Mkapa, Mahalu na udhaifu wa serikali... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa, Mahalu na udhaifu wa serikali...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ZeMarcopolo, May 8, 2012.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ukifuatilia ushahidi alioutoa Mzee wetu Rais mstaafu mh. Benjamin William Mkapa katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Balozi Costa Mahalu, utagundua kuwa kuna udhaifu mkubwa sana katika jinsi serikali yetu inavyoendesha mambo yake na udhaifu huo ni mwanya mkubwa kwa ubadhilifu serikalini.

  Alipoulizwa na wakili wa serikali juu ya jinsi serikali inavyowasiliana na balozi, mh. Mkapa alijibu hivi; "Balozi anaweza kuwasiliana na serikali yake kwa njia ya barua kwa Wizara ya Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi, Rais au kwa njia ya mdomo. Na mawasiliano siyo lazima yafanyike kwa njia ya maandishi tu kwa sababu maelekezo mengine ambayo anapewa balozi na serikali yake ni ya siri kwa maslahi ya taifa hivyo anaweza kuitwa nyumbani na kupatiwa maagizo hayo kwa njia ya mdomo"

  Baadae wakili alitaka kujua mh. Mkapa akiwa Rais alipewa na nani taarifa za kuwa muuzaji wa jengo la ubalozi anataka kulipwa kwa awamu mbili na katika akaunti mbili tofauti. Alijibu hivi; "Ni Mahalu na alinipa taarifa kwa mdomo na alikuwa ameandaa ripoti juu ya ununuzi na akawa anaomba ridhaa ya serikali kabla ya kulinunua"

  Naomba niwakumbushe kuwa hapa tunazungumzia biashara ya nyumba yenye thamani ya Euro milioni tatu!

  Wakili alipotaka kujua kama mh. Mkapa angeweza kuzuia ununuzi wa jengo hilo. Jibu alilotoa mh. Mkapa ni hili; "Eh! Mimi ndiye nilikuwa Rais wa nchi; nilikuwa na madaraka hayo na badala yake fedha hizo zingeelekezwa kwenye mahitaji mengine ila kwa sababu nilikuwa ninajua umuhimu na faida ya nchi kununua jengo lile ndiyo maana nikaridhia kwa mdomo linunuliwe"
  "Nilitoa maelekezo kwa njia ya mdomo kwa watendaji na maagizo hayo yalipaswa yatekelezwe na Wizara ya Mambo ya Nje na ilikuwa jukumu la Mahalu kuieleza wizara hiyo na ubalozi utekeleze maagizo yangu"

  Wakili akahitaji ufafanuzi iwapo Wizara ya Mambo ya Nje ilituma pesa kwenye akaunti mbili tofauti. Hivi ndivyo alivyojibu mh. Mkapa; "Inahusu nini sasa? Mimi nilitoa maagizo, hivyo lilikuwa ni jukumu la Balozi Mahalu kuieleza wizara yake. Sasa suala la hayo makaratasi ya kufanya mchakato wa kulinunua, mimi kama Rais siwezi kuingilia. Watendaji walipaswa watekeleze"

  Kwa maelezo yake mh. Mkapa ni kwamba maagizo kwa mdomo hutolewa iwapo taarifa ni siri kwa ajili ya usalama wa taifa. Katika zoezi hili la uuzaji wa nyumba, sijaona sababu ya mawasiliano kufanyika kwa mdomo. Mbaya zaidi, nyumba ya Euro bilioni tatu inanunuliwa kwa maagizo ya mdomo tu na tena maagizo yenyewe hapewi Waziri; anapewa Balozi ili akawaambie watendaji wa Wizara!!!
  Kinachomaanishwa hapa ni kwamba Balozi anaweza kwenda kwa watendaji wa Wizara akasema Rais kasema nipeni Bilioni 6, akapewa na kufanya atakachoamua!
  Huu ni udhaifu MKUBWA SANA katika jinsi ofisi ya Rais/Serikali inavyofanya mambo yake. Iwapo udhaifu huu utaachwa uendelee kuwepo basi tutakuwa kila siku tunajenga na kubomoa

  Hii ni hatari zaidi iwapo kitatokea kipindi cha mpito iwapo uongozi unaoingia madarakani haufungamani na chama kilichopo madarakani. Vigogo wanaohofia kuadhibiwa na serikali mpya kwa sababu moja au nyingine wanaweza kwenda kwa watendaji na kusema Rais amesema mnipe bilioni kadhaa, akapewa akakimbilia anakojua yeye. Rais mpya anaapishwa anakuta shamba limebaki mabua matupu.

  nchi yetu ina vitu vingi vinavyohitaji kurekebishwa, lakini hili linahitaji kurekebishwa ASAP...
   
Loading...