Mkapa: Kama kila Rais anakuja na mambo yake, hatuwezi yafikia maendeleo

Huwezi leo kutaka kujenga viwanda wakati kuna viwanda vikumbwa vinaoza mfano Urafiki au Mangula ambacho kinauwezo wa kutengeneza mataruma ya SGR.Tuna Chuma pale mchuchuma na Liganga ambayo ingesaidia kama kweli tuna nia ya kuwa na viwanda.Ila kama hata wale wafua majembe na mapanga tangu Stone age utahesabu ni viwanda au charahani za barazani basi BIG UP.
 
Alipoitwa ikulu pamoja na wastaafu wengine kwann hakumwambia hili?? Hebu muacheni afanye aonavyo vema
Ndivyo tulivyo
Nadhani kuna kitu alisema na kilikuwa cha muhimu wakati huo na unaweza kukiinganisha na hiki
 
Kura mnazopiga ndio zimetufikisha hapa,mnachagua watu wale wale kwenye majibo kwa kuwaleteeni chumvi na kibaba cha unga,mbunge ana zaidi ya miaka 15 bungeni na jimbo ni masikini yeye mwenyewe kwa kukosa Dira anakaa Dar es Salaam muda mwingi anafanya biashara..alafu huko kwenu mabondeni anatuma fedha za kuzuga,Mbunge hawezi ata kuandaa mchakato jimbo lake liwe na shule za mfano wa kuigwa,Mbunge au Diwani anashindwa kuwapanga wazee katika kaya za kwao kujua dira na mageuzi katika kuleta ustawi wa jamii,ushirika ukijengwa anashindwa kukemea ubadhirifu.Tabaka lililojengeka kati ya Maskini wa kutupwa na Matajiri linakuwa kila siku..Watu wamekuwa wakulia kila siku Misikitini na Makanisani kuomba japo dhiki ipungue lakini wapi! wengine wameamua kujikita katika Ushirikina ili wapate Mali (Dhambi)..Kwa sababu wale wanaojiita VIONGOZI wamesahau au kwa makusudi hawataki kuboresha maisha wanaacha watu wapambane na Hali zao..Kutukuza CCM au kuipamba CDM,CUF au TLP hakutatukomboa endapo RAIA wanashindwa kuchagua KIONGOZI MAKINI ata tukipewa Miaka 1000 na Mwenyezi MUNGU
 
Mkapa alikuwa na amekuwa mzizi mkuu wa tawala zilizofuata baada yake mpaka sasa chini ya CCM (JK na JPM). Amekuwa mmoja wa wanazi na wasiopenda mabadiliko ya aina yoyote, ukiacha yale yanayomnufaisha na kuendelea kumpa nafasi ya kupumua bila usumbufu pamoja na madhambi aliyofanya. HANA MSAADA KWA NCHI.

Mkapa alikuwa na nafasi ya kusimamia uimarishaji wa mifumo na vyombo mbalimbali vya kuongoza nchi ya kidemokrasia, kwa mfano katiba bora, taasisi zilizo huru za kuishauri serikali na kutekeleza sera, mfumo bora wa uchumi SHIRIKISHI unaomilikiwa na watanzania walio wengi, nk. YOTE ALISHINDWA AU ALIYAPUUZIA .

Ni maajabu leo huyu mzee wetu anaongea nyeupe, lakini nafsini hasa anataka nyeusi. Anaongelea mwendelezo lakini anataka katiba ya zamani ya rais kuwa kama mfalme (autocrat). Inaonyesha tamaa yake hasa aone huyu aliyepo anafanya yale tu yanayomfurahisha au aige(aendeleze) yale aliyoanzisha na aliyokuwa anayafanya.... UJUHA.

Mzee Mkapa kama ana nia ya kweli ya kulisaidia taifa basi nguvu zake angezimalizia kwenye kuunga mkono msukumo wa kutengeneza katiba bora inayowapa mamlaka wananchi kuchagua viongozi bora, na kuwawajibisha pale wanapokosea. Hayo mengine anayosemasema hana tena uwezo wa kuyatekeleza. Achague kukaa kimya au ajiunge na sisi tunaolalamikia mifumo ya hovyo hovyo inayolindwa na CCM ili angalau akumbukwe kwa hilo. Aige mfano wa watu kama akina Olusegun Obasanjo kufufua angalau demokrasia. FULL STOP.

Ukiangalia kwa umakini hii ongea ongea ni kujikosha tu ili kukwepa lawama mambo yanavyoenda mrama. HANA LOLOTE.
 
Viwanda huvioni kwa sababu ya makengeza - rejea theory za makundi na aina ya viwanda - vitu hivi viwili vinategemeana sana kwa kuwa:
(i). Ukilima pamba usipokuwa na kiwanda utalazimika kuiuza ikiwa raw (ghafi),
(ii). Ukilima mhogo bila viwanda vya kuongeza thamani utauza makopa,
(iii). Ukivua samaki bila kiwanda utauza alivyo

Dhana ya CCM juu ya viwanda ni nzuri na inaashiria bright future!!
Mhe. Dkt John Magufuli yuko kwenye njia sahihi
 
Ni kipi alichokiendeleza yeye baada ya kupokea kijiti kutoka kwa mzee Mwinyi? Na ni kwanini ushauri huo asimpe jiwe mwenyewe ama anamuogopa?
 
Rais mstaafu huenda kachoka kusikia ya kule sasa kaamua mwenyewe kuweka wazi na kuonyesha hisia na masikitiko yake, msikilize
ILA NI KWELI KWANI WALIMUSHAURI ASIWAGUSE ACASIA, SASA YEYE TAYARI AKAKAMATA MAKINIKIA NA WAKINA MWANYIKA NA WALE WALIODHURUMU WANANCHI WA TARIME
 
Kwahiyo ben anamwambia jamaa mwenzie alikuja na umeme wa gesi yeye anakujw na stigla joji gesi tupa kule wakati tumewekeza zaidi ya 1.5trilioni tena za mkopo
 
hahaha Mkapa ameona ayapooze malofa maana kwa kupenda kudanganywa na kupewa faraja ....sasahivi yamelainika na yatamuita kamanda,kamanda...hahahaha

2020 ikifika tunayaita malofa tena na baadae unayadanganya tena hahaha
 
Mkapa alikuwa na amekuwa mzizi mkuu wa tawala zilizofuata mpaka sasa chini ya CCM. Amekuwa mmoja wa wanazi na wasiopenda mabadiliko ya aina yoyote, ukiacha yale yanayomnufaisha na kuendelea kumpa nafasi ya kupumua bila usumbufu pamoja na madhambi aliyofanya.

Mkapa alikuwa na nafasi ya kusimamia uimarishaji wa mifumo na vyombo mbalimbali vya kuongoza nchi ya kidemokrasia, kwa mfano katiba bora, taasisi zilizo huru za kuishauri serikali na kutekeleza sera, mfumo bora wa uchumi unaomilikiwa na watanzania walio wengi, nk. Ila cha ajabu anaongea nyeupe, lakini anataka nyeusi. Anaongelea mwendelezo lakini anataka katiba ya zamani ya rais kuwa kama mfalme (autocrat). Inaonyesha anataka yale hata huyu aliyepo afanye kama yeye alivyokuwa anafanya.... UJUHA.

Msaada anaoweza kulisaidia taifa kwa sasa ni kuunga mkono msukumo wa kutengeneza katiba bora inayowapa mamlaka wananchi kuchagua viongozi bora, na kuwawajibisha pale wanapokosea. FULL STOP.
Hayo mengine anajikosha tu. HANA LOLOTE.
Huwa nina kawaida moja,mtu akitoa mchango wa hoja wenye maana, kama huu wako, humpa heshima mtu huyo kwa kumwambia kuwa,"wewe ni faida kwa familia yako na taifa."
 
hahaha Mkapa ameona ayapooze malofa maana kwa kupenda kudanganywa na kupewa faraja ....sasahivi yamelainika na yatamuita kamanda,kamanda...hahahaha

2020 ikifika tunayaita malofa tena na baadae unayadanganya tena hahaha
Lol wewe jamaa umeamua kuishi hapa duniani kwa kutegemea Ujinga,nina maana ya kuwa UJINGA WAKO NDIO UNAKUWEKA HAPA DUNIANI.
Sisemi kwamba ungekua una akili ungekwisha kuwa umekufa,hapana namaanisha kuwa ujinga wako ndio mtaji wako.
Nayasema haya kwa sababu wewe kazi yako ni kupindisha kila kila jambo linalokua kinyume chako.Masikini mkubwa wee.
 
Haya kila siku yanasemwa ila ni vile tu leo kaongea Mkulu mstaafu...
 
Back
Top Bottom