Mkapa, Mwinyi, Malecela waenguliwa rasmi NEC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa, Mwinyi, Malecela waenguliwa rasmi NEC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 13, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Ni mabadiliko makubwa katiba ya CCM
  [​IMG] Viongozi wastaafu kuwa na baraza lao  [​IMG]
  Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]


  Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imewaondoa rasmi viongozi wa taifa wastaafu kwenye vikao vya Kamati Kuu (CC) na Nec na badala yake wameundiwa baraza la ushauri.

  Viongozi walioondolewa ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi; Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa; Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mstaafu, John Malecela; Rais Mstaafu Zanzibar wa awamu ya tano Zanzibar, Dk.

  Salmin Amour na Rais Mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya sita, Abeid Aman Karume.
  Aidha, wajumbe wa Nec watakaochaguliwa kupitia wilaya watakuwa ni viongozi wa kazi za muda wote ili kuweka wazi zaidi wajibu wa

  wajumbe hao kuwa karibu na wanachama wa kushughulikia shida zao.
  Kwa maana hiyo, makada watakaochaguliwa kuingia NEC kupitia wilayani hawatakuwa wabunge wala wawakilishi.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Katibu wa NEC wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, alisema waliondolewa kuwa wajumbe wa Nec ni marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano ambao walikuwa wenyeviti wa CCM Taifa.

  Alisema wajumbe wengine walioondolewa katika ujumbe wa NEC ni marais wastaafu wa Zanzibar ambao pia walikuwa ni makamu wenyeviti wa CCM Zanzibar na makamu wenyeviti wa CCM Bara.

  “Baraza litakuwa na kazi ya kutoa ushauri kwa Chama cha Mapinduzi na serikali zinaoongozwa na CCM kwa madhumuni hayo katika jambo mahsusi,” alisema Nape.

  Alisema wajumbe wa baraza hilo wanaweza pia kualikwa ama wote au mwakilishi wao kuhudhuria vikao vya Chama ngazi ya Taifa.
  Alisema katika marekebisho hayo ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2010 na kanuni zake, NEC imeongeza idadi ya wajumbe kutoka 200 hadi 300.

  Pia alisema kuwa idadi hiyo ya wajumbe wa Nec imeongezeka kutokana na makundi mapya ya wajumbe yaliyobainishwa kwenye katiba hiyo.
  Aliyataja makundi hayo kuwa ni wajumbe wa Nec ngazi ya taifa ambao ni 20 kati yao 10 kutoka Tanzania Bara na 10 Tanzania Visiwani na

  wajumbe 10 wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho.
  Makundi mengine ni wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao ambao ni Mwenyekiti, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

  Pia aliyataja makundi mengine kuwa ni wajumbe wanaotoka kwenye vyombo vya uwakilishi ambao ni wabunge 10 na wawakilishi watano kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

  Nape alisema kundi lingine ni la wajumbe 221 wanaochaguliwa kutoka wilayani na watakaochaguliwa katika nafasi hizo ni wale viongozi wa kazi za muda wote kama vile wenyeviti wa wilaya, ili kuweka wazi zaidi wajibu wa wajumbe hao kuwa karibu na wanachama na kushughulikia shida zao.

  “Hii yote bado ni utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba, tulisema dhana hii itagusa maeneo mengi na eneo hili ni la kuhakikisha chama kinasogea karibu na wanachama,” alisema Nnauye.

  Alisema kupitia nafasi hizo za wilaya wanachama wa chama hicho watawakilishwa vizuri ingawa katika ngazi ya mikoa, bado Mwenyekiti na Katibu wa chama hicho wa mkoa wanabaki kuwa wajumbe wa Nec.

  Nape alisema kundi lingine la mwisho kuwa ni la wajumbe wanaochaguliwa kutoka kwenye Jumuiya za chama ambao ni Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nafasi 15 ambapo Tanzania Bara ni nafasi tisa na Zanzibar sita. UVCCM ni nafasi 10 Tanzania bara sita na

  Zanzibar wanne wakati Jumuiya ya Wazazi watano ni kutoka Bara ni watatu na Zanzibar wawili.
  Katika tukio lingine, mwanasiasa mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru, ameibua hisia za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, baada ya kukataa utaratibu wa kuwapata wajumbe wa kikao hicho katika ngazi ya wilaya.

  Kwa mujibu wa chanzo kutoka ndani ya kikao hicho, Ngombale-Mwiru alitaka wajumbe hao wapatikane kutoka mkoa badala ya wilayani kama ililivyokuwa katika Katiba ya sasa ya chama.

  Hata hivyo, kabla ya Nape kuzungumza na waandishi wa habari kutangaza maamuzi hayo, alikanusha taarifa kuwa wabunge hawataruhusiwa kugombea nafasi ya ujumbe wa NEC kupitia CCM ngazi ya wilaya.

  Alizungumza na NIPASHE kwa simu, alisema kumekuwa na taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari kwamba wabunge wamepigwa marufuku kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia wilaya wanazotoka wakati ukweli hakuna agenda kama hiyo ndani ya chama hicho.

  “Mimi ndiyo msemaji wa chama, kwa hiyo nisikilize mimi siyo vyombo vya habari, nasema hakuna ajenda ya kuwazuia wabunge kugombea NEC wilaya kama inavyoelezwa,” alisema Nape ambaye hata hivyo hakufafanua zaidi suala hilo.
  Taarifa kwamba wabunge wamepigwa marufuku kugombea NEC wilaya pia zilibainishwa na wabunge wenyewe juzi wakati Rais Jakaya

  Kikwete, alipokutana nao katika kikao kilichofanyika ukumbi wa White House mjini Dodoma juzi.
  Katika kikao hicho vyanzo vya habari vinasema Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba, ndiye aliyegusia suala la wabunge wa CCM kuzuiwa kugombea nafasi za ujumbe wa NEC kupitia wilayani na kumuomba Rais Kikwete awape ufafanuzi kuhusiana na suala hilo.

  Kutokana na madai hayo ya wabunge, Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, alijibu kuwa hakuna mpango wa kuwazuia wabunge kugombea nafasi za NEC katika mabadiliko ya katiba ya chama hicho.

  Kwa muda mrefu mambo ambayo yamekuwa yakipingwa na wabunge wa CCM kuhusiana na marekebisho ya katiba ni lile linalotaka wabunge wasigombee nafasi yoyote ya ujumbe wa NEC.
  Pendekezo hilo likipitishwa, wabunge wanaotaka kuwania uras watakuwa na nafasi ndogo ya kupitishwa kwani hawatakuwa wajumbe wa NEC wa wilaya.

  CHANZO: NIPASHE


   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wazee ni HAZINA
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Lowasa anazidi kuitikisa ccm. Hizi zote ni juhudi za kuhakikisha kuwa wafuasi na wale wote wanaoweza kumpigia kura lowasa wanaondolewa kwenye ngazi za maamuzi. Yangu macho.
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  lengo ilikuwa kumuondoa karume
  ambae ndo mpambe wa el
   
 5. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,212
  Trophy Points: 280
  Ccm oyeee!
   
 6. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,971
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Akuna chama duniani kisichokuwa na wazee!na ata ukoo bila wazee aupo.pia akuna mahakama bila wazee .nnaanza kuamini kuwa ule ubwabwa wa juzi pale Kirumba ni kweli ulikuwa wa Hitma ya hawa wasika hatamu ya njii hii
   
 7. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Wapumzike kwa amani
   
 8. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Lakini ndugu John Samwel Malechela yeye si alipewa ujumbe wa kudumu yaani mpaka aki rest in piece, sasa leo imekuwaje? sikumbuki vizuri ila nadhani ni kile kipindi ambacho bibi mbatia alidedi na ndugu yangu kapuya alipata ajali
   
 9. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Spika duh!
  akitoka TADEA bado atakuwa mjumbe?
   
 10. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  kama waliweza kuvunja azimio la arusha nyerere akiwa hai, itakuwa hao wazee ambazo nao wako smeared na ufisadi. Ni kama mafisadi wamepigana chini wenyewe kwa wenyewe tu!
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ni mbinu za JK kuhakikisha mwislam mwingine anaingia ikulu 2015.
   
 12. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  haya ndo magamba yaliyokuwa yanazungumziwa?
   
 13. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Sumaye anaangukia kundi lipi kwenye haya mabadiliko mapya?
   
 14. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Haya mambo mbona si mapya! Wengine tuliyategemea kwani yalijadiliwa ile NEC iliyopita. Leo ndio wameamua kuyawekea msingi wa kisheria. Hata hao wanaoonekana kama wamelengwa binafsi, walishatambua huu mtego tangu kipindi kile na wakaamua kubadili strategies. Kazi ipo
   
 15. G

  Gamba la Chuma JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,247
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wameondolewa kwa muda tu. Watarudishwa baada ya uchaguzi 2015. Hizo ni mbinu za JK kujiwekea mazingira ya kumuweka Rais anayemtaka.
   
 16. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  we kweli mdini, watu kama nyie si mkaishi somalia, au ethiopia huko, kama huna cha msingi cha kuongea ni kheri ukakaa kimya...
   
 17. MANI

  MANI Platinum Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu hao wanategemea CCM itatawala milele!
   
 18. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mijitu mingine bana! Hivi udini unakusaidia nini ?
   
 19. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna ajenda ya siri ya JK kumpitisha mtu wake.Ikumbukwe chaguo la JK nafasi ya makamu wa Rais ni Mama Zakia Meghji wazee wa CCM wakiongozwa na B Mkapa wakashilia bango Dr Shein akaendelea awamu ya pili JK akalazimishiwa Dr Gharib Bilal na kundi la wazee wa CCM.

  Mchakato wa mgombea uRais mwaka 2015 JK anajua wazi hawa wazee wa CCM wakiendelea kuwepo kwenye nafasi za maamuzi chaguo lake linaweza kukumbana na pingamizi za kirasimu kaamua kuwaundia kijibaraza cha kutwanga umbeya tena kisicho na maamuzi zaidi ya ushauri tu.Ushauri una sifa kuu mbili kukubaliwa au kukataliwa ha ha ha ha Baba MwanaAsha anajua kuchanga karata zake vyema.JK anajua ana uwezo wa kuwamudu akina Nape na vichakaramu vinavyotegemea fadhila za ukuu wa Mkoa,ukuu wa Wilaya,uBalozi na nafasi luluki alizorundikiwa na katiba ya JMT.
   
 20. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa AMRI yangu!

  Hawa ni wa kufunguliwa mashtaka haraka sana kwa kuiongoza serikali vibaya na hata kuipalilia UFISADI mpk leo imeshika mizizi,Yote haya ni kwa sababu yao tu!

  Jk akaja kupalilia kbs ufisadi na sasa imechanuka kwa 110%

  Tena ingewezekana Mkapa anyongwe kbs na Mwinyi apewe kifungo cha maisha pale Segerea na Malecela yule kwa kuwa alikuwa anaambiwa fanya hiki na kile afungwe kifungo cha nje kwa miaka yote ya uhai wake hapa Dunia!

  Mafisadi wakubwa na Kodi ya wanainchi!
   
Loading...