Mkasa Wa Kweli: Mfu Aliyerudiwa Na Uhai

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,444
sentido-morte.jpg


Naitwa Esma Mabruki, lakini watu wangu wa karibu walinikatisha na kuniita Esy. Mpaka leo Esy ndilo limekuwa maarufu.



Ni mzaliwa wa Dar es Salaam. Nilizaliwa katika Hospitali ya Mwananyamala na wazazi wangu walikuwa wakiishi hapohapo Mwananyamala.



Baba yangu mzee Mabruki alikuwa akifanya kazi ya udereva kwa mfanyabiashara aliyeitwa Saidi Omar au Alhakim. Kulikuwa na siku ambapo lilitokea tukio lililosababisha mguu wa baba yangu usagwe baada ya gari la polisi kuligonga gari la baba wakati likifukuza gari lililodaiwa kuwa na magaidi.



Baba alilazwa hospitali kwa miaka miwili. Madaktari waliuunga mguu wake kwa vyuma na akafanikiwa kuwa na miguu yake miwili. Baba aliporudi nyumbani, Alhakim alikuwa anafika kumsalimia. Hapo nyumbani ndipo Alhakim aliponiona na kunifahamu.



Siku nyingine nilikutana naye wakati ninatoka shule akasimamisha gari lake na kunipa lifti.



Alikuwa mtu mnene aliyekaribia umri wa miaka sitini. Alikuwa na nywele nyeupe anazoziziba kwa kofia yake ya darizi. Akaniuliza nilikuwa ninasoma kidato cha ngapi. Nikamwambia ninasoma kidato cha tatu.



“Mwakani ndiyo namaliza kidato cha nne.”

“Mmezaliwa wangapi?”

“Watano, lakini mwanamke ni mimi peke yangu.”

“Wewe ni wangapi?”

“Mimi ni wa mwisho.”



Tulipokuwa tunakaribia kufika nyumbani, Alhakim alitoa shilingi laki mbili akanipa kasha akasimamisha gari.



“Nadhani kwa hapa unaweza kwenda mwenyewe. Kuna mahali ninataka kufika. Naona nikuache hapa.”

“Asante, ninashukuru.”



Nikafungua mlango wa gari na kushuka kisha nikaanza kutembea kwa miguu. Baada ya kupiga hatua kumi hivi, niligeuka nyuma kumtazama. Niikaona hakuondoka. Alikuwa ameduwaa, akinitazama kwa nyuma. Alipoona nimemuona akaliondoa gari haraka na kwenda zake.



Nikaendelea na safari yangu hadi nyumbani. Sikuweza kufahamu kwa nini yule mzee amenitazama vile na alipoona nimemuona, akaliondoa gari haraka. Kwa vile nilikuwa ninazifahamu tabia za baadhi ya wanaume sikuendelea kumfikiria nikaendelea na shughuli zangu.



Siku iliyofuata ilikuwa ni sikukuu, hakukuwa na masomo. Alhakim na mwenzake ambaye sikumfahamu walifika nyumbani kumsalimia baba. Walizungumza chumbani mwake kwa karibu saa nzima kisha wakatoka. Ilipofika usiku wakati nimekaa na mama sebuleni akaniambia.

“Mwanangu umepata mchumba…”

Nikashtuka na kumuuliza.

“Ni nani?”

“Saidi Omar (Alhakim).”



Nikaduwaa kidogo. Nilifikiria alivyonipa zile laki mbili za bure nikafikiria vile alivyokuwa amesita, akinitazama wakati aliponishusha baada ya kunipa lifti. Kumbe kunitazama kule alikuwa na lake.



“Sasa yule si kama baba yangu?” Nikamuuliza mama.

“Kama baba yako kivipi?”



“Ni mtu mzima kisha yuko na baba.”

“Utu uzima wake si tatizo. Mwanaume hana cha utu uzima. Mwanaume mzee anaweza kumuoa binti mdogo. Lakini yule tumempenda kwa sababu ni mtu mwenye uwezo wake.”

“Kwani hana mke.”

“Amesema aliachana na mke wake.”

“Ana watoto.”

“Umeshasema ni mtu mzima, atakosa kuwa na watoto?

Watoto anao!”



“Kwa hiyo baba amemkubali?”

“Amempa sharti lake, amemwambia atoe kifunga uchumba cha shilingi milioni mbili, amekubali.”

“Sasa mama si mnafahamu kuwa ninasoma. Atanioa vipi?”

“Atakusubiri umalize masomo yako ndiyo akuoe.”



Kilichonifanya nisite sana ingawa Saidi Omar au Alhakim alikuwa na uwezo wa kipesa ni kwamba nilikuwa na mpenzi wangu ambaye tulipanga tuoane katika siku za mbele tutakapokuwa tayari. Sasa kitendo kile cha Saidi Omar kutaka kufunga uchumba na mimi kilikuwa ni kinyume na kile nilichokuwa nimepanga na mpenzi wangu.



Licha ya kwamba Alhakim alikuwa na uwezo, alikuwa mtu mzima sana na alikuwa na watoto wakubwa. Kwa vyovyote vile nisingeweza kuishi naye kwa amani. Yatakuwa ni mapambano kati yangu na watoto wake.



Lakini kwa vile wazazi wangu wametaka, nikanyamaza kimya huku nikiendelea kufikiria. Kuna siku nyingine nilikutana tena na Alhakim. Tulikutana Kariakoo. Mimi nilikuwa ninapita na hamsini zangu, yeye alikuwa akitoka katika duka la spea za magari.



Akaniona na kusimama.

“Habari yako?” Akaniuliza.

“Nzuri. Shikamoo…”

“Marahaba. Habari ya nyumbani?”

“Nzuri.”

“Baba anaendeleaje?”

“Anaendelea vizuri…”



“Mpaka pale mzee anaweza kutembea mwenyewe tunashukuru Mungu. Mimi nilihisi angekatwa mguu. Lakini tunashukuru sana,”

Alhakim akaniambia. Sikusema kitu. Nilikuwa nikitazama pembeni.

“Umepata salamu zangu?”

Akaniuliza.

“Kutoka wapi?”

“Kutoka kwa wazazi wako?”



Nikafahamu salamu zenyewe ni yale maneno niliyoambiwa na mama. Kwa vile nilikuwa ninamheshimu Alhakim, nilimwambia.

“Nimepata.”

“Umeridhika?”

“Bado ninafikiria.”



“Unafikiri nini Esma? Mimi nitakusubiri umalize masomo yako na ikiwezekana masomo yako nitayagharamia mimi hadi chuo kikuu. Ukimaliza masomo nitakununulia gari la kutembelea. Utaniambia unapenda gari la aina gani?”



Nilikuwa nimenyamaza nikiyafikiria maneno yake. Nilimtazama machoni kwa sekunde kama mbili tu kasha nikaugeuza uso wangu upande mwingine. Niligundua Alhakim alikuwa mtu mwerevu na mwenye hila.



Muda wote alikuwa akitabasamu. Kutokana na kile alichoonesha kuwa na uzoevu wa kuzungumza na wanawake, alikuwa habandui macho yake usoni kwangu. Yale macho yalikuwa na kazi ya kuzuga akili yangu ili maneno yake yaniingie.



“Kwani baba amekwambia nini?” Nikamuuliza.

“Baba yako nimeshakubaliana naye, umebaki wewe tu.”

“Kama mmeshakubaliana na baba, mimi nitasema nini?”

“Si umeniambia mpaka ufikirie?”



“Ni sawa. Binadamu unapoambiwa kitu lazima ufikiri. Huwezi kukubali tu. Kwa vile suala liko kwa wazazi watalimaliza wao.”



Mfu Aliyerudiwa na Uhai “Mimi nataka uniambie kwa kauli yako mwenyewe kwamba umeafikiana na uchumba wangu?”

Nikafikiri kidogo na kuona ni vizuri nimkubalie hivyo anavyotaka ili tusipoteze muda mrefu kwa suala hilo.



“Unachotaka wewe nikwambie tu kuwa nimeafikiana na uchumba wako?”

“Ndiyo.”

“Nimeafikiana nao…”



Mzee Alhakim akacheka kabla ya kuniambia. “Niambie kesho nitakuona wapi twende madukani nikufanyie shopping?”

“Nitakuwa nyumbani.”



“Si vizuri mimi kukufuata nyumbani kwa sababu pale kuna wazazi wako. Haitakuwa heshima kukufuata pale. Niambie mahali pengine.”

“Labda uniambie wewe.”



Alhakim aliwaza kidogo kasha akaniambia.

“Unakumbuka pale nilipokushusha na gari siku ile?”

“Ndiyo, ninapakumbuka.”

“Nisubiri pale.”

“Saa ngapi?”

“Saa nne asubuhi.”



“Si unafahamu kuwa saa nne nitakuwa shule labda nitakapotoka.”

“Unatoka shule saa ngapi?”

“Ninatoka saa tisa, lakini nitakusubiri pale saa kumi.”

“Hakuna tatizo kwa sababu saa kumi bado maduka yapo wazi. Nitakupitia saa kumi.”



Wakati tunataka kuagana alitia mkono mfukoni akatoa bunda la noti, akahesabu shilingi elfu hamsini akanipa.

“Chukua hii itakusaidia kwa usafiri.”



“Asante,” nikamwambia na kuzitia kwenye pochi yangu ndogo niliyokuwa nimeishika mkononi.



Je, nini kiliendelea?
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi @Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad @Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya Lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO @multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden@bwii ONTARIO Kobe The Vein mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya SITAKI ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo @shedede kamtu33 SteveMollel Ngushi DONALD stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 Ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny @Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90 Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero agprogrammer JoJiPoJi @Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga ABB SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe salaniatz Natasha Ismail jiwe jeusi chibalangunamchezo
John Mloy conjuget Van Pauser great G Mtoto wa nzi Zeus1 hindustan Sci-Fi MAN OF PEACE kashata emnly danny baraka bb MTOTELA kbosho TEMLO DA VINCA
 
SEHEMU YA 02



Wakati tunataka kuagana alitia mkono mfukoni akatoa bupa la noti, akahesabu shilingi elfu hamsini akanipa.

“Chukua hii itakusaidia kwa usafiri.”

“Asante,” nikamwambia na kuzitia kwenye pochi yangu ndogo niliyokuwa nimeishika mkononi.

SASA ENDELEA…

BAADA ya hapo tukaagana nikaendelea na safari yangu na yeye akaingia kwenye gari lake.


Wakati nikiwa katika nyendo zangu niligundua kuwa yule mzee alikuwa akinifuata na gari lake kimya kimya kunichunguza nilikuwa ninakwenda wapi. Bila shaka alifikiria kuwa nilikuwa ninakwenda kwa wanaume.

Nilipomuona nilizuga nikaingia katika duka fulani. Nikatazama tazama vitu na kuuliza bei kisha nikatoka. Nikaona alikuwa ameliegesha gari lake kwa mbali. Nikafahamu kwamba ataendelea kunifuata na mimi sikutaka afahamu nilikuwa nakwenda wapi, nikaahirisha safari yangu na kwenda kwenye kituo cha daladala. Nikapanda daladala na kurudi nyumbani.

Licha ya kile kitendo chake kutonifurahisha, nilifurahia pesa alizonipa ikiwemo ile ahadi yake ya kesho yake ya kwenda kunifanyia shopping.

Vile nilivyofahamu kuwa alikuwa na uwezo wa kipesa nilihisi kuwa angenifanyia shopping ya nguvu kwa vile nilivyomwambia kuwa nimeafikiana na dhamiri yake ya kutaka kunioa.

Nilimuona mzee tena mwenye watoto wa umri wangu. Na bado nilikuwa nafikiria mustakbali wake na wangu lakini kama wasemavyo wahenga; “Baniani mbaya, kiatu chake dawa.”

Kama kulikuwa na kitu chochote kilichokuwa kinanivutia kwake ni pesa zake tu alizokuwa akinipa mara kwa mara ambazo nilikuwa sizipati hata kwa mpenzi wangu niliyekuwa nampenda kwa dhati ya moyo wangu.

Niliwaza hata kama Alhakim atanioa bado nitaendeleza uhusiano wangu na mpenzi wangu. Sitakuwa tayari kumuacha labda kwa kifo kwa sababu nilikuwa nampenda wakati yule mzee sikumpenda.

Siku iliyofuata nilipotoka shule niliharakisha kurudi nyumbani. Nikaoga harakaharaka na kubadili nguo. Kwa kawaida ninapotoka nyumbani kwetu huwa sibanwibanwi sana bora tu niseme ninakwenda wapi ili watu wafahamu niko wapi.

Nikamwambia mama kuwa ninakwenda kwa rafiki yangu mtaa wa pili kusoma kwa sababu mtihani ulikuwa unakaribia.

Nilipotoka nyumbani nikaenda pale nilipoahidiana kukutana na Alhakim. Nilipofika nikakuta ameegesha gari lake pembeni mwa barabara akinisubiri. Nilikwenda kufungua mlango wa upande wa pili wa dereva nikaingia kwenye gari.

“Shikamoo,” nikamwamkia.

“Marahaba. Habari ya nyumbani?” akaniuliza huku akiliwasha gari.

“Nzuri.”

Alitia gia tukaondoka. Watu wa mtaa huo walikuwa wakitutazamatazama tangu ninaingia kwenye gari hilo hadi tunaondoka.

Si unafahamu tabia za binaadamu kutaka kudadisi kila kitu.

“Ulifika muda mrefu?” nikamuuliza Alhakim.

“Si muda mrefu sana.”

“Labda nimechelewa kidogo kwa sababu walichelewa kututoa shuleni,” nikamdanganya.

“Kulikuwa na nini?”

“Walimu walitupa kazi ya kusafisha mazingira kabla ya kuondoka.”

“Inabidi uvumilie, ndiyo maisha ya shule.”

“Ni kweli lakini wakati mwingine walimu wanatuchokesha.”

“Na ni kwa nini wanafanya hivyo?”

“Kiburi tu. Kwa vile ni walimu wetu basi wanataka kutuonesha kuwa wao ndio kila kitu. Mtu anafika shule na hasira zake anazimalizia kwa mwanafunzi.”

“Na nasikia kuna huu mtindo wa baadhi ya walimu kuwatongoza wanafunzi wao, ni kweli?”

“Ni kweli. Wapo walimu wenye tabia hiyo. Sasa pale ukimkataa ndio anakufanyia visa lakini chanzo ni hicho.”

“Kwa hiyo na nyinyi mliwakataa walimu wenu ndio wakaamua wawape kazi katika muda wenu wa kurudi nyumbani ili kuwakomoa?”

“Labda wenzangu lakini mimi sina muda na mwalimu. Pale tumefuata masomo si mapenzi.”

Pengine maneno yangu yalimkosha Alhakim, nikamuona ametoa meno akicheka.

Pakapita ukimya wa sekunde kadhaa kabla sauti ya Halhakim kusikika tena.

“Mmeshazungumza na wazazi wako kuhusu hili suala?”

“Nilizungumza na mama.”

“Baba hakukueleza chochote?”

“Mara nyingi mimi huzungumza na mama sio baba. Kama baba atanieleza itakuwa siku nyingine.”

“Mimi nikikuoa wewe utaweza kuwasaidia wazazi wako kipesa. Si unaona baba amepata tatizo la mguu na hataweza kufanya kazi tena. Atakuwa anawategemea nyinyi watoto wake.”

Alhakim aliponiambia hivyo sikusema kitu ingawa nilikuwa na mengi ya kumuuliza. Nilishindwa kumuuliza kwa sababu sikuwa nimemzoea ukizingatia pia alikuwa mtu mzima.

Ni sawa angenioa mimi na ningepata uwezo wa kipesa kuwasaidia wazazi wangu kutokana na yeye lakini watoto wake ameshawafahamisha kuwa anataka kuoa binti mdogo na kwamba watoto wake watakubali kuwa na mama ambaye wanamzidi kiumri?

Nikiwa mke wake, watoto wake wataniheshimu kama mama?

Ataweza kuwadhibiti watoto wake wasiingilie maisha yetu?

Isionekane nimekwenda kwake kutafuta pesa wakati yeye ndiye aliyenipenda mwenyewe.

Katika suala hilo la ndoa niliona kama ninakokotwa bila hiyari yangu kutokana na tamaa ya pesa.

“Umeshawahi kupanda ndege?” Alhakim akaniuliza ghafla na kuyakatiza mawazo yangu.

Nikatikisa kichwa.

“Sikuwahi kupanda ndege.”

“Safari nyingine tutakwenda kufanya shopping Zanzibar kwa ndege. Sifahamu kama baba yako atakubali uende na mimi Zanzibar.”

“Labda atakubali niende mwenyewe.”

“Atahisi nataka kwenda kinyume labda?”

“Mzazi yeyote ni lazima aoneshe kuwa anamdhibiti mwanawe hata kama kwenda mimi na wewe Zanzibar kusingekuwa na madhara. Hatuwezi kulaumu.”

Alhakim alitoa tena meno yake akacheka. Alikuwa mwepesi wa kucheka. Ingawa alitaka kunionesha uchangamfu na nimuone kuwa ni mtu mwema lakini licha ya utoto wangu nilifahamu kuwa watu wa aina yake ndio wanaokuwa madikteta ndani ya nyumba.

Anakuwa mwepesi wa kucheka kabla ya kukuoa lakini akishakuweka ndani anabadilika na kuwa nunda! Hakuna kucheka. Wakati wote anakuwa mkali na vile anavyofahamu kuwa kwetu ni masikini ndio hatanithamini kabisa.

Tukatokea katika maduka ya Kariakoo. Tuliingia katika maduka matatu tofauti. Aliniambia nichague vitu ninavyovitaka. Sikuona aibu. Nilimkomoa.

Nilichagua nguo na vitu vingine vyenye thamani ya karibu shilingi laki nne. Mzee alilipa.

Akanirudisha karibu na kwetu kisha akaniacha.

Nilipofika nyumbani sikumficha mama. Nilimwambia kwamba Alhakim ameninunulia nguo na vitu vingine vyenye thamani ya shilingi laki nne.

“Si unaona mwenyewe. Ndoa bado lakini anakugharamikia!” Mama akaniambia na kuongeza.

“Mimi nakushauri mwanangu kubali akuoe.”

Sikusema kitu. Nikapanga nguo zangu ndani ya kabati.

Siku za mwishoni mwa wiki ndizo siku ambazo hukutana na mpenzi wangu. Alikuwa anaitwa Macheo, mfanyakazi wa shirika la bandari.

Macheo alikuwa mzaliwa wa Tanga. Aliwahi kuniambia alizaliwa Mwarongo eneo lililopo katika barabara ya Pangani kilometa kadhaa kutoka Tanga.

Elimu ya msingi alisoma Tanga lakini elimu ya sekondari na chuo alisoma Dar na akapata kazi hapo hapo Dar.

Wakati tunakutana na kuanza uhusiano alikuwa na miezi kadhaa tangu ameanza kazi yake.

Kwa vile alikuwa ndio anayaanza maisha na mimi bado ninasoma, tuliweka mikakati ya kuoana siku za mbele baada ya mimi kumaliza masomo.

Lakini uhusiano wetu ulikuwa siri yetu mimi na yeye. Nyumbani kwetu walikuwa hawafahamu kitu.

Je, nini kiliendelea?
 
SEHEMU YA 03



Elimu ya msingi alisoma Tanga, lakini elimu ya sekondari na chuo alisoma Dar na akapata kazi hapohapo Dar.

Wakati tunakutana na kuanza uhusiano, alikuwa na miezi kadhaa tangu ameanza kazi yake.

Kwa vile alikuwa ndiyo anayaanza maisha na mimi bado ninasoma, tuliweka mikakati ya kuoana siku za mbele baada ya mimi kumaliza masomo.

Lakini uhusiano wetu ulikuwa siri yetu mimi na yeye. Nyumbani kwetu walikuwa hawafahamu kitu.

SASA ENDELEA…

SIKU
za mwishoni mwa wiki huondoka asubuhi na kwenda kushinda nyumbani kwake, Tabata.

Kulikuwa na siku wazazi wangu wote waliniweka kikao na kunieleza kwamba wameshachukua pesa za uchumba kutoka kwa Alhakim. Kwa hiyo baba alitaka nitambue kuwa nilikuwa mchumba wa mtu.

“Ukimaliza masomo tu mnaoana,” baba aliniambia.

Nilikuwa ninawaheshimu sana wazazi wangu kiasi kwamba nilishindwa kupingana nao kuhusu suala hilo. Kila nilichoambiwa nilikuwa ninaitikia tu.

Lakini sikuona sababu ya kuacha kwenda kwa Macheo kwa sababu nilikuwa ninampenda. Kama kutakuwa na kitu ambacho kitatia doa katika ndoa yangu na Alhakim ni uhusiano wangu na Macheo ambao niliamini hata nitakapoolewa, bado utaendelea kuwepo.

Wakati wote nilikuwa nikimficha Macheo kuhusu suala la uchumba wangu na Alhakim. Lakini baada ya kufikiri sana, nikaona nikampe ukweli. Nikafunga safari kwenda Tabata.

Kwanza nilipitia Kariakoo, nikanunua vitu nilivyokuwa ninavitaka. Lakini wakati ninazunguka kwenye maduka, nililiona gari ya Alhakim, lakini mwenyewe sikumuona.

Nikaondoka haraka kwenye eneo hilo. Nikiwa katika mtaa mwingine sasa nikielekea katika kituo cha daladala. Nikaliona tena gari la Alhakim nyuma yangu. Nikagundua kuwa Alhakim alikuwa akinichunguza.

Sasa nifanye nini?

Nikafanya kama sikuliona gari lake, nikatembea harakaharaka kuelekea katika kituo cha daladala. Kwa bahati nzuri nilipofika tu daladala likasimama. Nikaingia haraka na kukaa kwenye siti. Daladala likaondoka.

Wakati ninashushwa kwenye kituo cha Tabata, nikaona gari la Alhakim hatua chache nyuma ya daladala.

Nikasema: “Mama yangu wee!”

“Huyu mzee ameniamulia leo!” Nikasema kimoyomoyo nikiwa nimeduwaa kando ya barabara nikiigiza kama ninasubiri magari yapite ndiyo nivuke barabara.

Kwa pembeni mwa macho yangu nililiona gari la Alhakim bado limesimama nyuma ya daladala. Mahali liliposimama, Alhakim alikuwa akiniona vizuri.

Bila shaka alikuwa anasubiri kuona ninaelekea wapi aendelee kunifuata.

Sasa nilithibitisha waziwazi kuwa Alhakim alikuwa ananifuatilia. Iliwezekana alishagundua kuwa nina mtu wangu mitaa ya huku ndipo alipoamua kuiandama daladala niliyopanda aone mwisho wangu.

Pale nilikuwa sina mbinu tena.

“Sasa nifanye nini?” Nikaiuliza nafsi yangu iliyokuwa imegwaya.

Nikawaza kwamba kama nitaendelea na safari yangu, Alhakim ataendelea kunifuatilia na kugundua ninakwenda wapi.

Pia niliona kubadili mawazo na kurudi isingekuwa busara. Ingempa picha kuwa nimerudi baada ya kumuona yeye.

Bado angeweza kuniuliza nilikuwa ninakwenda wapi na kwa nini nimeamua kurudi. Nisingekuwa na la kumwambia.

Sikuwa nimepata ufumbuzi. Nikaliona daladala linaondoka baada ya kushusha watu na kupakia wengine.

Niliwaza kwamba kama nitabaki palepale huku daladala limeondoka, Alhakim angepata nafasi nzuri ya kunifuata na nisingeweza kumkimbia tena.

Nikaona niwahi kuvuka barabara kabla daladalaa hilo kunipita. Nikavuka barabara. Ingawa hakukuwa na gari lolote lililokuwa linapita, nilipiga mbio hadi ng’ambo ya pili.

Sikutaka hata kugeuka kutazama nyuma, nikaingia kwenye vichochoro. Nilifahamu kwamba asingeweza kunifuata kwa gari kwenye vichochoro labda kama angekuwa na pikipiki.

Baada ya kukatiza vichochoro viwili, vitatu, nilichanganyika na watu wengine waliokuwa wanapita. Kwa vile nilikuwa nimezibwa nikatazama nyuma.

Moyo wangu ulishtuka nilipomuona Alhakim akitembea kwa miguu kunifuata.

“Huyu mzee ana tatizo gani?” Niliwaza kwa hamaki.

Maisha yale ya kuchungwa nilikuwa siyataki.

Nikaurudisha mbele uso wangu haraka na kuongeza mwendo. Kama atagundua ninamkimbia yeye shauri yake. Nani alimwambia anifuatefuate, nilisema peke yangu nikiwa nimechukia.

Nilikatiza tena kwenye vichochoro vingine nikatokea katika mtaa aliokuwa anaishi Macheo, lakini sikwenda nyumbani kwake.

Niliwaza kwamba kama Alhakim yuko nyuma yangu ataona nikiingia.

Niliipita nyumba ya Macheo ili kumpoteza Alhakim. Nikatokea mtaa mwingine. Nikasimama kwenye kioski na kununua vocha. Hapo nilikuwa ninamtega Alhakim kuona kama atatokea.

Baada ya kununua vocha na nilipoona simuoni tena ndipo nikarudi tena kwenye mtaa wa akina Macheo.

Hata hivyo, bado nilikuwa ninatembea huku ninatazama nyuma. Mzee nilishamchenga. Sikumuona tena.

Nilipoifikia nyumba yake, nilisukuma mlango na kuingia ndani harakaharaka.

Macheo aliyekuwa ameketi sebuleni akitazama video za muziki alishtuka alipoona ninaingia bila hodi.

“Vipi?” Aliniuliza huku akinitazama usoni.

“Poa tu,” nikamwambia na kuketi kwenye sofa.

“Mbona unatweta?”

“Kulikuwa na mzee ninayemkimbia…”

“Unamkimbia? Ana nini? Kichaa?”

“Si kichaa, ni mzima na akili zake bali alikuwa ananifuatilia…”

“Anakufuatilia, anakufahamu?”

“Ndiyo nilikuwa nimefika kwako kukueleza kuhusu yeye, kumbe naye alikuwa ananifuatilia na gari. Nashuka tu kwenye daladala nikamuona. Nikamkwepa na kuingia kwenye vichochoro. Kumbe aliacha gari na kunifuata kwa miguu…”

“Sasa ana tatizo gani?”

“Baba yangu alikuwa anafanya kazi ya udereva kwake. Huyo mzee kila akifika nyumbani kumtazama baba baada ya kuumia mguu alikuwa ananiona. Akamwambia baba kuwa anataka kunioa. Baba akakubali, akamwambia ampe shilingi milioni mbili za uchumba. Mzee akazitoa…”

Nikamuona Macheo akigwaya.

“Kumbe mwenzangu umeshapata mchumba!”

“Nifanye nini wangu? Wazazi wangu wamemtaka!”

“Duh! Sasa mbona unaendelea kufika kwangu?”

“Hutaki nifike tena baada ya kukwambia hivyo?”

“Hapana. Nimepata uoga. Umekuwa mchumba wa mtu na mwenyewe anakufuatilia.”

“Huo uchumba wake hautaharibu uhusiano wetu…”

“Kweli?”

“Uhusiano wetu utaendelea tu. Kila mtu anataka mapenzi. Na mapenzi unayapata kwa yule umpendaye.”

“Kwa hiyo huyo mchumba hukumpenda?”

“Kwa kweli sikumpenda, kwanza ni mzee sana!”

“Lakini ana pesa?”

“Pesa anazo. Ameniambia ataninunulia gari na hivi karibuni tutakwenda kufanya shopping Zanzibar kwa ndege.”

“Walichokosea wazazi wako ni kwamba hawakutaka kufahamu mawazo yako. Kwa vile wao ni wazazi, wakaona watoe wao uamuzi.”

“Hilo ni kosa, lakini siwezi kuwalaumu kwa sababu hivi sasa baba yangu hafanyi kazi, lakini analipwa mshahara kila mwezi na Alhakim na ni kwa sababu yangu.”

“Sasa, hivi alivyokuona huku anahisi ni kwa nani wako?”

“Nadhani anashuku kuwa nina mtu wangu huku.”

“Akitugundua itakuwa vipi?”

“Sitaki agundue, ndiyo maana nimemkimbia na siku atakaponiuliza nitamwambia nilikuwa ninaenda kwa shangazi yangu.”

“Sasa utakuwa unafika huku kiwiziwizi?”

Je, nini kiliendelea?
 
SEHEMU YA 04



Huyo mtu atakuoa wakati huu unasoma au…”

“Anasubiri nimalize masomo.”

“Lini?”

“Hapo nitakapomaliza.”

“Kwa hiyo ukienda kidato cha tano na cha sita atakusubiri tu?”

SASA ENDELEA…

“WAO wana imani kuwa mwisho wangu ni kidato cha nne.”


“Kwa hiyo ukifaulu huendelei na masomo?”

“Nani? Nitaendelea na masomo. Anayetaka kunisubiri atasubiri akikata tamaa shauri yake.”

“Mara nyingi uchumba wa hivyo si mzuri. Lolote linaweza kutokea hapo katikati.”

“Na litokee tu, unioe wewe mpenzi wangu.”

“Siwezi kushindana na huyo mzee. Labda ashindwe mwenyewe.”

Siku zote ninapokwenda kwa Macheo ninashinda kutwa nzima, siku ile niliondoka mapema kwa sababu ya Alhakim.

Nilimwambia macheo asinisindikize kwa kuhofia tungeweza kukutana na Alhakim akiendelea kuranda na mitaa kunisaka. Yule baba ana wivu si mchezo!

Nilitembea huku nikiangaza kila upande hadi nikafika kwenye kituo cha daladala nikasubiri. Daladala ilipofika nikaondoka.

Nikiwa ndani ya daladala nilikuwa nikimuwaza Alhakim, mtu ambaye alikuwa katika safari ya kuwa mume wangu. Tukiwa katika uchumba tu alikuwa tayari kupoteza muda wake kunichunguza mimi, atakaponioa itakuwa vipi? Nikawaza.

Kwa kweli alishaanza kunitia hofu. Nilichogundua ni kuwa Alhakim alikuwa na wivu mkali au niseme wivu uliopitiliza.

Niliwaza kwamba nitakapokuwa mke wake sitaruhusiwa kutoka nyumbani peke yangu. Na kama nitalazimika kutoka peke yangu ni lazima atakuwa akinifuata nyumanyuma ili kuona kama nilikuwa ninakwenda safari niliyomuaga au ninakwenda safari nyingine.

Hayo hayakuwa maisha yaliyokuwa akilini mwangu, maisha ya kufuatana na mume kila mahali. Nitakuwa kama mtumwa wake nisiye na uhuru wa kuamua pa kwenda.

Kibaya zaidi ni kuwa Alhakim huyohuyo ndiyo amekuwa tegemeo kwetu. Wazazi wangu wanaona akinioa yeye ndiyo watakwamuka kiuchumi, ndiyo tutapata maendeleo, ndiyo maisha yangu na yao yatakuwa mazuri. Sikuwa na shaka yoyote kwamba hayo masuala ya wivu wake hayakuwa na uzito kwao.

Wakati nafika nyumbani nikaliona gari la Alhakim lipo barazani. Nikashituka sana. Miguu ilinitepeta kwa hofu. Nusura ningeanguka chini.

Niliwaza Alhakim amefuata nini nyumbani kwetu baada ya kunikosa kule alikokuwa akinifuata? Amefika kwetu kunishitakia au kunisubiri aniulize ni kwa nini nilimchenga?

Makubwa! Badala ya kuingia nyumbani kwa kutumia mlango wa mbele, nilitumia mlango wa nyuma ambao Alhakim alikuwa hautumii.

Uani sikukuta mtu, nikaingia ukumbini ambako pia sikukuta mtu lakini nilisikia sauti ya baba akiongea sebuleni. Nikaingia chumbani kwangu kimyakimya.

Nilibana mlango kisha nikalala kitandani na kuendelea kuwaza.

Mara nikaisikia sauti ya mama ukumbini.

“Sikumbuki kama yumo au hayumo kwa sababu aliniambia anakwenda kwa mama yake mdogo anaumwa,” nikamsikia mama anasema uongo kunitetea.

Hapohapo mlango wa chumbani kwangu ukasukumwa nikafumba macho yangu kama vile nilikuwa nimelala.

Nikamsikia mama akiniita. “Esma…!”

Nikafumbua macho yangu na kumuitikia.

“Abee…!”

“Umelala muda huu?”

“Kichwa kinaniuma.”

“Basi lala kama kichwa kinakuuma. Alhakim alikuwa anakuulizia.”

Mama akafunga mlango. Nikamsikia akisema huku akitembea ukumbini.

“Kumbe amelala…kichwa kinamuuma.”

Baada ya hapo sikuisikia tena sauti yake.

Sikuweza kufahamu Alhakim alipoambiwa nipo alisema nini wakati aliniona kule Tabata.

Niliendelea kubaki chumbani mpaka nilipolisikia gari la Alhakim limewashwa, ndipo nikatoka chumbani.

Nilikwenda uani nikamkuta mama akifua nguo.

Kwanza nilikwenda msalani, nilipotoka nikachukua mbuzi ya kukunia nazi na kwenda kukaa karibu yake.

“Kichwa kimetulia?” akaniuliza akiamini kuwa kweli kichwa kilikuwa kinaniuma.

“Kimetulia.”

“Ulikuwa umekwenda wapi na ulirudi saa ngapi?”

Kwa kudhani kwamba huenda Alhakim aliwaambia kuwa aliniona Tabata, nikaona niseme ukweli kuwa nilikwenda huko.

“Nilikwenda Tabata kuchukua kitabu changu.”

“Kitabu cha nini?”

“Kitabu cha shule, nilimuazima mwanafunzi mwenzangu na kesho kinatakiwa shule.”

“Mbona hukuaga kama unakwenda Tabata?”

“Nilipoondoka hapa nyumbani sikuwa na wazo la kwenda huko. Nilikwenda mtaa wa pili kwa rafiki yangu. Sasa nikiwa huko ndiko nikapata wazo la kwenda Tabata.”

“Unazunguka sana mwanangu wakati umeshakuwa mchumba wa mtu.”

“Hata kitabu changu nisikifuate kwa sababu nimekuwa mchumba wa mtu?”

“Unadhani mwenyewe akikuona atafikiri nini?”

“Kwani amesema ameniona?”

“Hakusema hivyo lakini nakuuliza mimi kama akikuona atafikiri nini?”

“Afikiri nini, kwani ameshanioa?”

“Hata kama, inakupasa uweke heshima na heshima ya mwanamke ni kutulia nyumbani kwao.”

“Sasa subiri nikwambie kitu mama. Huyu mzee ana tabia ya kunifuatafuata anaponiona.”

“Alikufuata wapi?”

“Ni mara nyingi. Ninaweza kuwa natembea nikashitukia ananifuata na gari lake. Hii leo pia alinifuata hadi Tabata nikamchenga.”

“Unasema kweli?”

“Nasema kweli. Ana tabia ya kunifuatafuata.”

“Si nimekwambia acha tabia ya kuzururazurura. Anaweza kukuona. Sasa kama hivyo unavyosema amekufuata hadi Tabata na ndiyo maana alifika hapa na kukuulizia.”

“Lakini hakusema kama aliniona?”

“Hakusema, labda alitaka tu kufahamu kama umesharudi.”

“Sasa maisha haya ya kufuatana hadi lini?”

“Yule ni mwanaume lazima akufuatefuate, afahamu nyendo zako.”

“Sasa hapo atakaponiona si itakuwa shida.”

“Hakuna shida yoyote. Hakuna mwanaume atakayekupa uhuru unaoutaka wewe.”

“Mmh….!”

Nilipoona mama hakubaliani na mimi nikainuka na kumuacha aendelee kufua nikarudi chumbani kwangu.

Siku iliyofuata nilikwenda shule. Wakati ninatoka shule nilikuwa na wenzangu tumefuatana tukizungumza.

Ghafla nikaliona gari la Alhakim. Lilikuwa limeegeshwa mbali kidogo na geti la shule.

Upande lilipoegeshwa ulikuwa tofauti na barabara tunayotumia tukitoka shule. Sisi tulipita barabara nyingine tukaendelea na safari yetu ingawa nilifahamu kuwa Alhakim alifika pale kunitega mimi.

Niliwahi kukariri maelezo ya mtaalamu wa saikolojia aliyesema kwamba baadhi ya akili za watu wenye umri kuanzia miaka sitini na kuendelea hupungua na kutazama suala hilohilo kila wakati na kila siku. Alitoa maelezo mengi lakini mimi nilishika hayo.

Niliamini Alhakim alikuwa miongoni mwa watu hao wanaotazama suala hilohilo kila wakati na kila siku. Kunifuatilia mimi ilikuwa ni agenda yake kuu. Hakuwa na lingine.

Sikumlaumu kwa sababu yalikuwa ni maumbile. Kila binadamu ana tabia yake tofauti na mwenzake na kila rika lina tabia zake tofauti na rika lingine. Kama nitakuwa na kazi ya kulaumu watu kutokana na tabia walizonazo, mimi pia ningelaumiwa kwani kwa vyovyote vile siamini kwamba vitendo vyangu vyote vinawapendeza wenzangu.

Niliendelea kutembea na wenzangu huku tukizungumza hili na lile. Kwa vile tulikuwa kundi kubwa tukaanza kupungua. Wengine walishika barabara nyingine inayoelekea kwao.

Baadaye nikabaki peke yangu. Ili uone kama yule mzee ananifuatilia, nililiona gari lake mbele yangu. Hapo sikuwa na mbinu ya kulikwepa.

Nikaenda kwenye mlango wa dereva. Alhakim alikuwa ametoa kichwa. Sikutaka kusubiri aniite, kwa vile nilishamuona ikabidi nimfuate.

“Shikamoo,” nikamwamkia.

“Marahaba. Ingia garini twende,” akaniambia.

Nikazunguka upande wa pili wa gari nikafungua mlango na kuingia

Je, nini kiliendelea?
 
SEHEMU YA 07



“Kwa vile mama yako ndiye amesema hivyo, nitafanya bidii nipate hizo pesa kabla ya wiki hii kumalizika.”

“Itakuwa vyema kama zitapatikana haraka.”




SASA ENDELEA…

“INA
maana kwamba Alhakim akirudishiwa hizo pesa na uchumba utakuwa umekwisha?”

“Sasa nani atamkubali mchumba aliyetiwa mimba na mtu mwingine?”

“Kwa hiyo mimi ndiye nitakuwa mchumba wako?”

“Si unafahamu mila zetu, wewe ndiye umeniharibu na ndiye utakayenioa.”

“Baba anafahamu hivyo?”

“Baba hafahamu chochote. Mama ndiye niliyezungumza naye. Sasa labda yeye atamwambia.”

“Kwa hayo mawazo kwamba nirudishe hizo pesa za Alhakim yametoka kwa mama?”

“Yametoka kwa mama. Ameona mambo yameshaharibika sasa anataka kuyaweka sawa. Alihisi tatizo kubwa ni pesa za watu.”



“Ni lazima tufahamu na mawazo ya baba, ni kama hayo ya mama au atakuwa na mawazo mengine.”

“Mshauri wa baba ni mama. Kama mama amesema hivyo, baba hatakuwa na kipingamizi. Watazungumza wenyewe.”

“Sasa mimi nitahangaikia hizo pesa. Kwa upande wangu pia sipendi yatokee matatizo kwa Alhakim.”

“Nitakwenda kumueleza mama ulivyoniambia.”

Kidogo nilimuona Macheo akiwa amepata ahueni. Na kutokana na maelezo ya Macheo, mimi pia nilipata ahueni.



Sote wawili tukahisi furaha ndani ya mioyo yetu. Tulikuwa kama tumeutua mzigo mzito uliokuwa unatuelemea.

Niliporudi nyumbani nikamueleza mama tulivyozungumza na Macheo.

“Sasa hizo pesa atazileta lini?” Mama akaniuliza.

“Ameniambia wiki hii.”

“Itabidi azilete yeye mwenyewe ili tuweze kumtambua.”

“Nitamwambia azilete mwenyewe. Kwani umeshamwambia baba?”



“Nilikuwa ninasubiri maelezo kutoka kwa huyo mwanaume. Sasa kama amesema atatoa hizo pesa, nitakuwa nimeshapata maelezo ya kumwambia baba yako ingawa ninafahamu kwamba atakasirika sana kwa sababu umeharibu heshima yake kwa Alhakim.” Hapo sikusema kitu. Nilinyamaza kimya.“Sasa utamueleza lini baba?”“Nitamueleza leo.”“Sasa akiniita nitamwabia nini?”“Swali hilo unamuuliza nani? Kwani mimi umenieleza nini?”“Wewe ni mama, yule ni baba. Si umesema ukimwambia atakasirika!” “Kama atakasirika utafanya nini na kosa limeshatokea?” “Basi akiniita na wewe uwe hapohapo.”

Mama hakukubali wala kukataa, nilipomwambia hivyo aliinuka na kwenda uani kuendelea na shughuli zake. Nikabaki peke yangu nikiwaza.



Nilikuwa ninamuonea haya sana baba kuliko mama. Akiambiwa ile habari na akifahamu nina mimba, kwa kweli nitamkwepa. Sitaweza kuusogeza uso wangu mbele yake.

Mzee yule mawazo yake yote yalikuwa kwa Alhakim. Kitendo cha Alhakim, mtu mwenye pesa zake, kunitaka mimi si tu kilimpa matumaini ya maisha baba yangu, bali kilimtia fahari kuona kwamba mwanawe ataolewa na mtu mwenye pesa.

Nilikuwa ninafahamu kwamba siku zote baba yangu alikuwa akiombea nimalize masomo ili niolewe na Alhakim. Sasa akisikia nimepata mimba, sikuweza kuelewa atafedheheka kiasi gani.

Lakini tatizo ndiyo limeshatokea. Tangu hapo Alhakim sikumpenda licha ya kuwa na pesa. Niliyekuwa nikimpenda ni Macheo ambaye nilianzana naye tangu nikiwa kidato cha tatu.



Lakini nguvu ya wazazi wangu ndiyo iliyonifanya nimkubali Alhakim licha ya kuwa mtu mzima kama baba yangu. Sikupanga nifanye ufisadi wowote wala Macheo hakupanga hivyo. Kilichotokea kilikuwa ni bahati mbaya. Sikupenda kitokee.

Siku ile ambayo mama aliniambia atazungumza na baba, asubuhi yake baada ya kunywa chai, baba akaniita sebuleni. Moyo wangu ulishtuka sana. Nilishafahamu nilichokuwa ninaitiwa. Nikaenda sebuleni kumsikiliza.

“Kaa hapo,” akaniambia.



Uso wake na sauti yake viliniashiria kuwa alikuwa amechukizwa.

Baada ya kukaa, akaniambia.

“Mwanangu kwa nini unanifanya hivi?”

Ili kukwepa macho yake makali yaliyokuwa yakinitazama, niligeuza uso wangu upande mwingine.

“Kama ulikuwa humtaki huyu mchumba ungesema kuliko kunifedhehesha kiasi hiki!” Baba aliendelea kuunguruma. Mama hakuwepo. Moyoni mwangu nilikuwa ninamuita mama awepo pale ili amtulize baba.



“Mama uko wapi?” Nilikuwa nikisema peke yangu.

“Sasa mimi nitamwambia nini Saidi Omar (Alhakim) wakati ameshatoa pesa zake kwa sababu yako?”

“Pesa zitatolewa.” Nilikuwa nikimwambia baba kimoyomoyo, lakini sikuthubutu kupandisha sauti.

“Saidi Omar ataona sisi si watu wastaarabu kabisa. Mimi sina hata uso wa kumtazama..!”

Sikumlaumu baba ingawa kweli nilikuwa nimemfedhehesha, lakini nilifahamu alikuwa akitetea maslahi yake kwa Alhakim. Alikuwa akipewa pesa burebure kwa sababu yangu. Alhakim akifahamu nimetiwa mimba hatampa tena pesa baba.



Baba aligeuza uso wake pembeni, akalitazama kwa ghadhabu kabati alilokuwa amelielekea kama vile ndilo lililomkosea.Pale ndiyo niliona kama baba alikuwa ameghadhibika.

“Wanaume walikuwa wanakusaidia nini. Kama ni pesa Saidi Omar alikuwa anakupa. Mama yako alikuwa ananiambia…” Baba alisema kama aliyekuwa akisema peke yake kwani uso wake ulikuwa umeelekea kwenye kabati.

Baada ya kimya cha sekunde chache, baba aliyarudisha macho yake kwangu.



“Sasa hebu niambie ni mwanaume gani uliyenaye,” akaniuliza. Alikwepa kuniambia ni mwanaume gani aliyekutia mimba.

“Anaitwa Macheo,” nikamwambia. Sauti yangu ilitokea kwa mbali kama niliyekuwa ndani ya shimo.

“Anaishi wapi?”

“Tabata.”

“Anafanya kazi gani?”



“Anafanya kazi bandarini.”

“Anafanya kazi gani, kazi ya ukuli au..?”

“Ni afisa…”

“Afisa gani anayeharibu mabinti wa watu?”

Aliponiuliza hivyo, macho yake yaliwaka kwa hasira. Alionekana alikuwa na mengi ya kunisema, lakini alishindwa kunimalizia maneno kwa sababu nilikuwa mwanaye, tena wa kike. Maadili yalikuwa yanamzuia. Vinginevyo angenichamba vya kutosha.

Baada ya kunitazama kwa sekunde kadhaa, akaendelea kuniambia.

“Huyo Macheo anaweza kurudisha pesa za watu?”



“Anaweza.”

“Ataleta hapa shilingi milioni mbili?”

“Ndiyo, ataleta.”

“Mama yako yuko wapi?”

“Yuko uani, ana kazi.”

“Hebu muite.”



Nikainuka kwenda uani. Mwili wote ulikuwa umetota kwa hofu.

“Mama unaitwa na baba,” nikamwambia mama.

Tulifuatana hadi sebuleni. Nikakaa mahali nilipokuwa nimekaa kwanza na mama akakaa kando yangu.

“Msikilize mwanao anavyosema. Ameniambia kwamba huyo mwanaume wake atatoa hizo pesa shilingi milioni mbili ili kutengua uchumba wa Saidi omar…” Baba alimwambia mama kisha akanitazama mimi.

“Si ndiyo ulivyosema hivyo?” Akaniuliza kwa mkazo.

“Ndiyo nimesema kwamba atatoa pesa hizo,” nikasema.

“Sasa atazileta lini?”

“Mpaka aambiwe!”



“Aambiwe na nani?”

“Yeye ndiye atakayemwambia,” mama akaingilia kati.

“Sasa mimi ninawapa wiki mbili. Huyo mtu afike hapa akiwa na hizo pesa.” Baba akasema.

“Sawa…”

Je, nini kiliendelea?
 
  • Thanks
Reactions: ita
hii story nilikuwa nafuatilia kwenye global pubishers tangu mwaka jana. haijaendeleaga ndio iliishia hapo hapo. kwa hyo poleni mnafuatilia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom