Mkapa ajitosa sakata la gesi, apendekeza njia ya mazungumzo kutafuta muafaka!

Nyie wana Mtwara hata Tanesco iliwasusa kwa kuona haiwezi fanya biashara na watu wasio na uwezo kifedha......Serikal ikaruhusu mtu binafs( ATMAS)awauzie Umeme kwa mitambo yake bado na yeye akaona hamstahil maana hakuna anachopata......Mkapa kwa bidii zake akawaokoa kwa kushirikiana na Serikal na Tanesco leo hii mna Umeme hata kukatika tu ni ngumu......Serikal ikiamua iwaachie hiyo Ges nyie wana Mtwara mnaweza kuichimba....?? je Dawa kwenye Mahospital mnaweaza pata....?? na mahitaji mengine mengi mengi sana ya kijamii ambayo nyie hamsatahili kama ingekuwa kila mkoa ufaidike na mali zake....!! Wana Mtwara amkeni sasa wanasiasa wanawapoteza......mtabaki na umasikin kwenu Mtwara huku wao Mikoa yao ikiwa Bora.....!! Hao woote Viongozi wanaopiga kelele na nyie wana majengo ya KIFAHARI DAR ES SALAAM mwisho wa cku watawaacha na huko huko na ujinga wenu.....AMKEN WANA MTWARA........!!
 
Mnataka wanamtwara wakae na nani? Rais wenu dhaifu ameikimbia nchi. mi naona wanamtwara wakaze buti tuu
 
Angalia historia
Mwalimu alistaafu akaenda Butima , Mwinyi kaenda kwao na sote tunajua anakoishi rasmi , huko Zanzibar wote wame enda maeneo yao .Mkapa si wa Mtwara ni mtu toka Tanga .Yeye akae kimya waachie watu na Mtwara yao .
 
Taarifa yake kwa sehemu kubwa,yaani asilimia 98 ametoa wito kwa wanaMtwara kuwa wavumilivu.
Na sentensi moja tu ya mwisho,ndiyo kainasihi serikali.. "LINALOWEZEKANA LEO....."
 
Mkapa kuwa na uzalendo? Hapana! Naona Mkapa kutumia neno hili kwa watu wa Mtwara siyo sahihi hata kidogo. Labda atuambie uzalendo wake ni upi? Kipi alichkifanya kwa mkoa wa Mtwara kitakachodhihirisha uzalendo wake? Mbaya zaidi Mkapa siyo mwenyeji wa Mtwara,so please akae kimya asituingilie.
 
Mkapa kuwa na uzalendo? Hapana! Naona Mkapa kutumia neno hili kwa watu wa Mtwara siyo sahihi hata kidogo. Labda atuambie uzalendo wake ni upi? Kipi alichkifanya kwa mkoa wa Mtwara kitakachodhihirisha uzalendo wake? Mbaya zaidi Mkapa siyo mwenyeji wa Mtwara,so please akae kimya asituingilie.

hata wewe che nkulia unamwambia mkapa sio wa mtwara?kweli mkapa amekalia kuti kavu kama hadi wala yeila wenzie mnamtosa
 
BMW is a man firm on issues, mbona daraja la Umoja halikua na maandamano,
Ongea na Nchomba nchumali waache fujo gas haiwezi bebwa na ndoo kama maji.
 
Hili jambazi kwa kukingiwa kifua na Kikwete katika ujambazi alioufanya alipokuwa madarakani hata siku moja hawezi kutoa kauli yoyote ile ya kumpinga Kikwete. Wanamtwara mngangamare kupambana kuhakikisha gesi haipelekwi kwa wakwere na kamwe msimsikilize huyu fisadi.
 
Uncle Benja, ujumbe wako hauko waz sn bwn umeuma na kupuliza hapa....unaposema tuache kufanya harakati kw lengo la kukaa meza moja na sirikali, unatupa walakini wanamtwara...JE NI WAPI NA LINI SIRIKALI IMEONESHA NIA YA KUKAA NASI KUFANYA MAZUNGUMZO?? Zaidi ya kuitwa wapuuzi,mambumbumbu, wahaini na mkuu wa kaya kutoa karipio kuwa mjadala wa gas amefunga!!! UNCLE MKAPA UNATAKIWA UMCHANE JK LIVE KUWA MKAKATI ULIKUW KUJENGA MITAMBO YA KUFULIA UMEME NA KUCHAKATA GAS MTWARA NA SI KUJENGA BOMBA. mapambano huku yanaendelea km kawa!!
 
Ivi mikoa mingine kama Shinyanga, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha kwanini wasiige hii staili walikuja nayo Mtwara? Bila kusahau kwa marehemu Chacha Wangwe?
 
Acha ushamba na ushabiki wa kufuata wezi bila kujua kwa kina kinachoongelewa wewe, kama hujui bora unyamaze sio lazima uchangie kila kitu. Wanachi wa mtwara sio kwamba hawataki gesi yao itumike kwa manufaa ya nchi kwa ujumla wake ila hoja ni je kwa nini hiyo plant ya kufua ges isiwekwe Mtwara ili izalishe ajira kwa watu wa mtwara na wakasafirisha gesi ambayo tayari imeshakuwa processed kwa ajili ya usambazaji tu. Na kwa nini lazima iprocessiwe Dar then Bagamoyo,Bandari B/moyo na kuboresha ya Mtwara au kwa sababu watu wa mtwara ni third class ya watanzania, first class na second wako Dar na B/moyo. Shame on you. Kwanza concentration ya uzalishaji sehemu moja kitaam inaongeza msongamano wa wtu ambao ndo tunapigia kelele kila siku Dsm. Kwa nini uzalishaji usifanyike nje ya Dar. Na hili kitaalam linawezekana kwa kuangalia kipi kati ya mali ghafi na products ni cost effective kiuchumi. Sasa wewe wadandia hoja tu eti kwa sababu Mkapa kasema, Mwizi wa Migodi huyo kama hujui.

Ishasemwa, Mkapa hana moral authority kuzungumzia gesi ama rasilimali ya Tanzania maana katika uongozi wake ndio mikataba yote ya gesi, mafuta na madini imeingiwa, ndio sheria zote za ovyo za uwekezaji na ubinafsishaji imetungwa, ikapitishwa na kusainiwa nayeyeye, ndio kipindi ambacho wamebonafsisha na kujiuzia mashirika, makampuni, migodi, mashamba na hata ng'ombe wa umma... Pili, sakata la fedha za Uswisi na gesi linamgusa yeye na Daniel Yona, aliyekua Waziri wake wa Nishati na Madini, yeye akiwa Rais na ni Yona ambaye walipora naye mgodi wa Kiwira na Kabulo Rig....
 
Nyie watu wa Mtwara Mkapa kawaokoa sana.....na kawasaidia sana,Maisha yenu yalikuwa mabaya kiasi cha mfanyakaz akihamishiwa huko anaacha kaz....leo hii mnamzarau Mkapa kwa ushauri wake wa kukaa mezan kujadiri....?? Hebu kumbuken mlikuwa mnatumia cku ngap kwa usafiri wa gar kuelekea Dar....?? Hiyo haitoshi uwanja wa ndege ulikuwa unatua ndege gan tofauti na Ndege ya Jeshi....?? leo hii mnasimama kuinua midomo kupasa saut ya Ges haiendi Dar kweli......?? Maendeleo hayo mliyonayo sasa mnahis ni pato Gan limepelekea nyie wana Mtwara kupata hata balabala.....??Acheni UJINGA TAIFA LISONGE MBELE.......!!
Tatizo hujui ulisemalo. Kwanza jitahidi kuijua Mtwara, sio kwa kusimuliwa tu; kwa kuiona kwa macho, ndio utakuwa na uwezo wa ku-comment kuhusu Mtwara.
 
M-aarifa
T-unayo
W-azawa
A-mkeni
R-ais
A-tatudhulumu.

Kirefu cha MTWARA- kuna flana nyingi tu zimechapishwa sasa zikiwa na kirefu cha MTWARA....na vijana wengi wanavaa fulana hizo kuhamasishana.

Nadhani hizo zitapigwa marufuku kama zile za '...sizitaki kura za wafanyakazi...'
 
Kukaa meza moja na wezi wa raslimali za taifa ambao wanastahili kuwa jela??!!!! Hata haiingii akilini!!!!
 
Nyie watu wa Mtwara Mkapa kawaokoa sana.....na kawasaidia sana,Maisha yenu yalikuwa mabaya kiasi cha mfanyakaz akihamishiwa huko anaacha kaz....leo hii mnamzarau Mkapa kwa ushauri wake wa kukaa mezan kujadiri....?? Hebu kumbuken mlikuwa mnatumia cku ngap kwa usafiri wa gar kuelekea Dar....?? Hiyo haitoshi uwanja wa ndege ulikuwa unatua ndege gan tofauti na Ndege ya Jeshi....?? leo hii mnasimama kuinua midomo kupasa saut ya Ges haiendi Dar kweli......?? Maendeleo hayo mliyonayo sasa mnahis ni pato Gan limepelekea nyie wana Mtwara kupata hata balabala.....??Acheni UJINGA TAIFA LISONGE MBELE.......!!

Acha kuonyesha ujuha wewe, wangapi Mtwara wanaweza kumudu gharama ya kupanda ndege? eti acheni ujinga Taifa lisonge mbele, kama huna la maana la kuandika kaa kimya badala ya kuonyesha ujuha wako.
 
Ni aibu sana kujibu coplex hoja with simple argument au complex issue using simple solution without even taking precautions, ila nasema hivi, simple approach itafanikiwa iwapo bado watu wako tayari kuwa suppressed.

Kwanini serikali isiweke mkataba husika wazi au na wenyewe ni siri na kufocuss mazungumo na utetezi kwenye mkataba na miakati husika? Haya yote yanaweza kuzungumzika ila kutishia na kudhani kuwa bado unaweza ktumia nguvu, kweli utatumia nguvu mahali fulani labda Arusha ila inaweza kwua tofauti kwa Mtwara.

Chama Changu Cha CCM hebu tumieni busara muonyeshe kweli mmekomaa achaneni na tabia ya kulaumu vyama vya upinzani imeptiwa na wakati, watu wamepevuka wekeni hoja na muongee kwa busara bila kutafuta mchawi, na muwaonyeshe watu kuwa mnaaminika na mnachokusudia si kwa ajili ya kuwakomoa CHADEMA kwakuwa wanachama wao kila siku wanarudi CCM na wa CCM wanarudi CHADEMA nikimaanisha mmepewa dhamana ya Raia hiyo tabia ya kuogopa kivuli chenu na kuhangaika na bwa mdogo CHADEMA inaonyesha udhaifu wa wazi.
 
SOUTHERN REGIONS DEVELOPMENT ASSOCIATION

BARUA YA WAZI,


MH, BENJAMINI WILLIAM MKAPA,
RAIS MSTAAFU,
LUSHOTO (PEPONI)

Salaam

Tumefuatilia ushabikiaji wako wa mradi wa kuhamisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam kwa umakini mkubwa sana.


Mheshimiwa utakumbuka kuwa mara tu ulipoingia madarakani 1995 ulikuwa umewakuta wananchi wa Mikoa ya kusini kupitia umoja wao wa Maendeleo ya Mikoa ya kusini (UMMK) tayari wamo kwenye mchakato wa kupinga mradi wa kutoa gesi ya Songosongo (Mkoa wa Lindi) kuja Dar es Salaam.


Baada ya jitihada za kiungwana ikiwa pamoja na kuonana ana kwa ana na Rais aliyekutangulia MH. ALLY HASSANI MWINYI (Tukiongozana na mlezi wetu Rais Mstaafu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Mzee ABBOUD JUMBE) kushindwa, tukalazimika kupeleka kilio chetu Mahakamani (Civil case No. 1, 1996).
Kwa msaada wa Mungu tukafanikiwa kusimamisha mradi huo kwa muda kusubiria upatikanaji wa muafaka.


Mheshimiwa wewe (serikali yako) ukajitosa kwa hali na mali kupambana na sisi maskini wanyonge kuhakikisha kuwa tumebwagwa ili mradi huo utekelezwe kwa nguvu ya dola kwa visingizio hivi hivi vya kisomi na kitaalam kwamba Wanachi wa Kilwa na Mkoa wa Lindi na Mtwara kwa ujumla pamoja na wananchi waishio eneo litakapopita Bomba hali yao ya maisha itabadilika.


Ndipo tarehe 26/05/1997 ukatuma ujumbe wa Full Council ya Wilaya ya Kilwa ukiongozwa na Mwenyekiti wake MZEE MTOPA na Mbunge wa Kilwa Kusini kuja kutuhadaa na kutughilibu tufute kesi kwa kuwa Serikali itatekeleza yote au baadhi ya wanayoyahitaji wananchi wa Kilwa.


Mkutano huo wa madiwani wote wa Kilwa na sisi UMMK ulifanyika tarehe 27/05/1997. Wizarani Ofisini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati wakati huo Mh. Patric Rutabanzibwa Waziri akiwa Mheshimiwa Kigoda. Sisi tulikubali hilo kwa manufaa ya Taifa letu. Siku chache kabla ya ujumbe huo walifika watu nyumbani kwangu nisiowafahamu na wala hawakujitambulisha kuwa wao ni nani na wanaatola wapi?. Walikuja na fedha ambazo walitaka wanipe kama zawadi endapo mimi nikiwa Mwenyekiti wa wadhamini nitaishawishi bodi ifute kesi. Nilipokataa wakaniuliza unataka nini?. Nilipowajibu kuwa ¡§Utu wangu¡¨ walisonya na kutoweka.


Siku iliyofuata tukiongozana na Serikali Mahakama Kuu mbele ya Jaji Mheshimiwa Marehemu Mapigano tukaomba kesi ifutwe tukakubaliwa. Sisi hatukufahamu mpango wa ghilba. Tulipumbazika kwa sababu ya Imani tuliyokuwa nayo kwa Serikali yetu tukufu kwamba kamwe isingeweza kusema uongo kwa makusudi. Ni ajabu lakini ndivyo ilivyotokea. Tunatoka tu nje ya Mahakama wewe Mheshimiwa (Serikali yako) wakaturuka kwamba mchezo umekwisha hakuna tena mazungumzo kuhusu mstakabali wa kuwapatia wananchi mrahaba au chochote kama tulivyoafikiana kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu. Tukabaki tumeduwaa.....!


Ndipo tukaamua kurudi tena Mahakamani na tukafungua kesi mpya CC No. 36 ya 1997. Mheshimiwa (Serikali yako) ulipogundua hilo la kesi mpya ndipo ukaamua kutupiga vita kisiasa. Ukaagiza baadhi ya Mawaziri wafanye mikutano ya hadhara ya kutudhalilisha na kutulaani ¡V bila kujali kesi iko Mahakamani au la ikapelekea sisi kushindwa kwa mazingira ya utata.


Mheshimiwa utakumbuka pia ni wewe (Serikali yako) ulipanga gesi ya Mnazi Bay (MTWARA) iwe kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi tu- kwamba Mikoa hiyo watakuwa na gridi yao pekee. Gesi ya Songosongo itapelekwa Dar es salaam haitahusika kwa maendeleo ya Mkoa wa Mtwara na Lindi. Sisi tulipinga
kutengwa na Watanzania wenzetu (Hansard ya tarehe 31/01/1997 uk.9) Aidha isingekuwa vema mali asili hii itumike sehemu moja tu ya nchi. Tulishauri uzalishwe umeme huku huku ilikopatiakana gesi (Mtwara na Lindi) kisha kuunganishwa kwenye gridi yetu ya Taifa. Na tulitoa sababu ya msingi ya faida ya mawazo yetu na hasara ya mawazo hayo ya Serikali. La ajabu leo hii tunasingiziwa sisi wa Mikoa ya Kusini ndio wenye mawazo hayo finyu.


Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi. Leo hii umma unapotoshwa kwamba wananchi wa Mtwara hawakuelimishwa kuhusu gesi.
Ni elimu ipi? Ni ile waliotuambia mpaka Bungeni kuwa gesi ile ilitengwa kwa ajili ya Lindi na Mtwara tu?, Au ya huu mpango mpya kwamba sasa ni kwa faida ya nchi nzima?. Hii nongwa imetoka wapi?. Mpango huu ulikuwa wa uwazi na ukweli. Haukuwa siri.


Mheshimiwa unafahamu, Mheshimiwa Kigoda anafahamu, TPDC wanafahamu. Wananchi wa Mtwara wanalaumiwa na kubezwa kwa kosa ambalo siyo lao!! Waheshimiwa mmenyamaza kimya. Mnaangalia mlipo angukia mlipojikwaa mnaficha (Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake tutarejea). Kundi la waheshimiwa wamesheeni Mtwara kwa mbwembwe za ahadi za viwanda na kutengeneza Mji wa Mtwara upendeze. Mkoa wa Lindi vipi? Maana hawana gesi tena, gesi ya mkoa huo imepelekwa Dar es salaam. Je huku sio kujikanganya?.


Mheshimiwa ombi letu kwako kama kweli unauchungu nasi wa Mikoa ya Kusini na unapenda Mikoa hii na watu wake kama kule Lushoto ulikokwenda kuishi, rudi uwe nasi huku Kusini. Aidha utatumia nafasi hii kutuonesha na kutueleza yale mema na mazuri kukumbukwa uliyotufanyia kwa muda uliokuwa Rais wa Nchi hii. Aidha wapelekee wananchi wa Mtwara, Kilwa wakaone mafanikio na faida waliopata wananchi wa Kilwa tangu bomba la gesi ya Songosongo kutua Dar es salaam. Hii itamsaidia Rais aliyechukuwa nafasi yako Mhe. JAKAYA MRISHO KIKWETE afuate nyao zako. Waheshimiwa Wabunge wote wa kusini na hasa wanakamati waliochaguliwa na Mheshimiwa Spika kwa ajili ya kushughulikia swala la gesi Mtwara waende Kilwa wakaone mafanikio ya gesi kuja Dar es salaam ili nao washughulikie kitu wanachokielewa faida yake kwa kuona kwa macho yao. Wasipelekwe pelekwe kiholela. Hawa ni wawakilishi wa Wananchi.Wanastahili kuheshimiwa.


Tunashauri kwa mara nyingine tena. Wananchi wasilaumiwe bila sababu ya maana. Hivi kweli Serikali haina uwezo wa kushawishi baadhi ya viwanda vilivyorundikana hapa Dar es salaam kwenda Kusini (Kilwa, Lindi na Mtwara). kama maskini ndugu zetu Wasukuma, Wamasai, Wagogo wameweza
kulazimishwa kuletwa kusini ambako kwenye nafasi ya ardhi kubwa na malisho tele!!. Je gesi sio malisho tele ya Viwanda?.


Kama wafugaji hawa walihamishwa ili wasiendelee kuharibu mazingira, je viwanda vilivyojazana hapa Dar es salaam haviathiri mazingira? Ugomvi baina ya wananchi na wenye viwanda, Wazo Hill, Mikocheni, Vingunguti kwa sababu ama kuziba njia au kutiririsha maji machafu yanayoashiria uvunjifu wa amani hamuoni umuhimu wa kukomesha hali hii?. Sema kweli Mheshimiwa unamatatizo gani na ndugu zako hawa wa Kusini? kama kuna kosa lolote tulikukosea tunachukua nafasi hii kukuomba radhi.


Mheshimiwa kwa heshima, taadhima na kwa unyenyekevu mkumbwa, na kuuliza swali. Ni ipi fedheha kubwa zaidi kati ya Serikali kusema uongo kwa makusudi na kwa kugharamia (Hata kama kwa mfano waliokusudiwa kudanganywa ni mbwa) na wananchi kuandamana kudai haki zao za msingi (Hazi za binadamu Article 25) hata kama maandamano hayo yalifanywa kwa makosa?


Natanguliza shukrani,


SAIDI.M. MANNORO
(UMMK)
Simu: 0784 548942
: 0715 648942



NAKALA:-
- Mhe. JAKAYA MRISHO KIKWETE
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO
TANZANIA

- WABUNGE WOTE

- WANANCHI WOTE WA MIKOA YA KUSINI.

-WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA
 
Kaka gesi haitoki Mtwara. Tumeshaiambia serikali ya kikwete na ccm kwamba GESI KWANZA MAISHA BAADAYE. Rejea TAMKO LA SHURA YA MAIMAMU MKOA WA MTWARA LA TAREHA 18/01/2013 pia tamko la MAASKOFU, TAMKO LA muungano wa vyama 9 vya upinzani lenye kauli mbio GESI KWANZA VYAMA BAADAYE, na tamko la ASIZE zisizo za kiserikali. GESI MTWARA HAITOKI, ila umeme ruksa kupelekwa kokote. Wabunge wote wakusini walirubuniwa kwa kupewa safari, walipelekwa Trinida & Tobago ati kujifunza kuhusu gesi ili warudipo watoe elimu kwa wapiga kura wao. Subutu, hakuna aliyejaribu kuitisha mkutano wa hadhara katika jimbo lake na kutoa elimu hiyo maana wametukuta wananchi tunajua zaidi faida ya gesi kuchakatwa Mtwara sasa watatuelimisha nini? Wakagwaya na kula kona kwa hakika walisoma alama za nyakati maana wangethubutu tu tungewapa kibano cha paka mwizi ampaka wangejuta. KAKA GESI HAITOKI MTWARA. na liwalo liwe. tulimsikia mtoto wa mkulima
 
Back
Top Bottom