Mkapa, Mwinyi kupasua kichwa wiki hii

Mkapa, Mwinyi kupasua kichwa wiki hii

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

Mkapa-29June2015.jpg

Rais mstaafu, Benjamin Mkapa

Hatimaye kile kikao cha Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachowahusisha pia marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, kinatarajiwa kufanyika wakati wowote wiki hii kujadili mwenendo wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho.

Taarifa kutoka chanzo kimoja ndani ya CCM kimeeleza kuwa Mwinyi, Mkapa na wazee wengine wanaounda Baraza la Wazee la Ushauri, watapasua kichwa wiki hii kujadili mwenendo wa urais ikiwa ni siku chache kabla ya kufikia Julai 2, mwaka huu, inayoonyeshwa katika ratiba ya uchaguzi ya CCM kuwa ndiyo siku ya mwisho ya kurejesha fomu kwa wanaowania urais.

Lengo la kikao cha Wazee ni kujadili kwa kina mwenendo wa mchakato wa kumpata mgombea urais na mwishowe kutoa mapendekezo yao juu ya namna bora ya kumpata mgombea kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM (CC)
"Kikao hiki ni muhimu kwa hatma ya mchakato wa uchaguzi... baada ya kutofanyika wiki iliyopita, sasa kitafanyika wiki hii, tena wakati wowote kuanzia kesho (leo)," chanzo kilieleza.

Awali, kikao hicho kilitarajiwa kufanyika Jumatano iliyopita jijini Dar es Salaam lakini kikaahirishwa na Katibu wa Baraza la Ushauri la Wazee, Pius Msekwa, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni baadhi ya viongozi wakuu wa CCM kuwa safarini.
Alipoulizwa na NIPASHE jana iwapo watakutana kaunzia leo, Msekwa hakuwa tayari kueleza kiundani na badala yake alimjibu mwandishi kwa kifupi: "Just pay attention (wee jiweke tayari tu) kama umesikia juu ya kikao chetu."

Kikao cha Baraza la Ushauri la Wazee ni mahususi kwa ajili ya ushauri juu ya watia nia 42 wa urais waliojitokeza kutaka kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera yake katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

WANAOUNDA BARAZA LA WAZEE
Wanaounda Baraza la Ushauri la Wazee kwa mujibu wa mabadiliko yaliyofanywa na CCM mwaka 2012 katika katiba yake ni marais wastaafu Mwinyi (Mwenyekiti), Mkapa (Mjumbe), Amani Abeid Karume (Mjumbe) na Dk. Salmin Amour (Mjumbe).

Wengine ni Waziri Mkuu mstaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais, John Malecela (mjumbe) na Pius Msekwa (Katibu).
Mkutano huo wa Baraza la Wazee CCM ni utangulizi wa mfululizo wa vikao vingine vya chama hicho vitakavyoanza Julai 5, mwaka huu.

Vikao vingine ambavyo viko katika maandalizi ya kukutana ni Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa itakayokutana Julai 7 na Kamati Kuu (CC) itakayokutana Julai 8, chini ya Rais Kikwete, ikifuatiwa na kikao cha NEC Julai 9, mwaka huu.

Jina la mgombea urais atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu litajulikana Julai 12 baada ya kupigiwa kura na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, ambao ni maalum kwa ajili kuchagua jina la mgombea mmoja kati ya watatu.

CHANZO: NIPASHE
 
Nilifikiri na Kingunge naye yupo miongoni mwao! Kwanini anatoa maneno yenye Mamlaka kwa chama wakati hayupo kwenye Jopo la wazee!
 
Nilifikiri na Kingunge naye yupo miongoni mwao! Kwanini anatoa maneno yenye Mamlaka kwa chama wakati hayupo kwenye Jopo la wazee!

kutokuwemo humo ndio kumempa uhuru wa kuongea maoni yake hadharani..angekuwemo humo angebaki nalo moyoni kama wenzake walivokaa kimya ndani ya hiyo kamati ...kumbuka kila mtu ana mtu wake ktk hilo kundi na hawendi kuwa suprised ni kila mtu anajua alitakalo...humu..
 
Ccm ya leo haina wazee tena kama ile ya nyerere
Ccm ya leo ina wazee wachumia tumbo na wanafiki
Hao wazee kwa vyovyote watapendekeza jina la mtu atakayeweza kuwalinda watoto wao waliopo kwenye medani za siasa
Sioni cha zaidi.
 
Wazee wenyewe ni miongoni mwa waliofanikisha nchi kuwa bora katika suala la umasikini, japo tajiri wa rasilimali duniani, nao pia wanataka kutoa maoni ya rais? Ili mawazo yao ya umaskini wa nchi yaendelee kutukuzwa kwa kupendekeza zao la umaskini pia?.

Hii ndio Tangazania, nchi iliyosheheni wajinga kiakili, na kimwili.
 
Lowassa hana lake hapo. Mtu pekee anayemuunga mkono ni Amaan karume pekee. Imekula kwake !!!
 
Tusubiri tuone .Ukawa endeleeni kunyatia polepole wakituletea wa kwao sisi tunawagunia .lazima tupate mtu wa kuja na mabadiliko kama sio ccm bc ni nje ya ccm.
 
chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi
chama chetu chajenga nchi
 
Wajumbe rafiki kwa Lowassa ni Karume, Mkapa na Mzee Mwinyi. Wajumbe adui wa Lowassa ni Malecella na Msekwa. Salmin Amour sijui msimamo wake.

Yote kwa yote, baraza hili halina nguvu yoyote ya kimaamuzi kuweza kupitisha au kukata jina la mgombea yoyote, zaidi wanaweza kutoa ushauri namna bora ya kufanikisha mchakato na sio zaidi.

Mara ya mwisho baraza hili lilitoa ushauri kwa chama kuachana na dhana ya kujivua gamba, na kupendekeza maridhiano yafikiwe na kamwe asifukuzwe mwanaCCM yoyote kwa issue za kushtumiwa.

*NOTE:
Baraza la ushauri la wazee la CCM liliundwa baada ya Kikwete kuivunja Kamati kuu na kuundwa upya na akapendekeza wazee wastaafu wasiwe wajumbe(Maana walikuwa wajumbe wa kudumu wa Kamati kuu) na hapo wadadisi wakasema ilikuwa ni Mpango wa Kikwete kupunguza wajumbe waliokuwa wanamlinda Lowassa ndani ya Kamati kuu ili agenda ya kumvua uanachama Lowassa akiletwa ndani ya kamati kuu ipite kwa urahisi.

Binafsi sioni impact yoyote ya maamuzi ya baraza hili kama yatakuwa NEGATIVE dhidi ya Fisadi Lowassa.
 
Watuletee mzalendo wetu ili turudishe imani kwa wananchi na wanachama wetu
 
Nilifikiri na Kingunge naye yupo miongoni mwao! Kwanini anatoa maneno yenye Mamlaka kwa chama wakati hayupo kwenye Jopo la wazee!

Wewe unatumia makalio kufikiri sasa angkuwepo huko angekua na sababu gani kusema
 
Wajumbe rafiki kwa Lowassa ni Karume, Mkapa na Mzee Mwinyi. Wajumbe adui wa Lowassa ni Malecella na Msekwa. Salmin Amour sijui msimamo wake.
*NOTE:
Baraza la ushauri la wazee la CCM liliundwa baada ya Kikwete kuivunja Kamati kuu na kuundwa upya na akapendekeza wazee wastaafu wasiwe wajumbe(Maana walikuwa wajumbe wa kudumu wa Kamati kuu) na hapo wadadisi wakasema ilikuwa ni Mpango wa Kikwete kupunguza wajumbe waliokuwa wanamlinda Lowassa ndani ya Kamati kuu ili agenda ya kumvua uanachama Lowassa akiletwa ndani ya kamati kuu ipite kwa urahisi.
Binafsi sioni impact yoyote ya maamuzi ya baraza hili kama yatakuwa NEGATIVE dhidi ya Fisadi Lowassa.
Karume, Mkapa, Mwinyi, Malecela na Msekwa si marafiki wa Lowassa sijui Salmin
Analysis yako ni nzuri naikubali lakini naona kwa msimamo wangu umeigeuza.
Kikao kilichomnyima Lowassa kuingia CC-CCM baadhi ya wazee alikuwa hawajatolewa ujumbe wa kudumu wa CC na bado walimkataa kwani alishaihonga NEC yote wakaona akiingia CC itakuwa balaa
Maamuzi ya Wazee hawa na System ndio wenye maamuzi ya kura kabla CC haijapelekewa majina

  • usije shangaa wazee wakamchinjia baharini mapema na kule likaenda jina la kusindikizia
    1. Zanzibar -watamuweka Augustino
    2. Mwanamke mmoja lazima
    3. hapa ndipo kapu la Wabara (watatu tu kati ya hawa)
      1. Makongoro
      2. Membe
      3. Mwandosya
      4. SittaLowassa
 
Hawa wazee wamechangia kwa kiasi kikubwa kuleta umasikini katika inchi wakati wa uongozi wao, na hata sasa inchi imejitawala yenyewe kwa miaka kumi,wenyewe WaPo tu,halafu Leo wakatuteulie kiongozi, tubuni msije mkapotea.
 
Back
Top Bottom