pongwer
Senior Member
- Mar 19, 2015
- 174
- 26
** MKASA MZITO **
Ilikuwa ni jioni moja baada ya kumaliza kazi zangu niliamua kwenda katika Hotel moja maarufu hapa Jijini Mtwara ili kupumzika nikipata vinywaji pmj na kuongea na jamaa zangu huku tukipata nafasi ya kubadilishana mawazo yenye lengo la kuboresha kazi zetu.
Kwa kawaida huwa sipendi sana kukaa sehemu za starehe mpaka mida mibovu kwani huwa napenda kuwahi kurudi nyumbani na kupata muda wa kuchat na kucheza na watoto pmj na mama yao na kamwe sikutaka chakula cha usiku nile nje ya nyumba yangu au kula huku watoto na mama yao wameshakula.
Ilipofika mida ya saa tatu kasoro niliagana na marafiki na kisha nikatoka zangu nje ili nianze safari ya kurudi nyumbani.
Nilipofika pale nje nilipopaki gari langu nilimkuta dada mmoja aliyekuwa kaegemea gari langu akilia kwa uchungu mkubwa.
Nilisimama pale kwa zaidi ya dakika moja bila kumwambia kitu chochote na baada ya uzalendo kunishinda pmj na muda kunitupa mkono nilimsogelea dada na kumsalimia ingawa hakunijibu nikamwomba asogee pembeni ili niondoke na gari langu.
Mbaya zaidi ni kwamba binti aliendelea kulia bila kunionesha dalili ya kunisikiliza na wakati huu nikawa mkali kidogo na kumwomba anipishe, lakini dada aliinuka na kuniangalia usoni na kusema" naombo kaka uniache nipumzike, nitakupisha kwani nina wakati mbaya sana hapa.
Kweli nilimpisha na kurudi ndani mara moja na kumvuta rafiki yangu mmoja aitwaye Chino na kumwambia yaliyonisibu nje.
Alinisihi kuwa ni vyema niende na kumhoji ana matatizo gani yaweza kuwa masuala ya mapenzi si wajua vibuti vinavyotawala siku hizi?
Basi nikatoka mpaka pale nje na kwa upole nikamuuliza ni yapi yalimsibu muda huu wa usiku kama huu.
Huku akitokwa na machozi yaliyoambatana na kilio cha kwikwi dada alianza kunisimulia kwa kusema"
"Kaka yangu mimi nimechumbiwa na kijana mmoja ambaye tulifahamiana naye miaka michache iliyopita, na tukaanza taratibu zote za harusi na hivi juzi ilikuwa iwe send-off yangu na amekuwa hapatikani na nilivyojaribu kumtafuta nikashindwa zaidi ya kusafiri kutoka Dar na kuja hapa mtwara.
Nimefanikiwa kuonana naye ila jibu alilonipa na nilichokishuhudia kwa macho yangu kimeniumiza sana kwani muda wote huo kumbe alikuwa ananitumia kwa kuwa niliachiwa mali nyingi na marehemu baba yangu na alitaka kuja kunitelekeza kabla ya mkewe wa ndoa kumshtukia....
Kaka nimeumizwa sana na sijui nifanyaje hapa nilipo kwani sina hata sent ya kunirudisha dar wala ya kunipatia malazi usiku huu" alimaliza kuongea bint huyo huku akiangua kilio cha uchungu kilichonipelekea na mimi kulengwa na machozi.
Kiukweli nilichukua waleti yangu na kutoa noti ya shilingi elfu kumi na nilipotaka kumpa wazo likanijia kuwa alihitaji msaada zaidi hivyo nikajivuta mpaka nyuma ya hotel na kumpigia mke wangu kumweleza hali halisi ya huyu bint na akakubaliana na mimi kuwa anahitaji msaada hivyo nirudi nae nyumbani na siku ya pili tumfanyie utaratibu wa kurudi Dar.
Tuliondoka pale na kufika nyumbani ambako mke wangu alitupokea na baada ya dakika chache familia nzima ikawa mezani kwa chakula cha usiku.
Tuliendelea na mazungumzo huku akitusimulia juu ya safari yake na majanga yaliyomsibu na wote tuliishia kumhuzunika na kumpa pole na kisha muda mfupi baadae alioneswa sehemu ya kupumzika na wote tukaenda kulala.
Asubuhi nikiwa katika maandalizi ya kuondoka mlango wa chumbani kwetu uligongwa na haraka mke wangu akajibu karibu akijua ni mtoto wetu ambaye alikuwa na kawaida ya kutuaga kabla ya kwenda shuleni.
Mke wangu aliyekuwa amelala aliamka na kwenda kuufungua mlango lakini cha Ajabu na cha kushangaza yule dada aliingia moja kwa moja mpaka chumbani na kuanza kupiga kelele akisema...
"yaani nimekuvumilia nimeshindwa ulidai nimdanganye kuwa mimi nina matatizo,na kuwa usiku ungemkimbia mkeo na kuja chumbani kwangu tulale wote lakini umepitiliza mpaka sasa,unaniona mimi kinyago wako? kama ni hvyo kwa nini uliniita toka dar na kwa nini leo hukunipangia hotel kama kila sikuunavyofanyaga"??
Hakika niliishiwa pozi,na nguvu pia na sikuweza kuongea kitu na kumwangalia mke wangu ambaye kwa wakati huo naye alikuwa hajui acheke au aliye kwa sauti au anipige nikiwa nini nifanye yule binti alizidi juniwashia moto kwa kusema" kwanza ulisema hii nyumba ni ya mwanangu People sasa kwa nini hzo document haunipi au nianze uchizi humu ndani???
nauliza??""
na kama hautaki kumwambia ukweli mkeo leo moto utawaka hapa ndani na siendi popote nimechoka kukaa Chilindima gest kwanza chafu na ni kama unanidhalilisha"
Nikanyanyuka na kumzaba kibao kimoja na wakati nikiwa natafakari nini kifanyike nilishangaa kuona mke wangu akipaki vitu vyake na kama haitoshi akaufunga mlango kwanje na kuondoka.
wakati huo machozi yalianza kunitiririka na kujuta kwa wema wangu jinsi ulivyoniponza na kuamua kumpigia rafiki yangu tuliokuwa wote jana usiku na kumpa mkasa mzima.
Alifika pale na kutufungulia mle ndani na hapo sasa nilimchapa yule bint na akatoka mbio bila kujua wapi alielekea...
Tukaanza safari yakumtafuta mke wangu ambaye hakuonekana kwenda mbali kwani kila kitu chake kilikuwa nje na baada ya muda mfupi kumtafuta nilifanikiwa kumkuta nje kidogo ya shamba letu la ndizi akiwa anahema kwa tabu sana na mapovu yakimtoka, kwa haraka nilimbeba na kuanza kukimbia nae ambapo hata kabla ya kufika hospital alinifia mikononi mwangu.
Nililia kwa uchungu mkubwa nikiomba msaada na hata kabla sijasikiwa kilio changu mara police wakaja wakiwa na yule binti akiwa na wenzake wanne na mtoto mdogo na kunirushia wakidai kua ni mtoto wangu.
nikiwa sijui hata nimshikaje huyo mtoto nisiyemfahamu mara polisi wakagundua kua mke wangu amekufa hvyo wakanichukua pamoja na maiti mke wangu ambaye kwa sasa ni marehemu na kunipeleka kituoni baada ya mke wangu kuwekwa mochwari.
Nilianza kulia huku nikiwaita watoto wangu huku nikijiuliza ni shida gani niliomkosea mungu mpaka kuniacha nikiwa hvi...
Wakati naendelea kutafakari kwa uchungu nikiwa pale polisi alipita kwa mbali bwana boniphace ambaye alikuwa ni mpinzani wangu k tk biashara na alisema kua angeipoteza furaha yangu na ndoto zangu kwa kua nilifanikiwa kumshinda ktk tenda moja ya kusambaza vitabu vya mashuleni akiwa amanicheka na kunipa alama ya dole gumba kama vile inshala ya kushinda vita.
Nililia kwa uchungu sana lakini kilio kile kilizimwa na kirungu kimoja nilichopigwa kichwani kutoka kwa afande mmoja akinitaka nitulie kwani nilikua nasumbua wenzangu na kirungu hcho kilinifanya nishtuke toka usingizini muda huo na kunefanya nigundue kua ilikuwa ni ndoto na hakuna ukweli wowote" kuangalia pembeni namshuhudia mke wangu akiwa kalala fofofo.....
Duuuh haki ya nani ndoto hii ni mbaya sana.