Mkapa TACAIDS, Kikwete NACP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa TACAIDS, Kikwete NACP

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mvaa Tai, Jun 8, 2011.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mkapa alipoingia madarakani alianzisha TACAIDS kwa madhumuni ya kupambana na janga la ukimwi Tanzania na alipoingia Kikwete alianzisha NACP kwa ajiri ya madhumuni hayo hayo na mbaya zaidi kwasasa baadhi ya watu waliopo TACAIDS wanahaha kwamba kifedha ni pagumu sana kufanyia kazi ukilinganisha na enzi za Mkapa, kwasababu mafungu mengi yanayohusiana na janga la ukimwi yanaelekezwa NACP. Wanaofahamu tofauti kati ya TACAIDS na NACP wanisaidie ili niondokane na fikra zangu kwamba NACP imeanzishwa na Kikwete kwasababu ya maslahi ya watu fulani, hasa ukifikiria kwamba Rais hawezi akaanzisha chombo kinachoshughulikia suala fulani ambalo tayali kuna chombo kinachoshughulikia suala hilohilo kilichoanzishwa na mtangulizi wake.

  TACAIDS=TANZANIA COMMISSION FOR AIDS (MKAPA)
  NACP=NATIONAL AIDS CONTROL PROGRAMME (KIKWETE)
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Mmmmmh!!
   
 3. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  inawezekana kabisa mkuu.
   
 4. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Yaani umenifanya nisign in. NACP ilikuwepo toka zamani sana na iko chini ya Wizara ya Afya, TACAIDS iko chini Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitarudi via mobile inachosha
   
 5. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  NACP ndo naisikia leo. Majina yanaonyesha kama yana malengo yanayofanana.
   
 6. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kama haiingii akilini? Mbona mnachanganya mambo? Kwanza angalia majukumu ya
  TACAIDS na yale ya NACP ndipo uje na hoja.
   
 7. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  TACAIDS ni idara inayojitegemea chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, ilianzishwa kwa sheria ya Bunge No. 22 ya mwaka 2001. NACP ni programme maalumu chini ya Wizara ya Afya na ilianzishwa mwaka 1988. NACP ilianzishwa hata kabla Mkapa na Kikwete kuwa rais. Majukumu ya TACAIDS na NACP ni tofauti na unaweza kutembelea website zao kwa taarifa zaidi.
  1. TACAIDS: Welcome to Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS)

  2. NACP: NACP::
   
 8. t

  tarmo Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
 9. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,044
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  NACP imekuwepo kwa muda mrefu sana nafikiri kabla ya mkapa kwa ajili ya malengo bofya hapa: NACP::

  TACAIDS hapa: www.[B]tacaids[/B].go.tz
   
 10. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  NACP ipo toka miaka ya '80, sikumbuki mwaka. Iko chini ya Wizara ya Afya. TACAIDS ilianzishwa wakati wa Mkapa, nia ikiwa kupanua wigo wa kupambana na UKIMWI, yaani kuondoa dhana ya kwamba mapambano dhidi ya UKIMWI ni ya Wizara moja tu, yaani Wizara ya Afya. TACAIDS imeanzishwa ili kuleta dhana ya kwamba kupambana na UKIMWI ni multi-sectoral, na ndiyo maana iko chini ya Waziri Mkuu
   
 11. B

  Bijou JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145


  ufafanuzi wako umeenda shule, ni kweli nakumbuka NACP ilianzishwa kwenye miaka ya 1983/84, kama muitiko wa janga la UKIMWI. Kwa maneno mengine unaweza kusema NACP imekaa kitaalamu zaidi na TACAIDS kisiasa zaidi ie uhamasishaji
   
 12. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hapana siyo! Vyombo hivi viwili ni tofauti kabisa na vina majukumu tofauti katika maandiko ya uanzishjwaji wao lakini katika hali ya sasa kuna kasoro kubwa katika utekelezaji wa majukumu yake vyombo hivi. Labda kwa faida ya watu wengi na mwanzilishi wa thread hii kwa kifupi tu nianishe majukumu ya kimsingi ya TACAIDS na NACP kama ifuatavyo;

  1. Madhumuni ya kuanzishwa kwa TACAIDS ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kuna upanuaji wa uwigo wa ushiriki wa wadau na ushiriki wao katika masuala ya ukimwi ili kushughulikia tatizo la ukimwi kama suala la kijamii zaidi na kupunguza makali ya kijamii kwa makundi mbalimbali yaliyoathiriwa na ukimwi kwa mfano yatima, wajane na wagonjwa.
  2. Kusaidia kuratibu shughuli za ukimwi kwa kutafuta vyanzo vya fedha nakusimamia rasilimili za miradi ya UKIMWI katika nchi. Pia majukumu mengine mengi yametajwa.
  3. Wakati TACAIDS ni wakala wa serikali NACP ni mpango/mradi chini ya wazara ya afya ambao unapaswa kujishughulisha na masuala ya tiba, utafiti na uzuiaji wa maambukizi yanayoweza kutokea wakati wa matibabu
  Mapungufu ya kiutendaji ni kwamba wakati TACAIDAS ilipaswa kutekeleza majukumu yake kutumia mamlaka za sasa za serikali sasa wamepanuka na kuajiri watu wanaitwa waratibu wa TACAIDS mikoani ukiangalia kazi zao zinafanana kabisa na zile za waratibu wa ukimwi wa mikoa kwa hiyo fedha badala ya kuwafikia walengwa zinatumika kuendesha taasisi hili ndiyo tatizo la kujadiliwa na wanajamii forum
  NACP badala ya kuangalia masuala ya kitabibu sasa inaangalia masuala ya kijamii kwa sababu labda wanahisi huko kuna fedha rahisi yale matangazo ya kwenye tv yanahusu kubadili tabia ambalo ni jukumu la TACAIDS. Kwa hiyo kuna mchanganyiko ambao hauna tija ndani vyombo hivi pia hili linaweza kujadiliwa na wanajamii kwa tija ya wananchi wa Tanzania
   
Loading...