Mkapa amwokoa Kikwete, azima hoja ya kumng'oa madarakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa amwokoa Kikwete, azima hoja ya kumng'oa madarakani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 28, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  na Salehe Mohamed
  Tanzania Daima


  RAIS mstaafu Benjamin Mkapa, alimnusuru Rais Jakaya Kikwete kwenye kitanzi cha kung'olewa kwenye wadhifa wa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.

  Kwa mujibu wa wajumbe waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) kilichomalizika Novemba 24 mwaka huu mkoani Dodoma, walibainisha kuwa baadhi ya wajumbe walijipanga kutoa hoja ya kumtaka Rais Kikwete kuachia wadhifa wake.

  Wanasema kuwa walipanga kufanya hivyo kwa madai kuwa katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete chama kimekuwa na migogoro mikubwa na kuifanya serikali iyumbe kila kukicha.

  Walibainisha kuwa fursa ya kutoa hoja hiyo haikupatikana baada ya Mkapa kumtaka Rais Kikwete kusitisha hoja ya kuvuana magamba, baada ya kuona upepo mbaya ulikuwa ukimvumia kiongozi huyo.

  Inadaiwa Kikwete alikubali ‘msaada' huo wa Mkapa ambapo alisema hoja hiyo imetosha kwa kuwa suala hilo lilirejeshwa kwenye kamati ya maadili, ambayo itapokea ushahidi wa tuhuma za makada hao pamoja na kuwapa fursa ya kuwasikiliza watuhumiwa.

  Kwa mujibu wa wajumbe hao wa NEC, waligawanyika makundi mawili, moja likitaka Lowassa atoswe kwenye uongozi huku jingine likipinga kwa madai kuwa tuhuma za kada huyo hazijathibitishwa.

  Lowassa alipopata nafasi ya kuchangia hoja hiyo, alieleza kusikitishwa na ufisadi wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond ambapo alisema kila alichokuwa akikifanya Rais Kikwete alikuwa anakijua kama si kumtuma.


  Aliongeza kuwa pamoja na kujua huko kwa Rais Kikwete juu ya kashfa hiyo, bado alishindwa kuwakemea watu waliokuwa wakimhusisha Lowassa na ufisadi wa Richmond, ambao inadaiwa ulifanywa na watendaji wa serikali.

  Rais Kikwete na wasaidizi wake mara kadhaa wamekuwa wakikana kiongozi huyo mkuu wa nchi kuijua na kuhusika na mkataba wa Richmond ambao ulifanya Bunge kuunda kamati teule kuchunguza mchakato ulioipa ushindi zabuni ya kampuni hiyo.

  Katika kikao hicho cha NEC, Lowassa alibainisha kuwa kama tuhuma zingekuwa zinamng'oa mtu madarakani bila kufanyiwa kazi, basi Rais Kikwete asingekalia kiti cha uenyekiti wa CCM kwani mwaka 2003 alizushiwa tuhuma za ukosefu wa maadili na kada mwenzao, Paul Sozigwa.

  Mbunge huyo alisema kama si busara za Mwenyekiti wa CCM wakati huo, Benjamin Mkapa, Rais Kikwete asingeukwaa urais, hivyo ni vema chama kifuate utaratibu waliojiwekea wa kushughulikia tuhuma zinazoelekezwa kwa makada wake.

  Baada ya Lowassa kutoa utetezi wake huo, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, alisema halikuwa jambo la busara kuwatuhumu watu na kutangaza tuhuma dhidi yao kabla ya kuthibitishwa kwa tuhuma zenyewe.

  Sumaye alionekana kukerwa na ukimya wa Rais Kikwete juu ya kuchafuliwa kwa Lowassa kulikokuwa kukifanywa na Katibu wa Itikadi na Unezi, Nape Nnauye pamoja na Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Chiligati.

  Sumaye alihoji iwapo kamati ya maadili itabaini kuwa Lowassa hakuwa na hatia, hatua gani zitachukuliwa dhidi ya Chiligati na Nape waliosambaza tuhuma hizo.

  Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa hoja ya kumng'oa Kikwete ilikuwa ikiungwa mkono kichini chini na vigogo wengi ambao hapo awali walikuwa wakidaiwa kumuunga mkono Rais Kikwete.

  Vigogo hao inadaiwa hivi sasa wamekuwa wakikerwa na jinsi Rais Kikwete anavyoyashughulikia matatizo ya chama hicho kwa kuendekeza siasa za makundi yanayohasimiana.

  Baadhi ya wajumbe wa NEC, wamelidokeza Tanzania Daima kuwa kama Rais Kikwete hatajirekebisha kwa jinsi anavyoshughulikia matatizo ya chama tishio la kung'olewa kwenye unyekiti wa chama hicho litaendelea kumuandamana.

  Waliongeza kuwa kwa hali ilivyokuwa ndani ya kikao hicho, Lowassa anaonekana kuwa bado ni tishio kwa vigogo wanaotajwa tajwa kuwania urais mwaka 2015.

  Walibainisha kuwa licha ya kuwepo mikakati ya kutaka kiongozi huyo asipate fursa ya kujenga mtandao wa kumsaidia kuingia ikulu, Lowassa anaonekana kuwa imara zaidi kukabiliana na wapinzani wake.

  Kabla ya NEC

  Awali kulikuwa na tetesi kuwa Rais Kikwete alipokea pendekezo ya kuwang'oa madarakani baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaodaiwa kuwa ndio chanzo cha mitafaruku ndani ya CCM.

  Miongoni mwa waliokuwa wakisemwa kung'olewa madarakani ni Lowassa, Sitta, Nape, Chiligati na Chenge.

  Inadaiwa kuwa baadhi ya makada wa chama hicho walikodishiwa usafiri kutoka kwenye maeneo yao na kulipwa posho ili kwenda kushangilia Lowassa, Chenge na wengineo wanavulia madaraka.

  Kundi jingine nalo linadaiwa kupelekwa mkoani Dodoma kwa lengo la kushangilia kung'olewa kwa Sitta, Nape na Chiligati.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaweka wazi kuwa uamuzi wa CCM kulirejesha suala la kujivua gamba kwa kamati kuu ambayo italipeleka suala hilo kwenye kamati ya maadili kutafutiwa ufumbuzi kutazidisha mtafaruku ndani ya chama hicho.

  Wameweka wazi kuwa hivi sasa mpasuko utakuwa zaidi ndani ya chama hicho hasa baada ya taarifa kuwa Chiligati na Nape walikuwa wakiwashambulia makada wenzao tofauti na maagizo ya kikao cha NEC kilichofanyika Aprili mwaka huu. Wamedokeza kuwa sasa makundi hasimu yatajiimarisha ili kuhakikisha makada wanaowaunga mkono hawapati adhabu pindi itakapobainika wamekwenda kinyume na maadili ya chama hicho.
   
 2. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Kaole style at work, watafunika kombe mpaka lini?
  Migongano si inaendelea kujengeka ? Usipokunywa krolokwini utaishia ICU . Any way bora iwe hivyo ili magamba yapasuke
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hili gazeti linazidi kupoteza muelekeo, Freeman asipomuondoa Kibanda kama mhariri mkuu na kumpa nafasi hiyo Ngurumo hili gazeti litapoteza umaarufu kama na kutoweka kama motomoto enzi za NCCR ya Mrema!

  Matumizi ya Kibanda yanayofanywa na Lowassa yanaharibu sifa ya TANZANIA DAIMA, Gazeti limekuwa likifanya kazi za CCM Lowassa!
   
 4. H

  Hosida Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unafika huwa una kikomo, na kikomo chake hakiachi fedheha nyuma. Kuhusu magamba sasa watavuana mpaka ngua za ndani wakifikiri ni magamba.
   
 5. M

  Madodi Senior Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 181
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  mmmmmmhhhhh........
   
 6. g

  gomezirichard Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ee Mungu eponye Tanzania, mi nashangaa ivi hawa watu wanatafuta nini kwenye nchi yetu pamoja na mapesa yote waliyo nayo, 2015 ni wakati Mungu kuiponya Tanzania hakika atatusaidia

  Mzee Gomezi
   
 7. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hamna jambo zuri litakalojenga mustakabali wa nchii hii kama kugombana hadharani na hatimaye kuvunjika urafiki kati ya EL na JK. Sasa hivi hii yote ni minong'ono na ugomvi wa chinichini, bado urafiki wao upo imara.
  Think of all the repercussions, hizi si zama za Nyerere ukigombana naye unakimbilia nje au unapotea kabisa, siku hizi ni hapahapa.
   
 8. m

  matawi JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hili zege limeshakorogwa lazima ukuta ujengwe
   
 9. President Elect

  President Elect JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 693
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Lowassa ni wetu (hatujakutana barabarani, nooo), CCM ni yetu na Ikulu ni kwetu. Kelele za mlango hazi.....mkitaka kikao na mh. Rais dr.JK leteni barua ikulu mtasikilizwa, mbona mifano iko wazi jamani!
   
 10. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kama unachofanyiwa wewe Lowassa ni uzushi,na unasema hata JK alifanyiwa uzushi,basi kwangu mimi na Watanzania wengi tunaoona ni ukweli Basi wewe Lowassa na Kikwete wote hamna maana na mmekosa legitimacy ya kutuongoza kwa sababu kila kitu ni kweli juu yako, hivyo basi na kwake ilikuwa kweli(Hatukukutana barabarani EL,2010-2011pp.1).Kulingana na article hii "JK hana Maadili" (Sozigwa 2003).
  Richmond inajulikana na Jakaya Kikwete (Edward Lowassa,2008-2011).
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  uliishandanganywa na kujiaminisha

  tulisema na tunasema huwezi kutofautisha, JK, EL, CDM, na Mbowe.........nje ya hapo ni ubishi na aibu!
   
 12. Kumbakumba

  Kumbakumba JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tutafika tu
   
Loading...