katikati ya mtaa huo upande wa kulia. Ilikuwa nyumba ya kawaida iliyoonekana kuwa tulivu.

Niliposimamisha teksi, msichana aliniuliza.
“Nikupe kiasi gani?”
“Elfu tano”

SASA ENDELEA

Nikadhani ataanza tena kulalamika kutaka kupunguziwe kiasi cha pesa. Lakini haikuwa hivyo, alifungua mkoba wake akatoa noti ya shilingi elfu tano na kuniambia.

“Shika”

Niligeuka nikaipokea kisha nikamfungulia mlango.

Akashuka haraka na kukimbilia kwenye baraza ya ile nyumba. Wakati anabisha mlango nikaiondoa teksi.

Nilirudi katika egesho langu lililokuwa karibu na hospitali ya Ngamiani.

Nililipendelea egesho hilo kwa maana. Kwanza lilikuwa karibu na hospitali ambapo mara kwa mara kunakuwa na wagonjwa wanaohitaji huduma ya teksi. Pili nilikuwa peke yangu na tatu kulikuwa na mahoteli mengi yaliyokuwa karibu na hapo na kufanya nipate wateja wengi.

Wakati naliegesha gari nilisikia mlio wa simu ndani ya gari. Nikashituka na kudhani ilikuwa simu yangu. Lakini niligundua haikuwa simu yangu. Simu yangu haikuwa na mlio kama huo niliousikia

Nikatega masikio yangu ili nijue mlio huo ulikuwa unatokea wapi. Nikapata jibu. Mlio huo ulitoka nyuma yangu. Nikageuza kichwa na kutazama nyuma. Ndipo nilipoiona simu ikiita kwenye siti.

Mara moja niligundua kuwa yule msichana niliyempakia alisahau simu yake. Ilikuwa simu ileile aliyokuwa akiitumia wakati nimempakia.

Sikuweza kujua ni nani aliyekuwa anapiga. Iliwezekana alikuwa yeye mwenyewe, aliamua kupiga baada ya kugundua kuwa aliisahahu simu ndani ya teksi yangu. Au alikuwa ni mume wake ingawa sikuwa na hakika kama alikuwa na mume.

Nikajiuliza niipokee ile simu au nisiipokee? Nikapata jibu kuwa nisiipokee kwa vile sikujua nani anapiga na isitoshe haikuwa ikinihusu.

Baada ya kuita kwa muda simu ikakatika lakini baadaye kidogo simu ikaita tena. Nikaiacha iite.

Kwa vile nyumba aliyoingia yule msichana ninaifahamu nitampelekea wakati wowote, nikajiambia.

Hata hivyo sikupata amani kwani simu ilikuwa ikiita kwa mfululizo. Ufumbuzi ulikuwa niizime au niipeleke kwa mwenyewe haraka. Kwa vile nilishindwa kuizima niliamua niwashe teksi nimrudishie mwenyewe.

Mvua sasa ilkuwa imeacha kabisa. Nilifika katika mtaa aliokuwa akiishi yule msichana. Tangu natokea katika mtaa huo niliona msichana amesimama kwenye baraza ya ile nyumba akiwa amejaa wasiwasi. Nilipokaribia zaidi niligundua kuwa alikuwa ni yule msichana niliyempakia.

Niliposimamisha teksi mbele ya ile nyumba aligutuka, akanikodolea macho ya tashiwishi.

Mara moja akashuka kwenye baraza na kuja kwenye mlango wa teksi wa dereva.

“Kaka umeniletea simu yangu?” akaniuliza kwa matumaini.

Kwa kutaka kumshitua a mimi nikamuuliza.

“Simu gani?”

“Jamani nilisahau simu yangu kwenye siti. Simu yenyewe niliinunua juzi tu shilingi laki tatu”

Nilipoona amehamanika nilimwambia.

“Hebu angalia kwenye siti uliyokuwa umekaa”

Akasogea mlango wa nyuma na kuchungulia kwenye dirisha.

“Si ile pale!” akasema huku akifungua mlango.

Aliingia ndani ya teksi akaichukua ile simu na kutoka.

“Asante kaka. Kumbe ulikuwa unanitania!”

Sote tukacheka. Huzuni ilikuwa imeshamtoka.

“Wewe ni muaminifu sana. Nitakuwa nachukua teksi yako kila siku” akaniambia.

“Kwaheri, nakwenda zangu” nikamuaga.

“Ulikuwa umeniletea simu yangu. Asante sana kaka, endelea kuwa na moyo huo huo”

“Asante bibie”

Wakati natia gea niondoe gari sauti yake ikanisitisha.

“Nipe namba yako. Nitakuhitaji tena siku nyingine”

Nikamtajia namba yangu.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 03

ILIPOISHIA

Akaijaza kwenye simu yake.

“Na mimi nipe yako” nikamwambia.

“Ngoja nikupigie. Unaitwa nani?”.

“Majombi Teksi”

Jina hilo likamchekesha. Alipolijaza kwenye simu akanipigia. Simu yangu iliita. Nikaishika na kuitazama.

“Hii ndio namba yako”

“Ndiyo hiyo”

“Unaitwa nani?”

“Mariam” akatamka haraka.

Nikahifadhi ile namba pamoja na jina lake kwenye simu yangu. Nilipomaliza nikamwambia “Sawa”

Nikaiondoa teksi.

Huo ukawa mwanzo wa kujuana na Mariam.

Kutoka siku ile akawa ananipigia simu mara kwa mara kuniita sehemu kwa ajili ya kuhitaji huduma ya teksi yangu. Kulikuwa na siku ambayo alinipigia simu saa tisa usiku. Nilikuwa nimesharudi nyumbani na nilikuwa nimelala. Nikaamka na kuangalia simu iliyokuwa inaita. Nikaona ni yeye aliyekuwa akinipigia. Nikashituka na kujiuliza kwanini alikuwa ananipigia simu usiku ule, alikuwa wapi na alikuwa na nini?

“Hallo Mariam …vipi?” nikamuuliza baada ya kupokea simu yake.

Nilikuwa nimekereka kukatishwa usingizi wangu lakini nilivumilia.

“Majombi uko wapi?” Sauti ya Mariam ikauliza.

“Niko nyumbani” nikajibu.

“Ninakuhitaji hapa Habours Club”

Habours ilikuwa klabu ya starehe ambayo ilikuwa ikitumiwa kwa maonesho ya miziki hasa miziki ya taarab.

“Unataka nikufuate hapo Habours Club?” nikamuuliza.

“Ndiyo”

“Nikupeleke wapi?”

“Nyumbani”

“Ulikuwa kwenye mziki?”

“Ndiyo”

Nilisita kumpa jibu. Kwa upende mmoja sikupenda kukatisha usingizi wangu kwani nilihitajika kuamka saa kumi na mbili asubuhi niingie kazini. Kurudi kwangu nyumbani ni saaa sita au saba usiku.

Lakini kwa upande mwingine sikutaka kumkatisha tamaa mteja wangu. Kwa vile ilikuwa ni kazi ya usiku nilijua ingeniingizia pesa nzuri. Nikaona nimfuate.

“Unasemaje, utanifuata?” Sauti ya Mariam ikakatisha mawazo yangu.

“Mko wangapi?” Nikamuuliza ili kupanga masilahi yangu.

“Tuko wawili, mimi na rafiki yangu”

“Nisubirini, nakuja”

“Sasa ukifika nipigie unishitue kwani tuko ndani”

“Sawa, nitakupigia”

Mariam akakata simu.

Niliondoka kitandani na kuanza kuvaa. Nilikuwa nikiishi eneo la Msambweni kwenye nyumba yangu mwenyewe. Ilikuwa nyumba ya urithi. Tuliirithi mimi na mdogo wangu wa kiume baaada ya baba yetu kufariki dunia.

ITAENDELEA
 
mzee majombi taxi unakatisha utamu sana mkuu.
 
SEHEMU YA 04

Baada ya kusubiri kwa dakika kumi hivi nikaona wasichana wawili wakifungua milango ya teksi yangu na kujipakia.

“Habari ya saa hizi?” Mariam akanisalimia.

“Nzuri” nilimjibu huku nikiirudisha gari kinyume nyume ksha nikabadili gea na kuondoka.

Wakati teksi ikiwa katika mwendo Mariam aliniambia.

“Mimi ninakwenda barabara ishirini na mwenzangu anakwenda Kange. Sijui utaanza wapi?”

Eneo la Kange liko karibu kilometa tano nje ya jiji. Kwanza niliwaza gharama ya mwendo wangu hadi huko kisha nikamwambia.

“Nitakupeleka wewe kwanza”

Kwa vile hawakuniuliza itakuwa kiasi gani sikuona haja ya kuanza mimi kuwaambia. Nikanyamaza kimya.

SASA ENDELEA

Nilimpeleka Mariam barabara ishirini. Niliposimamisha teksi aliniuliza.

“Ni kiasi gani?”

“Unauliza kiasi cha kukuleta hapa au cha kwenda mpaka Kange?”

“Kange atakulipa mwenyewe. Niambie gharama ya kunileta hapa”

“Ni elfu sita”

“Punguza, fanya tano. Mimi ni mteja wako wa kila siku”

“Haya nipe”

Mariam akafungua pochi na kutoa noti ya shilingi elfu tano akanipa. Akafungua mlango wa teksi na kushuka.

Aliagana na mwenzake na kwenda kubisha mlango wa nyumbani kwao. Nami nikaanza safari ya kuelekea Kange.

Nilipofika Kange Nilimuuliza msichana anakwenda mtaa gani, akaniambia nikate kushoto. Nilipokata kushoto akanielekeza mtaa ambao anaoishi.

Nilipofika katika mtaa huo alinionyesha nyumba aliyotaka nimpeleke. Ilikuwa nyumba nzuri kuliko aliyokuwa anaishi Mariam.

“Unanidai kiasi gani?” Msichana akaniuliza niliposimamisha teksi.

“Nipe elfu kumi”

Msichana hakubishana. Alifungua pochi yake akatoa noti ya shilingi elfu kumi na kunipa. Akafungua mlango na kushuka.

Alikwenda kwenye baraza ya ile nyumba na kupiga simu.

Nilimsikia akisema.

“Asiya nifungulie mlango”

Nikaiondoa teksi na kumuacha hapo hapo.

Wakati narudi jijini nilikuta gari limeegeshwa kando ya barabara. Taa zake za nyuma zilikuwa zinawaka. Wakati nalikaribia gari hilo niliona mtu aliyekuwa kando yake akinipungia mkono kunisimamisha.

Wazo nililolipata kwanza ni kuwa gari hilo lilikuwa limeharibika na kwamba mtu aliyekuwa akinipungia mkono ama alikuwa anataka msaada au alikuwa anahitaji huduma ya teksi yangu.

Kwa vile nilikuwa kwenye mwendo wa kasi nililipita gari hilo na kwenda kusimama mbele. Hapo hapo mawazo yangu yakabadilika. Niliwaza kwamba huenda gari hilo liliegeshwa kwa hila lionekane limeharibika kumbe ni majambazi wanaosubiri magari yasimame waanze kupora watu.

Nilikuwa nimechelewa kufikiria hilo. Nilikuwa nimeshasimamisha teksi na jamaa aliyenisimamisha alikuwa ameshafika kwenye dirisha la teksi yangu!

Chini ya siti yangu ya dereva, siku zote huweka parange (sime ya kimasai) kwa ajili ya kujihami endapo kutatokea tatizo la kuvamiwa na mtu au watu wenye nia mbaya.

Kwa vile sikuwa na uhakika kuwa mtu huyo aliyenisimamisha alikuwa na nia mbaya au nzuri, tayari nilishapeleke mkono wangu wa kulia kuushika mpini wa parange iliyokuawa chini ya siti niliyokalia.

Nilikuwa nimejiweka tayari, kama atakuwa na nia mbaya niweze kukabiliana naye.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 05

Lakini kwa upoande mwingine sikutaka kumkatisha tamaa mteja wangu. Kwa vile ilikuwa ni kazi ya usiku nilijua ingeniingizia pesa nzuri. Nikaona nimfuate.

“Unasemaje, utanifuata?” Sauti ya Mariam ikakatisha mawazo yangu.

“Mko wangapi?” Nikamuuliza ili kupanga masilahi yangu.

“Tuko wawili, mimi na rafiki yangu”

“Nisubirini, nakuja”

“Sasa ukifika nipigie unishitue kwani tuko ndani”

“Sawa, nitakupigia”

Mariam akakata simu.

Niliondoka kitandani na kuanza kuvaa. Nilikuwa nikiishi eneo la Msambweni kwenye nyumba yangu mwenyewe. Ilikuwa nyumba ya urithi. Tuliirithi mimi na mdogo wangu wa kiume baaada ya baba yetu kufariki dunia.

SASA ENDELEA

Mdogo wangu Kabwe naye hakumaliza hata miaka miwili akafariki. Alifariki Afrika Kusini alikokwenda kutafuta maisha.

Nilipta habari kuwa alipigwa na kuuawa na wenzake na kisha kuzikwa huko huko na Serikali baada ya ndugu zake kutoonekana.

Mimi nilikuja kufahamishwa na marafiki zake walionipigia simu kutoka Capetown. Wakaniambia kuwa Kabwe aliuawa na kuzikwa huko huko.

Baada ya kifo cha Kabwe nikaimiliki mimi nyumba yetu. Ilikuwa na vyumba sita vya ndani na vinne vya uani ambavyo nilikuwa nimevipangisha isipokuwa chumba kimoja ambacho nilikuwa nikiishi mwenyewe.

Wakati huo sikuwa na mke na pia sikuwa na mawazo ya kuoa, pengine ni kwa sababu sikuwa na wazazi wa kunipa msukumo wa kuoa.

Mara tu baada ya kuvaa nilichukua funguo ya gari nikatoka. Nilimuamsha mpangaji wangu wa chumba cha mbele na kumwambia afunge mlango wa mbele.

Teksi yangu ilikuwa barazani mwa nyumba yangu. Nilifungua mlango wa dereva na kujipakia. Nikawasha gari na kuondoka.

Nusu saa tu baadaye nilifika Habours Club ambayo ilikuwa eneo la Bombo. Nilikuta teksi nyingi pamoja na msongamano wa watu waliokuwa wakitoka katika klabu hiyo. Nilitafuta sehemu yenye nafasi nikaiegesha teksi na kuwasiliana na Mariam.

“Tayari nimeshafika” nikamwambia kwenye simu.

“Uko kwa wapi?”

Nakamuelekeza mahali nilipokuwa namsubiri.

“Tunakuja sasa hivi” akaniambia.

Baada ya kusubiri kwa dakika kumi hivi nikaona wasichana wawili wakifungua milango ya teksi yangu na kujipakia.

“Habari ya saa hizi?” Mariam akanisalimia.

“Nzuri” nilimjibu huku nikiirudisha gari kinyume nyume ksha nikabadili gea na kuondoka.

Wakati teksi ikiwa katika mwendo Mariam aliniambia.

“Mimi ninakwenda barabara ishirini na mwenzangu anakwenda Kange. Sijui utaanza wapi?”

Eneo la Kange liko karibu kilometa kumi nje ya jiji. Kwanza niliwaza gharama ya mwendo wangu hadi huko kisha nikamwambia.

“Nitakupeleka wewe kwanza”

Kwa vile hawakuniuliza itakuwa kiasi gani sikuona haja ya kuanza mimi kuwaambia. Nikanyamaza kimya.

Nilimpeleka Mariam barabara ishirini. Niliposimamisha teksi aliniuliza.

“Ni kiasi gani?”

“Unauliza kiasi cha kukuleta hapa au cha kwenda mpaka Kange?”

“Kange atakulipa mwenyewe. Niambie gharama ya kunileta hapa”

“Ni elfu sita”

“Punguza, fanya tano. Mimi ni mteja wako wa kila siku”

“Haya nipe”

Mariam akafungua pochi na kutoa noti ya shilingi elfu tano akanipa. Akafungua mlango wa teksi na kushuka.

Aliagana na mwenzake na kwenda kubisha mlango wa nyumbani kwao. Nami nikaanza safari ya kuelekea Kange.

Nilipofika Kange Nilimuuliza msichana anakwenda mtaa gani, akaniambia nikate kushoto. Nilipokata kushoto akanielekeza mtaa ambao anaoishi.

Nilipofika katika mtaa huo alinionyesha nyumba aliyotaka nimpeleke. Ilikuwa nyumba nzuri kuliko aliyokuwa anaishi Mariam.

“Unanidai kiasi gani?” Msichana akaniuliza niliposimamisha teksi.

“Nipe elfu kumi”

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 06

ILIPOISHIA
Kwa vile nilikuwa kwenye mwendo wa kasi nililipita gari hilo na kwenda kusimama mbele. Hapo hapo mawazo yangu yakabadilika. Niliwaza kwamba huenda gari hilo liliegeshwa kwa hila lionekane limeharibika kumbe ni majambazi wanaosubiri magari yasimame waanze kupora watu.
Nilikuwa nimechelewa kufikiria hilo. Nilikuwa nimeshasimamisha teksi na jamaa aliyenisimamisha alikuwa ameshafika kwenye dirisha la teksi yangu!
Chini ya siti yangu ya dereva, siku zote huweka parange (sime ya kimasai) kwa ajili ya kujihami endapo kutatokea tatizo la kuvamiwa na mtu au watu wenye nia mbaya.
Kwa vile sikuwa na uhakika kuwa mtu huyo aliyenisimamisha alikuwa na nia mbaya au nzuri, tayari nilishapeleke mkono wangu wa kulia kuushika mpini wa parange iliyokuawa chini ya siti niliyokalia.
Nilikuwa nimejiweka tayari, kama atakuwa na nia mbaya niweze kukabiliana naye.

SASA ENDELEA

“Samahani bwana” Mtu huyo akaniambia. Ingawa sauti yake ilikuwa tulivu nay a kibinaadamu, ilikuwa imeficha taharuki.
“Unasemaje?” nikamuuliza nikiwa nimemkazia macho kusoma mawazo yake.
“Mimi ni daktari wa hospitali ya Bombo. Nimepigiwa simu kuitwa hospitali, kuna mama mjamzito anahitaji kufanyiwa operesheni ya dharura sasa hivi. Kwa bahati mbaya gari langu limeharibika njiani. Naomba unipeke Bombo haraka” akaniambia.
“Kusema kweli nilimuelewa. Nikamuuliza.
“Na hilo gari lako je?”
"Naomba kama itawezekana unisaidie kulivuta niliondoe mahali hapa."
“Sema wewe”
“Kulivuta hilo gari lako pamoja na kukufikisha wewe Bombo utanilipa elfu ishirini”
“Sawa. Nitakulipa”
Alipokubali kima changu nilifungua mwa gari nikashuka.
“Una kamba?” nikamuuliza.
“Kamba sina’
Nilikuwa na kamba ya akiba kwenye boneti la teksi yangu. Nilikwenda nyuma ya gari, nikafungua boneti na kutoa kamba. Nikaiweka chini.
Kisha niliisogeza teksi mbele ya gari la mtu huyo lililokuwa pembeni. Nikashuka tena na kufunga ncha moja ya kamba nyuma ya gari langu na ncha nyingine nikaifunga mbele ya lile gari. Nilipomaliza nilimwambia mtu huyo ajipakie kwenye gari lake.
Wakati anajipakia na mimi nilikwenda kwenye mlango wa teksi nikaufungua na kujipakia. Nilitia gea na kuiondo teksi taratibu. Kamba ilinyooka na kukaza kabla ya kuanza kulivuta gari la nyuma.
Niliingia barabarani nikawa naendesha taratibu. Kwa vile niliendesha kwa mwendo mdogo tulifika Bombo saa kumi na mbili asubuhi.
Nilishuka kwenye teksi nikaifungua ile kamba na kuiweka kwenye boneti.
“Nakushukuru sana” Mtu huyo akaniambia baada ya kushuka kwenye gari lake.
Alitoa pochi mfukoni akaifungua na kutoa noti mbili za elfu kumi kumi akanipa.
“Sasa nipe namba yako, naweza kukuhitaji tena” Mtu huyo akaniambia.
Nikampa namba yangu ya simu akaiandika kwenye simu yake kasha akaniuliza.
“Unaitwa nani?”
“Andika Majomba Teksi”
Baada ya kuandika jina hilo aliniambia.
“Vizuri, nitakutafuta”
“Sawa” nikamjibu. Nilijipakia kwenye teksi yangu nikaiwasha na kuondoka.
Wakati naendesha nilijikuta nikumuwaza huyo mwanamke mjamzito aliyetakiwa kufanyiwa operesheni. Sikuwa na hakika kwamba alikuwa katika hali gani muda ule kwani kwa vyovyote vile yule daktari alikuwa amechelewa sana kufika pale hospitali kutokana na gari lake kuharibika.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 07

ILIPOISHIA JANA

“Ni elfu sita”

“Punguza, fanya tano. Mimi ni mteja wako wa kila siku”

“Haya nipe”

Mariam akafungua pochi na kutoa noti ya shilingi elfu tano akanipa. Akafungua mlango wa teksi na kushuka.

Aliagana na mwenzake na kwenda kubisha mlango wa nyumbani kwao. Nami nikaanza safari ya kuelekea Kange.

Nilipofika Kange Nilimuuliza msichana anakwenda mtaa gani, akaniambia nikate kushoto. Nilipokata kushoto akanielekeza mtaa ambao anaoishi.

Nilipofika katika mtaa huo alinionyesha nyumba aliyotaka nimpeleke. Ilikuwa nyumba nzuri kuliko aliyokuwa anaishi Mariam.

“Unanidai kiasi gani?” Msichana akaniuliza niliposimamisha teksi.

“Nipe elfu kumi”

SASA ENDELEA

Msichana hakubishana. Alifungua pochi yake akatoa noti ya shilingi elfu kumi na kunipa. Akafungua mlango na kushuka.

Alikwenda kwenye baraza ya ile nyumba na kupiga simu.

Nilimsikia akisema.

“Asiya nifungulie mlango”

Nikaiondoa teksi na kumuacha hapo hapo.

Wakati narudi jijini nilikuta gari limeegeshwa kando ya barabara. Taa zake za nyuma zilikuwa zinawaka. Wakati nalikaribia gari hilo niliona mtu aliyekuwa kando yake akinipungia mkono kunisimamisha.

Wazo nililolipata kwanza ni kuwa gari hilo lilikuwa limeharibika na kwamba mtu aliyekuwa akinipungia mkono ama alikuwa anataka msaada au alikuwa anahitaji huduma ya teksi yangu.

Kwa vile nilikuwa kwenye mwendo wa kasi nililipita gari hilo na kwenda kusimama mbele. Hapo hapo mawazo yangu yakabadilika. Niliwaza kwamba huenda gari hilo liliegeshwa kwa hila lionekane limeharibika kumbe ni majambazi wanaosubiri magari yasimame waanze kupora watu.

Nilikuwa nimechelewa kufikiria hilo. Nilikuwa nimeshasimamisha teksi na jamaa aliyenisimamisha alikuwa ameshafika kwenye dirisha la teksi yangu!

Chini ya siti yangu ya dereva, siku zote huweka parange (sime ya kimasai) kwa ajili ya kujihami endapo kutatokea tatizo la kuvamiwa na mtu au watu wenye nia mbaya.

Kwa vile sikuwa na uhakika kuwa mtu huyo aliyenisimamisha alikuwa na nia mbaya au nzuri, tayari nilishapeleke mkono wangu wa kulia kuushika mpini wa parange iliyokuawa chini ya siti niliyokalia.

Nilikuwa nimejiweka tayari, kama atakuwa na nia mbaya niweze kukabiliana naye.

“Samahani bwana” Mtu huyo akaniambia. Ingawa sauti yake ilikuwa tulivu nay a kibinaadamu, ilikuwa imeficha taharuki.

“Unasemaje?” nikamuuliza nikiwa nimemkazia macho kusoma mawazo yake.

“Mimi ni daktari wa hospitali ya Bombo. Nimepigiwa simu kuitwa hospitali, kuna mama mjamzito anahitaji kufanyiwa operesheni ya dharura sasa hivi. Kwa bahati mbaya gari langu limeharibika njiani. Naomba unipeke Bombo haraka” akaniambia.

“Kusema kweli nilimuelewa. Nikamuuliza.

“Na hilo gari lako je?”

“Ningeomba kama itawezekana unisaidie kulivuta niliondoe mahali hapa”

“Hiyo itakuwa ni kazi nyingine” nikamwambia.

“Naomba msaad wako kaka, sina jinsi na siwezi kuliacha hapa”

“Unataka nilivute hadi wapi?”

“Hadi Bombo. Nitaliegesha sehemu. Kutakapokucha nitajua la kufanya”

“Utanilipa kiasi gain?”

“Sema wewe”

“Kulivuta hilo gari lako pamoja na kukufikisha wewe Bombo utanilipa elfu ishirini”

“Sawa. Nitakulipa”

Alipokubali kima changu nilifungua mwa gari nikashuka.

“Una kamba?” nikamuuliza.

“Kamba sina’

Nilikuwa na kamba ya akiba kwenye boneti la teksi yangu. Nilikwenda nyuma ya gari, nikafungua boneti na kutoa kamba. Nikaiweka chini.

Kisha niliisogeza teksi mbele ya gari la mtu huyo lililokuwa pembeni. Nikashuka tena na kufunga ncha moja ya kamba nyuma ya gari langu na ncha nyingine nikaifunga mbele ya lile gari. Nilipomaliza nilimwambia mtu huyo ajipakie kwenye gari lake.

Wakati anajipakia na mimi nilikwenda kwenye mlango wa teksi nikaufungua na kujipakia. Nilitia gea na kuiondo teksi taratibu. Kamba ilinyooka na kukaza kabla ya kuanza kulivuta gari la nyuma.

Niliingia barabarani nikawa naendesha taratibu. Kwa vile niliendesha kwa mwendo mdogo tulifika Bombo saa kumi na mbili asubuhi.

Nilishuka kwenye teksi nikaifungua ile kamba na kuiweka kwenye boneti.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 08

ILIPOISHIA JANA

Alipokubali kima changu nilifungua gari nikashuka.

“Una kamba?” nikamuuliza.

“Kamba sina’

Nilikuwa na kamba ya akiba kwenye boneti la teksi yangu. Nilikwenda nyuma ya gari, nikafungua boneti na kutoa kamba. Nikaiweka chini.

Kisha niliisogeza teksi mbele ya gari la mtu huyo lililokuwa pembeni. Nikashuka tena na kufunga ncha moja ya kamba nyuma ya gari langu na ncha nyingine nikaifunga mbele ya lile gari. Nilipomaliza nilimwambia mtu huyo ajipakie kwenye gari lake.

Wakati anajipakia na mimi nilikwenda kwenye mlango wa teksi nikaufungua na kujipakia. Nilitia gea na kuiondoa teksi taratibu. Kamba ilinyooka na kukaza kabla ya kuanza kulivuta gari la nyuma.

Niliingia barabarani nikawa naendesha taratibu. Kwa vile niliendesha kwa mwendo mdogo tulifika Bombo saa kumi na mbili asubuhi.

Nilishuka kwenye teksi nikaifungua ile kamba na kuiweka kwenye boneti.

SASA ENDELEA

“Nakushukuru sana” Mtu huyo akaniambia baada ya kushuka kwenye gari lake.

Alitoa pochi mfukoni akaifungua na kutoa noti mbili za elfu kumi kumi akanipa.

“Sasa nipe namba yako, naweza kukuhitaji tena” Mtu huyo akaniambia.

Nikampa namba yangu ya simu akaiandika kwenye simu yake kisha akaniuliza.

“Unaitwa nani?”

“Andika Majomba Teksi”

Baada ya kuandika jina hilo aliniambia.

“Vizuri, nitakutafuta”

“Sawa” nikamjibu. Nilijipakia kwenye teksi yangu nikaiwasha na kuondoka.

Wakati naendesha nilijikuta nikumuwaza huyo mwanamke mjamzito aliyetakiwa kufanyiwa operesheni. Sikuwa na hakika kwamba alikuwa katika hali gani muda ule kwani kwa vyovyote vile yule daktari alikuwa amechelewa sana kufika pale hospitali kutokana na gari lake kuharibika.

Sikuendelea kumuwazia sana mwanamke huyo ambaye hata hivyo sikuwa nikimfahamu, nikajiambia sasa kumeshakucha. Nisingeweza tena kurudi kulala kwani muda ule ulikuwa ndio wa kuanza kazi.

Sikujali kupoteza usingizi wangu kwani nilikuwa nimeingiza zaidi ya shilingi elfu thelathini haraka haraka.

Nilichokuwa ninakiwazia ni kwenda kutia mafuta teksi yangu, nirudi nyumbani kuoga kisha nitoke tena.

Mpaka inafika saa mbili na nusu nilikuwa kwenye mgahawa mmoja nikipata kifungua kinywa. Nilikuwa nimeshaoga, kuvaa nguo nyingine na kuondoka nyumbani.

Baada ya kumaliza kufungua kinywa nilikwenda kwenye kituo changu jirani na hospitali ya Ngamiani. Nilipata safari mbili za haraka haraka, nikaingiza elfu kumi na mbili.

Wakati naegesha tena gari simu yangu ikaita. Nilipoipokea niligundua aliyekuwa akinipigia alikuwa ni yule daktari wa hospitali ya Bombo.

“Nimemaliza operesheni, sasa ninataka uje ulivute gari langu twende kwa Habib Garage pale Gofu”

“Sawa. Ninakuja”

Nilitazama saa yangu. Ilikuwa saa sita na robo. Nikaiondoa teksi yangu kuelekea hospitali ya Bombo.

Nilimkuta yule daktari ameliegemea gari lake ambalo tuliliegesha nyuma ya mti.

Nilisimamisha teksi mbele ya gari hilo nikashuka. Nilikwenda kufungua boneti la nyuma ya teksi nikatoa ile kamba. Ncha moja nikaifunga nyuma ya teksi na ncha nyingine nikaifunga mbele ya gari la yule daktari.

“Tayari” nikamwambia.

Daktari huyo akaingia kwenye gari lake. Na mimi nikaingia kwenye teksi yangu. Nilipowasha teksi tukaanza safari ya kuelekea Gofu.

Tulipofika huko nililiingiza gari hilo ndani ya gereji ya Habib. Daktari huyo akanilipa pesa yangu niliyotaka, nikaondoka.

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom