Mkapa to defend Mahalu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa to defend Mahalu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MartinDavid, May 6, 2011.

 1. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Retired President Benjamin Mkapa will be among key witnesses to testify in defence of Prof Costa Mahalu, who is accused of causing the government a Sh2.5 billion loss in the alleged fraudulent purchase of Tanzania's embassy in Rome.

  The unprecedented testimony by the former President adds an interesting turn in the high-profile corruption case against Prof Mahalu, who was Tanzania's ambassador to Italy at the time of the transaction.

  Defence lawyers filed Mr Mkapa's sworn affidavit at the Kisutu Resident Magistrate's Court on Monday, it was learnt yesterday.

  Prof Mahalu was arraigned in January 2006 along with a former counsellor at the Rome embassy, Ms Grace Martin, on charges of conspiracy to steal from the government. The two, who have denied the charges, are accused of using two separate contracts in the deal.

  But according to Mr Mkapa's affidavit, whose copy was made available to The Citizen, the government approved both the purchase and price of the building. He says the government's position was made clear in Parliament in August 2004.

  "This process, which involved the signing of two agreements (one formal and one commercial), which was necessitated by the prevailing customs and practice in Italy, was done with the full knowledge and approval of the government of the United Republic of Tanzania," Mr Mkapa says.

  The retired President, who inaugurated the building in February 2003, adds: "The practice of two agreements has been done before by the government of the United Republic of Tanzania where it was deemed to be in the national interest".

  The court in April 2009 ruled that Prof Mahalu and Ms Martin had a case to answer after considering the testimony of seven prosecution witnesses and nine exhibits.After the ruling, Prof Mahalu had asked for more time to decide whether or not he would call witnesses. His co-accused has lined up three witnesses.

  A lawyer defending Prof Mahalu, Mr Mabere Marando, yesterday said he had already submitted the affidavit to the Director of Public Prosecutions."Our intention is to use the affidavit without having to call the former President to court, but if the State will object, we will be willing to have him summoned to court to substantiate what he says in the affidavit," Mr Marando said."If they reject the affidavit, we are prepared to ask the court to summon him."

  Under the Evidence Act, a person who makes an affidavit under oath can be summoned for cross-examination. In his affidavit, Mr Mkapa showers praise on Prof Mahalu as a person who served the nation with honesty.

  "For the entire period I have worked with the ambassador in his various capacities in government service, I have known him as a person with a strong character, who is sincere, honest, obedient and a hard worker.

  He adds: "Those qualities led to his being awarded one of the highest national honours by the President of Italy on the Italian National Commemoration Day, long after he had left the country."

  He insists that the purchase of the building was in accordance with the government's policy of acquiring or building permanent offices and residences for Tanzania's missions abroad as a way of minimising costs.Mr Mkapa, who was President from 1995 to 2005, says the purchase of a chancery building in Rome was a matter of national interest.

  "Through the process of the government's machinery, I was made aware of the fact that the government's valuation reports for the building was established by the ministry of Works at $3million and ministry of Lands, Housing and Human Settlement Development at 5.5million euros."

  According to the former President, the state machinery also made him aware of the fact the building was purchased at $3 million and approved the whole process and procedures pertaining to the purchase of the building located on Vialle Cortina d'Ampezzo 185 in Rome.

  He says he was also made aware of the fact that Prof Mahalu was given full authority to oversee and execute the process which led to the purchase of the chancery through a government's power of attorney. The prosecution alleges that Prof Mahalu and Ms Martin, on diverse dates and places in Italy, Tanzania and elsewhere conspired to steal from the government.

  It is also alleged that on September 23, 2002 at the Tanzanian embassy in Italy, being persons in the service of the Tanzanian government, knowingly and with intent to deceive, the two used payment vouchers containing false particulars that the embassy building in Rome cost 3,098,741.58 euros.

  It was alleged that the accused on October 1, 2002 at the embassy used a sales contract dated September 1, 2002, claiming that the purchase price was for the abovementioned sum, and that the vendor of the building had received the money. The prosecution further alleges that on the same date and place the accused stole 2,065,827.60 euros.


  can this be true!!!!!!!!!!!?
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Thursday, 05 May 2011

  [​IMG]

  Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa

  Tausi Ally na James Magai

  RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameridhia kupanda kizimbani kumtetea aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na mwenzake aliyekuwa Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

  Mahalu na mwenzake wanakabiliwa na mashtaka hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakidaiwa kuhujumu uchumi kwa kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60.


  Wanadaiwa kusababisha hasara hiyo kupitia mchakato wa ununuzi wa jengo la ubalozi huo, wakati wa utumishi wao.

  Tayari Rais Mkapa amewasilisha mahakamani hapo hati yake ya kiapo akimtetea Profesa Mahalu na mwenzake kuhusiana na tuhuma hizo zinazowakabili.

  Kwa mujibu wa wakili wa kina Mahalu, Mabere Marando, ikiwa hati hiyo ya kiapo itakubaliwa na upande wa mashtaka na kisha kupokelewa mahakamani basi itatumika kama kielelezo cha ushahidi kwa upande wa utetezi bila Mkapa mwenyewe kulazimika kufika mahakamani.


  Lakini kama hati hiyo ya kiapo itakataliwa na upande wa mashtaka, basi Mkapa ameridhia kuwa yuko tayari kufika mahakamani mwenyewe na kutoa ushahidi wake mbele ya mahakama hiyo.


  Katika hati hiyo ya kiapo, Mkapa amemtetea Profesa Mahalu kuwa amefanya naye kazi kwa muda mrefu na anamjua kuwa ni mtu mwaminifu, mtiifu na mchakapakazi.

  Mkapa alieleza katika hati yake hiyo kuwa mchakato wa ununuzi wa jengo hilo ulifanyika wakati wa uongozi wake na kwamba alikuwa akijua kila kilichokuwa kikiendelea kuhusiana na ununuzi huo na kwamba ulifanyika kwa mujibu wa sheria.


  Alifafanua kuwa mpango wa ununuzi wa jengo hilo ulikuwa ni utekelezaji wa Sera ya Serikali wa kuwa na majengo yake ya kudumu katika kila ubalozi kwa kununua au kujenga ikiwa ni njia ya kupunguza gharama za upangaji.


  Aliongeza kuwa Serikali yake ilimpa Profesa Mahalu mamlaka yote ya kusimamia na kutekeleza mchakato wa ununuzi wa jengo hilo kupitia nguvu ya kisheria aliyopewa na Serikali yake.

  Mkapa alisisitiza kuwa kupitia utaratibu wa Serikali alikuwa akijua kuwa taarifa ya uthamini wa jengo hilo iliyofanywa na Wizara ya Ujenzi ilikuwa ni Dola za Marekani 3.0 milioni wakati Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilikadiriwa Euro 5.5 milioni


  "Kupitia utaratibu wa Serikali nilifahamu kuwa jengo hilo lilinunuliwa kwa gharama ya Dola za Marekani 3.0milioni sawa na Euro 3,098,741.40," alisema Mkapa na kuongeza:


  "Kupitia utaratibu wa Serikali nilikuwa nafahamu na hivyo kuidhinisha mchakato wote na taratibu za ununuzi wa jengo hilo lililoko Vialle Cortina d'Ampezzo 185 jijini Rome."

  Mkapa pia alisema kuwa alitambua kuwapo kwa mikataba miwili katika ununuzi wa jengo hilo na kwamba yeye mwenyewe ndiye aliruhusu kufanyika kwa kuwa ilikuwa ni muhimu katika kutimiza maslahi ya taifa.


  Pia Mkapa alisisitiza kuwa alikuwa na bado anatambua taarifa ya serikali bungeni ya Agosti 3, 2004 iliyoeleza na kuthibitisha kuwa taratibu zote za ununuzi wa jengo hilo zilifuatwa kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali na kwamba dalali alilipwa kikamilifu.

  "Kwa kipindi chote ambacho nimefanya kazi na Balozi Mahalu katika nafasi mbalimbali za utumishi wa Serikali ameonesha tabia thabiti na za dhati, uaminifu, utiifu, uchapakazi na ubora," alisema Mkapa.


  Alisema kuwa sifa hizo zilimfanya atunukiwe na Rais wa Italia tuzo ya Heshima ya Juu wakati wa kuadhimisha siku ya taifa hilo, muda mrefu baada ya kuwa ameondoka nchini humo.

  Jumla ya mashahidi 10 wanatarajiwa kumtetea Mahalu katika kesi hiyo. Mbali na Mkapa ambaye ameshawasilisha hati yake ya kiapo na kuridhia kupanda kizimbani kumtetea kama atahitajika, pia yumo Rais Jakaya Kikwete.


  Hata hivyo, Rais Kikwete ambaye tayari ameshapelekewa taarifa ya nia ya kumwita kufika kutoa ushahidi kwa siku na tarehe ambayo atakuwa na nafasi bado hajajibu kama atakuwa tayari au la.

  Mashahidi wengine ni pamoja na Basil Mramba ambaye pia anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11 bilioni pamoja na wenzake wawili, Daniel Yona na Gray Mgonja.


  Mahalu na Grace wanadaiwa kula njama na kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti na katika maeneo tofauti huko nchini Italia, likiwamo la kumpotosha mwajiri wao katika hati ya matumizi.

  Miongoni mwa mashtaka hayo ni kwamba Septemba 23 2002 jijini Rome, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walisaini vocha yenye namba D2/9/23/9/02 ikionyesha kuwa bei ya ununuzi wa jengo la ubalozi ni Euro 3,098,741.58, maelezo ambayo yalikuwa ni ya uongo na yenye nia ya kumdanganya mwajiri wao.
   
 3. n

  niweze JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi serikali ya Tanzania ni binadamu au nini. Huyu Mkapa si ndiye mwizi mkubwa na anataka immunity ili asichunguzwe, inakuaje anataka kupanda mahakamani wakati yeye tunataka tumweke ndani. Mafisadi bwana kweli akili hawana...If this is true basi hii ni another joke ya Republic of Tanzania.
   
 4. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wewe humjui Rais wako wa zamani? Kweli ni mtu wa uwazi na ukweli. Huu ni mfano wa kuigwa tofauti na wengine wanaowatoa wenzao kafara.
   
 5. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Na Mwandishi wetu (Gazeti la Uhuru)
  Thursday, 28 April 2011

  IKULU imekanusha habari kwamba imekuwa ikihaha kumsafisha Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, katika kesi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu.

  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Reyemamu, alisema jana kuwa Ikulu haiwezi kufanya hivyo, kwani Mkapa hahusiki na kesi hiyo. Alisema habari hizo ni za uongo zinazolenga kumhukumu mtu bila hatia.

  Rweyemamu alikuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kufuatia gazeti la MwanaHalisi kuandika habari ikisema: 'Mkapa kutinga kortini' na kwamba 'Ikulu yahaha kumuokoa Kikwete'.

  Gazeti hilo toleo namba 239 la Aprili 27 hadi Mei 4, mwaka huu, lilichapisha habari hiyo katika ukurasa wa mbele ikiwa na kichwa cha habari kisomekacho ‘Mkapa kutinga kortini'.

  "Ikulu inakanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki kuwa imekuwa ikihaha kumsafisha Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa. "Na inasisitiza kamwe haiwezi kufanya hivyo, kwani yeye si mhusika katika kesi hiyo," alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa kuandika habari hiyo huku kesi ikiendelea ni kuingilia uhuru wa mahakama.

  Rweyemamu alisisitiza Rais mstaafu Mkapa hahusiki katika kesi hiyo na kwamba badala yake anayehusika ni Profesa Mahalu, hivyo kuleta mijadala au kuingiza nje ya mahakama ni kuingilia mwendelezo wa kesi, jambo ambalo si busara.

  Aidha, Rweyemamu amewataka waandishi wa habari kuwa makini na kuzingatia maadili ya taaluma hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoingilia masuala ambayo yako mahakamani.

  Habari hiyo, ilidai katika hati ya kiapo cha Machi 31, mwaka 2011 chini ya sheria ya usajili wa nyaraka, Mkapa alitoa utetezi kuwa kila kitu kilichofanywa na Profesa Mahalu kilikuwa sahihi.
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/130596-ikulu-mkapa-hawezi-kupanda-mahakamani%3B-hahusiki-kesi-ya-mahalu.html#post1911020
   
 6. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,092
  Likes Received: 504
  Trophy Points: 280
  Akisha panda tu kizimbani,jamii itamtaka nae apandishwe kwa tuhuma mbali mbali zinazomkingama.
   
 7. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hayawi hayawi sasa yanakuwa, kwani kama mkapa anapanda kizimbani basi hata jk ni lazima apande kwa sababau yeye ndiye aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wakati huo.......mpaka kieleweke
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa nadhani umechanganya habari kidogo, hatukatai kwamba ni fisadi, ila ni vizuri tukaenda na mada, umeisoma habari nzima au sentensi mbili tu zimekutosha? Laiti ungejua kivuli nyuma ya kesi ya Mahalu ungeweza kuwa objective. Ningefurahi kama Kikwete naye angetoa ushahidi mahakamani ndo ungeelewa hii kesi inaendaje!
   
 9. m

  mkulimamwema Senior Member

  #9
  May 6, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku zote mzee Mkapa alikuwa kimya iweje sasa avunje ukimya je ni kumwokoa kijana wake au kuzuia mengine yasitokee...
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Source?
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Baada ya haya tutasikia ile kesi yake ya kujigawia mgodi wa Kiwira iko tayari kusomwa Kisutu.
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Umeshaambiwa source ni Mwananchi ya leo.
   
 13. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #13
  May 6, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yes na kagoda na richmond. Inasubiriwa mkutano wa NEC ya CCM watoswe kwanza uanachama then wapelekwe kwa pilato. Naapa lowasa atashinda kesi mwaka 2013 kwenye judgement day na atagombea. Then atashinda na atakuwa raisi ajaye watanzania Jacob Zuma juzi alikuwa na JK kumpa mbinu jinsi ya mshikaji wake atakapotumia kesi yake kujisafisha. Then atawanunua akina baliile, muhingo, pinto, kibanda, msaki watampa positive coverage mwaka mzima wa mwisho baada ya kushinda kesi.
   
 14. m

  mkulimamwema Senior Member

  #14
  May 6, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Source mwananchi ya leo tarehe 6.5.2011
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,546
  Trophy Points: 280
  Wangwana,

  Huyu Mkapa alipoulizwa kuhusu tuhuma zake mara tu zilipojulikana baada ya kumaliza awamu yake alijibu,"Mimi nimestaafu siko tena kwenye siasa." Je, inakuwaje tena leo apande kizimbani kumtetea Mahalu wakati yeye mwenyewe alikataa hata kujibu tuhuma zake mbali mbali ikiwemo ununuzi wa Rada, mikataba ya madini, ununuzi wa ndege ya Rais, kufanya biashara akiwa Ikulu, uuzaji wa nyumba za Serikali kwa bei ya kutupa, kusaidia katika kuiangamiza TANESCO baada ya kuwaleta Net Goup Solutions toka RSA ambao walikuwa hawajui lolote kuhusu umeme na kuwapa management positions na kuwalipa mabilioni ya shilingi na tuhuma nyingine chungu nzima.

  Kama yuko tayari kupanda kizimbani kumtetea Mahalu, basi na yeye aanza kujibu tuhuma zake mbali mbali alipokuwa Rais ambazo hadi hii leo hajazijibu.
   
 16. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hapa kesi ni ya huyo Prof, je ni kweli alifanya ufisadi au anaonewa? Kama anaonewa, ana haki ya kutetewa na mtu yeyote. Tusianze kumulika tochi kwa makosa ya Mkapa kwenye kesi ya Mahal. Tujaribu kuwa objective wa Tz wenzangu.

  Mkapa anafahamu jinsi mtu huyo anavyoonewa na watu wenye visasi, kwa moyo wa kibinadamu ameamua kutupilia mbali heshima yake kwa kukubali kupanda kizimbani kumtetea mtu aliyefanya kazi chini ya uongozi wake na kwa uadilifu. Mimi kwa hilo nampongeza sana Mh Ben Mkapa.
   
 17. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Happiness Katabazi

  HATIMAYE utetezi wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, umetua rasmi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam.

  Mkapa ambaye ni shahidi wa pili wa kesi hiyo alitoa utetezi huo ambao unaweza kuandika historia mpya katika mwenendo wa kesi nchini, kupitia kiapo chake ambacho kimewasilishwa mahakamani na wakili wa mshtakiwa huyo, Mabere Marando.


  Katika moja ya vipengele 13 vya kiapo hicho, pasipo kutaja jina, maelezo ya kiongozi huyo mstaafu yanamgusa Rais Jakaya Kikwete ambaye wakati Mkapa akiwa madarakani alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


  Hiyo inakuwa ni mara ya kwanza kwa rais mstaafu, kutoa utetezi mahakamani kwa kesi inayomgusa mmoja wa waliokuwa wateule wake wakati akiwa madarakani.


  Kesi hiyo Namba 1/2007 ambayo Mahalu anashtakiwa pamoja na Grace Martin inasikilizwa na Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ilivin Mugeta.


  Katika kesi hiyo, Mahalu na Martin wanatuhumiwa kwa wizi wa shilingi bilioni tatu katika ununuzi wa jengo la ubalozi mjini Rome.

  Katika hati ya kiapo chake cha Machi 31 mwaka huu, ambayo imeandaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Nyaraka (The Registration of Documents Act, Cap. 117 of 2002), Mkapa anaeleza kuwa kila kilichofanywa na Mahalu kilikuwa sahihi na kilikuwa na baraka ya serikali aliyokuwa akiingoza toka mwaka 1995-2005.

  Ushahidi huo wa rais Mkapa ambao Tanzania Daima inayo nakala yake, umeorodhesha maelezo yake yaliyoainishwa katika vipengele 13.


  Mkapa katika utetezi wake huo anadai kuwa mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo la ubalozi lililoko katika mtaa wa Vialle Cortina d'Ampezzo 185 mjini Rome ulizingatia sera ya serikali ya upatikanaji au ujenzi wa majengo ya kudumu ya ofisi na makazi na kwamba ulizingatia maslahi ya taifa.


  Hati hiyo ya kiapo ambayo tayari wakili Marando amesema ameishaiwasilisha pia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Eliezer Feleshi, inaanza kwa kusema, "Mimi Benjamin Mkapa, mtu mzima, Mkristo, mkazi wa Dar es Salaam, ninaapa kama ifuatavyo, 'nilikuwa Rais mtendaji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi viliwili mwaka 1995-2005 na nina uhakika wa yote haya nitakayosema ndani ya kiapo hiki.'


  Katika kiapo hicho Mkapa anadai pia kuwa alifahamishwa na watendaji wa serikali aliyokuwa akiingoza jinsi mchakato uliofanyika na ripoti za uthamini wa serikali zilizotumika katika kufikia hatua ya kununua jengo hilo la ubalozi.


  Anadai kuwa tathmini ya jengo hilo ambalo Mahalu anadaiwa kufanya udanganyifu na wizi kwa kulipa fedha kinyume na ilivyotajwa katika mkataba ambayo ilifanywa na serikali ya awamu ya tatu kupitia wizara mbili tofauti, Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Ardhi na Maendeleo Mijini.


  Anaendelea kudai kuwa, anatambua kuwa ripoti ya serikali ya uthamini wa jengo hilo iliandaliwa na Wizara ya Ujenzi kwa kiwango cha dola za Marekani milioni tatu na Wizara ya Ardhi kwa thamani ya euro milioni 5.5.


  Kwa mujibu wa ripoti hiyo kupitia mchakato wa ununuzi wa jengo hilo ulikuwa wa aina mbili, mmoja ni rasmi na mwingine wa kibiashara na kuongeza kuwa kwa mujibu wa taratibu ya serikali ya Italia na kuwa hilo lilifanyika kwa baraka za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  "Utaratibu kama huo wa mikataba miwili ushawahi kufanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale ambapo ilionekana haja kwa kuzingatia maslahi ya taifa kwanza....na kuwa ni mimi ndiye niliyezindua jengo hilo la ubalozi Februari 23 mwaka 2003," anadai Mkapa.


  Shahidi huyo wa Mahalu anadai pia kuwa kwa mujibu wa kiapo chake anakumbuka vyema taarifa ya serikali iliyotolewa bungeni Agosti 3 mwaka 2004 iliyosema na kuthibitisha kuwa taratibu zote zinazohusiana na manunuzi ya jengo kwa mujibu wa maelekezo ya serikali, zilifuatwa na kwamba muuzaji wa jengo hiilo alilipwa fedha zote.


  Kumbukumbu ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kwamba, Agosti 3, 2004, Kikwete alitoa maelezo bungeni kuhusu utata uliokuwapo awali kuhusu ununuzi wa jengo hilo la ubalozi.


  Kikwete katika maelezo yake hayo ambayo yako pia katika kumbukumbu rasmi za Bunge (Hansard) anaeleza, "Mheshimiwa Naibu Spika mwaka 2001/02 wizara ilinunua jengo la ubalozi counsel katika ubalozi wa Rome katika jitihada za kuondokana na tatizo la kupanga majumba ya watu huko nje na pia kupunguza gharama za kuendelea kulipa pango la nyumba kila mwaka.


  "Ununuzi wa jengo hili ulifuata taratibu zote za manunuzi ya majengo ya serikali kwa kuzishirikisha wizara za ujenzi, ardhi na maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Fedha.


  "...Jengo lilifanyiwa tathmini na wataalamu wetu na kukubaliana na ununuzi wa Euro 3,098,781.40 tarehe 6 Machi 2002 fedha za awamu ya kwanza katika ubalozi wa Rome zilipelekwa nazo zilikuwa shilingi 700,000,000 tarehe 28 Juni 2002 zilipelekwa shilingi 120, 000,000.


  "Mwishoni mwa tarehe 26 Agosti mwaka 2002 zilipelekwa shilingi 1,000,000,000 jumla ya fedha zilizokuwa zimepelekwa zikafikia shilingi 2,900,000,000 na baada ya hapo ubalozi wetu ulitekeleza taratibu zote za ununuzi wa jengo na kumlipa mwenye nyuma kiasi hicho cha fedha," alieleza Kikwete.


  Akimwelezea Mahalu katika utetezi wake, Mkapa alidai katika kipindi chote alichokuwa rais wa nchi alifanya kazi na mshtakiwa huyo katika nyadhifa mbalimbali za utumishi wa umma na kwamba mshtakiwa huyo ni mtu wa tabia njema, mkweli, mwaminifu na mchapaji kazi.


  Mkapa anahitimisha utetezi wake kwa kueleza kuwa, kutokana na mwenendo huo wa kutukuka, Rais wa Italia alimpatia moja ya tuzo za heshima yenye hadhi ya juu kabisa ya taifa hilo Profesa Mahalu, muda mrefu baada ya balozi huyo kuwa ameshaondoka nchini humo.


  Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha mahakamani ushahidi huo wa Mkapa jana, wakili Marando alisema mteja wake anakusudia kupeleka jumla ya mashahidi 10.


  Mashahidi hao ni mteja wake (Mahalu), Mkapa, Rais Jakaya Kikwete, kwani wakati akinunua jengo hilo ndiye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ndiye alimpa mteja wake nguvu ya kisheria ya kuendelea na ununuzi wa jengo hilo, aliyekuwa waziri wa Ujenzi wa John Magufuli na mashahidi wengine na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba ambaye pia anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bil. 11.7.


  Kuwasilishwa kwa hati ya kiapo cha Mkapa mahakamani hapo, kumekuja baada ya Hakimu Mkuu Mfawidhi Ilvin Mugeta kusema kuwa yeye ndiye amejipangia kusikiliza utetezi wa washtakiwa hao Aprili 28 mwaka huu.


  Hatua ya Hakimu Mugeta kusikiliza utetezi huo inakuja baada ya Machi 28 mwaka huu, Jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye ndiye aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo tangu awali kujitoa baada ya mawakili wa washtakiwa kuwasilisha sababu sita za kumwomba ajitoe kwa sababu kukosa imani naye Machi 25 mwaka huu.

  Mapema mwaka 2007, Jamhuri kupitia mawakili wake toka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincoln na Ponsian Lukosi iliwafikisha mahakamani hapo kwa mara ya kwanza washtakiwa hao kwa makosa ya uhujumu uchumi, wizi wa zaidi ya euro milioni mbili wakati wakisimamia ununuzi wa jengo la ubalozi mjini Rome nchini Italia.
   
 18. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #18
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  [FONT=&quot]Na Happiness Katabazi wa Tanzania Daima[/FONT]

  [FONT=&quot]HATIMAYE utetezi wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, umetua rasmi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mkapa ambaye ni shahidi wa pili wa kesi hiyo alitoa utetezi huo ambao unaweza kuandika historia mpya katika mwenendo wa kesi nchini, kupitia kiapo chake ambacho kimewasilishwa mahakamani na wakili wa mshtakiwa huyo, Mabere Marando.[/FONT]

  [FONT=&quot]Katika moja ya vipengele 13 vya kiapo hicho, pasipo kutaja jina, maelezo ya kiongozi huyo mstaafu yanamgusa Rais Jakaya Kikwete ambaye wakati Mkapa akiwa madarakani alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.[/FONT]

  [FONT=&quot]Hiyo inakuwa ni mara ya kwanza kwa rais mstaafu, kutoa utetezi mahakamani kwa kesi inayomgusa mmoja wa waliokuwa wateule wake wakati akiwa madarakani.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kesi hiyo Namba 1/2007 ambayo Mahalu anashtakiwa pamoja na Grace Martin inasikilizwa na Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ilivin Mugeta.[/FONT]

  [FONT=&quot]Katika kesi hiyo, Mahalu na Martin wanatuhumiwa kwa wizi wa shilingi bilioni tatu katika ununuzi wa jengo la ubalozi mjini Rome.[/FONT]

  [FONT=&quot]Katika hati ya kiapo chake cha Machi 31 mwaka huu, ambayo imeandaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Nyaraka (The Registration of Documents Act, Cap. 117 of 2002), Mkapa anaeleza kuwa kila kilichofanywa na Mahalu kilikuwa sahihi na kilikuwa na baraka ya serikali aliyokuwa akiingoza toka mwaka 1995-2005.[/FONT]

  [FONT=&quot]Ushahidi huo wa rais Mkapa ambao Tanzania Daima inayo nakala yake, umeorodhesha maelezo yake yaliyoainishwa katika vipengele 13.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mkapa katika utetezi wake huo anadai kuwa mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo la ubalozi lililoko katika mtaa wa Vialle Cortina d’Ampezzo 185 mjini Rome ulizingatia sera ya serikali ya upatikanaji au ujenzi wa majengo ya kudumu ya ofisi na makazi na kwamba ulizingatia maslahi ya taifa.[/FONT]

  [FONT=&quot]Hati hiyo ya kiapo ambayo tayari wakili Marando amesema ameishaiwasilisha pia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Eliezer Feleshi, inaanza kwa kusema, “Mimi Benjamin Mkapa, mtu mzima, Mkristo, mkazi wa Dar es Salaam, ninaapa kama ifuatavyo, ’nilikuwa Rais mtendaji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi viliwili mwaka 1995-2005 na nina uhakika wa yote haya nitakayosema ndani ya kiapo hiki.’ [/FONT]

  [FONT=&quot]Katika kiapo hicho Mkapa anadai pia kuwa alifahamishwa na watendaji wa serikali aliyokuwa akiingoza jinsi mchakato uliofanyika na ripoti za uthamini wa serikali zilizotumika katika kufikia hatua ya kununua jengo hilo la ubalozi. [/FONT]

  [FONT=&quot]Anadai kuwa tathmini ya jengo hilo ambalo Mahalu anadaiwa kufanya udanganyifu na wizi kwa kulipa fedha kinyume na ilivyotajwa katika mkataba ambayo ilifanywa na serikali ya awamu ya tatu kupitia wizara mbili tofauti, Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Ardhi na Maendeleo Mijini.[/FONT]

  [FONT=&quot]Anaendelea kudai kuwa, anatambua kuwa ripoti ya serikali ya uthamini wa jengo hilo iliandaliwa na Wizara ya Ujenzi kwa kiwango cha dola za Marekani milioni tatu na Wizara ya Ardhi kwa thamani ya euro milioni 5.5.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kwa mujibu wa ripoti hiyo kupitia mchakato wa ununuzi wa jengo hilo ulikuwa wa aina mbili, mmoja ni rasmi na mwingine wa kibiashara na kuongeza kuwa kwa mujibu wa taratibu ya serikali ya Italia na kuwa hilo lilifanyika kwa baraka za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[/FONT]

  [FONT=&quot]“Utaratibu kama huo wa mikataba miwili ushawahi kufanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale ambapo ilionekana haja kwa kuzingatia maslahi ya taifa kwanza....na kuwa ni mimi ndiye niliyezindua jengo hilo la ubalozi Februari 23 mwaka 2003,” anadai Mkapa.[/FONT]

  [FONT=&quot]Shahidi huyo wa Mahalu anadai pia kuwa kwa mujibu wa kiapo chake anakumbuka vyema taarifa ya serikali iliyotolewa bungeni Agosti 3 mwaka 2004 iliyosema na kuthibitisha kuwa taratibu zote zinazohusiana na manunuzi ya jengo kwa mujibu wa maelekezo ya serikali, zilifuatwa na kwamba muuzaji wa jengo hiilo alilipwa fedha zote.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kumbukumbu ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kwamba, Agosti 3, 2004, Kikwete alitoa maelezo bungeni kuhusu utata uliokuwapo awali kuhusu ununuzi wa jengo hilo la ubalozi.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kikwete katika maelezo yake hayo ambayo yako pia katika kumbukumbu rasmi za Bunge (Hansard) anaeleza, “Mheshimiwa Naibu Spika mwaka 2001/02 wizara ilinunua jengo la ubalozi counsel katika ubalozi wa Rome katika jitihada za kuondokana na tatizo la kupanga majumba ya watu huko nje na pia kupunguza gharama za kuendelea kulipa pango la nyumba kila mwaka.[/FONT]

  [FONT=&quot]“Ununuzi wa jengo hili ulifuata taratibu zote za manunuzi ya majengo ya serikali kwa kuzishirikisha wizara za ujenzi, ardhi na maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Fedha.[/FONT]

  [FONT=&quot]“...Jengo lilifanyiwa tathmini na wataalamu wetu na kukubaliana na ununuzi wa Euro 3,098,781.40 tarehe 6 Machi 2002 fedha za awamu ya kwanza katika ubalozi wa Rome zilipelekwa nazo zilikuwa shilingi 700,000,000 tarehe 28 Juni 2002 zilipelekwa shilingi 120, 000,000.[/FONT]

  [FONT=&quot]“Mwishoni mwa tarehe 26 Agosti mwaka 2002 zilipelekwa shilingi 1,000,000,000 jumla ya fedha zilizokuwa zimepelekwa zikafikia shilingi 2,900,000,000 na baada ya hapo ubalozi wetu ulitekeleza taratibu zote za ununuzi wa jengo na kumlipa mwenye nyuma kiasi hicho cha fedha,” alieleza Kikwete.[/FONT]

  [FONT=&quot]Akimwelezea Mahalu katika utetezi wake, Mkapa alidai katika kipindi chote alichokuwa rais wa nchi alifanya kazi na mshtakiwa huyo katika nyadhifa mbalimbali za utumishi wa umma na kwamba mshtakiwa huyo ni mtu wa tabia njema, mkweli, mwaminifu na mchapaji kazi.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mkapa anahitimisha utetezi wake kwa kueleza kuwa, kutokana na mwenendo huo wa kutukuka, Rais wa Italia alimpatia moja ya tuzo za heshima yenye hadhi ya juu kabisa ya taifa hilo Profesa Mahalu, muda mrefu baada ya balozi huyo kuwa ameshaondoka nchini humo.[/FONT]

  [FONT=&quot]Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha mahakamani ushahidi huo wa Mkapa jana, wakili Marando alisema mteja wake anakusudia kupeleka jumla ya mashahidi 10.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mashahidi hao ni mteja wake (Mahalu), Mkapa, Rais Jakaya Kikwete, kwani wakati akinunua jengo hilo ndiye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ndiye alimpa mteja wake nguvu ya kisheria ya kuendelea na ununuzi wa jengo hilo, aliyekuwa waziri wa Ujenzi wa John Magufuli na mashahidi wengine na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba ambaye pia anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bil. 11.7.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kuwasilishwa kwa hati ya kiapo cha Mkapa mahakamani hapo, kumekuja baada ya Hakimu Mkuu Mfawidhi Ilvin Mugeta kusema kuwa yeye ndiye amejipangia kusikiliza utetezi wa washtakiwa hao Aprili 28 mwaka huu.[/FONT]

  [FONT=&quot]Hatua ya Hakimu Mugeta kusikiliza utetezi huo inakuja baada ya Machi 28 mwaka huu, Jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye ndiye aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo tangu awali kujitoa baada ya mawakili wa washtakiwa kuwasilisha sababu sita za kumwomba ajitoe kwa sababu kukosa imani naye Machi 25 mwaka huu.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mapema mwaka 2007, Jamhuri kupitia mawakili wake toka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincoln na Ponsian Lukosi iliwafikisha mahakamani hapo kwa mara ya kwanza washtakiwa hao kwa makosa ya uhujumu uchumi, wizi wa zaidi ya euro milioni mbili wakati wakisimamia ununuzi wa jengo la ubalozi mjini Rome nchini Italia.[/FONT]
   
 19. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Licha ya wizi wa fedha, kosa kubwa ni la kuhama mjini Rome na kwenda hiyo bara bara ya Cortina D'Ampezzo, hapo ni nje ya mji, mitaa ya makaazi ya watu wa kawaida, kwa hapo Roma bora wangebaki maeneo ya mjini kulikochangamka kwa ajili ya kutangaza nchi yetu, huko waliko hapiti mtu, labda wafanyakazi wa ki sri lanka, kichina, au senegal, hawapiti wawekezaji au watu wa kipato cha juu hapo, linadhibitisha kuwa nia ilikuwa wagawane pesa tu, halafu jumba lenyewe kubwa halina kazi, wanakaa tu peke yao hao watanzania na kutizama TV cnn kutwa, hawajui kwa nini wamehamishwa huko? wanatamani wangepewa hata kisehemu kama ya Duka lakini mjini kulikochangamka ili wapate kutangaza nchi..

  Laana tupu Tanzania
   
Loading...