Mkapa Complex

Comrade Mfate

Member
Sep 26, 2006
9
0
Jamani kuna hili la uwanja mpya kuhangaikiwa kupewa jina kwa nini asipewe Brother Beni ambaye ndie tunaweza kusema alihakikisha unajengwa? na shangazwa na TFF kwa kutomualika hata katika mechi ya kwanza kuchezwa pale na hakuna kiomgozi yeyote anayestahili kubeba jina la uwanja ule.... Mwanakijiji unaonaje? na memba wote toeni mchango endelevu
 

Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
885
Kwa kweli Ben ndiye aliyehangika kutafuta wafadhili wa kujenga, mi sioni ubaya, maana ni kweli it's to his credit! Lkni si unajua bifu lao na JK katika misifa!
 

G.MWAKASEGE

Senior Member
Jun 29, 2007
153
13
Not neccessary tukaupa huo uwanja jina la Ben twaweza tafuta majina mengine.Currently kama sikosei mafuta house is naed after him na lile daraja la Mkapa pia sasa kama kila kitu itakuwa ni Ben basi itakuwa kero.
Otherwise tunaitaji kumpongeza kwa kuhangaika ilo ingawa kihistoria anaoneka alikuwa John kisomo ata sports alikuwa ana attend rarely.Bravo our beloved Ben
 

Nsololi

JF-Expert Member
Mar 8, 2007
298
80
Mimi naamini ina la uwanja mpya ndio linastahili kupewa jina lake hata kama daraja la mto Rufiki limekuwa named after his name. Lakini bila shaka hakuna atakaye bisha kuwa Uwanja mpya wa mpira ni mradi mkubwa na kitu kinachokuwa vinywani mwa watu zaidi kuliko hilo daraja la mto Rumiji.

naomba tuunge mkono jina la Uwanja mpya kuwa Benjamini Mkapa national Stadium. Huu mradi kauanzisha na kuanza mwenyewe siyo kama daraja la mto Rufiji ambalo awamu zote tatu za awali zilishirki sana ingawa credit wakampa Ben.
 

Nsololi

JF-Expert Member
Mar 8, 2007
298
80
Mimi naamini jina la uwanja mpya ndio linastahili kupewa jina lake hata kama daraja la mto Rufiki limekuwa named after his name. Lakini bila shaka hakuna atakaye bisha kuwa Uwanja mpya wa mpira ni mradi mkubwa na kitu kinachokuwa vinywani mwa watu zaidi kuliko hilo daraja la mto Rumiji.

naomba tuunge mkono jina la Uwanja mpya kuwa Benjamini Mkapa national Stadium. Huu mradi kauanzisha na kuanza mwenyewe siyo kama daraja la mto Rufiji ambalo awamu zote tatu za awali zilishirki sana ingawa credit wakampa Ben.
 

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
14
Nsololi, mh hapo panakuwa pagumu kaka.... Unajua hata kuna watu wengi mashujaa wa zamani kina Mkwawa, Morambo, Kinjekitile, Merinyo, Kambona (mtu muhimu sana kwenye historia yetu huyu jamaa) na wengine weeengi tu ambao wana deserve majina yao kutumiwa... Jamani sasa kama kila kitu kitaitwa majina ya hawa recent prezidaa si kila utakapoenda utakuta jaa anakwambia:
nenda Uwanja wa Mkapa kutokea lindi lazima uvuke daraja la Mkapa, ukifika barabara ya Nyerere utakata kulia utaona shule ya Mkapa upande wako wa kushoto. Usiende mbali mpaka Ali H MWinyi road, kata tu utaona kuna kibao kimendikwa "Uwanja wa ndege JK Nyerere".... ha ha haaaaa. unajua tatizo sis tuna maraisi wa4 tu mpaka sasa sasa kuzuia kuwachanganya vizazi vijavyo tujaribu kufungua wigo wetu wa kufikiri na kuwaenzi pia machifu wa zamani!!!
Kama nimekosea nipo tayari kusahihishwa lakini hili la kutumia majina lazima liangaliwe eti....

Naomba kuwakilisha...
 

Bowbow

JF-Expert Member
Oct 20, 2007
541
28
Mimi sikubaliana na mawazo yenu hata Moja.

Kwanza tukumbuke siku za nyumba Fedha zetu zilikua kila rais Mpya akipatikana anataka picha yake kwenye note na Coins ila baadae tuliachana na utaratibu huo na sasa tunahitaji kuondokana
na utadani.

Nani anajua jina halisi la eneo ambalo sasa linaitwa (Uwanja wa taifa), Naamini kulikuwa na jina la eneo hilo lakini limeshaulika

Kuna mashujaa wangapi waliokufa wakati wa harakati za Uhuru hawakuwa na cheo, butvery courageus na hadi leo hawatambuliki?

Tukisema BWM ndio alitafuta hao wafadhili, Je mkapa ndio alichora hiyo ramani, ndio aliyeandika proposal na hata kama ndio je wapishi wake, bodiguards wake na subordinates wengine wataonekana wapi? maana na wao walimwezesha kufanya hiyokazi.

Kama ni suala la heshima na kumbukumbu ya ukuu wa nchi, Daraja, former mafuta house, Secondary iliyopo jijini vinatosha.

Ila ni wakati sasa wa kuwapa watu mbali mbali heshima ofauti na wana siasa. Kuna watu waliokoa maisha ya watu mbalimbali katika majanga mbali, kuna reserchers, kuna wachezaji walioletea sifa nchi yetu, kuna wanajeshi waliofia nchi yetu wakati wa Vita na natural calamities hao wanakumbukwaje?
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,916
287,620
Na mabaya aliyotufanyia je mnayasahau? Alifanya biashara akiwa Ikulu nyuma ya migongo ya Watanzania na hana mpango wa kuwaambia Watanzania alifanya biashara gani na nani. Aliwaleta makaburu wa Net Group solutions ambao wameiacha Tanesco katika hali mbaya sana kifedha na hawakufanya lolote la maana pamoja na kulipwa mabilioni. Amechukulia katika mazingira ya kutatanisha Kiwira Coal Mining na kuishinikiza TANESCO kusaini na 'mgodi wake' mkataba wa shilingi 340 bilioni ambao hauna maslahi yoyote kwa Watanzania. Anahusika na kusaini mikataba ya madini na kuamua kuifanya siri kwa wenye mali wa rasilimali hizo ambao ni Watanzania.

Kwa kifupi ameonyesha dharau kubwa kwa Watanzania na ametuingiza gharama kubwa za mikataba ya madini, Makaburu wa Net Group, kujichukulia KCM hivyo kwa maoni yangu Watanzania hawastaili kumpa heshima yoyote ya kuita chochote kila jina lake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom