Mkapa Appointed as a New Member of International Crisis Group | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa Appointed as a New Member of International Crisis Group

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyauba, Jul 2, 2010.

 1. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  B.W.Mkapa, kachaguliwa kuwa mjumbe wa katika hiyo taaisisi ya kimataifa ya kukabiliana na migogoro akiungana na wajumbe wengine 14, venye rekodi imara kitaaluma na utendaji.

  mnyonge mnyongeni ila chenkapa kichwaa bwanaa....

  Go BEN.
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  namkubali sana huyu mzee kwenye upeo wa mamboo...
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mzee namkubali saaana pamoja na kutafuna Nchi
   
 4. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ben, mie pia namkubali sana tu sema kuna watu wamefundishwa kumchikia ndiyo tatizo.
  Lakini jamaa anamashiko siyo kama huyu "Mrisho Mpoto"
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hongera zake na sifa kwa nchi pia
   
 6. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,421
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Kweli Ben kichwa! Lakiniiiiii.......aliisaliti nchi yake kwa kuiuza na kuitafuna kwa pupa ya ajabu! hakuna mtu anafundishwa kumchukia huyu bwana....matendo yake ndio yamuandama. Hivi ninyi hamuoni walakini kwenye mtu huyu anayesifiwa kuwa na akili lakini akatumia hizo akili kuwatapeli wananchi wake?. Ben ni mzalendo 5% tu.....Nyerere aliingia mkenge hakujua huyu jamaa ana akili lakini hana uzalendo.

  Anyway, sisi wengine tuna wivu wa kike na ni wavivu wa kufikiri....kufuatana na viwango vya Ben "Kiwira".
   
 7. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nyauba,

  hapo red/bold waweza ku-edit ili sentensi ilete maana iliyokusudiwa?

  BMW: Pamoja na jeuri yake, lakini he can no be compared by ....
   
 8. J

  Jafar JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Go Ben, go.
   
 9. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  The Devil you know is better than the Angel you don't know! Kwangu mimi is an Angel I don't know, so namkubali Ben, pamoja na mapungufu yake lakini aliiacha TZ na uchumi wenye muelekeo! Thumb Up Ben!
   
 10. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  The Devil you know is better than the Angel you don't know! Kwangu mimi JK is an Angel I don't know, so namkubali Ben, pamoja na mapungufu yake lakini aliiacha TZ na uchumi wenye muelekeo! Thumb Up Ben!
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Mkapa ni too intellectual, hizo kazi za ma think tank na ma commitees zitamfaa sana, kuendesha nchi anaweza kuua watoto. Huyu rais wetu wa sasa on the other hand yuko kwenye the opposite end of intellectuallism, mening idiocracy.
   
 12. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida ya Watanzania na upumbavu wao. Mitanzania ndivyo ilivyo! Mara tu wanampigia debe Mkapa pamoja na makosa yake chungu nzima aliyoyafanya. Mkapa kichwa! angekuwa kichwa angefanya upumbavu alioufanya akiwa Ikulu? Kweli Miafrika ndivyo ilivyo!
   
 13. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Umefundishwa kumchUkia Ben, upumbavu gani wa ajabu?? kama ni kuchemka mbona hata mwalimu alikiri kuchemka?? ni kawaida kwa binadamu kukosea, lakini naona wewe umeshiba chuki dhidi ya Ben.....
  Haya basi Vasco ndiyo kichwa furahi......
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Anaweza kuwa kichwa kwa maana ya intellectual lakini asiwe kichwa katika mambo ya empathy/ emotion, hapo akawa imbalanced, asijali wananchi sana, akawalipisha madeni kama kichaa, akauza nchi kama hana akili nzuri.

  Ukimlaumu kwamba hakuendesha nchi vizuri kama kiwango cha usomi wake kilivyotaka nitakubali, ukisema hakuwa msomi bonafide nitakushangaa.

  Kuwa "kichwa" (depending on your definition of kichwa, here meaning the intellectual aspect) hakumaanishi kwamba mtu automatically ataiendesha nchi vizuri.

  Angalia Afrika Kusini huko ambako "kichwa" kingine (Thabo Mbeki is a bonafide intellectual) kimechemsha kuendesha nchi kwa kutokuwa discreet kuhusu pseudoscientific dispositions zake kwenye HIV, na sasa hivi huyu idiocrat Jacob Zuma ambaye hata shule inagomba anaelekea kumfunika Mbeki hata kwenye fight against AIDS.

  Kwa hiyo kuwa "kichwa" si jawabu la kuweza ku run nchi mara zote, in fact kuna wasomi wengine kwa mfano muandishi wa kiingereza Paul Johnson aliyeandika kitabu "Intellectuals : From Marx and Tolstoy to Sartre and Chomsky" ana argue kwamba there is a point of diminishing returns in the pursuit of intellectuallism, point ambayo ukiipita, unavyozidisha usomi ndivyo unavyozidi kupotosha ukweli, kukosa utu na empathy etc.

  Kwa hiyo usomi mwingi sana si kitu kizuri mara zote, hata waswahili walisema "Akili nyingi huondoa maarifa".
   
 15. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha upumbavu wewe! umetumwa hapa kuja kumpigia debe Mkapa? Tofauti ya Mwalimu na Mkapa, Mwalimu hakuwa mwizi wala mroho wa utajiri. Mkapa kafanya makosa mangapi? Hebu yahesabu kisha utwambie kama kweli aliingia madarakani ili kulinda maslahi ya nchi ama kujitajirisha
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Jamani URAIS unaharibu pia. Ben aliharibiwa na TAASISI hii ya Urais kisha Mama Anna akammalizia.
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Hizi habari za Mama Anna kumharibia Ben si za kweli hata kidogo.Kati ya watu wenye ma argument bongo, watu wenye ushawishi Ben Mkapa ni mmoja wapo.The man has been an Editor of the Daily News for aeons, hata kabla hajaenda foreign kina Kaduma walivyokuwa wanachemsha kwenye mazungumzo na ma Henry Kissinger huko Mkapa ndiye alikuwa anaenda ku save the day, this is way back in the late sixties and early seventies, baadaye Nyerere akamtupa balozini na halafu Foreign.

  Mkapa kaenda kwenye mkutano wa Commonwealth wakati wazungu wamempigia kampeni ya kumsuta Mugabe, akawageuzia kibao wazungu na kuwasema kisawasawa, kwa usomi wa hali ya juu, akamtetea Mugabe, na si hivyo tu, baada ya hapo mpaka Tony Blair akamuomba aje kufanya kazi naye.Huyu si mtu wa kuendeshwa endeshwa na mke wake kirahisi.

  Matatizo aliyojikuta nayo Mkapa yote aliyataka mwenyewe.Hizi habari za kumtupia Mama Anna lawama zinaturudisha kule kule kwenye mfumodume unaosema mwanamke ndiye chanzo cha matatizo, na Adam alifanya dhambi ya asili kwa sababu ya Eva.

  Hogwash.Mkapa alijua kila kitu alichofanya na alitaka kufanya hivyo.Mama Anna, kwa watu wanaoijua familia ya Mkapa on a personal level kama mimi, wanajua kwamba hakuwa na uwezo wa kumu influence Ben Mkapa hivyo.
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Awe tayari kushiriki ku mediate na crisis ya uchaguzi mwezi wa kumi Tanzania maana hapa tu watu wametunga sheria kwa mbwembwe na wanazivunja wao wenyewe hata kabla ya uchaguzi. Sasa sijui ata side upande gani!:A S confused:
   
 19. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  he deserves
   
 20. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Raia Mwema

  MZIMU wa uuzaji ya nyumba za Serikali mpango ambao ulitekelezwa kwa kasi katika Serikali ya Awamu ya Tatu, chini ya Rais Benjamin Mkapa, umeigharimu Serikali ambayo sasa inalazimika, katika mwaka huu wa fedha kutumia takriban Sh bilioni 5.7 kujenga nyumba mpya ili kuokoa mamilioni yanayotumika kuwalipia watumishi wanaolazimika kukaa hotelini kwa kukosa nyumba, Raia Mwema imebaini.

  Hata hivyo, kiasi hicho cha fedha kilichotengwa katika mwaka huu wa bajeti ni pungufu ikilinganishwa na kile kilichotengwa katika bajeti inayokwisha siku chache kuanzia sasa. Katika bajeti hiyo ya 2009/2010 Serikali ilitenga Sh bilioni 11.4 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zake.

  "Ujenzi wa nyumba za serikali mwaka 2009/2010 uliidhinishiwa Sh 11,385,000,000, mwaka huu wa 2010/2011 umetengewa makadirio y ash 5,696,670,000," inaeleza sehemu ya waraka wa kibajeti wa Wizara ya Miundombinu, kitengo cha Huduma za Ufundi na kufanya jumla ya fedha katika miaka miwili mfululizo kufikia Sh 17,081,670,800 (zaidi ya sh bilioni 17).

  Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa tangu kuanza kwa Serikali ya Awamu ya Nne, uteuzi wa baadhi ya viongozi wakiwamo majaji wapya, umekuwa ukifanyika huku wahusika wakilazimika kuishi hotelini kutokana na uhaba wa nyumba za Serikali katika maeneo vilipo vituo vyao vipya vya kazi. Baadhi wanaolala katika hoteli ni pamoja na wale wanaohamishwa kutoka mikoani na kupangiwa jijini Dar es Salaam.
  Kati ya uamuzi uliopata kukosolewa sana wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu ni uuzaji wa nyumba za Serikali uliofanyika kwa pupa nyingi ya nyumba zilizouzwa zikiwa ni pamoja na za maofisa wa polisi maeneo ya kambi zilizuzwa kwa maofisa hao na hivyo wahamiapo wengine kukosa sehemu ya kuishi.
   
Loading...